Somo la Katiba ya CCM kwa Nape & Co

Somo la Katiba ya CCM kwa Nape & Co

[h=5]ANA KADI MBILI YA CCM NA YA CHADEMA ANA MADEMU WAWILI JOSEHINE NA ROZIMARY ANA KAZI MBILI NI PADRE NA MWANASIASA NI MSOMI NA NI KILAZA NI WA MAMBO MAWILI MAWILI.. ANATAKA UBUNGE ANATAKA URAISI..
[/h]

- ni kweli bro mjinga ni mjinga tu uko 100% right!! you are a genius mamen!1

Es!

Kwahiyo mkuu hili ndio umeona lina maana sana kuliko somo husika hapo juu?
 
Kwa hiyo Nape angeweza pia kusema Dr SLAA anavaa suluali na Dr akakili, ninyi mgeshangilia na kuandika kwenye magazeti yenu? Kwa hiyo unajitetea kuwa Nape alisema tu kuwa Dr ana kadi bila kumaanisha chochote sawa tu na angesema Dr amekunywa chai asubuhi? La muhimu kwenu ni Dr kukili kuwa ndio nimekunywa chai asubuhi.

Hii ni tofauti kwa kuwa Slaa anawaambia watu wengine wampe kadi zao ili azichome wakati ya kwake kaweka ndani. Ingekuwa Dr Slaa anasimama kwenye majukwaa na kuwahamasisha watu wasinywe chai hala akatokea mtu akatustua kuwa yeye amemshuhudia Slaa anakunywa chai na juu ya hilo bado Slaa akakkiri kuwa ni kweli anakunywa chai basi ingekuwa ni habari. Kikubwa hapa ni UNAFIKI wa kusema mambo jukwaani kisha unarudi kwako unaishi tofauti.
 
hii ni tofauti kwa kuwa slaa anawaambia watu wengine wampe kadi zao ili azichome wakati ya kwake kaweka ndani. Ingekuwa dr slaa anasimama kwenye majukwaa na kuwahamasisha watu wasinywe chai hala akatokea mtu akatustua kuwa yeye amemshuhudia slaa anakunywa chai na juu ya hilo bado slaa akakkiri kuwa ni kweli anakunywa chai basi ingekuwa ni habari. Kikubwa hapa ni unafiki wa kusema mambo jukwaani kisha unarudi kwako unaishi tofauti.
[....../quote]

kikubwa hapa ni ujinga wa ccm kudai mtu nayewavua watu wake kadi na kuchoma eti ni mwanachamaw ao wa siri. Ukubwa wake unajaziwa na wingi wenu kutoelewa kuwa kama slaa angekuwa mfuasiw enu basi mngepaswa muadhibu kwa jinsi anavyo fanya irrepairable damages. Au katokomea in the wilderness?
 
Hii ni tofauti kwa kuwa Slaa anawaambia watu wengine wampe kadi zao ili azichome wakati ya kwake kaweka ndani. Ingekuwa Dr Slaa anasimama kwenye majukwaa na kuwahamasisha watu wasinywe chai hala akatokea mtu akatustua kuwa yeye amemshuhudia Slaa anakunywa chai na juu ya hilo bado Slaa akakkiri kuwa ni kweli anakunywa chai basi ingekuwa ni habari. Kikubwa hapa ni UNAFIKI wa kusema mambo jukwaani kisha unarudi kwako unaishi tofauti.
Tukufundishe tu zaidi kuwa sio kila mwanachama anaekihama chake hurudisha kadi, na pia sio lazima apokewe kwa jukwaa
 
Tukufundishe tu zaidi kuwa sio kila mwanachama anaekihama chake hurudisha kadi, na pia sio lazima apokewe kwa jukwaa

Huna unacho nifundisha, nafahamu fika wala haihitaji kuwa na PHD kujua kuwa si lazima kurudisha kadi ndio uwe umejivua uanachama wa chama cha siasa. Ndio maana majadiliano yanayoelekea upande huo nimewaachia wenye akili ndogo tu. Hoja zako za msingi unazikwepa nashangaa unataka kukomalia haya ya kijinga.
 
