South Africa na Rwanda mataifa yaliyodhamiria kuondokana na Corona

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
South Africa na Rwanda ndiyo mataifa pekee katika ukanda wetu yaliyodhamiria kwa dhati kabisa kuondokana na Corona.

This being once for all.

Ndani ya mwezi mmoja wenzetu hawa wakiwa huru kabisa bila ya kuwa na Corona au angalau kuwa na trend za wazi kuwa hali zao wamezidhibiti vilivyo, itakuwa si ajabu.

Siyo siri jamani mnyonge mnyongeni - they are enviable.

Nchi mbili hizi ambazo ziko katika ukanda wetu hazina mzaha hata kidogo na ugonjwa huu. Kama ilivyo kwa nchi zote ukanda wetu tunaoshirikiana kimikakati, wanaifahamu vyema:

1. kasi ya maambukizi ilivyokuwa kubwa.
2. kuwa inataka mgonjwa mmoja tu kuambukiza hata jamii nzima katika muda mfupi tu.
3. kuwa suluhu ya ugonjwa huu ni kwenye kuwafahamu wote walioambukizwa na kuchukua hatua stahiki.
4. kuwa inahitaji angalau siku 14 tu kuweza kumbaini mtu mwenye maambukizi.

Tofauti iliyopo ni kuwa wenzetu hawa wawili (tofauti na wengine) wameamua kuchukua hatua timilifu pasi ns kuchelewa zaidi.

Kongole kwao.

Katika kuhakikisha kuwa wagonjwa na walioambukizwa wote wanafahamika, Rwanda wamejiwekea siku 14 ambapo watu wote kabisa (kwa umoja wao) watasalia majumbani, wakiwabaini waathirika mmoja mmoja:

Covid-19: Rwanda Police Shoots 2 People Dead for Defying Lockdown

Kwa hakika ilikuwa sahihi kutambua hawa kuwa "hapo kazi tu!"

Afrika kusini wao tofauti kidogo, wananchi wanasalia (kabisa) majumbani kwa siku 21.

'Unprecedented': South Africa goes into coronavirus lockdown

Hawa nao ni sahihi kuwatambua kwa jitihada zao. Si haba wamejifunga vibwebwe, hadi mbivu na mbichi zifahamike.

Kweli penye nia pana njia.

Uganda, DRC na Kenya kwa hatua zao za nusu nusu walizo nazo, huu ugonjwa watakuwa nao bado kwa muda, japo itakuwa kwenye namna ambayo wataweza kuumudu.

Hawa bado ni kisebu sebu na kiroho papo.

Bado uchumi wanaukodolea macho. Wana mawazo ya kupata kote. Mwangata wawili moja humponyoka. Curfew zao hizi za muda muda siyo kwa Corona. Labda kama ingekuwa kwa al shabab.

BREAKING: Cabinet Tells Museveni to Shutdown Public Transport, Restrict Markets

Coronavirus: Positive cases remain 31 as curfew set to kick in

Coronavirus: SA records deaths, Kinshasa lockdown, cases up in East Africa | Africanews

Tanzania kwa hii ya kunawa nawa huku mikusanyiko kama ya masoko , ibada, usafiri wa umma, nk ikiendelea; kulikuwa hakuna hata haja ya kufikiria mambo uchaguzi mkuu.

Si vibaya kutambua hii hadithi za uchaguzi mkuu kwa sasa is a mere ploy. Pasipo na kupepesa macho - kwa ugonjwa huu na mikakati tuliyonayo hadi sasa, kwa hakika tumeyakalia mabomu hatari sana kuliko hata yale ya mbagala.

Maisha hayawezi kurudi kuwa ya kawaida kiasi cha kufikiria chaguzi bila ya kuwa na mkakati wa dhati wa kuiondosha Corona.

Hadi hapa tulipo Corona ingali iko huru ikipuyanga mitaani mwetu.
 
Ni sahihi hatujajiandaa na kuwaandaa watu vya kutosha.

Lakini nchi ulizozitaja hapo juu mkuu zina wagonjwa wengi.

Moja ina zaidi ya 40.

Nyingine inayozaidi ya 1 000.

SA walikuwa hawana namna....angalia kabla ya lockdown walichokuwa wakikifanya hapa chini


 
Rwanda: Total cases - 50
Burundi: Total cases - 0

Mkuu usihadaishwe na taarifa za kupikwa.

Kagera kuna dereva wa lori toka Burundi impounded in Tanzania ana Corona. Kaipata wapi kama si Burundi wanakosema hawana corona?

Hizi taarifa nani yupo kuzi verify?

Uliwahi kusikia matango pori hulishwa?
 
Hao polisi wangeua raia hapa Tanzania, comments zingebadilika.
Sisi tunajuana kwa vilemba..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sikubaliani kuwauwa hawa jamaa Ila bado inaonyesha jinsi gani wamedhamiria.

