Miujiza 40 ya mtume Muhammad (S.A.W)

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,942
3,608
Amani iwe kwenu enyi mliopata fursa ya kusoma haya ambayo huenda ikawa sababu ya uongofu kwa wenye kutafakari

Wengi wasio waislamu wamekuwa wakisema kwamba mtume muhammad s.a.w hajawahi kufanya miujuza.kwa kulipokea ilo ni wazi kwamba madai yao yanaonyesha wazi wanasema bila ya ujuzi wa mambo..pengine wanajua ila wameamua kupotosha ama hawajui ila haikuwapasa kutoa kama facts ilhali hujakaa kusoma na kuthibitisha...leo huenda ikawa ni mwisho wa ulongo wao na kujutia waliyo yazusha bila kuwa na elimu nayo..mitume wamepewa miujiza ili wapate kuaminika ktk ila miujiza sio guarantee ya mtu kuamini (watizame wana wa israel na mussa)..miujiza ipo kuwaongezea imani waumini na walau wale wenye nyoyo ngumu basi wapate kuamini.miujiza yote iliyofanywa na mitume hawakufanya kwa matashi yao ila kwa msaada wa allah.hapa nakubainishia baazi ya miujiza aliyoifanya mtume muhammad
MIUJIZA YA MTUME (S.A.W)
(1) QURAN
Hakika huu ni muujiza mkubwa kabisa katika historia ya mwanadam...Namna Quran ilivoshushwa kwa mtume toka kwa muumba kupitia kwa Jibril hadi kwa mtume MUhammad Hakika ni muujiza tosha.Kisha Quran ikahifaziwa ili isipate kuharibiwa kama vitabu vya mwanzoni nayo hadi sasa maandiko yake yanatimia na kulindwa kama ilivyo ahidiwa na Allah.Huu ni muujiza endelevu tangu Muhammad hadi kiama muujiza huu utasimama. Hakika Qur'ani pamoja na kuwa ni kitabu cha kielimu, utamaduni hukumu, haki, maadili, adabu, siasa na uchumi, ni muujiza wa mbinguni na wa milele wenye athari kubwa ya kiroho na kimaaanawia ya hali ya juu.Hii ndio Qur'ani ambayo ni muujiza, na hiki ndio kitabu cha mbinguni cha milele, kitabu ambacho ndani yake kuna mambo yamfikishayo mwanadamu kwenye saada na maisha ya neema na raha, kitabu ambacho hueneza kheri na baraka kwa watu wote, na hutawanya amani na salama katika ardhi hii na katika nchii zote, kumepokelewa riwaya mbali mbali kuhusiana na ubora wa kujifunza kitabu hiki na kukisoma pia kukihifadhi na kutekeleza maamrisho yake, na kufanya matendo kwa mujibu wa maamrisho ya kitabu hicho na zingine nyingi ambazo zinazo muhimiza mwanadamu kukitilia umuhimu.

(2) CHAKULA CHAONGEZEKA
Katika siku za vita ya Tabuki, njaa ilikuwa imeenea katika Bara Arabu. Kwa hiyo jeshi la Kiislamu halikuwa na vyakula vingi vya kutosha. Lakini kile kiasi kidogo walichokuwa nacho pia kilikuwa karibu kuisha na wanajeshi wa Kiislamu wakapata taabu ya njaa. Hapo baadhi ya masahaba walimwomba Mtume s.a.w. wapewe ruhusa ya kuwachinja ngamia waliokuwa wakitumika katika vita ili waweze kuondoa njaa yao kwa kuzila nyama hizo. Mtume s.a.w. aliruhusu kuchinja ngamia wa kivita, kwani kulikuwa hakuna njia nyingine ya kupata cho chote cha kula. Lakini Seyidna Umar r.a. alipopata habari hii yeye akafika haraka kwa Mtume s.a.w. na akasema. “Kama tutachinja ngamia, basi tutapungukiwa wanyama wa kupanda na kwa hiyo tutapata taabu kubwa sana. Basi, Ewe Mtume s.a.w. uwaamrishe watu wakusanye vyakula vyao vilivyobaki na kisha umwombe Mwenyezi Mungu atie baraka ndani yake, asaa Mwenyezi Mungu 3 akabariki.” Mtume s.a.w. alikubali shauri hilo. Basi, Mtume s.a.w. akaagiza tandiko kubwa la ngozi na akatangaza kuwa mtu ye yote ambaye anacho cho chote kile akilete hapa. Basi baadhi ya watu walileta mahindi kidogo sawa na kiganja kimoja tu, na baadhi wengine walileta tende na wengine wakaleta makombo kidogo ya mkate. Ilimuradi kiasi kidogo sana kikakusanywa kwenye tandiko lile. Mtume s.a.w. akaomba dua kwa kubariki kiasi hicho kidogo cha chakula, na kisha akatangaza kuwa kila mtu ajaze vyakula hivyo katika mifuko yake. Hapo kila mtu akaanza kujaza mfuko wake, na mifuko yote ya chakula ikajaa. Wote wakala mpaka wakashiba, na chakula kingi kilibakia vile vile, na wanajeshi hao walikuwa 30,000. Hapo Mtume s.a.w. alisema, “Ninashuhudia kuwa hakuna apasaye kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu, na kwamba MIMI ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Kisha alisema, yule mtu atakayehudhuria mbele ya Mungu ilihali ana imani katika mambo hayo mawili, Mwenyezi Mungu hatamnyima pepo. Mwujiza huu wa ajabu umeelezwa katika kitabu mashuhuri cha hadithi za Mtume s.a.w. kiitwacho Sahih Muslim, kitabul-Iman.

(3) MAZIWA YA BARAKA
Seyidna Abu Hurairah r.a. alikuwa ni sahaba mashuhuri sana wa Mtume s.a.w. Yeye aliposilimu aliahidi ya kwamba siku zote atakaa pamoja na Mtume s.a.w. ili kujifunza dini. Alikuwa mwenye kiu ya ajabu ya kusikiliza maneno matukufu ya Mtume s.a.w. hata kwamba wakati mwingine alikuwa haendi nyumbani kwake kula chakula kwa kufikiria pengine nyuma yake Mtume s.a.w. atatokea na kusema maneno ya hekima naye atakosa kuyasikia kama ataondoka hapo. Na wakati mwingine alikuwa anashinda mlangoni pa Mtume s.a.w. mpaka alikuwa anasikia njaa sana, lakini asiondoke hapo.Seyidna Abu Hurairah (r.a) na kisa chake cha ajabu.Seyidna Abu Hurairah r.a. anasema kuwa yeye safari moja aliposikia njaa sana, Mtume s.a.w. alipita karibu naye na akautambua ubaya wa hali yake. Bwana Abu Hurairah r.a. anasema kuwa, "Mtume s.a.w. aliniambia nifuatane naye mpaka nyumbani, nami nikamfuata. Tulipofika nyumbani kwa Mtume s.a.w., yeye akaingia ndani nami pia niliingia pamoja naye kwa idhini yake. Kikaletwa kikombe kimoja cha maziwa. Mtume s.a.w. akauliza nani ameleta maziwa haya? Akaambiwa kuwa bibi fulani ameyaleta kama zawadi.” Seyidna Abu Hurairah r.a. anaendelea kusimulia. “Mtume s.a.w. aliniamrisha niwaite watu wa suffa. Hao jamaa walikuwa hawana nyumba zao wala kazi, walikuwa wanashinda msikitini na kufanya ibada siku zote. Mtume s.a.w. alipokuwa analetewa mali ya sadaka alikuwa anawapelekea zote hao jamaa; lakini kama alikuwa analetewa zawadi, basi alikuwa anatumia mwenyewe vile vile, na pia alikuwa anawapelekea. “Mtume s.a.w. aliponiambia kuwaita hao watu wa Suffa, nilihangaika moyoni kwa kufikiri kwamba kikombe kimoja tu peke yake kitawatoshaje watu wengi hao; nilihitaji zaidi maziwa haya. Kwa vyo vyote, hii ilikuwa ni amri ya Mtume s.a.w.; basi, nikawaita wote hao. Walipofika hao jamaa na kukaa chini mahali pao, Mtume s.a.w. aliniambia niwape hao kikombe hicho cha maziwa zamu kwa zamu. Nikafikiri moyoni mwangu kwamba sasa maziwa haya sitaweza kuyapata. Lakini kulikuwa hakuna njia yo yote isipokuwa kutii tu amri ya Mtume s.a.w. Mimi nikashika kikombe na kumpa mtu mmoja; yeye aliposhiba nikampa wa pili naye pia alikunywa mpaka akashiba, basi nikampa wa tatu. Nikaendelea mpaka wote wakanywa na kushiba, na mwishowe nikampa Mtume s.a.w. kikombe. Mtume s.a.w. 5 akaweka kikombe mkononi mwake na akatabasamu kwa kunitazama mimi, kisha akasema ‘Sasa sisi wawili tu tumebaki’. Nikaitika, ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hapo Mtume s.a.w. aliniambia, sasa kaa wewe na kunywa. Nikakaa na nikanywa. Nilipoisha Mtume s.a.w. akasema, ‘Kunywa’. Nikanywa tena. Kila nilipoacha kunywa akaniambia ‘Kunywa’, mpaka nikashiba sana na nikamwambia Mtume s.a.w. “Naapa kwa yule aliyekutuma kwa haki kwamba sasa hamna nafasi tumboni”. Hapo Mtume s.a.w. akashika kikombe, akamsifu Mwenyezi Mungu, na kisha kusema Bismiliahi akanywa maziwa yote. (Bukhari, Kitabur-Riqaaq). Mwujiza huu ni mkubwa sana. Kwa kikombe kimoja tu peke yake jamaa wengi wakashiba na maziwa yakabaki vile vile!!

(4) CHEMCHEM YABUBUJIKA
Vita ya Tabuki ilitazamiwa kupiganwa kati ya Waislamu na jeshi la mfalme wa Kirumi. Kwa hakika mfalme wa Rumi alipoona Waislamu wanazidi siku zote kupata nguvu, yeye aliamua kupigana nao ili kuwaangamiza. Kwa hiyo yeye akakusanya malaki ya wanajeshi wenye silaha tele. Mtume s.a.w. alipopata habari hii, naye vile vile akatangaza Waislamu wajitayarishe kupambana na jeshi la Kirumi. Basi, Mtume s.a.w. pamoja na jeshi lake (Masahaba 30,000) alitoka nje ya Madina mpaka alifika mahali paitwapo Tabuki. Lakini Jeshi la Kirumi lilipopata habari kuwa Waislamu wamekwisha fika Tabuki kupambana nao, wakaingiwa na woga, hawakuja tena kupigana na Waislamu. Mtume s.a.w. pamoja na masahaba walisubiri, huko Tabuki kwa siku 10, na kisha wakarudi Madina. Waislamu walipokuwa wanarudi Madina, njiani walipita katika 6 bonde liitwalo Bonde la Mushfiq, walisikia kiu sana. Hapo palikuwa na chemchem moja iliyojulikana kwa watu. Lakini chemchem hii haikuwa na maji mengi. Maji yalinyinyirika kidogo kidogo ambayo yaliweza kutosha kwa watu wawili tu. Kwa hiyo Mtume s.a.w. alitangaza kwamba mtu ye yote asianze mwenyewe kuyanywa maji yale bila watu wote kufika pale. Masahaba walikuwa watiifu, walifanya alivyoamrisha Mtume s.a.w. Lakini baadhi ya wanafiki waliokuwa katika jeshi la Kiislamu walitangulia kufika kwenye chemchem, nao wakanywa maji yote yaliyokuwa yamekusanyika shimoni mwa chemchem ile. Mtume s.a.w. alipofika pamoja na masahaba zake maji yalikuwa yananyinyirika kidogo kidogo. Mtume s.a.w. akakaa karibu na chemchem ile na akachukua maji yake kidogo mkononi mwake, naye akamwomba Mwenyezi Mungu ayabariki maji ya chemchem ili yaongezeke na kuwatosha masahaba wote. Baada ya kuomba Mtume s.a.w. akapiga maji yale ya mkononi mwake juu ya chemchem, mara chemchem ikapanuka na maji yakaanza kububujika kwa kasi. Basi masahaba wale wakanywa na, wakawanywesha wanyama wao vile vile. Soma Tarikhe Islam, iliyotungwa na A.A. Shauq, ukurasa 270.

(5)CHAKULA KIDOGO CHASHIBISHA WATU 1,000
KATIKA mwaka wa 5 baada ya Mtume s.a.w. kuhamia Madina kulitokea vita kali sana kati ya Waislamu na makafiri wa Makka. Wajuao historia ya Kiislamu wanaelewa vizuri sana kwamba makafiri wa Makka walikuja pamoja na silaha zao nyingi mno za vita, na idadi ya wanajeshi wao katika vita hii ilikuwa karibu 24,000. Lakini upande wa Waislamu wanajeshi walikuwa wachache sana, nao vile vile hawakuwa na silaha nyingi na nzuri. Vita hii inajulikana katika historia kwa jina la vita ya Ahzaab au vita ya Khandak. Vita hii yaitwa vita ya Khandak kwa sababu kwa kuwazuia makafiri wasipate kuingia mjini Madina, Waislamu walichimba handaki refu sana mipakani mwa Madina. Kuchimba handaki refu sana kwa kuziba njia yote ya kuingilia mjini ni kazi kubwa na ngumu. Waislamu walifululiza siku tatu kuchimba handaki hilo refu sana. Wakati huo Waislamu walikuwa hawana chakula kingi na kile kidogo walichokuwa nacho kikaisha upesi mpaka hawakubakiwa na cho chote cha kula. Ilikuwa dhiki kubwa kabisa kwa Waislamu, mpaka hata Mtume s.a.w. mwenyewe alipata taabu sana ya njaa. Masahaba wengine nao wakaendelea kuchimba handaki bila kula cho chote, mpaka hali yao ikawa mbaya kwa sababu ya njaa. Masahaba pamoja na Mtume s.a.w. walijifunga mawe matumboni kwa kupunguza ile taabu ya njaa. Katika hali hii mbaya Bwana Jabiri bin Abdallah r.a., ambaye vile vile alikuwa pamoja na wanajeshi wengine, alikumbuka kwamba yeye anacho chakula kidogo nyumbani. Basi akafikiri aende nyumbani kwa kutafuta chakula kidogo kwa ajili ya Mtume s.a.w. Bwana Jabir r.a. mwenyewe anasimulia ya kwamba: 1 “Baada ya kumwomba Mtume s.a.w. ruhusa nikaenda nyumbani na nikamwuliza mke wangu, je, kuna cho chote nyumbani, kwa maana nimeona hata Mtume s.a.w. yuko taabani kwa sababu ya njaa. Mke wangu akasema ninazo shayiri kidogo na mbuzi mmoja. Basi mimi nikachinja mbuzi na kusaga mbegu za shayiri, na nikamwambia mke wangu apike chakula, nami ninamkaribisha Mtume s.a.w. kwenye chakula. Hapo mke wangu aliniambia, tazama, usiwaite watu wengi, maana hatuna chakula kingi; lakini umwombe Mtume s.a.w. alete ndugu wachache tu pamoja naye.” Bwana Jabir r.a anaendelea kusimulia mwenyewe ya kwamba mimi nikaenda taratibu nikamwambia Mtume s.a.w., “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ninacho chakula kidogo nyumbani, basi nakuomba we we pamoja na masahaba wengine wachache twende tukale pamoja”. Bwana Jabir r.a. anasema kuwa yeye alimwambia kwa sauti ndogo sana ili wengine wasipate kusikia, kwani chakula kilikuwa hakiwezi kuwatosha watu wengi. Mtume s.a.w. akamwuliza unacho chakula kiasi gani nyumbani, naye akaambiwa. Hapo Mtume s.a.w. akasema chakula hicho ni kingi sana! Kisha Mtume s.a.w. akatazama kuko na huko na akaanza kutangaza kwa sauti ya juu, “Enyi Maansar na Muhajirina, bwana Jabir ametukaribisha kwenye chakula, twende, basi, kwenye karamu hiyo!” Mara moja masahaba wapatao 1,000 pamoja na Mtume s.a.w. wakaelekea nyumbani kwa bwana Jabir r.a. Bwana Jabir alihangaika sana hapo, akifikiri, lo, itakuwaje leo, hatuna chakula kingi nyumbani! Mtume s.a.w. alimwambia bwana Jabir kwamba aende nyumbani haraka na kumwambia mkewe asiondoe chungu jikoni wala asianze kupika mikate. Bwana Jabir r.a. mara moja alikimbilia nyumbani na kumwambia mkewe habari yale pamoja na agizo la Mtume s.a.w. kwamba asiondoe chungu toka kwenye jiko wala asianze kupika mikate. 2 Mama huyo alihangaika sana kwa kufikiri watu elfu moja watawezaje kushiba ilhali chakula ni kidogo sana nyumbani kwetu! Mtume s.a.w. alipofika nyumbani mwa bwana Jabir r.a. akabariki unga na kitoweo kwa maombi yake, kisha akasema mikate ianze kupikwa. Na yeye akaanza kupeleka chakula mbele ya wageni. Bwana Jabir r.a. anasimulia kwamba. “Ninaapa kwa yule ambaye uhai wangu umo mkononi mwake kwamba watu wale wakala mpaka wakashiba, na hali chungu chetu bado kilikuwa kinachemka juu jikoni na unga ulisalia, na mikate ilikuwa inapikwa.” Kisa hiki chote kimesimuliwa na Bwana Jabir r.a. mwenyewe katika Bukhari, mlango wa Ghazwatul-Ahzaab.

(6) MWUJIZA WA KUONGEZEKA MAJI
Safari nyingine tena ikatukia hivyo hivyo. Wakati wa sala uliwadia na jamaa ambao nyumba zao zilikuwa karibu na msikiti wakainuka kwenda nyumbani kutawadha, lakini wengine ambao nyumba zao hazikuwa karibu wakabaki pale pale. Mtume s.a.w. akaletewa maji kidogo ili naye pia aweze kutawadha. Mtume s.a.w. akataka kuingiza mkono wake chomboni mwa maji, lakini kwa kuwa chombo chenyewe kilikuwa si kipana cha kutosha, basi mkono haukuingia ndani. Hapo mtume s.a.w. akakunja vidole vyake vizuri na akaingiza mkono ndani. Basi kwa mwujiza wa Mtume s.a.w. watu wote waliokuwa wamebaki wakatawadha kwa maji hayo kidogo sana. Tukio hilo alilishuhudia bwana Anas r.a. mwenyewe, na alipoulizwa walikuwa ni wangapi waliotawadha, akasema 80. (Bukhari).

(7) MWUJIZA WA MAJI YA BARAKA HUDAIBIYYA
Hadhrat Jabir bin Abdillahi r.a. anasimulia kuwa siku tulipokuwa kule Hudaibiyya watu walisikia kiu ya ajabu. Mtume s.a.w. alikuwa na chombo cha ngozi ndani yake mna maji kidogo; naye akatawadha kwa maji hayo. Watu walipoona wakafika haraka haraka kwa Mtume s.a.w. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akauliza mna nini? Wakasema hatuna maji kwa kutawadha wala kunywa isipokuwa kiasi hiki tu kilicho mbele yako. Mtume s.a.w. aliposikia hayo akatia mkono wake ndani ya chombo hicho cha ngozi, basi maji yakaanza kububujika vidoleni mwake mfano wa chemchem. Basi sote tukatawadha na kunywa Bwana Jabir r.a. alipoulizwa kuwa hao watu walikuwa wangapi kwa jumla, akasema tulikuwa 1,500, lakini hata kama tungelikuwa laki moja, maji yangetosha sana (Bukhari).

(8) MWUJlZA KISIMANI
Huu nao ulitukia huko Hudaibiyya. Hadhrat Baraa anasimulia ushuhuda wake ya kuwa Mtume s.a.w. alipofika Hudaibiyya pamoja na masahaba zake karibu 1,400, tulitoa maji mengi sana katika kisima cha Hudaibiyya mpaka kisima kikakauka. Basi ikawa taabu kupata maji tena. Hapo Mtume s.a.w. akafika kisimani na akaagiza maji kidogo. Kaletewa. Akasukutua kidogo na kutema maji hayo kisimani. Tukasubiri kidogo kisha tukapata maji mengi mno tukashiba sisi na wanyama wetu vile vile. (Bukhari).

(9) MAJI YAKABUBUJIKA VIDOLENI MWA MTUME
Amesimulia Hadhrat Abdullah ushuhuda wake ya kuwa safari moja Mtume s.a.w. pamoja na masahaba zake walikwenda safari. Njiani maji yakabaki kidogo sana; basi Mtume s.a.w. akaagiza maji yale yaliyokuwa yamebaki, nayo yalikuwa kidogo mno. Mtume s.a.w. akaingiza mkono wake katika chombo cha maji kisha akasema, “Njooni mapate maji ya baraka, na baraka hiyo imetoka kwa Mwenyezi Mungu” Msimuliaji anasema, “Mimi nilishuhudia maji yakibubujika baina ya vidole vya Mtume s.a.w.” (Bhakari).

(10) TENDE NAZO ZAONGEZEKA
Hadhrat Jabir r.a. anasimulia kisa chake cha ajabu. Anasema kuwa baba yake alipofariki alikuwa anadaiwa fedha. Basi, yeye Bwana Jabir akamwendea Mtume s.a.w. na kumpasha habari ya deni la baba yake, na akasema, “Kwa kweli sina mali isipokuwa ninachopata toka mitende ya baba yangu; na kiasi hicho si kikubwa mpaka niweze kumaliza deni na nibakiwe na cho chote 9 kwa chakula changu kwa miaka hii ya njaa. Bwana Jabir r.a. akaendelea, “Kwa hivyo, basi, ufuatane nami ili wanaodai wasinitukane. Basi, Mtume s.a.w. akaenda na akazunguka pembezoni mwa rundo la tende na akaomba dua; akazunguka tena, na kisha akakaa karibu na rundo na akasema, “Toeni”. Basi akawapa wote waliodai sawasawa na hata hivyo tende zilisalia kiasi kile kile alichowapa hao. (Bukhari).

(11) MBUZl WA UMMI MA’BAD
Mtume s.a.w. aliposumbuliwa sana pamoja na wafuasi wake kule Makka, Mwenyezi Mungu alimwamuru kuhamia Madina. Katika safari yake hii ya kuhamia Madina njiani alilazimika kujificha ndani ya pango la Thaur ambamo alionyesha mwujiza utakaoelezwa mbele. Hapa naeleza mwujiza wake mwingine. Mtume s.a.w. alipoondoka toka ndani ya Pango la Thaur kuelekea Madina, njiani alipita karibu na banda la Bi Ummi Ma'bad. Mama huyu alitokana na kabila la Khuza'ah, naye alijulikana sana kwa sababu ya ukarimu wake. Kwa kuwa kibanda chake kilikuwa njiani, wasafiri walikuwa wanapumzika kwake, naye alikuwa akiwakaribisha na kuwapatia maji ya kunywa. Mtume s.a.w. alipofika kwenye kibanda hicho, akamwuliza, “Je, mama, unacho cho chote?” Mama akajibu, “Kama, ningekuwa na kitu cho chote wakati huu ningekupeni bila ya wewe kuuliza” Mtume s.a.w. akaona katika pembe ya nyumba kuna mbuzi mmoja amesimama. “Kwa nini mbuzi huyu amesimama hapa”, Mtume s.a.w akauliza. Bi Ummi Ma’bad akajibu kwamba mbuzi huyu tangu siku nyingi hali yake ni hivyo hivyo tu. Hakukua vizuri, ni mnyonge sana na mdhaifu, hawezi kwenda kamwe na mbuzi wengine malishoni. Mtume s.a.w. akauliza, “Je, unaturuhusu tukamue maziwa yake?” Mama akasema kuwa 10 mbuzi huyu hana cho chote; kama unaweza basi unayo ruhusa Mtume s.a.w. akamwomba mama huyu chombo, na kisha kwa kusema Bismillahi akaanza kukamua maziwa. Kwa mwujiza wa Mtume s.a.w. maziwa yakaanza kutoka ndani ya chuchu za mbuzi huyo sana sana mpaka chombo kikajaa. Maziwa hayo yaliweza kuwatosha watu kama 9 hivi. Mtume s.a.w. na wengineo wakanywa mpaka wakashiba. Akakamua tena maziwa ambayo akayaacha kwa mama huyo. Kisha Mtume s.a.w. pamoja na masahaba zake wakaondoka. Baada ya kitambo kidogo mumewe Ummi Ma'bad, aliyekuwa hayupo kibandani, aliporudi akaona chombo kimejaa maziwa. Akashtuka na kushangaa, na akauliza maziwa haya yametoka wapi? Bi Ummi Ma'bad akamjibu kwamba alifika kwetu mzee mmoja mtawa sana na maziwa hayo ni matokeo ya baraka yake. Mumewe akasema “Inaonekana huyo ndiye sahibu wa Makuraishi ambaye namtafuta toka zamani; hebu nieleze sura yake ilikuwa namna gani?” Bi Ummi Ma'bad akaeleza sura ya Mtume s.a.w. na kadhalika. Hapo mumewe alisema bila shaka huyu ndiye sahibu wa Makuraish, nina shauku sana ya kumwona, nami nitajaribu kuonana naye. Tazameni, Mungu akusaidieni, ni mkubwa ulioje mwujiza huu wa Mtume Muhammad Mtukufu s.a.w. Soma Tarikhe Islam iliyoandikwa na A. R. Shauq, ukurasa wa 134, jalada la kwanza.

(12) MAJI YAONGEZEKA
Hadhrat Anas bin Malik r.a. anasimulia ya kuwa safari moja Mtume Muhammad s.a.w. alipokuwa katika mahali paitwapo Zaura, akaletewa chombo kidogo cha maji kwa kutawadha kwa sala. Maji hayo yalikuwa kidogo sana ilhali watu karibu 300 11 walitaka kutawadha. Basi, Mtume s.a.w. akaingiza mkono wake mtukufu wenye baraka chomboni, mara maji yakaanza kububujika vidoleni mwake mpaka jamaa hao wote wapatao 300 wakatawadha wala hakubaki hata mmoja. (Bukhari).

(13) CHAKULA KINAONGEZEKA
Imesimuliwa na Bwana Anas r.a. aliyekuwa Sahaba wa Mtume s.a.w. ya kuwa safari moja Bwana Abu Talha r.a. alihisi kuwa Mtume s.a.w. anasikia njaa; yeye alifanya haraka kufika nyumbani kwake na akamwuliza mkewe, Ummi Sulaim, “Je, kuna cho chote cha kula? Kwani nimetambua kwamba Mtume s.a.w. ana njaa” Mama huyu akajibu ndiyo ninayo mikate michache ya unga wa shayiri kisha akachukua hiyo mikate na kumpa Bwana Anas ra kwa kufunika ndani ya kitambaa ili ampelekee Mtume s.a.w. Bwana Anas akachukua mikate na akaondoka kwa kumpelekea Mtume s.a.w. Wakati huo Mtume s.a.w. alikuwa amekaa msikitini pamoja na baadhi ya watu wengine. Bwana Anas r.a. aliingia msikitini na akasimama karibu na Mtume s.a.w. Bwana Abu Talha amekutuma?” akasema Mtume s.a.w “Ndiyo”, kaitika Bwana Anas r.a. Mtume s.a.w. akasema, “Umeleta chakula?” Bwana Anas r.a. akajibu ndiyo, yeye amekupelekea chakula kidogo. Mtume s.a.w akisikia jibu hilo akatangaza, inukeni, twende nyumbani kwa Bwana Abu Talha” Basi ikawa hivi ya kwamba wote waliokuwa pale wakafuatana na Mtume s.a.w. wakielekea nyumbani kwa Bwana Abu Talha r.a. Bwana Anas r.a. anasimulia kuwa nilipoona hali hii nikafanya haraka kuwatangulia jamaa hao ili nimpashe habari bwana Abu Talha r.a. kuwa Mtume s.a.w. pamoja na watu wengi sana wanakuja kwako. Bwana Abu Talha r.a. alipojua habari hii akahangaika na kumwambia mkewe kwamba Mtume s.a.w. pamoja na watu wengi sana anakuja 12 nyumbani kwetu, nasi hatuna chakula kingi cha kuwatosha hao wote. Lakini mkewe akasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi”. Basi, bwana Abu Talha r.a. akatoka nyumbani kwa kumlaki Mtume s.a.w. Mtume s.a.w. na bwana Abu Talha r.a. wakaingia nyumbani pamoja, Baada ya kuingia ndani Mtume s.a,w. alimwambia Bi Ummi Sulaim amletee chakula chote alicho nacho nyumbani. Akaletewa mikate michache. Mtume s.a.w. akaamrisha kuikata mikate hiyo vipande vipande, tena akatia samli kidogo ndani yake na kuchanganya. Kisha akabariki chakula hicho kwa maombi, na akasema watu kumi waingie ndani. Wakapewa idhini watu kumi; wakaingia nyumbani nao wakala mpaka wakashiba. Kisha Mtume s.a.w. aksema kumi wengine waingie, nao wakaingia vile vile na wakashiba vizuri na wakatoka. Kila baada ya kushiba watu kumi na kutoka nje, Mtume s.a.w. akasema waingie wengine kumi; na kwa njia hiyo watu karibu 80 wakashiba. Na mwishowe akala Mtume s.a.w. na watu wa nyumbani. Wote wakashiba na chakula kilibaki vile vile. Mwujiza huu umeelezwa ndani ya kitabu kitukufu kinachojulikana sana katika Waislamu kwa jina la Sahihi Bukhari. Utakuta maelezo hayo katika mlango wa ‘AlaamaatunNubuwwat Fil-islam (Kitabul-Manaakib).

(14) MWUJIZA MWINGINE MKUBWA WA MAJI
Hadhrat 'Imran bin Huswain ametoa ushuhuda wake ya kuwa siku moja Mtume s.a.w. alipokuwa anasafiri pamoja na masahaba zake, njiani wakasikia sana kiu. Hawakuwa na maji, kwa hiyo wakaendelea na safari yao katika hali hiyo hiyo ya kiu sana. Njiani wakamkuta mwanamke mmoja aliyekuwa amebeba vyombo viwili. Masahaba wakamwuliza je, kuna maji hapa 13 karibu? Akajibu, hapana. Wakauliza tena ya kuwa wataweza kupata maji umbali gani toka hapo. Akajibu mama huyu ya kuwa ni mwendo wa siku moja, usiku na mchana. Masahaba wakampeleka bibi huyo kwa Mtume s.a.w. Baada ya kuzungumza naye, Mtume s.a.w. akabariki ukingo wa vyombo vile viwili, na kisha akawaambia masahaba wanywe maji toka humo. Mara moja masahaba wakaanza kunywa na kuchukua maji katika vyombo vyao. Masahaba hao walikuwa 40 kwa jumla, wote wakanywa mpaka wakashiba sana, bali wakajaza viriba vyao vyote, wala hakikubaki hata kimoja kisichojazwa maji. Kisha Mtume s.a.w. akasema, “Leteni cho chote mlicho nacho”. Basi vikakusanywa vipande vya vyakula na tende, na akapewa yule mama. Mama huyu aliposhuhudia mwujiza huu wa Mtume s.a.w. akaathirika sana moyoni; na aliporudi kwao akawaambia watu wa kabila lake ya kuwa, “Nimeonana na mtu mmoja ambaye ni mchawi mkubwa kabisa, la sivyo ni Nabii wa Mwenyezi Mungu kama watu wake wanavyomfikiria.” Basi, Mungu akawaongoza watu wake kwa njia ya mama yule. Mama huyu pia akasilimu na watu wale wa sehemu yake vile vile wakaingia katika Uislamu. Mwujiza huu umeandikwa katika Bukhari mlango wa ‘Alaamaatun-Nubuwwat Fil-Islam.

(15) SAMLI YA BARAKA
Sahaba mmoja wa Mtume s.a.w. bwana Jabir r.a. ametoa ushuhuda wake ya kuwa Bi Ummi Malik alikuwa anampelekea Mtume s.a.w. zawadi katika kiriba kidogo cha kuwekea samli. Kiriba hicho kidogo kikawa kilibarikiwa ajabu. Kila mara watoto wa bibi huyu walipotaka kitoweo, basi, Bibi huyu alipokuwa anaona hamna kitu nyumbani, yeye alikuwa anaelekea kile kiriba na kila mara akakuta humo samli imo. Na hali hii ikaendelea siku zote na samli isiishe. Mpaka siku moja bibi huyo akatoa 14 samli yote kwa kukamua kiriba. Kisha baadaye alipohudhuria mbele ya Mtume s.a.w. Mtume akamwuliza. Je, umekamua kiriba? Kajibu: ndiyo. Hapo Mtume s.a.w akasema. “Kama ungekiacha tu hivi bila kukamua, kingedumu katika hali yake ile ile (ya kutoa samli kila mara).” Ushuhuda huu wa Hadhrat Jabir r.a. tunaukuta umeandikwa ndani ya kitabu mashuhuri cha Muslim, mlango wa Miujiza ya Mtume s.a.w.

(16) SHAYIRI YA KIMWUJIZA
Anasimulia tena bwana Jabir r.a. ya kuwa mtu mmoja alifika kwa Mtume s.a.w. kuomba chakula. Mtume s.a.w. akampa nusu Wasqi (Kilo 80) ya shayiri (mbegu ndogo kuliko ngano). Basi mtu huyu pamoja na mkewe na wageni wawili wakaendelea kutumia siku nyingi shayiri hizo ambazo hazikupungua. Lakini siku moja mtu huyo akazipima, basi zikaisha hapo upesi. Mtu huyo alipofika mara nyingine kwa Mtume s.a.w. Mjumbe wa Mungu akamwambia. “Kama msingelizipima mngekula siku zote kwa kudumu” (Muslim).

(17) MWEZI KUPASUKA
Mtume s.a.w. alipokuwa bado hajahama Makka, makafiri wakamwomba aonyeshe Mwujiza wo wote kama yeye ni mkweli. (Bukhari na Muslim). Hapo Mtume s.a.w; akaashiria upande wa mwezi kwa kidole chake, mara mwezi ukapasuka, ukawa vipande viwili; kisha ukaungana pamoja tena. Mtume s.a.w. alipoonyesha mwujiza huu akasema, “Muwe mashahidi, muwe mashahidi”. (Bukhari na Muslim). Huu ni mwujiza mkubwa ajabu nao umetajwa ndani ya Kurani Tukufu vile vile. Na kama mtu mmoja leo anasema kuwa ni 15 uzushi tu bali mwujiza huu haukuonyeshwa, tunamwuliza kwa nini makafiri walinyamaza walipousoma ndani ya Kurani Tukufu mwujiza huo. Makafiri mara moja wangesema, “Mbona unaandika uwongo ndani ya Kitabu chako kuwa mwezi ulipasuka ilhali hatukushuhudia lo lote?” Lakini hawakusema hivyo; ila walikiri kuwa wameona tukio hili, lakini walisema huu ni uchawi. Na hii ni desturi ya maadui siku zote kuwa wanapoona mwujiza husema ni uchawi, au ni nguvu ya shetani. Yesu pia aliambiwa na maadui zake ya kuwa yeye anaonyesha miujiza kwa nguvu ya Belzabuli. Hapa tunataka kuandika maneno ya Kurani Tukufu jinsi yalivyoeleza tukio hili la mwezi kupasuka: “Saa imekaribia na mwezi umepasuka. Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema; Uchawi unaoendelea! Na walikadhibisha na wakafuata tamaa zao; na kila jambo limewekwa kwa wakati wake. Na kwa yakini zimewafikia baadhi ya habari zenye kukataza, zenye hekima kamili - lakini maonyo kwao hayafai”. (54:2-6). Aya hizi zinaeleza tukio la mwezi kupasuka, na Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa katika mwujiza huo kuna hekima pia. Yaani sio mwujiza tu usio na hekima ndani, bali habari kuu imedokezwa ndani ya mwujiza huu. Habari gani hiyo? Tunajua kuwa mwezi ulikuwa ni alama maalum ya utawala wa Waarabu. Na mwezi kupasuka kulikuwa na maana ya kuwa hivi karibuni utawala wa watu wa Makka utavunjika. Na ilitukia vivyo hivyo. Kwani, baada ya mwujiza huu Mtume s.a.w. alihamia Madina na kisha vita vingi vilipiganwa kati ya Waislamu na Makafiri wa Makka. Na mwishowe Mtume s.a.w. aliingia katika Makka pamoja na watukufu elfu kumi na kuiteka bila kumwaga damu; ndipo utawala wa udhalimu wa Makka ulivunjika kabisa. 16 Kwa hakika mwujiza huu ni mtukufu sana. Kwani, kwanza ni mwujiza binafsi, tena ndani yake habari ya utawala wa Makka kuondolewa imetabiriwa pia. Na Waarabu walijua sana ishara hii. Ndiyo maana walipoona kuwa habari hii imetimia na utawala wa Makka umevunjika, basi karibu wote wakasilimu.

(18) KASHINDWA KUMWUA MTUME
S.A.W. Sasa twaandika namna alivyoshindwa adui mkali wa Mtume s.a.w. kumwua yeye kwa mwujiza wa Mtume s.a.w. Tukio hili lilitukia wakati Mtume s.a.w. alipokuwa anarudi pamoja na masahaba zake toka vita ya Dhatir-Riqaa. Vita hii ilipatikana katika mwaka wa 7 wa Kiislamu. Mtume s.a.w. alitoka nje ya Madina pamoja na jeshi la Kiislamu lisilopungua wanavita 700. Maadui walichochea kwanza lakini walipoona jeshi la Kiislamu limekwisha jitokeza kupambana nao wakatishika na kuacha nia ya kupigana na Waislamu; kwa hiyo na Waislam vile vile wakawaacha, na vita haikupiganwa. Basi Mtume s.a.w. akarudi Madina pamwe na masahaba zake. Walipokuwa wakirudi, njiani wakapita katika bonde moja lenye miti mingi iliyosongamana. Kwa kuwa jeshi lilikuwa limechoka na safari ndefu, Mtume s.a.w. akaamua kupumzika pale. Masahaba wakatawanyika huko na huko kwa kupumzika chini ya vivuli vya miti mbalimbali. Mtume s.a.w. naye akalala chini ya mti mmoja, na upanga wake akauning’iniza mtini. Wote walipolala usingizi mara akaja mushirikina mmoja aliyekuwa adui. Adui huyo akachukua upanga wa Mtume s.a.w. toka mtini na kumwamsha Mtume s.a.w. Alipoamka Mtume s.a.w. akamwona adui amesimama, upanga mkononi. Adui huyu akamwambia Mtume s.a.w.: “Je, huniogopi?” Mtume s.a.w. akajibu kwa utulivu sana “HAPANA”. Kisha mushirikina huyu 17 akasema, “Nani anaweza kukuokoa wakati huu mkononi mwangu?” “MUNGU” akasema Mtume Muhammad s.a.w. Aliposikia tu adui huyu neno “MUNGU” midomoni mwa Mtume s.a.w. upanga ukaanguka mkononi mwake. Mtume s.a.w, akauchukua upanga na kamwuliza, “Na ni nani, sasa, anayeweza kukuokoa mkononi mwangu?” Bedui huyo mushirikina akahangaika sana na akajibu. “Wewe u mwema, nifanyie hisani.” Mtume s.a.w. akamwacha, naye akaenda zake, na akawaambia wenziwe kuwa nimefika kwenu toka kwa mtu ambaye ni mbora kuliko watu wote,” Tukio hilo limesimuliwa na Bwana Jabir r.a. ambaye mwenyewe alihudhuria katika vita hiyo pamoja na Mtume s.a.w. Katika simulizi lake anasema kuwa tulipolala sote, mara tukasikia Mtume s.a.w. anatuita. Tulipofika tukaona bedui mmoja amesimama akitetemeka mbele ya Mtume wa Mungu s.a.w. Na kisha Mtume s.a.w. alitueleza yote yaliyotukia. Ukitaka ushahidi wa maandishi, fungua mlango wa Ghazwatu Dhatir-Riqaa katika kitabu mashuhuri cha Bukhari.

(19) ABU JAHLI KASHUHUDIA MWUJIZA WA NGAMIA MKALI
Tunajua kuwa Abu Jahli ambaye alijulikana zaidi katika uhai wake kwa lakabu yake Abul-Hakam, alikuwa ni adui mkali wa mwisho wa Mtume s.a.w. Yeye alijaribu kwa kila njia kumwudhi Mtume s.a.w. Popote alipokuwa anamwona Mtume s.a.w. yu peke yake, mjeuri huyo alikuwa anamtukana na kumfedhehesha. Safari moja, bwana mmoja, jina lake Irasha, alifika mjini Makka kwa kuuza ngamia zake. Abu Jahli akanunua kwake ngamia kadhaa, lakini baada ya kukabidhiwa ngamia akakataa kulipa bei ya ngamia hao. Bwana Irasha alijaribu mno kumsihi na kumbembeleza, lakini bure. Abu Jahli alikuwa ni mtu mkubwa 18 na kiongozi mashuhuri naye alikuwa ni mwenye nguvu sana, kwa hiyo maskini bwana Irasha akashindwa mbele yake, ingawaje aling’ang’ania sana kwa siku chache. Baada ya kushindwa, bwana Irasha akafika kwa baadhi ya wakuu wa Makka waliokuwa wamekutana karibu na Ka’aba wakizungumza mambo mbalimbali, na akawaeleza shida yake na kuwaomba wamsaidie kumpatia haki yake. Hao wakuu walijua kuwa hawawezi kufanya lolote mbele ya Abu Jahli, lakini mara moja wakapata wazo la kumfedhehesha Mtume s.a.w. Wakamwambia bwana huyo ambaye alikuwa ni mgeni tu katika Makka, ya kuwa sisi, bwana, kwa kweli hatuwezi kukusaidia katika shida yako hiyo, isipokuwa tunakuelekeza kwa mtu mmoja jina lake Muhammad - yeye bila shaka ataweza kukusaidia mpaka shida yako ikaondoka. Hao wakuu walikuwa na shabaha kuwa Mtume s.a.w. ataogopa kumwendea Abu Jahli basi atafedheheka mbele ya bwana Irasha. Na kama atakwenda, basi Abu Jahli atapata nafasi nzuri sana ya kumtukana Mtume s.a.w. na kumfedhehesha. Bwana Irasha hakujua mpango wa hao wakuu, akaelekea nyumbani kwa Mtume s.a.w. Wakuu hao wahuni wakamtuma mtu mmoja miongoni mwao afuatane naye na kushuhudia litukialo. Bwana Irasha alifika moja kwa moja nyumbani kwa Mtume s.a.w. na kumweleza shida yake. Mtume Muhammad s.a.w. bila kujali lolote akafuatana naye mpaka nyumbani kwa Abu Jahli. Akapiga hodi, Abu Jahli alipotoka nje, Mtume s.a.w. akamwambia: Ee bwana, kwa nini unamnyima huyu maskini haki yake? Tafadhali umpe fedha zote anazokudai. Abu Jahli akaitika mara moja kwa kusema, “Ee Muhammad, subiri kidogo; namletea hela zake zote sasa hivi”. Kisha akaingia ndani na kuleta fedha zote na kumkabidhi Bwana Irasha! Bwana huyo akamtolea shukrani nyingi Mtume s.a.w. kwa msaada wake wa ajabu na akaondoka. Lakini kabla hajaondoka Makka aliamua kwanza 19 awaendee wale wakuu waliomwongoza kwa Mtume s.a.w. ili awashukuru. Akawaendea na kuwatolea shukrani na ahsante nyingi. Hao wakuu walishtuka mno kwa kujua kwamba Abu Jahli amekubali maneno ya Mtume s.a.w. Bwana Irasha alipoondoka, wakuu hao walimwuliza yule mtu aliyetumwa kwa kuchungulia linalotukia, je, bwana, kweli Abu Jahli hakumtukana na kumfedhehesha Muhammad? Mtu huyo alisema nimeona leo jambo la ajabu kabisa. Muhammad alipomwambia Abul-Hakam (Abu Jahli) amrudishie bwana Irasha fedha zake, wakati huo hali ya Abul-Hakam ilikuwa ya kushitusha ajabu. Akaonekana kana kwamba ni mwili mtupu bila roho ndani yake. Na Muhammad alipomwambia tu atoe fedha za Bwana huyo, AbulHakam kaingia ndani na akaleta haraka hela zote. Punde si punde, Abu Jahli vile vile akafika penye mkutano wa hao wakuu. Wote wakamwuliza, “Ee Abul-Hakam imekuwaje mbona ulimwogopa Muhammad kiasi hiki?” Abu Jahli akajibu “Wallahi nilipomwona Muhammad mlangoni pangu, ikawa niliona ngamia mmoja mkali wa kutisha amesimama pamoja naye; na ikaonekana kwamba kama nikikataa tu mwito wa Muhammad, ngamia huyo atanishambulia na kunirarua.” Tazameni, ni wenye utukufu mkubwa ulioje huu mwujiza wa Mtume Muhammad s.a.w.! Watu wengine hawakumwona yule ngamia mkali, isipokuwa ni Abu Jahli tu afiyemshuhudia, mpaka akaitika haraka mwito wa Mtume s.a.w. na kumrudishia Bwana Irasha fedha zake. Mwujiza huu umeelezwa ndani ya kitabu mashuhuri cha Sirat Ibni Hishaam na vitabu vingine vya Historia ya Kiislamu.

(20) KAPONYA KIMWUJIZA
Mtume Muhammad s.a.w. alipohama Makka kuelekea Madina, Seyidna Abu Bakr r.a. pia akafuatana naye. Makafiri wa Makka walikuwa na mpango wa kumwua Mtume s.a.w. usiku huo alioondoka Makka. Asubuhi makafiri walipojua kuwa Mtume s.a.w. amekwisha salimika mikononi mwao kwa sababu ya kuondoka Makka, walitangaza kuwa mtu ye yote atakayemleta Mtume s.a.w. Makka akiwa hai au amekwisha uawa, mtu huyo atapewa zawadi kubwa ya ngamia 100. Kwa hiyo watu kadha wa Makka wakajaribu kumtafuta Mtume s.a.w. ili wakapate zawadi hiyo kubwa. Baadhi ya makafiri walifika karibu sana na Mtume s.a.w. wakimtafuta. Kwa hiyo Mtume s.a.w. pamoja na Seyidna Abu Bakr r.a. wakajificha ndani ya pango moja liitwalo pango la Thaur katika njia ya kwenda Madina. Kabla ya Mtume s.a.w. kuingia pangoni, Seyidna Abu Bakr r.a. akaingia ndani na akasafisha vizuri na akaziba matundu matundu kwa vitambaa alivyochana shuka lake; kisha akamwomba Mtume s.a.w. aingie ndani. Nafasi ilikuwa ndogo sana mle ndani. Seyidna Abu Bakr r.a. alikaa, na Mtume s.a.w. akalala kidogo kwa kupumzika akiweka kichwa chake juu ya paja la Seyidna Abu Bakr r.a. Katika hali hii mara Seyidna Abu Bakr r.a. aliona kumbe kuna tundu moja lingine ambalo halikuzibwa. Seyidna Abu Bakr r.a. hakupenda kuinuka kwa kuziba tundu lile isije Mtume s.a.w. akapata taabu; bali akaliziba kwa kuweka mkono wake juu ya tundu. Kumbe mle ndani mlikuwa na mdudu fulani mkali, akamwuma Seyidna Abu Bakr r.a. Seyidna Abu Bakr akasikia uchungu sana kwa sababu ya sumu ya mdudu, lakini hata hivyo hakuondoa mkono wake toka tundu hilo kwa hofu, isije mdudu huyo akatoka nje na kumwuma Mtume s.a.w. Akavumilia maumivu hayo yote makali 21 na machungu. Lakini kwa sababu ya maumivu machozi yake yakamtoka na kuanguka usoni mwa Mtume s.a.w. Mara Mtume s.a.w. akaamka na kumwuliza, “Kuna nini Bwana Abu Bakr, mbona machozi yanakutoka?” Seyidna Abu Bakr r.a. akamweleza habari yote. Mtume s.a.w. akamwambia nionyeshe mkono wako. Mtume s.a.w. akatia mate yake ile sehemu ya maumivu mara Seyidna Abu Bakr r.a. akapona.

