Somo la CHADEMA Arusha CCM limewaingia?

Somo la CHADEMA Arusha CCM limewaingia?

Somo lipi swahiba? kata nne wewe unaona ni ushindi?. Tulichojifunza ni kitu kimoja tu..nacho ni kujipanga kwa 2015 kwani tumejifunza ni wapi tumeteleza. Ninyi mnayo kazi moja nayo ni kutekeleza zile ahadi zote mlizokuwa mkizitoa majukwaani. Mnapaswa kukumbuka kwamba waliowapigia kura hawahitaji maandamano. Ninataka kuwahakikishia kuwa huu ni mwanzo wa mapambano kuelekea 2015 wakati ambapo sera zenu hazitakuwa na mashiko kwani hata watu binafsi watasimama kugombea.
Mkuu acha kujifariji Mzee Mwanakijiji amelonga vyema hususani hii paragraph; CCM iangalie watu wake wanaoifanyia kampeni kama ni watu ambao wanastahili kuendelea na hilo kwani zaidi ya kuwafanya wapoteze kura, watu hao wamezidi kuifanya CCM ionekane ni kituko na kejeli na kudharaulika. CCM ikiendelea na watu wale wale na mbinu zile zile wapinzani hawana la kufanya isipokuwa kuendelea kucharaza watu bakora ya kura; ndio utamu wa demokrasia.

 
Last edited by a moderator:
Tumetia aibu ya mwaka kwenye uchaguzi wa madiwani arusha,mimi ni mkeleketwa wa chama changu c,c,m.
Kwa aibu hii chonde kusudi tusije angukia pua 2015. Natoa ushauri ufuatao kwa mheshimiwa kikwete.1.kusalimika kwa chama chetu muondoe mwigullu nape wassira nikwazo kwa usitawi wa chama chetu.Mbona wapo watu makini na wenye uzalendo na chama chetu?Hawa ni vinara wa kukipaka matope chama chetu;Zingatia ushauri wa bure bure nimimi mwanachama hai.
 
Nimepapenda zaidi hapa

"...CCM iangalie watu wake wanaoifanyia kampeni kama ni watu ambao wanastahili kuendelea na hilo kwani zaidi ya kuwafanya wapoteze kura, watu hao wamezidi kuifanya CCM ionekane ni kituko na
kejeli na kudharaulika. CCM ikiendelea na watu wale wale na mbinu zile zile wapinzani hawana la
kufanya isipokuwa kuendelea kucharaza watu bakora ya kura; ndio utamu wa demokrasia..."

Wananchi wanapata hasira zaidi pale wapitapo vituo vya mafuta na kukuta ukisomeka:
  • Petrol Tshs 2170=
  • Diesel Tshs 2200=
  • Kerosene Tsha 2190=
 
Ukizama kwa undani kutafuta the motive behind ushindi huu, utakubaliana na mimi kuwa Chadema imeshinda kwa sababu CCM imechokwa hivyo CCM imekataliwa!.

CCM haijachokwa please CCM si chama cha siasa tena ni chama dola hakina siasa nakubaliana na wewe KIMEKATALIWA

Ushindi kwa sababu adui amekataliwa pia ni ushindi, ila sio sustainable!.

Nimeishauri Chadema, kushereherekea ushindi kwa kujipanga zaidi na zaidi badala ya kubetweka na kukataliwa kwa CCM, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, Chadema itupe sababu ya kukichagua besides watu kuicvhoka na kuikataa CCM!.

Ushindi wenye solid reasons za kwa nini tuichague Chadema, besides kuchaguliwa kwa sababu CCM imechokwa, ndio ushindi sustainable wa kuhalalisha Chadema kukabidhiwa rasmi ikulu ya Magogoni come 2015!.

Suala la "sustainability" halipo kwenye siasa, kama ujuavyo kuna masuala yanajiri kwa mda mfupi wa kati na muda mrefu yote yanaiondoa serikali au kuiweka kwa njia ya kidemorasia. Kama ulikuwa na maana ya kuwa na mfumo "sustainable" wa kuendesha chaguzi za kidemokrasia si suala la Chadema bala la taifa zima(ndiyo maana ya zoezi la kuwa na katiba nzuri). Chadema watapimwa kwa kukidhi hoja, matakwa na utayari wa kuwajibika unaowagusa wapiga kura kwa wakati husika. Hayo lazima yabadirike ndio msingi wa siasa za kidemocrasia. Sababu kuu za kutufanya baadhi yetu tuichague Chadema ni:-

Wana maona ya mfumo bora ya namna ya kuendesha siasa nchini kwa kuwa na Katiba Madhubuti. Ina maana wana maono ya kuwapata viongozi wanaokidhi uwakilishi unaotakiwa na wapiga kura.

Kwa kauli zao na matendo yao wamejitofautisha sana na CCM inayojikanganya. Katiba ya CCM ya 1977 haindani na ilani zake na wala ahadi(mikakati yake) zake. Inawezekani ahadi zimetekelezwa lakini hazina uwiano na mahitaji ya wapiga kura.

Sababu muhimu za wananchi 'kuichoka" CCM si kutokuwa na sera na mikakati "sustanable"; bali ni kukinzana kwa katiba na mikakati yake ambayo CCM hawawezi kuzitotelea maelezo ya kushawishi.

Unapenda sana kauli ya kukabidhiwa Ikulu kana kwamba kuna mtu kakaa mahali kazi yake kukabidhi Ikulu. Hayo ni mambo ya kizayuni kuwa Mungu kasema. Kilichopo ni maamuzi ya wapiga kura. Uchaguzi wa Arusha ulikuwa unahusu hilo uamuzi wa wapiga kura. Wapiga waliwahi kumweka Hitler madarani, walimuweka Kennedy madarakani, na kama ni kweli JK kawekwa madarakani na wapiga kura. Je hawa wote wamekidhi vipi matakwa ya wapiga kura wao?

Nashauri uwe na mtazamo mbadala kuwa udhifu wa CCM si uimara wa Chadema mbele ya wapiga kura. Kilichopo ni mfumo upi unaowapa wapiga kura kuichagua CCM badala ya Chadema na kinyume chake ili waongoze na si watawale kama ilivyo sasa.

Na ninaamini hizo sababu zikitolewa na kuwa strong enough, zitatosha kabisa kuwafanya wana CCM, wasiichague tena CCM na badala yake waichague Chadema, hivyo kujikuta inashinda sio tuu kwa kupata support ya wananchi wa kawaida, bali hadi support ya wana CCM wenye bonafide and genuine interest ya Tanzania yenye neema inawezekana!.

Nitashanga sana kama wana CCM wataasi chama chao wanachokiamini kwa kuipigia Chadema. Ni imani yangu watakapoasi watakuwa wamekiuhama chama rasmi; na sitashangaa kama watahamia Chadema. Wakifanya hivyo wataondokana na unafiki lakini watatimiza ukweli kuwa HAKUNA SIASA "STATIC" siasa ni "DYNAMIC". Kwa msingi wa ubaguzi wa CCM kuwa watasimamia support ya wananchi wa kawaida kwa Chadema hilo si sahihi, hata support ya wana CCM wenye bonafide and genuine interest ya Tanzania yenye neema pia haiwezekani!.

Pamoja na pongezi hizi kwa Chadema, mimi mgombea wangu bado ni yule yule na chama kile kile!.

Pasco.

Till death do part you, CCM and your candidate. Congratulations
 
Back
Top Bottom