Pamoja na matokeo ya kidato cha 4 kuongezeka ufaulu, kidato cha 2 na darasa la 4 kwa mujibu wa taarifa/ripoti ya Baraza la Elimu Tanzania limesema kuwa bado ufaulu wa Somo la Hisabati uko chini sana.
Nimekuwa nikijiuliza sana tatizo ni nini lkn majibu yamekuwa yalitolewa na wadau wa elimu ni yaleyale kila mwaka eti;
1. Mtazamo wa wanafunzi kudhani kuwa somo lenyewe la Hisabati ni gumu.
2. Ukosefu wa walimu weledi n.k
Sababu hizo zimekuwa zikitolewa miaka nenda miaka rudi, nadhani tangu tumepata uhuru sababu ni hizohizo!
Kwanini NECTA isifanye utafiti ikaja na majibu sahihi ya tatizo hili? kuliko kila mwaka wanatuambia ufaulu wa somo la Hisabati uko chini!!
Wataalamu wamejazana Wizarani/Idara ya Elimu.
Inawezekana ikawa sababu sio hizo inawezekana ikawa mitihani inayo tungwa ni migumu sana, au siyo standard, hayo yote tutayajua tu endapo tutafanya utafiti na tukaja na ufumbuzi.
Tuanze kwenye Shule za Msingi, maana hapo ndipo tatizo linapo anzia.
Msingi mbovu.
Kwa maoni yangu Somo la Hisabati sio Gumu.