Yericko Nyerere, km umeona trends hapa utaona kuwa CCM hawana kipya wal aakili mbadala.hawapo flexible hata kw avitu vidogo.Wamekuja na ujinga wakidhani utahit ghafla wakajagundua kuwa imekuwa ngumu wanaishia kurudiarudia vitu vile wakiamini kuwa vitakuwa kweli baadaye.Ni kama watu wanaodhani wakirudia otesha mahindi yaliyochemshwa mwishowe yataota.
 
Guys do you real have time to urge with Nape? I kindly urge you to reserve your energy for something useful.
 
Huna unacho nifundisha, nafahamu fika wala haihitaji kuwa na PHD kujua kuwa si lazima kurudisha kadi ndio uwe umejivua uanachama wa chama cha siasa. Ndio maana majadiliano yanayoelekea upande huo nimewaachia wenye akili ndogo tu. Hoja zako za msingi unazikwepa nashangaa unataka kukomalia haya ya kijinga.

Kumbe una akili nzuri tu ila umepumbazwa na ushabiki mkuu?

Inasikitisha kuona unajua fika lakkini unapindsha tu mbambo kwa faidi ya ushabiki wako!

Nafurahi kuona kupitia mjadala huu nimeweza kugundua kume huwa unaigiza tu ugonjwa ulio nao!

Asante ishi na kukulia hapo ulipo mkuu!
 
Kumbe una akili nzuri tu ila umepumbazwa na ushabiki mkuu?

Inasikitisha kuona unajua fika lakkini unapindsha tu mbambo kwa faidi ya ushabiki wako!

Nafurahi kuona kupitia mjadala huu nimeweza kugundua kume huwa unaigiza tu ugonjwa ulio nao!

Asante ishi na kukulia hapo ulipo mkuu!


Sina muda wa kujadili watu, nataka tusimame kwenye hoja. Rudi posti yangu ilikuwa namba mbili hapa kwenye hii thread, ujibu hoja.
 
Guys do you real have time to urge with Nape? I kindly urge you to reserve your energy for something useful.

Something useful like learning how to write English vocabularies.
 
- Huwezi kumtumikia Mungu huku umemficha Shetani nyumbani uvunguni mwa kitanda chako, unatakiwa kumchukia shetiani kwa akili zako zote na uwezo wako wote, Slaa anapopewa kadi za wasioitaka CCM na huku yeye binafsi anajua anayo vipi akili au nafsi yake haimsuti?

- I mean kama Slaa ana kadi ya CCM airudshe now, kuendelea kuwa nayo ni dalili kwamba ahana uhakika na anachokifanya huko kwenu, hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja!! mbona ni simple common sense tu!

Es!

tumeipiga kiberiti !
 
Hivi hizi hoja zipo sawa?
1) Bwana Nyerere ana kadi ya TLP
2) Bwana Nyerere ni mwanachama wa TLP

Nadhani umekimbia hadi umepitiliza kwenu.

Naomba niijibu hii posti unayodai ni hoja ninayoikimbia mkuu.

Hoja yako hapa unataka kuwianisha uhusiano wa kadi na uanachama?

Iwe ndivyo au sivyo najibu ifuatavyo mkuu.

Kuwa na kadi na kuwa mwanachama havi tofautiani ila kimantiki vinatofautiana, kadi ni utambulisho wa mwanachama husika.

LAKINI:

Uanachama wa mwanachama UTAKOMA pale utakapokiuka katiba ya chama hicho mfano kwa ccm ukikiuka hayo niliyoyaeleza hapo juu.

Ukiivunja katiba ya chama na katiba hiyo ikakuchukulia hatua zinazostahiki, KADI yako na uanachama wako HUFUTIKA, hivyo kadi hiyo hata ukae nayo miaka 2000 ijayo hautatambuliwa kuwa mwanachama wa chama kile.

Narudia kukufunda mkuu, Dr Slaa si mwanachama wa ccm na HANA kadi ya ccm bali ana KUMBUKUMBU ya ILIYOKUWA kadi YAKE ya uanachama wa ccm tu.

Kadi hiyo ni kumbukumbu YAKE, ni mali YAKE, hakuna mwenye mamlaka ya kuichukua.

Anaweza kuamua kuichoma moto, kufungia vitumbua, kuichana, au kumpa mwanae ajifunzie kuandika!

Kwalugha nyingine huitwa Kadi mfu.
 
13.
(1) Uanachama wa mwanachamautakwisha kwa:-

(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na Chama kingine chochote
cha siasa.


