Somo la CHADEMA Arusha CCM limewaingia?

Somo la CHADEMA Arusha CCM limewaingia?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,175
Reaction score
43,935
DSC06266.JPG
Umati wa wanachama, mashabiki na watazamaji wakisikiliza viongozi wa CDM wakihutubia mjini Arusha

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) kimerejesha kata nne zilizokuwa zinagombaniwa katika uchaguzi mdogo mjini Arusha siku ya Jumapili na hivyo kuendeleza ubabe wake dhidi ya chama tawala katika mji huo ambao ni lango kuu la maeneo ya utalii nchini. Ushindi huo wa ngurumo umekuja baada ya waliokuwa wanachama na madiwani wa CDM kuvuliwa uanachama baada ya kufanya uasi na kusababisha viti vinne vya udiwani kuwa wazi kitu kilichosababisha kuitishwa kwa uchaguzi mdogo. Uchaguzi wa kata hizi nne umefanyika zikiwa zimepita karibu wiki kadhaa tangu kufanyika kwa chaguzi nyingine ndogo ambapo katika kata za Arusha uchaguzi wake uliahirishwa kufuatia mlipuko wa mabomu katika mkutano wa kampeni wa CDM ambapo watu watatu waliuawa na wengine zaidi ya sabini kujeruhiwa.

Matokeo ya uchaguzi huo -kwa kadiri yalivyopokewa jana- yako kama hivi:
Themi
CHADEMA-678
CCM-326
CUF-313
Kimandulu
CHADEMA-2665
CCM-1169
Kaloleni
CHADEMA-1019
CCM-389
CUF-169
Elerai
CHADEMA-1715
CCM-1239
CUF-213

Kimsingi, CDM imeshinda kwa zaidi ya asilimia 61 ya jumla ya kura halali zilizopigwa; ni ushindi wa radi! CCM wametumiwa ujumbe mzito wa kuwafanya watafakari kama wapo watu wenye kutafakari.

Kilichofanyika Arusha ni kichapo cha mwaka; ni uthibitisho kuwa kukataliwa kifikra hutangulia kukataliwa kivitendo na hapa vitendo ninamaanisha kura. Kwamba, kabla ya watu hawajabadilisha kura zao ni lazima wabadilishe fikra zao kwanza; wananchi wa Arusha walishabadilisha fikra zao kuhusu Chama cha Mapinduzi tangu 1995 walipomchagua Makongoro Nyerere wa NCCR-Mageuzi na toka wakati ule mahusiano yao na CCM hayajawa ya kawaida. Na siyo Arusha mjini tu ni katika Arusha ambapo tumeona upinzani ukizama hadi vijijini – Karatu, Mbulu, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini kote ni wabunge wa upinzani na wote ni wa CDM. Ni mkoa wenye wabunge wengi wa CDM kuliko mkoa mwingine na mahali ambapo kama isingekuwa mizengwe basi Halmashauri karibu tatu za miji mbalimbali zingekuwa chini ya CDM.

Kwa matokeo haya na kama hakutakuwa na mizengwe ya CCM Meya ajaye wa Arusha atatoka CDM.

Wananchi wa Arusha hawakujali sana ahadi, vitisho, kejeli na vioja vya watawala; na ni wazi kabisa kuwa hawakujali zaidi milipuko ya mabomu na unyanyasaji uliopitiliza wa vyombo vya dola. Ni Arusha ambapo viongozi karibu wote wa CDM wamejikuta wakidhalilishwa, kufunguliwa mashtaka na kunyanyaswa na wale wenye madaraka ya kutawala. Kuanzia Mbowe hadi Slaa, Bi. Mushumbusi hadi Lema wote wamepata kibano chao mjini Arusha. Katika mazingira ya kawaida watu wanaweza kufikiria kuwa ili wawe “salama” na ili mambo yao yafanyike kwa “utulivu” si bora wachague CCM tu? Ni rahisi kabisa kuamini kuwa kwa kuchagua CCM Arusha ingekuwa imetulia na watu wake wana amani.

Kwanini pamoja na ahadi hiyo ya nchi ya “maziwa na asali” wananchi wa Arusha bado wameikataa CCM?
Jibu linaweza kuwa ni gumu kidogo na lina mambo mengi. Kwa kuanzia tunaweza kusema kuwa wananchi wa Arusha wamekataa kupiga magoti mbele ya wanaowadhulumu na mbele ya watawala walioshindwa. Mwanadamu akinyanyasika sana kuna mahali anafika ambapo katika kukataa kwake kunyanyasika zaidi anaamua kukataa – kwa kiburi – kupiga magoti. Historia imejaa watu wa namna hiyo; watu ambao kwa kujitambua utu wao na thamani yao hawakuwa tayari kujisalimisha mbele ya watawala ili wapate amani ya uongo.

