Ni jambo linalosikitisha sana kuona chama kikongwe kama hiki kukosa kumbukumbu sahihi za kiutendaji, ni hii ndo kansa iliyokuwa kwa kasi katika hadi kwenye asasi za kiserikali, ni vigumu sana kuamini ila huu ndo ukweli,
Kumekuwepo na uvumi mwingi sana kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya ccm, lakini mimi hapa nina maswali mengi sana kwa KATIBU MWENEZI bwana Nape Nnauye,
1. Naomba utoke uueleze uma, je Dr Slaa aliajiuzulu uanachama wa ccm mwaka gani?
2. Ni kifungu kipi au utaratibu upi ulio rasimi unaotumika kuhusu kadi iwapo mwanachama anaamua kuasi chama chake
3.Je ni lini Dr Slaa kalipIa ada ya uanachama kwa mara ya mwisho?au hakuna ada ya uanachama?
4.Je mtu anahesabika si mwanachama baada ya kushindwa kulipa ada ya uanachama wake baada ya muda gani?
Ukinijibu hapa nadhani tutakuwa na mjadala mzuri wenye tija kwa taifa juu ya PROPAGANDA zinazoonezwa na watu wenye hila na fitina kwa vyama vya upinzani! najua hiyo ndo siasa ila lazima siasa ilenge ukweli na si kupotosha uma.