Soma na utoe maoni yako

noiselessly hunter

JF-Expert Member
Oct 20, 2013
3,426
2,000
Salaam kwa wanabodi,
hivi ikitokea wewe mke au mume kwenu yaani kwenye familia yenu mmeuza nyumba au shamba au kuna mgao fulani wa fedha umepata,may be milioni 5 au kumi au kias chochote kingi.
Je utamshirikisha mume/mkeo kwenye matumizi ya zile pesa zako au utapanga matumizi jinsi unavyojua wewe?
Na mwenza wako atakua na hako yoyote hapo?
Wenye maarifa zaidi watufahamishe.
Faiza foxy mama wa jf,mchango wako unahitajika hapa.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,405
2,000
Inategemea ndoa yenu iko kwenye misingi gani. Kama mnaaminiana na mna mawazo sawa.

Sasa nijue mume ni mlevi mshahara wake mwenyewe haumtoshi na tuna madenibya kodi ya nyumba. Si kher hizo milioni tano nipandishe tofali kama tuna kiwanja nitamwambia ukweli siku ya kuhamia makazi mapya.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
32,760
2,000
Inategemea.

Ila si atajua tu mmegawana kwenye familia yenu? Ukizitumia si atajua pia umezitumia?

Siku naye akiwa na zake akazitumia ipasavyo utafurahi? Kila mmoja akiwa na yake unadhani mnajenga familia ya namna gani? Nimejaribu kuyafikiria tu haya.
 

mbalizi1

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
14,619
2,000
Hii inadhihirisha aina ya watoto na vijana wanaokuzwa ktk familia za sasa ambao ndio Taifa la kesho.

Ndoa ni nini? Tafuta majibu ya swali hilo ndio majibu ya swali lako
 

Sakayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
56,544
2,000
Inategemea jinsi mnavyoishi!
Kuna familia nyingine baba hajui kipato cha mama wala mama hajui kipato cha mume!

Mmoja wapo akipata mgawo wa hivyo sidhani kama atasema!
 

walitola

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
3,456
2,000
Hapo inategemea na mawazo na hakili ya mtu mfano mimi nikipata hizo pesa nitamshirikisha mke wangu kwakuwa mama watoto wangu ana mawazo ya kimaendeleo lakini wanawake wengine utakuta anawaza madela mda wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,627
2,000
Pesa yeyote inayoingia kwny familia ni vema mkapanga pamoja jinsi ya kuitumia haijalishi umeiba au umepewa sadaka
 

noiselessly hunter

JF-Expert Member
Oct 20, 2013
3,426
2,000
Nimejaribu kuleta huo mjadala kwa kuwa kuna jirani rafiki yangu,wameuza nyumba yao,marehemu baba yao aliwaachia nyumba kama 7 hapa bandari ya salama,sasa mgao umepita kalamba jiwe 7 (yaani milioni saba) sasa watu wanampa ushauri mbalimbali,
wengine wanamwambia mkeo hazimuhusu hizo ni zenu fanyia unavyotaka
wengine wanamwambia kapange na mkeo nini cha kufanya,
wengine wanamwambia,kama angekua mkeo amepata za upande wa kwao ungesikia stori tu
jamaa hajui aamue nini..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom