Somo la leo:Zaburi 12 3-8

Somo la leo:Zaburi 12 3-8

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,828
Reaction score
15,608

Zaburi 12:3-8 BHN​

Ee Mwenyezi-Mungu uikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu, na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia. Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo tunayo, nani awezaye kututawala?” Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Kwa sababu maskini wanadhulumiwa, na wahitaji wanapiga kite, sasa naja, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.” Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi, safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri, naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba. Utulinde, ee Mwenyezi-Mungu, utukinge daima na kizazi hiki kiovu. Waovu wanazunguka kila mahali; upotovu unatukuzwa kati ya watu.
 
2 Timotheo : 2 : 4 - Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
 
Back
Top Bottom