SpaceX Wamejaribu Kudaka Pua ya Roketi yao — Lakini Wameikosa

Newzfid

Member
Feb 23, 2018
5
34
f9-govsat.jpg



Baada ya kuirusha roketi ya Falcon 9 toka California jana, SpaceX walitumia neti kubwa kujaribu kuidaka pua au 'nose cone' ya roketi pale itakapo dondokea bahari ya Pacific. Kwa mara ya kwanza jaribio liligonga mwamba, kipande kimoja cha pua kilikoswa na neti ambayo ilifungwa kwenye meli na kudondokea pembeni hivyo kikapotelea baharini.

Sehemu hiyo ya roketi pia inaitwa 'payload fairing', ile pua yenye umbo la cone inakaa mbele ya roketi, kulinda mzigo wa ndani ya roketi wakati wa kurushwa kwenda hewani. (Tazama kuanzia dakika 2: 24 kwenye video ifuatayo uone pua ya roketi ikikatika na kuwa vipande viwili)




Mara baada ya roketi kufika angani, pua hiyo inavunjika kuwa vipande viwili na kurudi tena duniani. Kikawaida, makampuni hayapotezi akili na mda wa kutaka kukomboa au 'recover' vipande hivyo, Lakini kwa CEO wa SpaceX, Elon Musk anaonyesha shauku ya kutaka kuvirejesha duniani vikiwa vizima. "Fikiria unakuwa na $6 million kwenye kibegi kikielea hewani lakini kinakuja kupotelea baharini" Musk alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari mwezi machi,2017. "Hivi utajaribu kuokoa? Ndio. Ndio lazima utafanya hivo"

SpaceX wamekuwa maarufu kwa kuzifanya roketi zao zitue tena duniani baada ya kurushwa ili zirushwe kwa mara nyingine tena.


Lakini njia ambayo wanataka watumie kuokoa pua za roketi ni kitu cha tofauti na kile wanachofanya kwenye mhimili wa roketi. Booster za Falcon 9 huwa zinawasha injini zake zinapokuwa zikirudi duniani, ili kupunguza spidi yake na kuipa mwongozo mzuri wakati wa kutua. Pua za roketi za kawaida hazina injini wala chochote kile. Lakini SpaceX wameweka mfumo na injini ndogo zinazoiongoza pua ya roketi wakati ikishuka toka angani kitaalamu zinaitwa 'Thrusters'

Pale vipande vikiwa viko karibu na uso wa dunia, mwavuli au parachute ndogo zinafunguka kupunguza kasi ya kuanguka. Kwenye uso wa dunia, ambao ni bahari kunakuwepo meli ya SpaceX inayoitwa Mr. Steven ambayo inajaribu kudaka vipande kwa kutumia neti kubwa kama makucha.

Kwa bahati mbaya, meli hiyo ikashindwa kudaka ingawa pua hiyo haikuharibika kwa kuwa haikudondoka kwa kasi sana. Bila kujali jaribio hilo, Elon Musk kasema kuwa ndani ya miezi sita atahakikisha wanaweza kukomboa pua za roketi zao
 
Wanasayansi hao siyo sisi njaa mingi tunawaza tumnunue nani aje kwenye chama chetu....wenzetu wanarusha vitu vyao angani, sisi tunarushia binadamu (RIP Akwelina)
 
Wanasayansi hao siyo sisi njaa mingi tunawaza tumnunue nani aje kwenye chama chetu....wenzetu wanarusha vitu vyao angani, sisi tunarushia binadamu (RIP Akwelina)
yaan unachoongea ni sahihi kabisa, lakini naamini kama kutakuwa na sera nzuri ya kuunga mkono ugunduzi wa kisayansi nchini kwetu basi siku moja hii nchi itarusha japo hata roketi yetu moja
 
Wanasayansi hao siyo sisi njaa mingi tunawaza tumnunue nani aje kwenye chama chetu....wenzetu wanarusha vitu vyao angani, sisi tunarushia binadamu (RIP Akwelina)
Hizo hela za manunuzi wangenipatia mimi, ningeanzisha Chuo cha intelligencia ambacho kingetengezea na kutoa vichwa vya hatari ambavyo vingeibadirisha nchi kwenda kwenye world class levels bila hata ya rais kutoa macho, kukaza misuli ya shingo, kujitia jeuri kuongea sana. Pia vingeleta mabadiriko bila ya damu kumwagika kama hivi
Cc Malcom Lumumba
 
Wanasayansi hao siyo sisi njaa mingi tunawaza tumnunue nani aje kwenye chama chetu....wenzetu wanarusha vitu vyao angani, sisi tunarushia binadamu (RIP Akwelina)

Kurusha risasi angani kisha ikapiga reverse au kukata kona angani ni technology ya juu kuliko hata kurusha
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom