Somo ulilolipenda sana darasani

Somo ulilolipenda sana darasani

Physics au Engineering science make Technical drawing iko Technical school ambako hakuna Physics.
Mkuu Physics ipo Japo inaitwa engineering science, TD ni tofauti lenyewe ni michoro tu mimi ni mwana kiungani viva TTS
 
Somo la kutoroka kwa kuchupa nililipenda sana sena ukiingia maabara kufanya practical Mara ajali hiyo ya kubambwa na kula bakora za hatari.
 
Mkali wa Namba!
Hakuna Somo nililowahi kupenda sana kama namba
na ndiyo somo ambalo toka std 1 mpaka form six niliweka A
But ndiyo hivyo sikuendelea nayo University
But am proud nilichosoma pia kinahesabu
 
Napenda sana Mathematics tena kutoka moyon kabisaa, ndoto zangu ilikua baada ya kumaliza form4 niende DIT kusoma Mec engineering lakini mwisho wa siku Math nikapata B, phy C, Chem D (CSEE 2011). "D" ya chemistry ikasababisha nishindwe kuchaguliwa DIT nikapelekwa Advance PCM. Advance sikufanya vizuri sana ila kwasasa nipo chuo flani nasoma bachelor of education(science) mwezi wakumi mwaka huu naingia mwaka watatu. Lakini naamini ipo siku moja nitakuja kusoma Automobile Engineering hata kwa level ya diploma(vigezo vya kusoma degree vimebadilika). Yani nasoma ualimu huku sina furah, kwani nahisi Mathematics ndio kilakitu kwangu

Inauma sana kusoma kitu usichokipenda. Pole mpendwa, ila penye nia pana njia. Nami nilichepuka ila now I am back with my Biology enjoyyyyyyyying
 
asee mm ngeli nilikuwa naipenda balaa kutoka shule ya msingi..huwezi amini nilihitimu shule mwaka 1997 tena huko kjjn interior lakini nilikuwa naweza kugonga ung'eng'e ...baada ya kuhitimu hakuna aliyefaulu darasani kwetu nikaingia kitaa na umombo wangu nikawa machinga huku natembea na mivitabu yakimombo....nilikaa miaka 7nikaamua kurudi shule ...thank god sasa hivi nina bachelor of with ed....linguistics& literature in engl as teaching subjects

Ha ha haaaaa ung'eng'e, kweli ndoto haifi, ukiamua inawezekana. Hongera
 
nilikuwa nampenda mwalimu mrembo wa kiswahili darasa la nne.
mwalimu wa hesabu alikuwa shemale
 
Binafsi mie nilikuwa mzuri wa Biology, nilifaulu sana na kulead in class ila cha kushangaza, baada ya form six nikaenda kusoma uchumi in which sikufanya vizuri kabisa darasani. Nilipomaliza chuo nilipata kazi ila still kichwani Biology iliniita kila wakati mpaka nilipoamua kuirudia and now ninafuraha ya maisha na ni best scientist kwenye kada ninayofanyia kazi.

Nawashauri hata wengine, somo unalolifeel sana ndilo litakalokutoa maishani. Achana na kelele zikuzungukazo. Mf, mtu uko vzr kiswahili ila unang'ang'ania Physics mwishoe unakula F na kubaki unalialia. Si kila aliye na maisha mazuri kasoma masomo unayofikiria ndiyo leading. Wazazi tujifunze kuwashauri wanetu na pia kuwasoma nini wapendacho ili mbeleni kiwasaidie kuwa na furaha ya kazi zao. Si kila anayepata mshahara mkubwa ana furaha kazini.

Kazi nzuri ni ile uifanyayo toka ndani kwa furaha.
Je wewe ulipenda na kuliwezea somo gani?
Somo la anatomy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom