Sophia Simba: Siasa na tendo la ndoa

Sophia Simba: Siasa na tendo la ndoa

Kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 21/06/2010 mwenyekiti wa UWT na pia waziri wa Utawala bora, Sophia Simba, amewashauri wanawake ambao ni wanachama wa CCM kutowapa unyumba waume zao ambao si wanachama wa CCM.

Sasa siasa na ndoa vinaendana kweli? Huku sio kuongeza soko la machangudoa Ohio na kuchochea maambukizi ya Ukimwi? Hao ma-housegirl watapona kweli? Au ndio kasi zaidi, nguvu zaidi, ari zaidi imekwisha anza? Hivi huku sio kuvunja katiba ya nchi ambayo inatoa uhuru kwa kila mwananchi kujiunga au kutojiunga na chama chochote cha siasa?

Hivyo mume hapati unyumba mpaka aoneshe kadi halisi ya uanachama wa CCM? Basi wanaume wengi watakaojiunga na CCM muda huu itakuwa ni utekelezaji wa ushauri wa mama Simba?

Kwani huyo mama anajua haki za mume kama hana mume? Anaelezea nadhani watu wanaogawa bidhaa hiyo kiholela bila TBS kuhusishwa, ndio wanaoshauriwa wasiwape wasio wanaCCM. Ni machangu wenzake. Umesikia wapi kwamba kaolewa? Hukumbuki juzi alipokuwa anakaribishiwa wageni wake bungeni Jumamosi alipotajwa kijana wake aliyezaliwa na Meya wa zamani wa DSM? Huyu mama inamaanisha ni mgawaji mzuri kwa wanasiasa wa CCM na hivyo anawatahadharisha wenzake warfanye kama yeye kwa kumwiga kama mfano bora. Asituumize vichwa hapa. Kwani CCM ndio ina mtalimbo bora kuliko wanaume wengine?

Hebu tujifunze kuwapuuza watu wasiotumia mantiki katika kueleza mambo ya kimsingi bali :dance:
 
It baffles me that such a woman is a minister for Good Governance. To me, it is completely strange that the woman of her integrity is given such an important portfolio in our government. I don't understand this and when it comes to her remarks, I would say I am dismayed but NOT SURPRISED at all. After all nimeshakuwa surprised sana tu na appointment yake.
 
Anaona kumnyima mume haki yake ya ndoa ni jambo rahisi..........inawezekana kwa hawara sio mume! Yeye kama amezoea kumnyima hawara yake ile kitu kwa tofauti za misimamo ya kisiasa its okay sio ushauri tunaotarajia toka kwa Serikali. Tamko la waziri ni tamko la Serikali.

Sometimes huwa najiuliza hivi hizi ziara Presidaa huwa anaenda US, EUROPE etc huwa kuna vitu pia wanajifunza au ni kuomba misaada tu? Upuuzi kama huu walipaswa kujifunza toka kwa wenzetu kuwa nafasi yako kama kiongozi wa serikali inakunyima uhuru wa kupayuka payuka..!
 
RAIS Jakaya Kikwete wakati akipanga safu yake ya uongozi muda mfupi tu tangu alipoapishwa, hakuficha dhamira yake kwa kutamka bayana kwamba katika uongozi wake atahakikisha anawateua wanawake wenye sifa za uongozi.

Nadiriki kukiri bila kumng’unya maneno kwamba rais amejitahidi kuitekeleza kwa vitendo dhamira hiyo.


Nasema hivyo kwa sababu tumeshuhudia wanawake wengi ukilinganisha na awamu zilizopita, ambao wameweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi.


Ni nia njema ya rais wetu kutaka kutuinua sisi wanawake ili tuweze kushiriki kwenye ngazi za uamuzi, lakini ili wananchi waendelee kuamini anachoamini rais kwamba wanawake wanaweza kama walivyo wanaume, ndiyo maana ameamua kuwabeba kwa mbeleko.


Lakini Juni 20, mwaka huu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (CCM) Taifa,Sophia Simba(Pichani), ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), aliwataka wanawake wa jumuiya hiyo wanaoishi na wanaume ambao si wanachama wa CCM kuwanyima waume wao unyumba kwa lengo la kuwakomesha.