Lakini kubwa zaidi tunaweza kusema kuwa watu wa Arusha tofauti kulinganisha na mji kama wa Dar wengi wao ni wafanyabiashara na wanajitegemea wao wenyewe kwa maisha yao. Ni watu ambao wanashughuli mbalimbali ambazo hazitegemei ajira ya serikalini. Jiji kama la Dar kwa mfano lipo kundi kubwa sana la kipato cha kati ambalo linategemea maisha yake serikalini. Kundi hili kwa kiasi kikubwa ni kikwazo sana cha mabadiliko Jijini Dar kwani hawa ni watu ambao hata kama wanachukia yanayoendelea ni vigumu kuchagua upinzani kwa sababu hawaoni kama maslahi yao yatalindwa.

Arusha na miji mingi ya pembezoni wako huru zaidi kuchagua bila ya kujali athari zozote kwenye ajira zao. Pamoja na kuchagua upinzani wananchi wa Arusha wameendelea kujipatia vipato vyao na ajira zao na utulivu ambao unatarajiwa kuja baada ya kuchagua chama wanachotaka kunaweza kurejesha amani na utulivu zaidi kama serikali na Chama cha Mapinduzi havitaendelea kuleta mizengwe.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huu yanatuma ujumbe mwingine zaidi. Kwamba, bado juhudi kubwa sana ya kukandamiza upigaji kura zinafanyika nchini na hili tumeanza kuliona tangu 2010. Katika hali ambayo haijawahi kutokea kabla ya 2010 upigaji kura ulikuwa chini ya asilimia 70 (asilimia karibu 40 hivi). Chaguzo zote kuu za nyuma yake upigaji kura ulikuwa kati ya asilimia 69 kwenda juu. Hata hivyo CCM ikitumia mbinu zinazoeleweka sana – vitisho, kukatisha tamaa, kufanya upinzani uonekane ni shetani, n.k imefanikiwa sana kukatisha tamaa ya kupiga kura hasa kwa wazee na kina mama. Hivyo, upinzani umekuwa ukitegemea kura za vijana zaidi kuliko za makundi mengine. Kundi hili la vijana sasa ndio ngome kuu ya upinzani nchini; na hawa ni vijana hasa ambao ama walipiga kura kwa mara ya kwanza 2010 au ndio wanapiga kura kwa mara ya kwanza sasa.

Lakini kuna kitu kingine ambacho naamini ni kweli zaidi kuliko hivi vingine na nilikidokeza katika posti yangu ya Facebook mapema leo; CCM inazidi kukataliwa na ahadi zake hazivutii tena kama zamani, vitisho vyake haviogopeshi na utukufu wake hautukuzwi tena. Ni wazi kabisa kuwa kukiwa na Tume huru, na mfumo mzuri wa uchaguzi CCM itapata shida sana kushinda na badala yake inahitaji sana kutegemea dola (polisi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa n.k) kuweza kushinda. Hili ndilo tatizo kubwa sana; CCM ili kujirejeshea uhalali siyo tu ikubali kushindwa baada ya uchaguzi bali ichague njia yenye kuonesha kuwa uchaguzi ni huru na wahaki na hakuna njia nzuri ya kufanya hivyo kama kuhakikisha uhuru wa vyombo na uhuru wa sheria ya uchaguzi.

Hivyo, walichokifanya watu wa Arusha ni kuamua kuicharaza CCM kwenye sanduku la kura; kwani ni hapo tu ndipo sauti za raia zinaweza kusikika vizuri. Hofu ile ya kuwa CCM wataiba kura ni hofu ambayo imezuia watu wengi kupiga kura kwa sababu wanajiambia kuwa ‘CCM itashinda tu’ na matokeo yake hawaendi kupiga kura. Watu wa Arusha wamejua nguvu ya kura yao na wanajua sauti yao ni kura yao. Hawawezi kushindana na polisi na usalama wa taifa; hawawezi kushindana na Mkuu wa Mkoa na IGP; lakini wanajua sehemu pekee ambapo wana uwezo wa kushindana ni kwenye kupiga kura. Na hivyo wamejitokeza kupiga kura. Ni kama walipewa fimbo na kuambiwa waende wakawachape CCM na kuwachapa wamewachapa. Haikujalisha nani aliipigia kampeni CCM au jinsi gani CCM ilibebwa, mwisho wa siku (siku ya uchaguzi) uamuzi wa mwisho ni wa mtu mmoja mmoja; watu ambao walishafanya uamuzi wao kwenye fikra wakaenda kuuthibitisha kama kutia sahihi kwenye sanduku la kura.

Wananchi wetu wengi wakielewa nguvu hii kuu waliyonayo na nguvu ambayo inafanya demokrasia inoge watatambua kuwa iwe kwa mbinde au kwa upinde wataenda kupiga kura. Kwamba, haijalishi mabomu, polisi, kejeli au vitisho, ikifika wakati wa kupiga kura wataenda kupiga kura na kusema kile ambacho hawawezi kukisema kwa maneno.

CCM imekataliwa. Na huu ni mwendelezo tu wa yale ambayo tumeyaona tangu 2010. Kazi kubwa ni kuwashawishi mamilioni ya wananchi wengine ambao kwa woga au kutokujua wanafikiri kuwa CCM inatakiwa kutawala milele.
Arusha wamesema hapana na wamerudia kusema hivyo tena na tena. CCM iheshimu uamuzi wa wananchi wa Arusha na iache mizengwe kwani haikisaidii chama kupendwa zaidi; CCM iangalie watu wake wanaoifanyia kampeni kama ni watu ambao wanastahili kuendelea na hilo kwani zaidi ya kuwafanya wapoteze kura, watu hao wamezidi kuifanya CCM ionekane ni kituko na kejeli na kudharaulika. CCM ikiendelea na watu wale wale na mbinu zile zile wapinzani hawana la kufanya isipokuwa kuendelea kucharaza watu bakora ya kura; ndio utamu wa demokrasia.

Hata hivyo yote ni sehemu ya demokrasia; Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye amesema vizuri kuelezea hili katika mtandao wa JamiiForums baada ya kipigo cha Arusha “Kuna watu wameuliza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)”.

Tusubiri mtanange mwingine.
 
Tofauti ya takribani 200, 500, etc mi inaniumiza sana. Yani hichi chama bado kinawapiga kura?!
 
Nimepapenda zaidi hapa

"...CCM iangalie watu
wake wanaoifanyia kampeni kama ni
watu ambao wanastahili kuendelea
na hilo kwani zaidi ya kuwafanya
wapoteze kura, watu hao wamezidi
kuifanya CCM ionekane ni kituko na
kejeli na kudharaulika. CCM
ikiendelea na watu wale wale na
mbinu zile zile wapinzani hawana la
kufanya isipokuwa kuendelea
kucharaza watu bakora ya kura;
ndio utamu wa demokrasia..."
 
Binafsi huwa ninatamani mwamko huo wa wananchi usiishie kwenye ushabiki tu na ufurukutwa, bali uwe chachu ya maendeleo ya kuukomboa uchumi wetu kwa watu kufanya kazi kwa bidii na taadhima.
 
Let's be honest here folks; ukweli ni kuwa hata hao wanaoishabikia ccm (nilishaacha siku nyingi kutumia capital letters ninapoitaja ccm ya leo ili kuitofautisha na CCM aliyoiacha Mwalimu) wanajua kuwa imechokwa na itaendelea kukataliwa unless ifanye mabadiliko makubwa. Bahati mbaya aina ya viongozi waliopo ccm si wale wenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya kuiifanya ccm hii irejeshe imani kwa wananchi wa leo ambao uwezo wao wa kupambanua mambo unazidi kuongezeka kila kukicha.
 
Mtaokeo ya siasa chafu na utawala mmbovu ndi hayo. Na wanachokivuna ccm ivi sasa ndio walichokipanda.
 
Well presented. It an indication of what is going to happen in 2014 and 2015. With the coming new constitution CCM must think twice!
 
CCM watafute mbinu nyingine za ushindani, na tena ziwe za kawaida kabisa. Fitina, vurugu, uchongezi, uonevu, kutumia vibaya vyombo vya dola na kutoa kafara/rehani roho za watu kutawagharimu sana CCM. Na sio Arusha tu bali ni nchi nzima na kupelekea kuangua vibaya kwa chama chetu, nina kadi na sina mpango wa kuirudisha ila jamani tuwe makini tubadilike
 
DSC06266.JPG

Umati wa wanachama,

CCM imekataliwa. Na huu ni mwendelezo tu wa yale ambayo tumeyaona tangu 2010. Kazi kubwa ni kuwashawishi mamilioni ya wananchi wengine ambao kwa woga au kutokujua wanafikiri kuwa CCM inatakiwa kutawala milele.
Arusha wamesema hapana na wamerudia kusema hivyo tena na tena. CCM iheshimu uamuzi wa wananchi wa Arusha na iache mizengwe kwani haikisaidii chama kupendwa zaidi; CCM iangalie watu wake wanaoifanyia kampeni kama ni watu ambao wanastahili kuendelea na hilo kwani zaidi ya kuwafanya wapoteze kura, watu hao wamezidi kuifanya CCM ionekane ni kituko na kejeli na kudharaulika. CCM ikiendelea na watu wale wale na mbinu zile zile wapinzani hawana la kufanya isipokuwa kuendelea kucharaza watu bakora ya kura; ndio utamu wa demokrasia.

Hata hivyo yote ni sehemu ya demokrasia; Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye amesema vizuri kuelezea hili katika mtandao wa JamiiForums baada ya kipigo cha Arusha "Kuna watu wameuliza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)".

Tusubiri mtanange mwingine.

Mkuu hapo umenena vizuri sana tatizo CCM hawataki kujitambua kwamba wamekataliwa na ili kujinusuru kwa hilo ni lazima wakubali kuanza upya kama chama kipya (upinzani) ili iliwapate muda wa kujipanga naamini wakifanya hivyo itakuwa ni salama yao.
 
Kwa wale wenye akili timamu na busara zao huko CCM (ambao naamini ni wachache sana kwa sasa) kamwe hawawezi kukubali kwenda kujidhalilisha, laiti CCM wangecheza fairplay basi tungewaona hata akina Mzee Mwinyi akiunga mkono kampeni hizi, can you Imagine chama cha miaka tele hakina Mzee hata mmoja anayeongoza siasa za chama chake? Akina Kingunge wanaipinga CCM, wanaondolewa na kuambiwa kaeni kando. Wazee waliokuwa kwenye NEC wametolewa kimtindo na kuundiwa baraza lao eti baraza la ushauri....ok, wameamua kukaa kimya sasa na matokeo ndio hayo sie na CDM yetu tunapeta tu pamoja na kuumizwa na kuuwawa. Hakika wazee waliona mbali
Nimepapenda zaidi hapa

"...CCM iangalie watu
wake wanaoifanyia kampeni kama ni
watu ambao wanastahili kuendelea
na hilo kwani zaidi ya kuwafanya
wapoteze kura, watu hao wamezidi
kuifanya CCM ionekane ni kituko na
kejeli na kudharaulika. CCM
ikiendelea na watu wale wale na
mbinu zile zile wapinzani hawana la
kufanya isipokuwa kuendelea
kucharaza watu bakora ya kura;
ndio utamu wa demokrasia..."
 
Nimepapenda zaidi hapa

"...CCM iangalie watu
wake wanaoifanyia kampeni kama ni
watu ambao wanastahili kuendelea
na hilo kwani zaidi ya kuwafanya
wapoteze kura, watu hao wamezidi
kuifanya CCM ionekane ni kituko na
kejeli na kudharaulika. CCM
ikiendelea na watu wale wale na
mbinu zile zile wapinzani hawana la
kufanya isipokuwa kuendelea
kucharaza watu bakora ya kura;
ndio utamu wa demokrasia..."

Pamoja na hayo tatizo la CCM ni lakimfumo zaidi na mfumo uliostawi kiasi ambacho umekuwa kama saratani inayowatafuna taratibu na wao hawataki kuamini hivyo hata kwa kuambiwa au kuona wao wenyewe kwani wakiamini hivyo lazima watu wengine wangolewe ndani ya chama ilikujisafisha ( kuondoa hiyo saratani) sasa hili si rahisi kwani hakuna anayetaka kutoka au ambaye anaubavu wa kumuondoa mwengine so chama chao kitawafia mkononi mwao.
 
