Naam!
Wako nyoka aina nyingi tu,,, wa nchi kavu na majini kama sijakosea !
Je Nini kifanyike endapo umemuona nyoka ndani, katika harakati za kumthibiti akafanikiwa kukukimbia ?
Ni kweli mafuta ya taa yanamuathiri nyoka ? Kuna dhana kwamba ngozi yake inababuka na hatimae nyoka hufa na kuoza,,, ndio maana nyoka akiingia kwenye shimo huwa tunashauriwa kumwaga mafuta ya taa ?
Kuna dhana pia ukishamjeruhi nyoka lazima ataenda kufa huko aendako ? Hii imekaaje Kuna ukweli? Means ngozi yake haiponi jeraha ?
Kuna ukweli wowote kuwa kipindi Cha baridi nyoka hupendelea Sana kuingia katika makazi/nyumba ya binadamu kwa lengo la kupata joto ?
Kuna lile jiwe unaweka pindi upatapo ajali/umegongwa na nyoka,,,je Nini kinafanyika baada ya hapo ili jiwe liendelee kuwa active kwa matumizi ya baadae ? Linaoshwa? Kuchemshwa kwenye maji ya Moto au likianikwa juani inatosha,, ?
Yote kwa yote nyoka wametofautiana katika sumu zao,,, Kuna ambao Wana sumu Kali Sana ndani ya muda mchache unaweza kufariki !