Lakini kwa kuwa nafasi za uwaziri zilikwisha kurahisishwa siku nyingi, bado ataendelea kutesa na kutesa, kwani ana shida gani wakati akili yake imeganda kwenye ngono na hicho ndicho kilichompa uwaziri?
Kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 21/06/2010 mwenyekiti wa UWT na pia waziri wa Utawala bora, Sophia Simba, amewashauri wanawake ambao ni wanachama wa CCM kutowapa unyumba waume zao ambao si wanachama wa CCM.
Sasa siasa na ndoa vinaendana kweli? Huku sio kuongeza soko la machangudoa Ohio na kuchochea maambukizi ya Ukimwi? Hao ma-housegirl watapona kweli? Au ndio kasi zaidi, nguvu zaidi, ari zaidi imekwisha anza? Hivi huku sio kuvunja katiba ya nchi ambayo inatoa uhuru kwa kila mwananchi kujiunga au kutojiunga na chama chochote cha siasa?
Hivyo mume hapati unyumba mpaka aoneshe kadi halisi ya uanachama wa CCM? Basi wanaume wengi watakaojiunga na CCM muda huu itakuwa ni utekelezaji wa ushauri wa mama Simba?