(2) Mwanachama ambaye uanachama
wake unakwisha kwa sababu yoyote ile
hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada
aliyotoa wala michango yoyote
aliyoitoa.ibu wa katiba ya ccm
 
Chadema mnatia huruma sana badala ya kupambana CCM mnapambana na Nape.
 
Nape amewekwa pale kama condom...akishatumiwa atasukumwa kule,subiri wenye mtandao wakamate ofisi utaona atakapokimbilia!yeye kazi yake kuwasumbua CDM kwa chochote kile kama pumba,uzushi,urongo,ili mradi awemo kwenye media siku zote akijibu majibu mepesi kwa hoja makini!kaulizwa mna mkakati gani kupunguza umasikini uliopitiliza na njaa kwa wananchi?yeye kadakia anasema Dr Slaa ana kadi ya CCM!inahusu nini?hata JK anajua kuwa yeye si tu ana kadi ya CCJ bali ni muasisi wa CCJ!
 
mkubwa unafikiri hawajui hila na unafiki wao tu, ndiyo unaowasumbua.
 
MAELEZO kutoka kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuhusu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa kuendelea kumiliki kadi ya CCM ni propaganda zinazokiuka misingi ya ukweli, uhuru na haki. Nitaeleza kwa nini.

Kwanza, kulingana na ibara ya 8 ya Katiba ya CCM, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi ndio hufikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya uanachama.


Pili, kulingana na ibara ya 12 (1), baada ya mtu kukubali kuwa mwanachama inabidi atekeleze mambo yafuatayo, kabla ya kusajiliwa kwenye rejesta ya wanachama wa CCM: lazima atoe kiingilio cha uanachama; lazima alipe ada ya uanachama kila mwezi; na lazima atoe michango yoyote inayoamuliwa na viongozi wa CCM.

Tatu, kulingana na ibara ya 13(1) ya Katiba ya CCM (2010) uanachama wa mtu katika CCM unakwisha kutokana na sababu mojawapo kati ya sababu sita zifuatazo: kufariki, kujiuzulu, kuachishwa kwa mujibu wa Katiba, kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba, kutotimiza masharti ya uanachama, au kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

Na nne, kulingana na ibara ya 13(4) mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Kwa kuzingatia vifungu hivi vinne vya katiba ya CCM (2010), mambo kadhaa yanafuata kimantiki.

Kwanza, ni wazi kuwa ibara hizi zinawakataza viongozi watendaji katika CCM kupokea kiingilio cha uanachama au ada ya uanachama kutoka kwa mtu ambaye ni mwanachama wa Chama kingine chochote cha siasa mbali na CCM. Yaani, kiongozi wa CCM anayepokea kiingilio cha uanachama au ada ya uanachama kutoka kwa mtu ambaye sio mwanachama wa CCM anakuwa ni kiongozi mwenye asiyefikiri sawasawa.

Na pili, kwa kuzingatia vifungu hivi vinne vya katiba ya CCM, ni wazi kuwa, mwanachama wa CCM ambaye anathibitika kuwa, baada ya kujiunga na CCM, ameamua kuwa mwanachama wa Chama kingine chochote cha siasa mbali na CCM, anapaswa ama kuachishwa kwa mujibu wa Katiba au kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Hii maana yake ni kwamba, kiongozi wa CCM anayefahamu kuwa kuna mwanachama wa CCM ambaye amefanikiwa kuwa Katibu Mkuu au mbunge kupitia chama kingine chochote cha siasa lakini akasita kusimamia mchakato wa mtu huyo kuachishwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM au mtu huyo kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo, anakuwa ni kiongozi asiyefikiri sawasawa. Anakuwa ameisahau katiba yake.

Kwa kuzingatia mahitimisho haya mawili muhimu, sasa tunaweza kutambua kwa kurejea kauli ya Nape dhidi ya Slaa kuwa na kadi ya CCM, yeye (Nape) ni kiongozi wa namna gani.

Nape Nnauye, Katibu Mwenezi na Itikadi (CCM), amesema na kuandika katika mitandao ya kijamii maneno yafuatayo:
"Katika matamshi yangu hakuna mahali nilipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu kubwabwaja kuwa sijui Katiba ya CCM wanakurupuka kwa sababu ndogo sana… nilichosema (ni kuwa) Dk. Slaa na baadhi ya vigogo wa (CHADEMA) wana kadi za (uanachama wa) CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka leo.