(21) KAFIRI ALIONA MWUJIZA
Baada ya kukaa katika pango la Thaur kwa siku tatu Mtume s.a.w. pamoja na Seyidna Abu Bakr r.a. wakaondoka humo wakaelekea Madina. Maadui walikuwa bado wanamtafuta. Baada ya kutembea kwa siku moja Seyidna Abu Bakr r.a. akaona kwamba nyuma yao kafiri mmoja aliyepanda farasi na mkuki mkononi alikuwa anawafuata kwa kasi. Seyidna Abu Bakr r.a. akahangaika sana lakini Mtume s.a.w. akamtuliza. Kafiri huyu alikuwa ni Bwana Suraqa bin Maliki. Yeye mwenyewe anasimulia kisa chake hivi:- “Mtume s.a.w. alipoondoka Makka, makafiri walitangaza kuwa mtu ye yote atakayemkamata Mtume akiwa hai au maiti, huyo mtu atapewa zawadi kadha wa kadha. Siku moja mimi nilipokuwa nimekaa pamoja na watu wa kabila langu Bani Mudlaj, tulifikiwa na mtu mmoja miongoni mwa Makuraish. Mtu huyo aliniambia kuwa yeye amewaona baadhi ya watu upande wa pwani, naye akadhani kuwa hao ni Mtume s.a.w. na watu wake. Mimi nilitambua mara moja kwamba bila shaka hao ndio watu wa Muhammad. Lakini kwa sababu ya tamaa ya kujinyakulia zawadi, nilitaka kuficha habari hiyo, nami nikasema hao sio watu wa Muhammad, bali ni watu fulani ambao hivi karibuni wamekwenda upande ule. 22 “Lakini, mimi mara moja nikafika nyumbani nikachukua mkuki, nikapanda farasi, na huku nikijificha ficha, nikaelekea kwa haraka upande wa hao watu ili nipate kumkamata Mtume s.a.w.” “Nilipofika karibu na Mtume s.a.w. farasi wangu alijikwaa na nikaanguka chini. Lakini nikainuka mara moja, nikapiga mshale sawa na desturi ya Waarabu kwa kujua kwamba je, nijaribu tena kumfuata Mtume s.a.w. au nisijaribu. Jibu lilikuwa “hapana”. Lakini hata hivyo sikujali hilo, bali nikampanda farasi tena na nikamfuata Mtume s.a.w. kwa sababu ya uadui na tamaa ya kupata zawadi. Safari hii nikafika karibu sana na Mtume s.a.w. hata nikasikia sauti ya Mtume s.a.w. akisoma aya za Kurani Tukufu. Niliona kwamba Mtume s.a.w. hata mara moja hakutazama nyuma bali aliendelea kutembea kwa utulivu; lakini Bwana Abu Bakr r.a. kwa sababu ya hofu juu ya Mtume s.a.w. alikuwa anatazama nyuma mara kwa mara. “Mimi nilipofika karibu zaidi na Mtume s.a.w. mara farasi wangu akajikwaa tena na safari hii miguu yake ilididimia sana katika mchanga, nami nikaanguka tena chini toka mgongoni mwa farasi. Niliinuka na nikamkuta farasi wangu kwamba miguu yake imedidimia sana mchangani mpaka farasi akashindwa kuing’oa. Akajaribu sana mpaka akaweza kuing’oa miguu yake. Na kwa sababu ya kujaribu kwake sana kung’oa miguu yake kila mahala pembezoni mwangu yakaenea mavumbi. Wakati huo tena nikapiga mshale kwa kujua niendelee na nia yangu au niiache. Jibu lilikuwa lile lile kama lilivyokuwa mara ya kwanza; yaani niache nia ya kumkamata Mtume s.a.w. “Hapo nikaacha nia yangu, na nikamwita Mtume s.a.w. na watu wake kwa ajili ya suluhu, nao wakasimama.” (Wakati huo pamoja na Mtume s.w.a. na Seyidna Abu Bakr r.a. kulikuwa na Bwana Amer bin Fahira r.a. vile vile ambaye alikuwa ni mtumishi wa Seyidna Abu Bakr r.a. Yeye kila siku alikuwa anawaletea Mtume s.a.w. na Seyidna Abu Bakr r.a. maziwa ya mbuzi katika pango la Thaur kwa 23 kujificha ficha na maadui. Baada ya Mtume s.a.w. kuondoka pango la Thaur, Bwana Amer bin Fahira r.a. vile vile akafuatana naye. Kwa hiyo hao walikuwa ni watu watatu: Yaani, Mtume s.a.w. Seyidna Abu bakr r.a. na bwana Amer bin Fahira). Bwana Suraqa anaendelea kusimulia kisa chake, “Nilifika kwa Mtume s.a.w. na watu wake nikimpanda farasi wangu. Nilielewa kwa sababu ya hayo yote niliyopata kwamba mtu huyu bila shaka atapata ushindi siku moja. Kwa hiyo nikamweleza Mtume s.a.w. habari yote ya nia yangu na kwamba sasa ninaacha nia yangu ile na ninarudi Makka. Nikampa Mtume s.a.w. matumizi kidogo ya safari lakini hakukubali, isipokuwa alisema kuwa nisimwambie mtu ye yote habari ya safari yake.” Kwa kuwa nilikuwa na yakini kwamba Mtume s.a.w. lazima atashinda siku moja, basi nikamwomba aniandikie cheti cha amani. Yaani aniandikie kwamba katika siku za ushindi wake nitapewa amani. Hapo Mtume s.a.w. akamwambia Bwana Amer bin Fahira aniandikie, naye akaniandikia cheti nilichohitaji. “Nilipotaka kurudi, Mtume s.a.w. akasema, “Itakuwaje hali yako utakapovishwa bangili za Mfalme Kisra mikononi mwako! “Nikasema, ‘Bangili za Mfalme Kisra bin Hurmuz?’ Mtume s.a.w. akasema ndiyo.” Kisa hicho chote kimeelezwa na Bwana Suraqa bin Malik mwenyewe ndani ya Bukhari, mlango wa Al-Hijrat. Huyu adui mkali wa Mtume s.a.w. aliona mwujiza mkubwa sana, na akashindwa kumkamata Mtume s.a.w. Tena siyo hivyo tu bali anaambiwa kuwa siku moja atavishwa bangili za Mfalme wa Iran. Bedui mmoja wa bara Arabu avishwe mikononi mwake bangili za Mfalme Mkubwa sana wa zama zile! Lakini ishara hii ilitimia wakati wa ukhalifa wa Seyidna Umar r.a. ambapo 24 Waislamu walishinda nchi ya Iran, na Mfalme Kisra akashindwa mbele ya Waislamu. Na katika mali ya mateka iliyotekwa kulikuwapo bangili za mfalme Kisra vile vile. Na hizo bangili zikavishwa mikononi mwa bwana Suraqa bin Maliki. Huu ni mwujiza mkubwa wa Mtume s.a.w. Yeye anamwambia Bedui mmoja asiye na heshima yoyote kwamba atavishwa bangili za Mfalme Kisra. Nani anaweza kusema hayo ilhali anakimbia mji wake kwa sababu ya mateso ya watu? Tena nani anaweza kumuambia mwingine kwamba ataweza kuishi mpaka muda kadhaa? Lakini Mtume s.a.w. alimwambia Bwana Suraqa bin Maliki kuwa ataweza kuishi mpaka Waislamu watakapomshinda Mfalme Kisra wa Iran na bangili zake Bwana huyo atavishwa! Na kweli yote hayo yakatimia. Mkubwa ulioje Mwujiza huu!

(22) HABARI YA GHAIBU
Katika vita ya Badr iliyopiganwa kati ya Waislamu na Makafiri wa Makka katika mwaka wa 2 baada ya Mtume s.a.w. kuhamia Madina, Mtume s.a.w. akawaonyesha masahaba zake kwa kuashiria kwa kidole mahali atakapouawa Abu Jahli na mahali Watakapouawa maadui zake Utba na Shaiba na wengineo. Masahaba wa Mtume s.a.w. wanatoa ushahidi wao ya kuwa baada ya vita kwisha tuliona kweli kila adui alikuwa ameuawa pale pale alipoashiria Mtume s.a.w. na tuliona maiti zao. Soma kitabu kinachoitwa Zaadul-Ma’adi, ukurasa wa 85, mlango wa Ghazwa Badr. Sasa, ni nani awezaye kusema mapema kuwa adui wake fulani atauawa mahali fulani na adui mwingine mahali fulani n.k.? Je, si mwujiza huu?

(23) SUMU KATIKA CHAKULA
Katika mwaka wa 7 baada ya Mtume s.a.w. kuhamia Madina kulitokea vita baina ya Waislamu na Mayahudi wa Khaibar. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Waislamu wakapata ushindi. Katika vita hiyo Seyidna Ali akamwua adui mkubwa wa Waislamu, jina lake Marhab. Baada ya vita kwisha Mtume s.a.w. akakawia kidogo huko Khaibar. Hapo binti wa nduguye Marhab, yaani bwana Harith, alimwalika Mtume s.a.w. kwenye karamu ya chakula. Jina la binti huyu ni Zainab, Mtume s.a.w. akakubali kula chakula nyumbani kwa bibi huyo naye akaenda akifuatana na Bwana Bishr Bin Baraa kwenye karamu hiyo. Mwanamke huyo aliweka mbele ya wageni wake nyama ya mbuzi; wakaanza kula. Mtume s.a.w. alikuwa bado hajameza lile tonge la kwanza, akaacha kula na akasema, “Mbuzi huyu ambaye hii ndiyo nyama yake ananiambia kuna sumu kwenye nyama.” Mtume s.a.w. akamwuliza mwanamke huyo Myahudi habari ilivyo, naye akakubali kuwa kweli alitia sumu ndani ya chakula, lakini, shabaha yangu ilikuwa kwamba kama wewe ni Mtume mwongo utakufa na dunia itasalimika na upotevu wako,” mwanamke Myahudi akasema. “Na kama u mkweli”, akaendelea kusema, “basi Mungu atakujulisha kwamba kuna sumu kwenye chakula nawe utasalimika.” Mtume s.a.w. aliposikia hayo akamsamehe. Mwujiza huu umeandikwa katika kitabu kinachoitwa ZaadulMa’adi, Jalada la 12 katika mlango wa Vita ya Khaibar.

(24)UMAIR KASILIMU KIMWUJIZA
Katika vita ya Badr viongozi wengi wakubwa wa Makafiri waliuawa, na Waislamu walipata ushindi mkuu juu ya watu wa Makka. Katika vita hiyo Abu Jahli, Utbah, Shaibah na wengineo waliuawa, na makafiri walishindwa vibaya sana mbele ya 26 Waislamu. Kwa hivyo, watu wa Makka walighadhibika sana na wakajaribu kumwua Mtume s.a.w. kwa hila. Siku chache tu baada ya vita ya Badr, Bwana Umair bin Wahb na Safwaan bin Umayyah bin Khalaf walipokuwa wanawalilia waliouawa vitani, mara huyu Safwaan akasema, “Sasa hamna utamu katika maisha baada ya kushindwa vitani”. Umair akatambua mara moja mwenzake aliashiria nini, na akasema, “Mimi niko tayari kujiingiza hatarini, lakini niwazapo juu ya watoto wangu na deni nililo nalo, basi najizuia; waila ni rahisi mno kufika Madina kujificha-ficha na kumwua Muhammad”. Kaongeza kusema: “Tena mimi ninayo sababu vile vile ya kwenda Madina, kwani mtoto wangu amekamatwa vitani, naweza kujisingizia kuwa nimekuja Madina kumwachisha mtoto wangu”. Safwaan akamjibu, “Usijali, Bwana, ile shauri ya deni, mimi nitalipa deni lako; nami nitaangalia watoto wako nyuma yako.” Kwa vyo vyote wakapatana juu ya mpango wa kumwua Mtume s.a.w. Umair akachukua upanga wake uliopakwa sumu na akamwaga mwenzake. Umair akafika Madina moja kwa moja. Alipofika mbele ya Mtume s.a.w. akaulizwa kwa nia gani amekuja Madina. Umair akasema nimekuja kwa kukuomba mtoto wangu aachwe huru. Mtume s.a.w. akauliza, “Lakini kwa nini umechukua upanga?” Umair akajibu, “Panga zimefanya kazi gani katika vita ya Badr!” Mtume s.a.w. akamwuliza tena, “Hapana; niambie waziwazi shabaha yako ya kufika hapa”. Yeye akajibu, “Nimekwisha kuambia mapema jibu la swali lako, sina la kuongeza”. Hapo Mtume s.a.w. akasema, “Je hukupanga mpango wo wote pamoja na Safwaan katika Kaa’ba?” Ehee, Umair akapumbazwa asiweze kutamka lo lote; lakini akathubutu kusema: “Sikufanya mpango wo wote”. Mtume s.a.w. akasema waziwazi. “Je, hukutengeneza mpango wa kuniua? Lakini utambue Mungu hatakuwezesha 27 kuniua!” Hapo bwana Umair akanyamaza akifikiri Muhammad s.a.w. amejuaje habari hii tuliyozungumzia kisirisiri? Kisha akasema, “Wewe umesema sawa; kweli tulipanga hivyo. Inaonekana Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe na ndiye aliyekupasha habari hii yote, kwani kulikuwa hakuna mtu wa tatu pamoja nasi katika shauri yetu”. Akaendelea kusema, “Yaonekana hayo yote yalipangwa na Mungu ili nipate kuongoka; kwa hiyo basi NASILlMU!” Bwana ‘Umair r.a. aliporudi Makka, na ilipojulikana kuwa ameisha silimu, Bwana Safwaan alishtuka sana. Bwana ‘Umair r.a. akaanza kuwahubiri watu, na watu kadha walisilimu kisirisiri. Soma Ibni Hishaam na Tabari ukajue habari hii kwa ukamilifu zaidi.

(25) MAITI YA ADUI
Anasimulia Bwana Anas r.a. ya kwamba kulikuwa na Mkristo mmoja wakati wa Mtume s.a.w. aliyesilimu na akawa mwandishi wa Mtume s.a.w. Lakini baadaye akatanasari tena. Baada ya kuingia katika Ukristo tena alizoea kusema “Muhammad hajui cho chote isipokuwa yale tu niliyomwandikia mimi”. Basi, ikawa Mwenyezi Mungu akamfisha, na watu wakamzika. Lakini asubuhi wakaona kuwa ardhi imeitupa maiti yake nje. Watu wakasema bila shaka hii ni kazi ya Muhammad na masahaba zake, kwani marehemu huyo alijitenga nao na kutanasari tena; basi wamemfukua na kutupa nje maiti yake. Wakristo hao wakamzika tena kwa kuchimba zaidi sana kuliko mara ya kwanza, lakini asubuhi wakashuhudia kwamba ardhi tena imemtupa nje. Basi, wakasema, “Kwa kuwa bwana huyu aliwakimbia, wamemtupa nje.” Wakamzika tena; na safari hii wakachimba sana kadri walivyoweza. Lakini asubuhi ikaonekana tena kwamba ardhi imeisha itupa maiti hiyo nje. Hapo 28 wakatambua kuwa hiyo si kazi ya binadamu, basi wakaiacha vivi hivi. (Bukhari).

