RIP Prof Tarimo. Mungu awape wepesi ndugu, jamaa, marafiki na waSUASO kwa kuondokewa na mwamba huyu.Mzee wetu Prof A.J.P Tarimo aliyekuwa anafundisha "Plant Physiology" amefariki Bwana na walimzika pale nyumbani kwake Wami Dakawa wiki 3 zilizopita.
View attachment 3329644
Hapo unaposema kilianzishwa 1984,Mwanzo kiitwaje?,Kuna mjomba wangu alisoma hapo Kabla!Introduction
Nimeamua kuanzisha uzi huu mahsusi unaohusu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kama njia ya kukienzi chuo hiki kikongwe na cha kipekee nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Awali ya yote naomba ku declare interest kwamba mimi ni mhitimu kutoka SUA miaka mingi iliyopita wakati huo mfumo wa ufundishaji ukiwa wa Term System. Kwa sasa ufundishaji unafanyika kwa mfumo wa Semester System au ukipenda unaweza kuuita Mfumo wa Mwendokasi.
About the University
Kama jina la chuo linavyosadifu, chuo kilianzishwa kwa jitihada na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama njia ya kuzalisha wasomi kwenye fani ya kilimo (ukulima na ufugaji) mnamo mwaka 1984 na kupewa jina la aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, ndugu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kupata taarifa zaidi kuhusu SUA, tembelea tovuti rasmi ya chuo (Welcome to Sokoine University of Agriculture (SUA) )
View attachment 2088281
Nembo ya chuo
Academics
Ili kufanikisha utoaji wa elimu kwa wanafunzi na wadau wengine, chuo kimegawanyika katika colleges 5 na deparments 6 (kwa mujibu wa tovuti ya chuo).
View attachment 2088293
Colleges
View attachment 2088302
Departments
Mwaznoni chuo cha SUA kilijikita kwenye ufundishaji wa masuala ya kilimo tu na kutoa shahada kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor’s degree) na kuendelea mpaka shahada ya uzamivu (PhD) pamoja na kozi fupi lakini kwa sasa kinatoa hadi kozi za astashahada na cheti katika fani mbalimbali. Sasa hivi kinafundisha masuala mengi yakiwemo ualimu, maendeleo vijijini na mwasiliano (tazama kielelezo hapo chini). Kwa hiyo, hiki si chuo cha kilimo tu kama wengi wanavyodhani bali sasa hivi kinajikita kufundisha kozi mtambuka zinazofundishwa katika vyuo vingine vya kawaida.
View attachment 2088303
Kozi zinazofundiswa
Academic facilities
Mojawapo ya hazina ambayo chuo cha SUA kinajivunia ni uwepo wa maktaba kubwa ya kitaifa ya kilimo ijulikanayo kama The Sokoine National Agricultural Library (SNAL) iliyoanzishwa rasmi mwaka 1991. Maktaba hii imesheheni vitabu, journals na machapisho mbalimbali ambayo wanachama wake nchini Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanaweza kuyafikia na kujisomea.
View attachment 2088305
The Sokoine National Agricultural Library (SNAL)
Pamoja na uwepo wa maktaba kubwa ya kimataifa, chuo pia kina kumbi mpya na nzuri za mihadhara tofauti na zile nilizoziacha miaka ile. Kwa ujumla miundombinu na huduma za ufundishaji zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
View attachment 2088307
Kumbi mpya za mihadhara (MLT9 & 10)
Kwa ushirikiano na wenzangu waliosoma na ambao bado wanasoma kwenye chuo hiki kikongwe na maarufu, tutajitahidi kuwaletea upadates mbalimbali zinzohusu chuo kwa kadri itakavyowezekana. Samahani mods naomba uzi huu uwe pinned ili wadau waweze kuupata kwa urahisi.
Nawasilisha.