Sijazungumzia uanachama wao...najua kuwa kwa katiba ya CCM ukishakuwa mwanachama wa chama kingine uanachama wako CCM unakufa hapo hapo.

Kwa mujibu wa nukuu hii, Nape Nnauye amejenga hoja mbili tata ambazo nakusudia kuzipa muundo wa kimantiki na kisha kuzihakiki kwa lengo la kumpa somo. Hoja ya kwanza ambayo Nnauye ameijenga kwa njia ya mzunguko ni hii hapa:

"Kwa mujibu wa katiba ya CCM, kila mwanachama hai anapaswa kulipa kiingilio cha uanachama na ada ya uanachama; Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na baadhi ya vigogo wenzake katika CHADEMA wana kadi za uanachama wa CCM na baadhi yao wanafanya malipo haya mpaka leo; Kwa hiyo wao ni wanachama hai wa CCM. Hata hivyo, haya matamshi yangu dhidi yao hayahusianishi kadi za CCM walizonazo kina Dk. Slaa na uanachama wao katika CCM."

Katika hoja yake hii, Nape Nnauye ananishangaza mambo mawili. Kwanza anajaribu kutuambia kuna wanaCCM ambao ni wanaCHADEMA pia. Lakini pili, anatuambia kwamba, yeye haijui katiba ya CCM. Nitaanza na hili la pili nikiwa nimefanya dhahania (assumption) kwamba, siku ile Nnauye anatoa kauli zake inawezekana, angalau kimantiki, kwamba Dk. Slaa na wenzake wanaotajwa naye tayari walikuwa wameamua kuchukua uanachama wa CCM lakini wakasitisha nia yao baadaye kidogo.

Katika mtazamo wake kuhusu katiba ya CCM, tatizo liko hivi: Nnauye amemwongelea Dk. Slaa pamoja na "vigogo wengine" wa CHADEMA katika sentensi yenye kiunganishi cha "na." Hivyo, anachokiongelea kitaalamu tunakiita "mazingira ya kitu hiki pamoja na kitu kile" (both/and scenario), ambapo kuna Dk. Slaa kwa upande mmoja na "vigogo wengine" wa CHADEMA kwa upande mwingine. Anasema kwamba wote wanazo kadi za CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka sasa.

Ni wazi kuwa, Dk. Slaa kama Katibu Mkuu wa CHADEMA anayo kadi ya uanachama wa CHADEMA tangu alipohamia katika chama hiki karibu miaka 15 iliyopita. Kwa hiyo, kiunganishi cha "na" katika sentensi ya Nnauye kinamaanisha kuwa, baadhi ya wale "vigogo wengine" wa CHADEMA anaowataja wana kadi za CHADEMA pia.

Na maneno "baadhi yao wanalipia kadi" katika sentensi yake yanamaanisha kuwa ama Dk. Slaa au mmojawapo kati ya hao vigogo wengine wa CHADEMA waliotajwa analipia ada ya uanachama wa CCM. Huwezi kulipa ada ya uanachama wa CCM kama sio mwanachama wa CCM. Kwa hiyo, kwa kuzingatia ukweli huu, inafuata kimantiki kuwa kauli ya Nnauye kuwa "baadhi yao wanalipia kadi" za CCM inaongelea uanachama wa kina Dk. Slaa katika CCM.

Hivyo, ni kinyume cha kanuni za mantiki, kwa Nnauye kusema kwamba, matamshi yake haya "hayahusianishi kadi za CCM walizonazo kina Dk. Slaa na uanachama wao katika CCM." Huu ni usahaulifu.

Kuna hoja ya pili ambayo imesanifiwa na Nape Nnauye na ambayo inakoleza zaidi mtazamo wangu huu dhidi yake na wenzake. Katika nukuu yake hapo juu, kwa njia ya mzunguko, Nnauye pia amejenga hoja ifuatayo:

"Kwa mujibu wa katiba ya CCM, kila mwanachama hai anapaswa kulipa kiingilio cha uanachama na ada ya uanachama; Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na baadhi ya vigogo wenzake katika CHADEMA wana kadi za uanachama wa CCM na wanafanya malipo haya mpaka leo; Kwa hiyo, viongozi watendaji wa CCM wanapokea kiingilio cha uanachama na ada ya uanachama kutoka kwa wanachama wa vyama vingine vya siasa! Hii maana yake ni kwamba, baadhi ya wanachama wa vyama vingine vya siasa ni wanachama wa CCM pia, jambo ambalo ni kinyume cha katiba ya CCM."