(26) HABARI YA GHAIBU TAARIFA MUBASHARA
Katika mwaka wa 8 baada ya kuhamia Madina, Mtume s.a.w. alimtuma Bwana Harith Bin Umar ampelekee mtawala wa Basra barua ya Mtume s.a.w. Lakini kwa bahati mbaya mjumbe huyo alipofika mahali panapoitwa Muta, akauawa na ‘Amr bin Shurahbil. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa mno la maadui. Hata siku hizi kuuawa kwa balozi au mjumbe wa nchi fulani katika nchi nyingine ni kosa kubwa, mpaka vita hasa vyaweza kuchemka kati ya nchi hizo mbili. Basi, Mtume s.a.w. alipopata habari ya kuwa mjumbe wake ameuawa na maadui kule Muta, akawaamrisha masahaba kujitayarisha kwa vita na hao wachokozi, Masahaba karibu 3,000 wakaondoka Madina kuelekea Muta. Kabla jeshi la Kiislamu halijaondoka, Mtume s.a.w. akamfanya Bwana Zaid bin Harith kuwa kiongozi wa jeshi hilo, na akaagiza kuwa Bwana Harith atakapouawa, mara moja Bwana Ja’far bina Abi Talib ashike uongozi; na Bwana huyu pia atakapouawa vitani basi Bwana Abdullah bin Ruwaha ashike bendera. Jeshi la Kiislamu lilipofika Muta, likapigana na jeshi kubwa la Kirumi. Idadi ya hao Warumi ilikuwa laki moja wakisaidiwa na makafiri vile vile laki moja wa bara Arabu. Sawa na habari iliyotolewa na Mtume s.a.w. kwanza Bwana Zaidi bin Harith aliuawa vitani, na kisha Bwana Ja’far naye akawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na tena Bwana Abdallah Bin Ruwaha vile vile akauawa na maadui vitani. Baada ya kuuawa kwa hao waliowekwa na Mtume s.a.w., Waislamu wakamkubali Bwana Khalid bin Walid r.a. kuwa kiongozi wao katika vita. Basi, chini ya uongozi wa Bwana 29 Khalid r.a., Waislamu walipigana vikali mpaka Mwenyezi Mungu akawapa ushindi, na jeshi la Kirumi pamwe na jeshi la Waarabu wakashindwa na kukimbia kiwanjani. Ni la ajabu kuwa kule vitani masahaba hao watatu wameuawa na wakati huo huo Mtume s.a.w. akawatangazia Waislamu katika Madina kuwa jamaa hao watatu wamekwisha uawa katika njia ya Mungu. (Bukhari. mlango wa Vita ya Muta). Katika siku hizo kulikuwa hakuna njia nyepesi za kupeleka habari toka mahali pamoja hadi pengine, lakini Mtume s.a.w. akajua habari hii ya ghaibu wakati ule ule walipouawa hao watatu vitani, na vita bado ilikuwa inapiganwa. Bila shaka Mtume s.a.w. aliambiwa na Mwenyezi Mungu habari hii. Ushuhuda huu umetolewa na Sahaba mmoja wa Mtume s.a.w. maarufu sana yaani Hadhrat Anas r.a.

(27) UTABIRI MKUU
Tulieleza nyuma habari ya vita ya Handaki, ya kwamba katika siku za vita hiyo mwujiza wa kuongeza chakula ulionyeshwa na Mtume s.a.w. Sasa napenda kueleza mwujiza mwingine ambao vile vile unahusiana na vita hiyo ya Handaki ambayo pia inaitwa Vita ya Ahzaab. Jambo lenyewe ni kwamba katika vita hiyo baada ya kushauriana na masahaba. Mtume s.a.w. alikubali shauri la Hadhrat Salman Alfarisi r.a. ya kwamba handaki refu sana lichimbwe kwa kuzuia maadui wasipate kuingia Madina mara moja. Masahaba wakaanza kuchimba handaki kwa nguvu na bidii sana. Walipokuwa wakichimba wakakuta humo mwamba ambao uliwashinda masahaba wote. Wakajaribu mno kuupasua wasiweze. Kisha walipoona wameshindwa wakampasha habari Mtume s.a.w. kwamba tumepata jiwe gumu sana ambalo 30 halipasuliki kwetu. Ijapokuwa Mtume s.a.w. vile vile hali yake ilikuwa dhaifu kwa sababu ya njaa, lakini hata hivyo alifika pale penye mwamba na akapiga sururu juu ya mwamba kwa nguvu. Alipopiga kwa nguvu ukatoka humo ndani ya jiwe mwako wa moto mara moja. Hapo Mtume s.a.w. alisema kwa sauti ya juu “Allahu Akbar”, maana yake Mungu ni Mkuu kuliko kila kitu; na akasema nimeona nimepewa funguo za ufalme wa Shamu. Na alisema “Wallahi, naona majumba mekundu ya nchi ya Shamu”. Kwa sababu ya pigo hili mwamba ukapasuka kidogo. Akapiga mara nyingine sururu juu ya mwamba. Zikatoka cheche tena. Na akasema kwa sauti kubwa. “Allahu Akbar”, nimepewa funguo za nchi ya Uajemi! Naona wakati huu majumba meupe ya Madain. Safari hii jiwe lile likapasuka zaidi. Akapiga mara ya tatu. Mwako ukadhihirika, tena. Na Mtume s.a.w. akasema tena kwa sauti ya juu kabisa, “Allahu Akbar”, safari hii nimepewa funguo za Yeman; Wallahi, wakati huu naonyeshwa milango ya San'aa.” Safari hii jiwe likavunjika kabisa, na masahaba wakaendelea na kazi zao za kuchimba handaki. Ni la ajabu ya kuwa Mtume s.a.w. akaona nchi za Shamu, Uajemi na Yeman ya kuwa funguo za utawala wa nchi hizo amepewa yeye. Wakati huo Waislamu walikuwa katika dhiki kubwa ajabu. Bali walidharauliwa na kufukuzwa katika Makka. Walipohamia Madina, wadhalimu wakafika kule vile vile ili kuwaangamiza Waislamu hao waliokuwa wachache sana kuliko makafiri. Kwa kuona onyesho hilo la ajabu Mtume s.a.w. aliwaambia Waislamu kwamba ijapokuwa wanadhulumiwa wakati huu lakini utafika wakati ambapo Waislamu wataondolewa dhiki na taabu ya kila namna, bali watatawala nchi hizo. Wanafiki waliposikia utabiri huu wa Mtume s.a.w. wakaudharau na kuucheka wakisema, “Kumbe hao jamaa wanadai watatawala nchi za wafalme Kaisar na Kisra, ilhali hawawezi hata kutoka nje ya Madina. Maneno hayo ya wanafiki yameandikwa katika Ibne Hisham.” Lakini ni 31 la ajabu kabisa kwamba utabiri huu mkuu ulitimia barabara katika zama za makhalifa wa Mtume s.a.w. Chungulia ndani ya historia ukaelewe ukweli wake sawasawa!

(28) UTABIRI WA KWELI
Bibi Aisha r.a., mkewe Mtume s.a.w., amesimulia ya kuwa Mtume s.a.w. alipougua maradhi aliyofia, akamwita bintiye Bi Fatima r.a. na kumwambia jambo fulani la siri. Bi Fatima aliposikia akaanza kulia. Kisha akamwambia jambo jingine la siri; mara Bi Fatima akaanza kucheka. Mama wa Waminio, Bi Aisha r.a., anasema kuwa nikamwuliza Bi Fatima aliambiwa nini na Mtume s.a.w. mpaka akalia na kucheka. Hapo Bi Fatima r.a. akasema ya kuwa kwanza Mtume s.a.w. alinipasha habari kwamba yeye Mtume s.a.w. atafariki kwa maradhi hayo, basi nikalia. Na kisha akaniambia kuwa mimi ni mtu wa kwanza katika watu wa nyumbani mwake nitayemfuata nyuma; basi hapo nikafurahi na kucheka, (Bukhari). Na twajua sana ya kuwa habari hii ya ghaibu ikatimia sawasawa, kwani baada ya Mtume s.a.w. kufariki Bi Fatima r.a. akawa ni wa kwanza miongoni mwa ahali za Mtume s.a.w. aliyefariki dunia!

(29) MVUA INANYESHA
Mwujiza huu wa kunyesha mvua nao umeelezwa ndani ya kitabu cha Bukhari. Katika siku za uhai wa Mtume s.a.w. safari moja mvua ilikosekana sana katika bara Arabu, na kulienea njaa kubwa sana bara zima. Bwana Anas bin Malik r.a. aliyekuwa sahaba mashuhuri na mtukufu wa Mtume s.a.w. anasimulia kuwa:- Katika siku ya Ijumaa, Mtume s.a.w; alipokuwa anatoa hotuba msikitini, mtu mmoja aliingia katika mlango unaotazamana na mimbari. Mtu huyo akisimama pale akaanza kumwambia Mtume 32 s.a.w., “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mali na wanyama wameangamia na njia zimekatika; basi umwombe Mwenyezi Mungu atunyeshelezee mvua”. Bwana Anas r.a. anasema kuwa Mtume s.a.w. akainua mikono yake na akaanza kumwomba Mwenyezi Mungu, kwa kusema: “Ee Mola wetu tunyweshe, Ee Mole wetu tunyweshe, Ee Mola wetu tunyweshe”. Bwana Anas r.a. anaendelea kusimulia kuwa, “Wallahi, tulikuwa hatuoni wingu au kipande chake mbinguni. Wala kulikuwa hakuna nyumba au kitu cho chote kati yetu na kilima cha Sal’a; kote kulionekana kweupe kabisa. Basi, mara kipande kimoja cha wingu kikajitokeza toka nyuma ya kilima kile. Na kilipofika juu katikati mbinguni kikapanuka na kuenea; na kisha mvua ikaanza kunyesha. Ikanyesha sana mno, na kwa juma zima ikaendelea bila kusimama; wallahi hatukuona jua kwa wiki nzima”. Bwana Anas r.a. anaendelea, “Ilipofika Ijumaa Iliyofuata, mtu mmoja akaingia msikitini kupitia mlango huo huo, na Mtume s.a.w. alikuwa anatoa hotuba. Mtu huyo akaanza kusema, “Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia na wanyama wamekufa na njia zimekatika; kwa hiyo umwombe Mungu azuie mvua”. Basi, Mtume s.a.w. akainua mikono yake na kaomba, “Ee Mola wetu, nyesheleza pembezoni mwetu, wala si juu yetu. Nyesheleza milimani na mabondeni na mahali panapostahili kuota miti”. Bwana Anas r.a. anasema kuwa mvua ikaisha mara moja na tulipotoka msikitini tukatembea katika jua. Mwujiza huu umeelezwa katika mlango wa “Istisqaai”, katika Bukhari.

(30) HABARI YA GHAIBU
Katika siku za uhai wa Mtume s.a.w., mfalme wa Uhabeshi. Bwana Najjashi aliyekuwa Mkristo alisilimu. Bwana Najjashi alipofariki katika nchi yake ya Uhabeshi, Mtume s.a.w. alikuwa 33 katika Madina. Katika siku hizo kulikuwa hakuna njia nyepesi za kupeleka habari mara moja toka mahali pamoja hadi mahali pengine. Bali habari zilikuwa zinapelekwa kwa kutumwa mtu aliyekuwa anasafiri kwa kupanda ngamia au farasi kupeleka habari mahali pengine. Kwa hiyo habari ilikuwa taabu kufika haraka huko na huko. Lakini, Bwana Abu Hurairah r.a. anasimulia kuwa Mtume s.a.w. alitutangazia habari ya kifo cha Bwana Najjashi, mfalme wa Uhabeshi, siku ile ile aliyofariki Bwana huyo. Na siku hiyo hiyo Mtume s.a.w. akasalisha sala ya jeneza ya mfalme Najjashi. (Someni Kitabu cha Bukhari ilimoelezwa habari hii katika Mlango wa “Attakbiru A’lal-janaaizi Arab’an”). Huu ni mwujiza wa ajabu unaoshangaza sana. Kwani habari ya kifo cha Bwana Najashi ilifika Madina baada ya siku kadhaa, lakini Mtume s.a.w. aliambiwa na Mwenyezi Mungu habari ya msiba huu siku ile ile aliyofariki mfalme huyo!