“Ninyi wanawake wenzangu ambao waume zenu wapo katika vyama pinzani na mnajua wazi kuwa hawawapi ushirikiano wowote katika siasa ya CCM wanyimeni ‘nonino’, muone kama hawatarejea katika chama tawala, nonino nikiwa na maana ya tendo la ndoa,” alisema Sophia huku akishangiliwa na wanawake wote kuonyesha kuwa alilolisema limewagusa.


Agizo la Waziri Simba kwa wanawake wa CCM, ni wazi kabisa limetia doa jitihada za rais za kuwapa madaraka wanawake, kwani si siri, baadhi ya wananchi wamekuwa wakihoji uwezo wa kiutendaji wa kiongozi huyo.


Wananchi wameibuka na maswali kutokana na waziri huyo mara kadhaa kunukuliwa na vyombo vya habari akitoa matamko ambayo hayarandani na nyadhifa alizonazo.


Hakuna ubishi kwamba taifa hili limo kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi, pia ongezeko la watoto wa mitaani, lakini cha kushangaza, waziri halioni hilo hadi anaamua kutoa agizo la wanawake wa CCM kuwanyima unyumba waume wao ambao ni wanachama wa vyama vya upinzani.


Kwa mtazamo wangu, binadamu aliyekamilika na ambaye yumo ndani ya ndoa, kuna wakati huhitaji unyumba, sasa kama mwanadamu huyo ambaye ni mume wa mwanamke wa CCM, asipopewa haki yake ya ndoa, eti kwa sababu waziri amewaambia wake zao wawanyime unyumba, ni wazi wanaume wengi wataamua kutafuta njia mbadala, ili kuwapata wanawake wengine pembeni.


Nao wanawake watakapohitaji tendo la ndoa, je waende wapi?Au tayari ameishawatafutia wanaume wengine ambao watawatimizia hamu hiyo?


Kama tunavyojua, ukimwi umetamalaki, mwanamume huyo anapokwenda kutafuta mwanamke mwingine, tuna uhakika gani kuwa mwanamke huyo mpya hajaambukizwa maradhi ya ukimwi?


Si kuambukizwa ukimwi tu, je, ikitokea mwanamume aliyenyimwa unyumba na mkewe akahamia nyumba ndogo, si ni wazi anaweza kutelekeza familia yake na wakati mwingine kusahau au kupunguza kupeleka matunzo kwa familia yake ya awali?


Hivi watakaopata shida si watoto ambao hawana hatia na mwanamke aliyerubuniwa na agizo la Simba?

Hivi huyu Simba alivyotoa agizo la kipuuzi kama hili huku akijua yeye ni Waziri ambaye wizara yake inaziongoza idara nyeti kama Idara ya Usalama wa Taifa,hivi anataka watumishi wa idara hiyo wananchi kwa ujumla wamueleweje?Je waendelee kumheshimu kama Waziri wao au sasa waanze kuamini waziri wao amejigeuza na kuwa Somo au Kungwi? Hatukuelewi.


Na yote hayo yakishatokea mwisho wa siku huyo mwanamke aliyetekeleza agizo la Simba, si atakuwa wa kwanza kulalamika kwamba mumewe kamtelekeza na kukimbilia mahakamani kudai haki na mwisho wa siku watoto watakosa ada za shule na wengine kujikuta wakijiingiza kwenye vitendo haramu vya uvutaji bangi, ukahaba na ombaomba mitaani?


Wakati umefika kwa viongozi wanawake wote mliopewa madaraka kama rais wetu alivyoahidi kuwainua wanawake, mchunge kauli zenu na nyendo zenu, muwajibike kwa masilahi ya taifa ili hata wale wote waliokuwa wakiibeza dhamira hiyo ya rais wakose la kusema.


Namshauri Waziri Simba achague maneno ya kuongea mbele ya umma, kwani kwa agizo hilo endapo litatekelezwa ni wazi litavunja ustawi wa jamii yetu.


Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.


0716 774494
Imeandikwa na HAPPINESS KATABAZI
 
kila kundi lina mbinu zake za kujiendeleza. tusilaumu sana pengine huo ni mkakati uliowekwa na jumuiya hiyo ndiyo maana akatangaza kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
 
Kama mama huyo ametamka maneno hayo basi amewadhalilisha sana wanawake wenziwe, amezidi kuiaibisha Serikali ya CCM na chama kwa ujumla. Angepaswa hata kufukuzwa kwenye chama.
 
Hii ni hasara kwa viongozi wakinamama kwa kweli. Kwa kiwango chake cha elimu alipaswa kufahamu kwamba Government has no business in people's bedrooms. Hivi haya matatizo yote yanayowakabili wakinamama na watanzania kwa ujumla, ameona suala la kuwanyima wanaume ujumba ndio suala muhimu kweli? kwa nini isiwe unemployment, poverty, AIDS, teen pregnancy, illiteracy, equal representation and domestic violence? matatizo ambayo yanaendelea kuwarudisha wanawake nyuma. Yeye anaona "NONINO" ndio suala muhimu. Hakika Gender equality bado inasafari ndefu sana kama mambo yenyewe ndio hivi. :jaw:
 
Huyo ndo mteule wa JK anayeaminiwa wengine photocopy, kumbe yeye mpaka amefika hapo ametoa nonino
mpaka imeota sugu imekuwa kama ya kenge anayeibuluza chini! Jamani wanawake wa nchi wana matatizo
mengi yanayohitaji ufumbuzi sio kuwaambia mambo ya nonino!
 
Maneno hayo yanatamkwa na wale mapashikuna wanaoshinda wakila kungu na kuvizia waume wa wenzao,hivyo kuyasikia kutoka kinywa cha mtu mwenye wadhifa wa Sofia Simba ni kielelezo cha maafa tuliyo nayo Watz ya kupata viongozi sampuli ya sofia.Pia ni kielelezo cha mkuu wa nchi tuliye naye kwani ndiye aliyemteua na haonyeshi kukerwa na kauli za kijinga anazotamka huyu shangingi kila mara.
 
Sophia Simba wengi wetu humu tunamfahamu ni Waziri bogus namba 1 katika awamu hii...lakini hao wanawake walioshangilia nao inaelekea ni wa aina yake.Au ndo siasa za kujipendekeza kwa wakubwa hata wakipayuka na kuongea pumba??hii pia inanikumbusha hotuba ya Prezidaa alipotutukana na kututishia Wafanyakazi wa Tanzania na kupigiwa makofi mazito na wale wazee
 
its enough sasa jamani hata kama tunayo haki ya kusema lolote katika nchi yetu, huyu mama ana mambo mengi mazuri anayafanya pia katika utawala bora vinginevyo nchi isingekwenda vzr, but kila siku tumekuwa wajanja wa kuandika mabaya yake tu as if sisi wote ni wasafi ambao hatukuwahi kufanya dhambi, hebu tuache hizo
 
its enough sasa jamani hata kama tunayo haki ya kusema lolote katika nchi yetu, huyu mama ana mambo mengi mazuri anayafanya pia katika utawala bora vinginevyo nchi isingekwenda vzr, but kila siku tumekuwa wajanja wa kuandika mabaya yake tu as if sisi wote ni wasafi ambao hatukuwahi kufanya dhambi, hebu tuache hizo
Hebu tutajie hayo mazuri aliyofanya
 
Nafasi za uwaziri duniani ni chache sana hivyo jamii zinaamini kuwa waziri anatakiwa awe ni mtu mwenye upeo, busara na anayefahamu uzito wa dhamana aliyopewa.

Kutokana na unyeti wa nafasi hiyo ya uwaziri mteuaji wa nafasi hiyo huwa ni mkuu wa serikali tu.
Kwakuwa uwaziri ni dhamana, ni vigumu kutenganisha utu na uwaziri wa waziri mhusika.

Sofia Simba, Waziri ofisi ya Rais, Mwenyekiti wa UWT, Mjumbe wa CC na NEC ya CCM na dhamana yake kubwa kwenye nchi hii ni Utawala bora.

Pamoja na majukumu hayo, SS ni mweupe kama ubongo wa kichanga,hana lolote katika fikra zake kinachokaribia kumnyanyambua majukumu yake. Ni waziri wa Marupurupu tu na mshahara tu.

Mtu mzima anakaa kuwaambia wanawake wa CCM kuwa kama waume zao wanawasaidia wapinzani basi njia ya kuwakomoa ni kuwanyima tendo la ndoa. Yani SS kwake tendo la ndoa ndio big deal kutumika kama silaha.

Hivi huyu mama ni mkware?? Yani kwa uelewa wake woooooote anaona hawezi kuwaza kingine isipokuwa ngono tu?!

Sofia kila anapomwangalia mwanamke mwenzake anaona ni mashine ya kumtuliza mwanaume ki ngono tu, kwake yeye anachowaza ni ngono tu!

Sofia!!!!!! Amenishangaza sana.

MZITTO
 
Kwenye msafara wa mamba hata kenge wapo,hayo ni madhara aliyojitakia mkuu wa kaya yetu kulipa fadhila kwa wale walimsaidia kwa njia moja ama nyingine uwepo wake madarakani. Siasa halikuwa chaguo lake sahihi huyu mama,zaidi ilifaa awepo kwenye bendi f'lani ya mipasho.
 
"birds of a feather flock together" maana yake Sophia na Mrisho hawana tofauti kwa mambo ya ovyo! Kumwondoa Sophia madarakani kwanza unaanza na kumwondoa JK katika kiti cha urahisi! No vote 2010!! Nafikiri yule katibu wa UWT aliyepigwa zengwe na kuondolewa alikuwa na busara na makini na kazi yake. Sababu mojawapo ya kumwondoa nasikia ni kwamba alikuwa anavaa vizuri kuliko 1st lady, Salma Kikwete!!!
 
Aaaah Da Sofie mie hunimaliza sana...siwezi kusahau yale mahojiano yake na klh news?
 
Leo nimesoma gazeti la mwanahalisi ukurasa wa 10 kuna makala iliyo andikwa na Mbasha Asenga, yenye kichwa cha habari "Akili ya Sofia haiwezi kuwaza zaidi ya ngono"


Naomba kunukuu mistari kadhaa ya habari hii iliyo ni changanya zaidi.


"Pamoja majukumuvyote haya, Sofia ni mweupe kama ubongo wa kichanga cha leo. Hana lolote katika fikra zake kinachokaribia kumfanya kutambua majukumu yake......."

Naomba kuruka huo mstari maana kuna manono siwezi ya andika hapa.

akaendelea

" Lakini kwa kuwa nafasi za uwaziri zilikwisha kurahisishwa siku nyingi , bado ataendelea kutesa,kwani ana shida gani wakati akili yake imeganda kwenye ngono na hicho ndicho kilimpa uwaziri?"




Ina maana Sofia Simba alipata uwaziri kwa *****?
 
Leo nimesoma gazeti la mwanahalisi ukurasa wa 10 kuna makala iliyo andikwa na Mbasha Asenga, yenye kichwa cha habari "Akili ya Sofia haiwezi kuwaza zaidi ya ngono"


Naomba kunukuu mistari kadhaa ya habari hii iliyo ni changanya zaidi.


"Pamoja majukumuvyote haya, Sofia ni mweupe kama ubongo wa kichanga cha leo. Hana lolote katika fikra zake kinachokaribia kumfanya kutambua majukumu yake......."

Naomba kuruka huo mstari maana kuna manono siwezi ya andika hapa.

akaendelea

" Lakini kwa kuwa nafasi za uwaziri zilikwisha kurahisishwa siku nyingi , bado ataendelea kutesa,kwani ana shida gani wakati akili yake imeganda kwenye ngono na hicho ndicho kilimpa uwaziri?"




Ina maana Sofia Simba alipata uwaziri kwa *****?

Woohhhh!!!!!! I am speechless
 
Back
Top Bottom