Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 7,817
- 10,861
Nakumbuka kipindi nasoma shule ya msingi nilikuwa nikiambiwa na wazazi wangu pia na waalimu wangu soma ili upate kazi, nikitoroka shule na kwenda kucheza mpira nilichapwa sana na kuambiwa nacheza na shule maisha yatakunyoosha, nikionekana naimba mziki naonekana mtukutu nacheza na shule maisha yataninyoosha, hakika kila Jambo nililofanya tofauti na masomo ya darasani nilionekana nacheza na elimu.
Hakika tulisisitizwa kwamba soma uje kuwa rubani, daktari, mwalimu, nesi ,mhandisi, mwanajeshi, polisi,mfamasia hakika sikuwahi sikia mwalimu au mzazi wangu akiniambia soma uje kujiajiri na kufanya biashara zako mwenyewe. Labda familia za wafanyabiashara waliambiwa haya.
Dhumuni la bandiko hili ni kuomba kuanzishwa kwa somo ambalo litafungua milango ya fahamu kwa vijana tangia wakiwa wadogo ili watambue vipaji vyao na wakati wao ujao umewandaa kuwa wakina nani?
Mada ambazo inatakiwa ziwepo katika somo ili ni kama zifuatavyo:-
1) Sheria za uanzishaji wa kampuni na usajili wa kampuni nchini..
2) Ujasiliamali.
3)Biashara.
4) kazi unazoweza kufanya na kujiajiri kutokana na taaluma uliyosomea.
5) Jinsi ya kupata mtaji wa biashara.
6) Jinsi ya kutafuta soko na wateja.
7) Michezo , muziki na burudani.
Elimu yetu inatuandaa vijana wengi kutegemea ajira ambazo zinatengenezwa na serikali, ambapo serikali ya awamu ya tano imefeli kutengeneza ajira ni wakati sasa wa kuwaandaa vijana tokea wadogo na masomo ambayo yatatanua fikra zake katika soko la ajira na kujiajiri.
Karibu kwa mawazo yenu,