Somo lipi swahiba? kata nne wewe unaona ni ushindi?. Tulichojifunza ni kitu kimoja tu..nacho ni kujipanga kwa 2015 kwani tumejifunza ni wapi tumeteleza. Ninyi mnayo kazi moja nayo ni kutekeleza zile ahadi zote mlizokuwa mkizitoa majukwaani. Mnapaswa kukumbuka kwamba waliowapigia kura hawahitaji maandamano. Ninataka kuwahakikishia kuwa huu ni mwanzo wa mapambano kuelekea 2015 wakati ambapo sera zenu hazitakuwa na mashiko kwani hata watu binafsi watasimama kugombea.
DSC06266.JPG
Umati wa wanachama, mashabiki na watazamaji wakisikiliza viongozi wa CDM wakihutubia mjini Arusha

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) kimerejesha kata nne zilizokuwa zinagombaniwa katika uchaguzi mdogo mjini Arusha siku ya Jumapili na hivyo kuendeleza ubabe wake dhidi ya chama tawala katika mji huo ambao ni lango kuu la maeneo ya utalii nchini. Ushindi huo wa ngurumo umekuja baada ya waliokuwa wanachama na madiwani wa CDM kuvuliwa uanachama baada ya kufanya uasi na kusababisha viti vinne vya udiwani kuwa wazi kitu kilichosababisha kuitishwa kwa uchaguzi mdogo. Uchaguzi wa kata hizi nne umefanyika zikiwa zimepita karibu wiki kadhaa tangu kufanyika kwa chaguzi nyingine ndogo ambapo katika kata za Arusha uchaguzi wake uliahirishwa kufuatia mlipuko wa mabomu katika mkutano wa kampeni wa CDM ambapo watu watatu waliuawa na wengine zaidi ya sabini kujeruhiwa.

Matokeo ya uchaguzi huo -kwa kadiri yalivyopokewa jana- yako kama hivi:
Themi
CHADEMA-678
CCM-326
CUF-313
Kimandulu
CHADEMA-2665
CCM-1169
Kaloleni
CHADEMA-1019
CCM-389
CUF-169
Elerai
CHADEMA-1715
CCM-1239
CUF-213

Kimsingi, CDM imeshinda kwa zaidi ya asilimia 61 ya jumla ya kura halali zilizopigwa; ni ushindi wa radi! CCM wametumiwa ujumbe mzito wa kuwafanya watafakari kama wapo watu wenye kutafakari.

Kilichofanyika Arusha ni kichapo cha mwaka; ni uthibitisho kuwa kukataliwa kifikra hutangulia kukataliwa kivitendo na hapa vitendo ninamaanisha kura. Kwamba, kabla ya watu hawajabadilisha kura zao ni lazima wabadilishe fikra zao kwanza; wananchi wa Arusha walishabadilisha fikra zao kuhusu Chama cha Mapinduzi tangu 1995 walipomchagua Makongoro Nyerere wa NCCR-Mageuzi na toka wakati ule mahusiano yao na CCM hayajawa ya kawaida. Na siyo Arusha mjini tu ni katika Arusha ambapo tumeona upinzani ukizama hadi vijijini – Karatu, Mbulu, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini kote ni wabunge wa upinzani na wote ni wa CDM. Ni mkoa wenye wabunge wengi wa CDM kuliko mkoa mwingine na mahali ambapo kama isingekuwa mizengwe basi Halmashauri karibu tatu za miji mbalimbali zingekuwa chini ya CDM.

Kwa matokeo haya na kama hakutakuwa na mizengwe ya CCM Meya ajaye wa Arusha atatoka CDM.

Wananchi wa Arusha hawakujali sana ahadi, vitisho, kejeli na vioja vya watawala; na ni wazi kabisa kuwa hawakujali zaidi milipuko ya mabomu na unyanyasaji uliopitiliza wa vyombo vya dola. Ni Arusha ambapo viongozi karibu wote wa CDM wamejikuta wakidhalilishwa, kufunguliwa mashtaka na kunyanyaswa na wale wenye madaraka ya kutawala. Kuanzia Mbowe hadi Slaa, Bi. Mushumbusi hadi Lema wote wamepata kibano chao mjini Arusha. Katika mazingira ya kawaida watu wanaweza kufikiria kuwa ili wawe "salama" na ili mambo yao yafanyike kwa "utulivu" si bora wachague CCM tu? Ni rahisi kabisa kuamini kuwa kwa kuchagua CCM Arusha ingekuwa imetulia na watu wake wana amani.

