Kama tungefundiswa somo la madini, tungelikuwa mabilionea

DAMA2025

JF-Expert Member
Dec 30, 2023
338
496
Nchi ya Tanzania ina madini ya kila aina katika sehemu mbalimbali. Kuna madini mengi sana mkoani Geita, na sehemu nyingine za nchi yetu. Kama watunga sera wa Wizara ya Elimu na mawaziri wote wa elimu wangekuwa na ubunifu mkubwa, wangeweza kuanzisha somo la madini katika shule za msingi za Tanzania badala ya kufundisha somo la historia ambalo halina manufaa kwa maisha yetu ya kila siku.

Mfano, tunasoma historia kuhusu Vasco Da Gama, ambayo ni vitu visivyokuwa na manufaa kabisa. Juzi zimeanzishwa kozi za Islamic Knowledge, Divinity, Arabic, na Chinese ambazo hazina impact kubwa kwa Mtanzania. Lakini tukiwa tunafundishwa kuhusu madini ni nini, thamani yake ni nini, na soko lake ni lipi, tungetajirika sana.

Vijana wangemaliza shule za msingi na sekondari wakiwa na ufahamu huo. Pale Tunduru kuna watu wa Sri Lanka wengi sana wanaonunua madini na wana vifaa vya kutambua madini. Inaonekana wamesomea vizuri kuhusu hayo madini na wanajitajirisha hivyo hivyo wakati raslimali ni yetu.

Vijana wengi wa Tanzania wanachimba madini na wanapata, lakini wanatapeliwa tu kwa sababu hawajui thamani ya hayo madini. Mtu anaweza kupata madini yenye thamani ya million 600 na kuyauza kwa bei rahisi ya million 20 kwa sababu hajui thamani yake.

Kwa sasa, Wachina nao wanachimba madini na sisi hatujui kabisa kuhusu hayo madini, hivyo wanufaika watu wa nje tu. Ni muda mzuri kwa serikali yetu chini ya Mama Samia kufikiria juu ya kuwa na masomo kama haya mashuleni, ambayo yatawasaidia wengi na kusaidia kuondoa umaskini wa kujitakia.
 
Ni muda mzuri kwa serikali yetu chini ya, mama Samia kufikiria juu ya kuwa na masomo kama haya mashuleni, ambayo yatawasaidia wengi na kusaidia kuondoa umasikini wa kujitakia.
Mkuu hili taifa lina mikataba ya SIRI ya kibiashara na nchi za ULAYA na MAGHARIBI. Mikataba hio inatuzuia sisi kufanya baadhi ya vitu fulani, ili sisi tubakie kuwa ni WATEJA, na wao waendelee kuwa WAUZAJI.
 
Pana jamaa yangu msrililanka kila mwezi anarudi kwao kupeleka shehena ya madini aliyonunua Bei Chee tunduru yanaenda ongezwa thamani Kisha wanauza ulaya kwa pesa ndefu.
 
Sisi hata tukizipata pesa hiso za madini zaidi ya kufanyia ngono kipi Cha ziada tufanyie.
 
Back
Top Bottom