Huyo ndiye Nape Nnauye katika rangi zake halisi! Ameivua nguo CCM! Alichofanya hapa ni kulitangazia taifa na dunia nzima kwamba, CCM inaendeshwa nje ya utaratibu wa kikatiba!

Ni hivi: Kama anachokisema ni kweli, basi jambo hili ilipaswa kuwa sababu ya kutosha ya vikao husika ndani ya CCM kuanzisha mchakato wa kikatiba ili kufanikisha kuachishwa au kufukuzwa kwa kina Dk. Slaa kutoka CCM. Vinginevyo, vikao vya juu vinapaswa kuisambaratisha sekretarieti ya CCM ya sasa kwa kuvunja katiba ya CCM!

Nape Nnauye na sekretarieti yake lazima washughulikiwe kwa sababu wao wamethibitisha kwamba ni viongozi wenye kusumbuliwa na tatizo la kutokujipanga na kusimamia katiba ya chama chao.

Na kwa kuhitimisha basi, nataka niseme kwamba, Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM, pamoja na sekretarieti yake yote inayofanya madudu haya aliyoyatangaza kwa dunia nzima tayari wamepoteza sifa ya kubaki katika ofisi wanazoziongoza.

Tutawashangaa sana kina Jakaya Kikwete (Mwenyekiti CCM), kama wataendelea kuwakumbatia viongozi hawa wanaosumbuliwa na tatizo la usahaulifu wa kiwango hiki kuhusu katiba ya chama chao, wakati ndani ya chama chao kuna watu wenye umakini mkubwa wa kushika nafasi hizi za uongozi.
 
UBARIKIWE KWA UCHAMBUZI MAKINI NA WA KINA.SISI TUMEYAZOEA HAYA MATAMSHI YA HUYU BWANA NA INAWEZEKANA VIONGOZI WOTE WA CCM WANAYATEGEMEA SANA NA NDO MAANA BADO AMEPEWA NAFASI HIYO YA KUTOA MATAMKO BILA UTARATIBU.NAKUMBUKA SIKU SILIZOPITA AMEWAHI KUTOA TAMKO KUHUSU KESI YA ARUSHA INAYOWAKABILI VIONGOZI WA CHADEMA KWAMBA WAO WANA UHAKIKA WA KUSHINDA KESI HIYO JAMBO AMBALO LILISABABISHA WAKILI WA CHADEMA KUOMBA MAHAKAMA IMTAKE NAUYE AJE ATOE UDHIBITISHO WA KAULI YAKE KITU AMBACHO MPAKA LEO HAJAFANYA.KWA UPANDE WANGU NAAMINI KAULI HII YA DR.SLAA KUMILIKI KADI YA CCM AMETUMWA NA RAIS WAKE NA KWAKUWA ANAMWAMINI ANAFURAHI KWA KAULI ZAKE.LAKINI PIA HII INAASHIRIA KUISHIWA SERA NA HATA KUKOSA CHA KUFANYA KATIKA OFISI ZAO.KWELI KIFO CHA NYANI MITI YOTE INATELEZA.:glasses-nerdy:
 
Hahahahahaha Hili la Slaa nadhani limewashika pabaya, mnatafuta kila njia ya kutokea! RIP CHADEMA! Laana ya ubaguzi dhidi ya vyama vingine kuviita CCM B haiwezi kuwaacha!
 
Najiuliza hivi slaa akiamua ingia ktk mkutano sensitive wa CCM,je wataweza mfukuza kwa jinsi wanajikangaja na sheria zao?

Je kama ni mwanachama hawajawahi fikiri amwajibisha?kwani kama wanamkubali kuwa mwanachama mbona hapatai makaripio wanayopata wana CCM wengi tuu, kama Sitta, na wabunge wengine wanaodhibiwa kila siku kwa ku damage chama.AU slaa ni boss pia wa CCM na hawathibitu mwajibisha kama mwanachama wao?
 
Back
Top Bottom