Kwanini pamoja na ahadi hiyo ya nchi ya "maziwa na asali" wananchi wa Arusha bado wameikataa CCM?
Jibu linaweza kuwa ni gumu kidogo na lina mambo mengi. Kwa kuanzia tunaweza kusema kuwa wananchi wa Arusha wamekataa kupiga magoti mbele ya wanaowadhulumu na mbele ya watawala walioshindwa. Mwanadamu akinyanyasika sana kuna mahali anafika ambapo katika kukataa kwake kunyanyasika zaidi anaamua kukataa – kwa kiburi – kupiga magoti. Historia imejaa watu wa namna hiyo; watu ambao kwa kujitambua utu wao na thamani yao hawakuwa tayari kujisalimisha mbele ya watawala ili wapate amani ya uongo.

Lakini kubwa zaidi tunaweza kusema kuwa watu wa Arusha tofauti kulinganisha na mji kama wa Dar wengi wao ni wafanyabiashara na wanajitegemea wao wenyewe kwa maisha yao. Ni watu ambao wanashughuli mbalimbali ambazo hazitegemei ajira ya serikalini. Jiji kama la Dar kwa mfano lipo kundi kubwa sana la kipato cha kati ambalo linategemea maisha yake serikalini. Kundi hili kwa kiasi kikubwa ni kikwazo sana cha mabadiliko Jijini Dar kwani hawa ni watu ambao hata kama wanachukia yanayoendelea ni vigumu kuchagua upinzani kwa sababu hawaoni kama maslahi yao yatalindwa.

Arusha na miji mingi ya pembezoni wako huru zaidi kuchagua bila ya kujali athari zozote kwenye ajira zao. Pamoja na kuchagua upinzani wananchi wa Arusha wameendelea kujipatia vipato vyao na ajira zao na utulivu ambao unatarajiwa kuja baada ya kuchagua chama wanachotaka kunaweza kurejesha amani na utulivu zaidi kama serikali na Chama cha Mapinduzi havitaendelea kuleta mizengwe.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huu yanatuma ujumbe mwingine zaidi. Kwamba, bado juhudi kubwa sana ya kukandamiza upigaji kura zinafanyika nchini na hili tumeanza kuliona tangu 2010. Katika hali ambayo haijawahi kutokea kabla ya 2010 upigaji kura ulikuwa chini ya asilimia 70 (asilimia karibu 40 hivi). Chaguzo zote kuu za nyuma yake upigaji kura ulikuwa kati ya asilimia 69 kwenda juu. Hata hivyo CCM ikitumia mbinu zinazoeleweka sana – vitisho, kukatisha tamaa, kufanya upinzani uonekane ni shetani, n.k imefanikiwa sana kukatisha tamaa ya kupiga kura hasa kwa wazee na kina mama. Hivyo, upinzani umekuwa ukitegemea kura za vijana zaidi kuliko za makundi mengine. Kundi hili la vijana sasa ndio ngome kuu ya upinzani nchini; na hawa ni vijana hasa ambao ama walipiga kura kwa mara ya kwanza 2010 au ndio wanapiga kura kwa mara ya kwanza sasa.

Lakini kuna kitu kingine ambacho naamini ni kweli zaidi kuliko hivi vingine na nilikidokeza katika posti yangu ya Facebook mapema leo; CCM inazidi kukataliwa na ahadi zake hazivutii tena kama zamani, vitisho vyake haviogopeshi na utukufu wake hautukuzwi tena. Ni wazi kabisa kuwa kukiwa na Tume huru, na mfumo mzuri wa uchaguzi CCM itapata shida sana kushinda na badala yake inahitaji sana kutegemea dola (polisi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa n.k) kuweza kushinda. Hili ndilo tatizo kubwa sana; CCM ili kujirejeshea uhalali siyo tu ikubali kushindwa baada ya uchaguzi bali ichague njia yenye kuonesha kuwa uchaguzi ni huru na wahaki na hakuna njia nzuri ya kufanya hivyo kama kuhakikisha uhuru wa vyombo na uhuru wa sheria ya uchaguzi.

Hivyo, walichokifanya watu wa Arusha ni kuamua kuicharaza CCM kwenye sanduku la kura; kwani ni hapo tu ndipo sauti za raia zinaweza kusikika vizuri. Hofu ile ya kuwa CCM wataiba kura ni hofu ambayo imezuia watu wengi kupiga kura kwa sababu wanajiambia kuwa ‘CCM itashinda tu' na matokeo yake hawaendi kupiga kura. Watu wa Arusha wamejua nguvu ya kura yao na wanajua sauti yao ni kura yao. Hawawezi kushindana na polisi na usalama wa taifa; hawawezi kushindana na Mkuu wa Mkoa na IGP; lakini wanajua sehemu pekee ambapo wana uwezo wa kushindana ni kwenye kupiga kura. Na hivyo wamejitokeza kupiga kura. Ni kama walipewa fimbo na kuambiwa waende wakawachape CCM na kuwachapa wamewachapa. Haikujalisha nani aliipigia kampeni CCM au jinsi gani CCM ilibebwa, mwisho wa siku (siku ya uchaguzi) uamuzi wa mwisho ni wa mtu mmoja mmoja; watu ambao walishafanya uamuzi wao kwenye fikra wakaenda kuuthibitisha kama kutia sahihi kwenye sanduku la kura.

Wananchi wetu wengi wakielewa nguvu hii kuu waliyonayo na nguvu ambayo inafanya demokrasia inoge watatambua kuwa iwe kwa mbinde au kwa upinde wataenda kupiga kura. Kwamba, haijalishi mabomu, polisi, kejeli au vitisho, ikifika wakati wa kupiga kura wataenda kupiga kura na kusema kile ambacho hawawezi kukisema kwa maneno.

CCM imekataliwa. Na huu ni mwendelezo tu wa yale ambayo tumeyaona tangu 2010. Kazi kubwa ni kuwashawishi mamilioni ya wananchi wengine ambao kwa woga au kutokujua wanafikiri kuwa CCM inatakiwa kutawala milele.
Arusha wamesema hapana na wamerudia kusema hivyo tena na tena. CCM iheshimu uamuzi wa wananchi wa Arusha na iache mizengwe kwani haikisaidii chama kupendwa zaidi; CCM iangalie watu wake wanaoifanyia kampeni kama ni watu ambao wanastahili kuendelea na hilo kwani zaidi ya kuwafanya wapoteze kura, watu hao wamezidi kuifanya CCM ionekane ni kituko na kejeli na kudharaulika. CCM ikiendelea na watu wale wale na mbinu zile zile wapinzani hawana la kufanya isipokuwa kuendelea kucharaza watu bakora ya kura; ndio utamu wa demokrasia.

Hata hivyo yote ni sehemu ya demokrasia; Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye amesema vizuri kuelezea hili katika mtandao wa JamiiForums baada ya kipigo cha Arusha "Kuna watu wameuliza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)".

Tusubiri mtanange mwingine.
 
Nami pia nimeipongeza Chadema kwa ushindi huu mnono wa hizo kata za Arusha.
Ukizama kwa undani kutafuta the motive behind ushindi huu, utakubaliana na mimi kuwa Chadema imeshinda kwa sababu CCM imechokwa hivyo CCM imekataliwa!.

Ushindi kwa sababu adui amekataliwa pia ni ushindi, ila sio sustainable!.

Nimeishauri Chadema, kushereherekea ushindi kwa kujipanga zaidi na zaidi badala ya kubetweka na kukataliwa kwa CCM, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, Chadema itupe sababu ya kukichagua besides watu kuicvhoka na kuikataa CCM!.

Ushindi wenye solid reasons za kwa nini tuichague Chadema, besides kuchaguliwa kwa sababu CCM imechokwa, ndio ushindi sustainable wa kuhalalisha Chadema kukabidhiwa rasmi ikulu ya Magogoni come 2015!.

Ni kwa Chadema to give solid reasons kwa nini tuichague, ndiko kutakakopelekea kada ya watumishi wa umma, jeshi, polisi na wanausalama wetu, kujiandaa kisaikolojia kuitumikia serikali ya Chadema based on the streghths of reasons given besides kuchokwa kwa CCM!.

Na ninaamini hizo sababu zikitolewa na kuwa strong enough, zitatosha kabisa kuwafanya wana CCM, wasiichague tena CCM na badala yake waichague Chadema, hivyo kujikuta inashinda sio tuu kwa kupata support ya wananchi wa kawaida, bali hadi support ya wana CCM wenye bonafide and genuine interest ya Tanzania yenye neema inawezekana!.

Pamoja na pongezi hizi kwa Chadema, mimi mgombea wangu bado ni yule yule na chama kile kile!.

Pasco.
 