Wanajua kama Boris Johnson ana Corona. Wote wanaweza toweka. Hakuna utani kwenye hilo:

https://www.bbc.com/news/live/world-52058788

Hukuyasikia ya Mambosasa na akina Bulaya na Mdee? Si unajua yalifanyika kwa jina la nini hadi kuwa acha wadada wale mikono imevunjika?
 
asee hiyo video hapo nimeipenda.imenikumbusha enzi za akina sogy dogy coco beach.hayo ndo maisha bwana watu wanakula kwaito mpaka basi.corona atapita tu watu waendelee na maisha yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani wewe upo na corona tu...
Yaani namba inavyosoma kidogo kidogo hapa Tanzania roho inakukereketa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu niko na Corona kwa sababu hatari iliyopo iko wazi. Ni ajabu na kweli kama wewe huoni.

Hata hivyo waswahili wanasema "mwenye macho haambiwi tazama".

Mengine wasiwasi wako tu. Kwa hakika kwa namba yoyote kubwa au ndogo kwangu haina maana kama hazipo hatua madhubuti za kuudhibiti ugongwa huu.

Waziri Mkuu wa England, Boris Johnson amegua Corona.

https://www.bbc.com/news/live/world-52058788

Hamdhani kuwa sote, sote kabisa wakiwamo kina Magufuli tuko hatarini kama huyu kirusi hajawekewa hatua thabiti za kumdhibiti.

Mkuu usijidhanie kuwa u mzalendo kuliko wengine.

Inawezekana nikawa na Corona, vile vile inawezekana unayo. Kwani waliopata Corona wamemkosea nini Mungu?
 
Ni sahihi hatujajiandaa na kuwaandaa watu vya kutosha.

Lakini nchi ulizozitaja hapo juu mkuu zina wagonjwa wengi.

Moja ina zaidi ya 40.

Nyingine inayozaidi ya 1 000.

SA walikuwa hawana namna....angalia kabla ya lockdown walichokuwa wakikifanya hapa chini




Mkuu, mafanikio ya lockdown kama nilivyoainisha kwenye mada itaanza kuonekana baada ya siku 14 za kwanza.

Ndiyo kwanza lockdown inaanza, kwa hiyo kudai kuwa wenye lockdown wana namba hii ya wagonjwa nadhani ni irrelevant kabisa. Au siyo mkuu?
 
Mkuu, mafanikio ya lockdown kama nilivyoainisha kwenye mada itaanza kuonekana baada ya siku 14 za kwanza.

Ndiyo kwanza lockdown inaanza, kwa hiyo kudai kuwa wenye lockdown wana namba hii ya wagonjwa nadhani ni irrelevant kabisa. Au siyo mkuu?
Ni sahihi uyasemayo mkuu.


Ila SA nadhani lockdown ilihitajika mapema.
 
Ni sahihi uyasemayo mkuu.


Ila SA nadhani lockdown ilihitajika mapema.

La kheri kuona nisemayo ni sahihi. Ni kweli lockdown South Africa imechelewa. Ni kuchelewa huko huko kunaonekana kote ikiwamo Tanzania.

Hata hivyo hadi total lockdown itakapo kuwa effected mahali popote pale ndipo countdown ya kuelekea kwenye kuifuta Corona itaanza.

Tofauti ni hii nchi inapochelewa athari zinakuwa ni kubwa zaidi. Hii ni ki maisha ya watu, uchumi, raslimali nk.

Kiufupi hakuna faida yoyote kuchelewa kwenda total lockdown maana ni suala la muda tu.
 
La kheri kuona nisemayo ni sahihi. Ni kweli lockdown South Africa imechelewa. Ni kuchelewa huko huko kunaonekana kote ikiwamo Tanzania.

Hata hivyo hadi total lockdown itakapo kuwa effected mahali popote pale ndipo countdown ya kuelekea kwenye kuifuta Corona itaanza.

Tofauti ni hii nchi inapochelewa athari zinakuwa ni kubwa zaidi. Hii ni ki maisha, uchumi, raslimali nk.

Kiufupi hakuna faida yoyote kuchelewa kwenda total lockdown maana suala la muda tu.
Lakini raia wengine wanapingana nalo...wanadai watakufa njaa...

Japo utaratibu upo wa watu kununua mahitaji ya muhimu.
 
Corona haina tofauti na Surua ni airborne

Nadhani kwa taarifa zilizopita siyo airborne per se. Ndiyo maana kuna hii misisitizo ya kunawa nawa.

Hata hivyo kama partial airborne au fully airborne nadhani waliona bomu la mbagala tulilokalia ukizingatia mikusanyiko iliyopo kwenye masoko, ibada, usafiri wa umma nk.

Kwamba prince Charles, Boris Johnson nk, ni waathirika; uwezekano Corona ni airborne.

Tusidanganyane.

Wanyonge tuwanyonge Rwanda na South Africa wako vizuri.

Rwanda wanabakiwa na siku takribani 7 kumaliza lockdown.

Mvumilivu hula mbivu.
 
Lakini raia wengine wanapingana nalo...wanadai watakufa njaa...

Japo utaratibu upo wa watu kununua mahitaji ya muhimu.

Mkuu South Africa wanagawiwa chakula na serikali.

Mambo ya TWAWEZA kazi kidogo.

Wafe njaa vipi wakati chakula bure?
 
Back
Top Bottom