(31) MWUJIZA KUMHUSU MFALME KISRA
Mfalme Kisra alipochochewa na baadhi ya Mayahudi waliokuwa huko nchini Iran nao walikuwa na heshima mbele ya mfalme huyo, yeye mfalme Kisra alimwandikia Gavana wake wa sehemu ya Yeman kwamba yeye amfikishe Mtume s.a.w. mbele yake mara moja. Gavana wa Yeman alipopata amri hii ya Kisra, aliwatuma wajumbe wawili wa serikali waende kumpasha habari Mtume s.a.w. kwamba yeye anatakiwa kufika mbele ya mfalme Kisra. Wajumbe hao wakafika Madina na kumpa Mtume s.a.w. barua ya Gavana wa Yeman. Mtume s.a.w. aliposomewa barua hiyo akawaambia wajumbe hao kuwa kesho watapewa majibu ya barua hiyo. Wajumbe walisema ya kwamba ikiwa Mtume s.a.w. atahudhuria mara moja barazani mwa Mfalme Kisra hapo Gavana wa Yeman ameahidi kuwa yeye atamwombea mbele ya 34 mfalme. Lakini kama Mtume s.a.w. hatatii amri, basi mfalme atamwua yeye pamoja na masahaba zake wote. Lakini Mtume s.a.w. hakujali maneno hayo. Kesho yake wajumbe walipohudhuria mbele ya Mtume s.a.w. ili kupata jibu la barua ile, Mtume s.a.w. akawaambia, “Mfalme amekwisha uawa na mwanawe, kwa hiyo basi hata amri yake vile vile imefutika". Pia aliwaambia kuwa wampashe habari Gavana wa Yeman, Bwana Baadhaan, ya kwamba asilimu. Wajumbe walishangaa sana kwa maneno ya Mtume s.a.w.; wakaondoka kuelekea Yeman. Wakampasha habari yote Bwana Baadhaan. Bwana huyu akastaajabu sana, na akasema, “Kama habari ya kuuawa kwa Kisra itaonekana ni kweli, basi hakutakuwa na shaka yo yote katika ukweli wa Mtume huyu; na kama sivyo, atatendewa ipasavyo”. Siku hizo kulikuwa hakuna njia, nyepesi za kupeleka habari mara moja toka mahali pamoja hadi pengine. Baada ya siku chache kupita Baadhaan akapokea barua ya mfalme wa Iran. Aliposoma, akashituka sana. Kumbe barua hii iliandikwa na mtoto wa mfalme Kisra. Na mle ndani akaeleza kuwa, “Nimemwua baba yangu, kwa hiyo toka sasa mimi mwenyewe ni mfalme badala yake.” Akaongeza kuandika, “Unaamrishwa usimkamate yule Mtume wa Uarabuni, ninafuta ile amri ya baba yangu kumhusu yeye.” Gavana, Bwana Baadhaan, aliposoma habari hii akasilimu mara moja pamoja na watu wengi sana, na kisha baadaye Yeman nzima ikaingia katika Uislamu. Huu ni mwujiza mkubwa ajabu ambao unajulikana katika historia ya Kiislamu. Waweza kuchukua kitabu cho chote cha Historia ya Kiislamu hutaona habari hii imekosekana humo.

(32) UPEPO MKALI UTAVUMA
Mtume s.a.w. pamoja na masahaba zake walipokwenda Tabuk kupigana na Warumi, baada ya kuwasili Tabuk Mtume s.a.w. aliwaambia masahaba kwamba, “Usiku huu upepo mkali sana utavuma kwa nguvu, kwa hiyo mtu ye yote kati yenu asisimame. Na aliye na ngamia, amfunge kamba kwa madhubuti sana”. Bwana Abi Hamid r.a. anayesimulia habari hii, anasema kuwa kweli usiku huo upepo mkali kupita kiasi ukavuma. Na mtu mmoja aliyesimama kwa bahati mbaya, upepo ukamtupa vilimani, Ushuhuda huu umepatikana katika Kitabu cha Muslim. Msiingiwe na wasiwasi ya kuwa hata siku hizi wataalamu wanatabiri hali ya hewa mapema, basi kama Mtume s.a.w. alitabiri si jambo kubwa. Tujue ya kuwa katika siku zile za Mtume s.a.w. kulikuwa hakuna vyombo vya kuchunguza hali ya hewa, kwa hiyo utabiri wake haufanani na utabiri wa wanasayansi wa siku hizi, kwani hawa wanatumia vyombo maalum vya kuchungua hali ya hewa; lakini Mtume s.a.w. alikuwa hana vyombo kama hivi.

(33) MATOKEO MABAYA YA KUMPINGA MTUME S.A.W.
Imesimuliwa na Hadhrat Abu Said Khudri r.a. ya kuwa safari moja Mtume s.a.w. alipokuwa anagawa mali katika watu akaja kule mtu mmoja wa kabila la Bani Tamim na akasema, “Ee Mtume, fanya uadilifu.” Mtume s.a.w. akamjibu, “Uangamie; kama mimi sifanyi adili, ni nani mwingine anayeweza kufanya adili?” Seyidna Umar r.a. aliposikia maneno ya mtu huyo akamwomba Mtume s.a.w. ruhusa ya kumwua pale pale. Lakini Mtume s.a.w. akasema, “Mwache”. Kisha akatoa utabiri kumhusu 36 mtu huyo. Akasema Mtume s.a.w. ya kuwa, “Hakika mtu huyu atakuwa na wenziwe ambao hamtapenda kusali nao pamoja, wala kufunga nao saumu pamoja; hao watasoma Kurani lakini haitapita chini ya mitulinga yao. Watatoka katika dini kama vile mshale unavyotoka upande wa pili ukimpenya aliyelengwa - Inapoangaliwa ile sehemu ya mbele ya mshale hakionekani cho chote (damu wala nini); na kisha sehemu yake ya mwisho inapoangaliwa, pia hamna cho chote; na sehemu ya katikati ikiangaliwa, haina lo lote; na manyoya yake pia hayana alama yo yote. Mshale huu umepita mavi na damu (bila kupata athari yake). Alama ya hao watu ni kuwa kutapatikana kati yao mtu mmoja mweusi ambaye sehemu ya juu ya mkono wake itakuwa imevimba kama titi la mwanamke. Hao watu watapigana na kundi bora la watu.” Hadhrat Abu Said r.a., msimuliaji wa maneno hayo ya Mtume s.a.w. anasema, “Nashuhudia nimesikia hadithi hii toka kwa Mtume s.a.w. na ninashuhudia ya kuwa Seyidna Ali r.a. aliwahi kupigana nao; nami nilikuwa pamoja naye. Baada ya vita yeye, Seyidna Ali r.a., akaamrisha atafutwe mtu mwenye alama zilizoelezwa na Mtume s.a.w. Basi akatafutwa na kaletwa, na nilipomtazama, kumbe alikuwa vile vile alivyokuwa ameeleza Mtume s.a.w.” (Bhukari). Sasa, ebu, angalieni jinsi ulivyotimia utabiri wa Mtume s.a.w. miaka mingi baada ya kufariki kwa Mtume s.a.w.

(34) WARUMI KUSHINDA VITANI
Wasomao historia wanajua sana ya kuwa wakati wa Mtume Muhammad s.a.w. kulikuwa na vita kati ya nchi za Rumi na Uajemi. Warumi walikuwa ni Wakristo lakini Waajemi wa wakati huo walikuwa waabuduo moto. Waajemi walikuwa na nguvu nyingi, nao wakawashinda vibaya sana Warumi. Kwa miaka kama 37 20 hivi Waajemi wakapigana na Warumi mpaka nguvu za Warumi zikasagwa na kukanyagwa chini ya miguu ya Waajemi. Ni katika mwaka wa 616 A.D. ambapo Waajemi waliweza kupata ushindi mkuu juu ya Wakristo. Wakati huo Mtume s.a.w. alikuwa bado hajahama Makka. Warumi waliposhindwa mbele ya Waajemi, makafiri wa Makka walifurahi sana; Wakasema, Wakristo wanafanana na Waislamu, lakini Waajemi wanazo itikadi kama zile zetu, kwa hiyo hata nasi pia tutawashinda Waislamu, kama Waajemi walivyowashinda Warumi. Hapo Mtume s.a.w. akapokea wahyi toka kwa Mwenyezi Mungu uliokuwa na utabiri mkuu kuhusu habari hiyo. Mwenyezi Mungu akasema: “Mimi ni Mungu nijuaye sana. Warumi wameshindwa katika nchi iliyo karibu; nao baada ya kushindwa kwao watashinda katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla na baadaye; na siku hiyo Waaminio watafurahi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu; Humsaidia amtakaye; naye ni mwenye nguvu mwenye rehema. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mungu havunji ahadi yake, lakini watu wengi hawajui, (Sura 30 ya Kurani, aya 2 - 7). Katika aya hizo ilielezwa kuwa ijapokuwa Warumi wameshindwa, lakini katika miaka michache wataweza kuwashinda Waajemi. Na siku ya ushindi wa Warumi, Waislamu nao watapata furaha kubwa vile vile kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Katika aya ya Kurani neno lililotumiwa ni ‘miaka bidh'a.’ Bidh’a kwa Kiarabu maana yake ni idadi ya 3 hadi 9. Basi katika aya hizo ilitabiriwa ya kuwa Warumi watawashinda Waajemi katika muda wa hadi miaka 9, lakini sio kabla ya miaka 3. Habari hii ikaenezwa sana na Waislamu katika Makka; kati yao alikuwa Hadhrat Abu Bakr r.a. vile vile. Yeye alipotangaza utabiri huu ya kuwa hivi karibuni Warumi watapata ushindi juu ya Waajemi, 38 basi watu wa Makka wakabisha sana, na mmoja wao, Bwana Ubaiyy bin Khalf, akajitokeza na kaweka sharti ya kuwa kama kweli Warumi wataweza kushinda katika miaka 3, basi nitampa Abu Bakr r.a. ngamia 10, la sivyo kama habari hii haitatimia Abu Bakr r.a. atanipa ngamia kiasi hicho hicho. Seyidna Abu Bakr r.a. akakubali sharti hilo. Mpaka wakati huo kuwekeana masharti namna hiyo hakukuwa mwiko katika Uislamu. Mtume s.a.w. alipojua ya kuwa muda wa miaka 3 umewekwa katika sharti, akamwambia Abu Bakr r.a. ya kuwa Mungu hakusema miaka 3, bali amesema miaka Bidh’a; na bidh’a maana yake ni 3 hadi 9. Kwa hivyo unatakiwa kumwambia Ubayy bin Khalf ya kuwa muda wa miaka 9 uwekwe katika sharti, na kuwa idadi ya ngamia iwe 100 badala ya 10. Basi wakapatana hivyo. Wote wakaanza kusubiri. Mwishowe ikatokea vile vile ilivyotabiriwa na Mtume s.a.w. kwa kupata habari toka kwa Mungu. Katika mwaka wa 624 A.D. Mfalme wa Rumi, Hirakla, akaweza kuwashinda Waajemi, bali akaingia katika hekalu lao la kuabudia moto la Gondzak (Gazaca) na kuliangamiza. Habari ikatimia sawasawa kabisa. Mpaka wakati huo, yule Ubayy bin Khalf alikuwa ameisha fariki, kwa hiyo Seyidna Abu Bakr r.a. akachukua ngamia 100 toka kwa mrithi wake. Na imesimuliwa kuwa Mtume s.a.w. akamwambia Abu Bakr r.a. atoe ngamia hao wote 100 sadaka, naye akatoa. Someni Tirmidhi na Baidhawi. Katika utabiri huo pia ilitabiriwa ya kuwa siku Warumi watakapowashinda Waajemi, Waislamu nao vile vile watapata furaha kubwa. Hii sehemu pia ilitimia wazi wazi. Warumi walipopata ushindi, Waislamu nao wakawashinda vibaya sana makafiri wa Makka katika vita ya Badr. Katika vita hiyo viongozi wakubwa wakubwa wa makafiri kama vile Abu Jahli na wengineo wakauawa Na sawa na utabiri wa Biblia katika muda wa mwaka mmoja ulianguka na kuangamia utukufu wa Kedari. Na mabaki 39 ya hesabu ya wavuta pinde hao mashujaa wakawa wachache, (Isaya 21 :16,17). Kedari ndio hao Makuraishi wa Makka. Baada ya Mtume s.a.w. kuhamia Madina, vita ya Badr ilipiganwa baada ya mwaka mmoja kupita, ambamo utukufu wa Kedari ukaangamia. Jinsi ulivyotimia utabiri huu mkuu hata Sir William Muir pia amekiri. Ameandika katika kitabu chake ‘Life of Muhammad’, uk 119 hivi, “Wakati ambapo mafuriko ya ushindi wa Uajemi yaliendelea mbele kwa nguvu, Muhammad (s.a.w.) akatabiri katika Sura ya 30 ya kuwa karibuni Warumi watawashinda Waajemi, na kama tulivyoona kweli utabiri huo ukatimia sawasawa.” Je, huu si mwujiza mkubwa sana!

(35) MWUJIZA KUMHUSU UMAYYA
Hadhrat Abdullah bin Mas'ud amesimulia ya kuwa safari moja bwana Sa'd bin Mu'aadh alikwenda Makka kufanya ibada ya Umra (hija ndogo), na huko alishinda kwa Umayya bin Khalf Abi Safwaan. Huyu Umayya naye alikuwa anafika kwa Bwana Sa'd alipokuwa anapitia Madina akielekea Shamu. Bwana Sa'd alitaka kufanya Umra, lakini Umayya akamwambia asubiri kidogo. Bwana Sa'd anasema kuwa wakati wa saa sita mchana watu walipoghafilika nikatoka kuzunguka Ka'ba. Alipokuwa anazunguka Ka'ba, kumbe akaja Abu Jahli, na akauliza, “Nani anazunguka Ka'ba?” Bwana Sa'd akaitika mara moja. “Mimi Sa'd,” Basi, Abu Jahli akachemka, “unazunguka Ka'ba kwa amani ilhali mmewapa makazi Muhammad na watu wake”. Bwana Sa'd akajibu, “ndiyo, Bwana”. Basi wale wawili wakajibizana vikali. Yule Umayya akamsihi Bwana Sa'd, “Usipaaze sauti juu ya Abul Hakam (Abu Jahli), kwani yeye ni kiongozi wa hapa 40 bondeni. Lakini, bwana Sa'd akaendelea, “Wallahi, kama utanizuia kuzunguka Ka'ba nitaharibu biashara yako katika Shamu”. Bwana Umayya akazidi kumwambia Sa'd asipaaze sauti yake; na akajaribu kumzuia. Hapo Bwana Sa'd akaghadhibika na akasema “Acha Bwana, sikiliza, nimemsikia Muhammad s.a.w. akisema kuwa yeye ATAKUUA!” Loo, “Ataniua mimi” kasema Umayya. Akasema, ndiyo. Akasema, “Wallahi Muhammad hasemi uwongo”. Basi yeye akafika kwa mkewe na kumwambia, Je, hujui aliyoniambia ndugu yangu wa Madina? Kauliza, “Amesema nini?” Kajibu, "Amesema kuwa amemsikia Muhammad akisema kuwa yeye ataniua" Mkewe akanena, "Wallahi, Muhammad hasemi uwongo". Basi, makafiri walipotoka kupigana na Waislamu vita katika Badr, mkewe Umayya akamwambia mumewe, "Je, hukumbuki aliyokuambia nduguyo wa Yathrib (Madina)?" Hapo bwana huyo akataka asifuatane na jeshi la makafiri. Lakini Abu Jahli akamwambia, "Wewe u miongoni mwa waheshimiwa wa bondeni, kwa hiyo nenda kwa siku moja au mbili pamoja na jeshi." Basi akafuatana nao, na akauawa. (Bukhari). Angalieni jinsi alivyotabiri Mtume s.a.w. mapema kuwa Umayya atauawa, bali akapashwa habari hii mapema, na akapenda sana kujilinda pia, lakini hata hivyo akauawa kama ilivyokuwa imetabiriwa mapema sana.

(36)SAFARI YA ISRAI NA MIIRAJ
MWEZI wa Rajabu ndio mwezi Mtume (s.a.w.) alipopelekwa zile safari mbili maarufu za Israi na Miiraji.
Israi ni safari ya hapa hapa ardhini, kutoka Msikiti Mtukufu wa Makka mpaka Baytil Maqdis, kule Jerusalem. Na Miiraji ni safari ya mbinguni, kutoka Baitil Maqdis kwenda hadi anga za juu.Safari iyo ya ardhini ilikuwa ni safari ambayo ingemgharim mtu kuchukua miezi katika zama izo kusafiri lakini mtume alichukuliwa safari zote na kuonyeshwa yote ndani ya usiku mmoja.NAAHIDI ALLAH AKITUAFKISHA NITAKILETA CHOTE HAPA NA JUU YA MAFUNZO YAKE NA KUPITIA KISA HICHI NDICHO KILIMFANYA SWAHABA ABUBAKAR KUITWA SWADIK (MSWADIKISHAJI) NI KIREFU NAWEZA KUIITA MAKALA

(37)MAJI YAONGEZEKA
Anasimulia Hadhrat Anas r.a. ya kwamba safari moja Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. alitoka pamwe na masahaba zake katika safari yake. Walipokwenda umbali fulani ukafika wakati wa sala, lakini walikuwa hawana maji ya kutawadhia. Hapo mtu mmoja akatoka na kaleta maji kidogo katika chombo. Mtume s.a.w. akashika chombo hicho na akatandaza vidole vyake juu ya chombo, kisha akasema inukeni mkatawadhe. Basi wote waliohitaji kutawadha wakatawadha, nao walikuwa karibu 70 hivi. (Bukhari).

(38)MUUJIZA WA MTI KUSOGEZWA
Hii imesimuliwa katika hadithi kadhaa ikiwemo simulizi ya Anas Ibn Malik (r.a).Anas anasimulia kwamba baada ya mtume kufedheheshwana makafiri basi alimuomba Allah awaonyeshe Muujiza kupitia mti uliokuwa bondeni.Mtume alisema " Ewe Muumba!Nipe ishara ambayo itafanya asiwepo yeyote mwenye kuwa na wasiwsi na mimi" nao mti ukaja hadi alipo.Kisha akauamrisha urudi ulipokuwa mahala pake nao ukatii.
The miracle of the tree that obeys the order – 1
Foremost, the same miracle was narrated by Imam Ibn Maja, Darimi, Imam Bayhaqi, Hazrat Anas Ibn Malik from Hazrat Ali; Bazzaz and Imam Bayhaqi narrated it from ‘Umar:
When the Noble Messenger (pbuh) was saddened at the denial of the unbelievers, he said:
“O my Sustainer! Give me a sign that I shall no longer see anyone who contradicts me!”

According to Anas, Gabriel was also there present before the occurrence of this miracle. There was a tree at the side of the valley. Upon the instruction of Gabriel, the messenger of Allah called that tree. The tree came near him. He then told the tree to “go back”; it returned and settled itself in its place.SOMA ZAIDI KUHUSU MUUJIZA WA MTI

(39)WANYAMA WALIOZUNGUMZA
Lakini kuna visa vingine vya wanyama wawili waliozungumza vinavyopatikana katika Sahiyh Al-Bukhaariy Mjalada wa 3 Nambari 517, navyo ni:Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wakati mtu alikuwa amempanda ng'ombe, alimgeukia na kusema:"Sikuumbwa kwa ajili hii (yaani kumpakia mtu) bali nimeumbwa kwa ajili ya kuambua ardhi". Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaongeza: ((Mimi, Abu Bakar na 'Umar tumeamini kisa (hiki) )). Kisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaendelea: ((Mbwa mwitu alimteka kondoo na mchungaji alipomfukuza, mbwa mwitu alisema, "Nani atakayekuwa mlinzi wake siku itakayokuwa ya wanyama wa pori wakati hakutakuweko wachungaji isipokuwa mimi?". Baada ya kusimulia, Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Mimi, Abu Bakar na 'Umar pia tumeamini (kisa hiki))). Abu Salama (msimulizi mwingine alisema: "Abu Bakar na 'Umar hawakuweko (wakati huo)"
Vile vile imesimuliwa kuwa mbwa mwitu pia alizungumza na mmoja wa maswahaba wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) karibu na Madiynah kama ilivyohadithiwa na Fat-h al-Baariy.
Imetoka kwa Unays bin 'Amr: "Ahban bin Aws alisema: 'Nilikuwa na kondoo wangu. Mara mbwa mwitu alimteka kondoo nikampigia kelele. Mbwa mwitu akaukalia mkia wake na kuniambia: 'Nani atakayemchunga (yaani kondoo) siku ambayo utakuwa umeshughulika na hutoweza kumchunga? Je unanizuilia rizki ambayo Allah Ameniruzuku?' Ahban akaongeza: "Nilipiga makofu na kusema: Naapa kwa Allah, sijapata kuona jambo la kushangaza na la ajabu kama hili! Hapo mbwa mwitu akasema: 'Kuna maajabu zaidi ya haya, nayo ni Mjumbe wa Allah katika ile mitende akiwaita watu kwa Allah (Kuingia Uislamu)' Unays bin 'Amr aliendelea kusema, "Kisha Ahban akaenda kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia yaliyotokea na akaingia Uislamu". [Sahiyh Al-Bukhaariy Mjalada wa 3 Nambari 517]
Kisa kama hicho kimesimuliwa kwa usimulizi mwingine kama ifuatavyo:
Kutoka kwa Sa'iyd al-Khudriyyi (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba (mchungaji alipokuwa na kondoo wake) mara mbwa mwitu alimteka kondoo na kukimbia. Mchungaji akamkimbiza mbwa mwitu na akamkamata kondoo wake. Mbwa mwitu akaukalia mkia wake na akamwambia mchungaji: "Mkhofu Allah, unanichukulia rizki yangu Aliyoniruzuku Allah". Mchungaji akasema: "Maajabu haya! Mbwa mwitu amekalia mkia wake na kunisemesha mimi kwa lugha ya binaadamu". Mbwa mwitu akasema: "Nikuambie yaliyo maajabu zaidi kuliko haya? Kuna Muhammad yuko Yathrib (al-Madiynah) anawajulisha watu khabari za kale". Mchungaji akaelekea (Madiynah) akimuendesha kondoo wake hadi akaingia (mji wa) Madiynah. Akamuweka kondoo wake pembezoni akaenda kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuelezea kisa chote. Mjumbe wa Allah, akaamrisha Swalah ya jamaa kisha akamwambia mchungaji awaelezee watu (kisa chake) naye akawaelezea. Kisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Yeye (mchungaji) amesema ukweli. Naapa kwa Yule (Allah) Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, Siku Ya Kufufuliwa (Qiyaamah) haitofika hadi wanyama wa kuwinda watasema na binaadamu na fimbo pamoja na nyuzi za viatu vya mtu vitazungumza naye na mapaja yake yatamjulisha kuhusu yanayotokea kwa familia yake (nyumbani kwake) akiwa yeye hayupo)) [Musnad Ahmad Mjalada wa 3]

(40) ALIKUWA ANAONA NA KUSIKIA WASIVYOONA NA KUVISIKIA WATU WENGINE JAPO WANAKUWA MAHALA PAMOJA
Mara nyingi mtume Muhammad alikuwa akiwaambia masahaba zake mambo yanayomjia na kuyaona ilhali wao hawaoni mfano akitembelewa na jibrili na kuletewa habari,kuyaona majini na kuzumza na maiti na wanyama.Ndio kwasababu utasikia simulizi nyingi mtume akisema ALINIJIA/AMENIJIA....
SOMA ZAIDI KUHUSU MIUJIZA YA MTUME MUHAMMAD S.A.W
 
Acha upotoshaji na story zako za kuokoteza mkuu

Leta aya kutoka kwenye quran kama miujiza hiyo ni ya kweli maana huwa mnadai quran ndiyo kila kitu Muhammad hajawahi kufanya muujiza wowote na hapa quran inakiri allah hakuwahi kumteremshia Muhammad ishara maana alikuwa mwonaji tu
( وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ )

العنكبوت (50) Al-Ankaboot

Na walisema: Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu.

Sasa wewe unapingana na quran yako
 
Acha upotoshaji na story zako za kuokoteza mkuu

Leta aya kutoka kwenye quran kama miujiza hiyo ni ya kweli maana huwa mnadai quran ndiyo kila kitu Muhammad hajawahi kufanya muujiza wowote na hapa quran inakiri allah hakuwahi kumteremshia Muhammad ishara maana alikuwa mwonaji tu
( وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ )

العنكبوت (50) Al-Ankaboot

Na walisema: Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu.

Sasa wewe unapingana na quran yako
Tafuta tafsiri ya hiyo aya,acha kukurupuka.
 
Acha upotoshaji na story zako za kuokoteza mkuu

Leta aya kutoka kwenye quran kama miujiza hiyo ni ya kweli maana huwa mnadai quran ndiyo kila kitu Muhammad hajawahi kufanya muujiza wowote na hapa quran inakiri allah hakuwahi kumteremshia Muhammad ishara maana alikuwa mwonaji tu
( وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ )

العنكبوت (50) Al-Ankaboot

Na walisema: Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu.

Sasa wewe unapingana na quran yako
WAO WALIULIZA KAMA BAAZI YA WATU WALIVYO ULIZA....MIUJIZA WALIFANYIWA KAMA IYO NA WAKAISHIA KUSEMA "SIJAPATA KUONA UCHAWI KAMA HUU"....KAFIRI KAFIRI TU
 
Acha upotoshaji na story zako za kuokoteza mkuu

Leta aya kutoka kwenye quran kama miujiza hiyo ni ya kweli maana huwa mnadai quran ndiyo kila kitu Muhammad hajawahi kufanya muujiza wowote na hapa quran inakiri allah hakuwahi kumteremshia Muhammad ishara maana alikuwa mwonaji tu
( وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ )

العنكبوت (50) Al-Ankaboot

Na walisema: Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu.

Sasa wewe unapingana na quran yako
Hujaelewa maana take hata kidogo
 
WAO WALIULIZA KAMA BAAZI YA WATU WALIVYO ULIZA....MIUJIZA WALIFANYIWA KAMA IYO NA WAKAISHIA KUSEMA "SIJAPATA KUONA UCHAWI KAMA HUU"....KAFIRI KAFIRI TU
Unaita wenzio KAFIRI wakati unamwabudu KAFIRI mpaka kwenye avatar yako! Ha ha ha ha
 
KAFIRI NI KILA ANAYEPINGA QURAN SO KAKA NA WEWE UNAPINGA QURAN BASI NA WEWE NI KAFIRI
Huyo uliyemuweka kwenye Avator yako yeye alikuwa anaikubali Quran takatifu?

Wewe bila shaka nawe ni Kafiri huwezi kumuabudu kafiri ea kwenye avator yako! Hahahaa
 
Back
Top Bottom