Wao wana jeshi, mabomu, risasi, mahakama. Lakini sisi tumewapiga kupitia sanduku la kura
 
Pasco hutakaa ujibiwe hili swali kwani vijana wengi ukiwauliza kwanini wanaichukua CCM na kuipenda CHADEMA hakuna atakayeweza kukupa jibu. Hata kiongozi wa Chadema ukimuuliza kama CCM wanaaamini katika siasa ya Ujamaa na kujitegemea (ilikuwa zamani) wao Chadema wanaamini katika nini vile vile hawawezi kukupa jibu. Kwa kifupi siasa zimekuwa kama mikutano ya walokole ukiona wenzako wanaanguka chini na wewe unaaanguka chini
 
Kaka PASCO nakubaliana na wewe mahali fulani lakini kwa historia hasa katika nchi zetu hizi ambazo Demokrasia ni ya kubembelezea kuchokwa kwa chama tawala inakuwa ngumu sana kurudisha imani kwa wananchi mfano ipo.

Ndani ya CCM kunatatizo ambalo ndilo linaloipelekea kukatatiliwa na wananchi hasa waliopo mjini wenye uelewa na muamko wa masuala ya siasa, tatizo kubwa mbalo linakitafuna chama hiki aidha wanalijua au la lakini hawana ubavu wa kulitatua kwani linahusisha mapungufu ya kimfumo (mambo yaliyozoeleka yakawa ni sehemu ya mfumo).

Mfumo huo umekuwa kama saratani ambayo inakuwa taratibu kadri muda unavyosonga.

Ili CCM wawe imara tena kama CCM tuliichezea Chipukizi ya kutimiza Miaka kumi 1987 lazima wakubali kukifanyia marekebisho ya mfumo huo, na huenda marekebisho hayo yakakikuta chama hicho kinakuwa chama cha upinzani. Hapo ndipo mahali pekee wataweza kujitafakari na kupata ujasiri wa kuondoa saratani hiyo kwani itakuwa wamefika mahali ambapo ni point of no return.

Wakati huu CCM hawawezi kufanya mabadiliko kwani kufanya hivyo ikitwaacha na makovu ambayo hakuna mwenye ubavu wa kuyavumilia watapaurua sana ndiyo maana wanaoona salama yao ni kuyafumbia macho kwanza wakijidanganya kuwa ni upepo tu unapita mambo yatakuwa salama tu kumbe wanajidanganya.

Pasco hutakaa ujibiwe hili swali kwani vijana wengi ukiwauliza kwanini wanaichukua CCM na kuipenda CHADEMA hakuna atakayeweza kukupa jibu. Hata kiongozi wa Chadema ukimuuliza kama CCM wanaaamini katika siasa ya Ujamaa na kujitegemea (ilikuwa zamani) wao Chadema wanaamini katika nini vile vile hawawezi kukupa jibu. Kwa kifupi siasa zimekuwa kama mikutano ya walokole ukiona wenzako wanaanguka chini na wewe unaaanguka chini

Sio kweli Ndachuwa, vijana waliowengi kwa sasa wanaelewa ni kwanini hawaitaki CCM, labda uniambie watwala wa CCM ndio ambao hawajui kwa nini vijana wameichoka CCM au wameamua kupuuzia na kusababisha vijana wengi kutaka mabadiliko. Kwani naamini kama watawala wangeelewa au kukubali hizo sababu basi wangechukua hatua kukirekebisha chama ili kurudisha imani kwa wananchi hasa vijana. Kufahamu tatizo ni hatua moja muhimu katika kuweza kulipatia utatuzi.
Watawala wa CCM wamekazana tu kwenye kujinadi katika yale ambayo wameyafanya kwa takribani miaka 36 ya uhai wa chama, madai yao wananchi hawayaoni maendeleo inabidi waoneshwe! Ndio maana serikali iliwekeza pesa nyingi katika kuelezea mafanikio ya Serikali.
 
Mhe. MM,
Heshima mbele, hata mtoto wako ukiwa unamchapa kila siku, ukumbuke unamwandalia kuwa sugu, anajua baba kazi yake kupiga kelele tu. Ndivyo hali ilivyo kwa chama tawala, badala ya kuelimisha wananchi wao wanatumia maguvu mengi bila kuwaelimisha nini kinaendelea. Kuwadanganya wananchi kuwa upinzani utaleta vujo, mtaona msipochagua ccm na kila aina ya ubaguzi wanawasingizia upinzani kwa kutumia vyombo vya usalama, wakaona kumbe wimbo ndiyo ule ule, ndiyo maana wakaona sasa basi...ndicho kilichotokea ar na kitasambaa kila kona ya nchi. Usambaaji wake utakuwa kwa kasi kama hawata mdhibiti kijana anaejiita msomi class one ya uchumi pale udsm. Chama tawala waendelee kufumba macho..
 
Back
Top Bottom