Pia soma:
![]()
Chuo cha Sokoine (SUA) chashika namba moja Tanzania (Citations)
Moja kati ya kazi kuu za chuo chochote duniani ni TAFITI. Chuo chochote hapa duniani kitaonekana bora kama kina wana sayansi (academicians) bora walio tuliza akili na kuandaa tafiti na ku publish tafiti zao kwenye juornal za kitaifa na kimataifa! Kwa kuongoza kwenye citation ni ishara wazi...www.jamiiforums.com
![]()
Ubora wa elimu unaotolewa SUA, UDOM na UDSM
Habarini za muda wana jamvii kama kichwaa cha habari kinavo jieleza hapo juu kuna tofauti gani wa ubora wa Elimu unaotolewa chuo kikuu cha kilimo morogoro SUA na ile inayotolewa chuo kikuu cha Dodoma UDOM & UDSM hususan katika zile course za kilimo? Binafsi nina wanangu wanasoma course zinazo...www.jamiiforums.com
hapo kabla hakukuwa na SUA, kile chuo kilikuwa ni sehemu ya UDSM, na ile ilikuwa Faculty of Agriculture, Forestry and Veterinary Science. Graduation ilikuwa inafanyika UDSM main campus.Hapo unaposema kilianzishwa 1984,Mwanzo kiitwaje?,Kuna mjomba wangu alisoma hapo Kabla!
Hahahahaha mwalimu wangu huyu pale mazimbu nilimuacha (Allaah amuhifadhi)Ngoja nikutajie mmoja kwanza , Al Akh Ibn Ghulaam unamjua ?
Kivipi mkuu? Nawe kimeharibu future yako? Kimeiharibuje?Hivi hiki chuo bado kipo hakijafungwa tu, mbona nilisikia hakina tija yoyote kwenye nchi hii hivyo wanakifunga
Usije logwa ukampeleka mtoto wako pale unaenda kumvurugia future yake tuu
Wewe ulienda sua kujifunza uafisa ubashiri?Kivipi mkuu? Nawe kimeharibu future yako? Kimeiharibuje?
ulisikia kutoka kwa nani?Hivi hiki chuo bado kipo hakijafungwa tu, mbona nilisikia hakina tija yoyote kwenye nchi hii hivyo wanakifunga
Usije logwa ukampeleka mtoto wako pale unaenda kumvurugia future yake tuu
Inasikitisha sana , nimewasliana na Wanafunzi ambao wapo wanasoma hizo kozi zilizounganishwa wanasikitika sana hali zao. Kuanzia Wanafunzi mpaka MaLecturer wanaona ugumu sasa.Siku hizi elimu ya chuo kikuu imekuwa kama elimu ya sekondari. Inawezekanaje lecturer mmoja afundishe wanachuo 500? Hii ni zaidi ya shule ya msingi.
Madudu yapo mengi ila sitaki kuandika sana naona haitosaidia kitu , maana mimi nimemaliza karibuni .Siku hizi elimu ya chuo kikuu imekuwa kama elimu ya sekondari. Inawezekanaje lecturer mmoja afundishe wanachuo 500? Hii ni zaidi ya shule ya msingi.
Unashauri nini kifanyike kurekebisha hii hali mkuu?Madudu yapo mengi ila sitaki kuandika sana naona haitosaidia kitu , maana mimi nimemaliza karibuni .
Elimu ya bongo 🚮🚮🚮 ukiwa na hela usiruhusu mwanao asome bongo , sisi hatuko siriazi kwenye mambo muhimu.
Suala la kudoji ni ujinga wa mwanafunzi mwenyeweInasikitisha sana , nimewasliana na Wanafunzi ambao wapo wanasoma hizo kozi zilizounganishwa wanasikitika sana hali zao. Kuanzia Wanafunzi mpaka MaLecturer wanaona ugumu sasa.
Inasikitisha sana yaani wasomi wanapanga mambo bila kufanya hesabu ya miundombinu na mazingira kama yanasapoti pamoja na kuwa na vitendea kazi na mifumo Imara ?
1. Mitihani ya test ikisahishwa hairudishwi , na sijui kama Mwalimu anasahisha na test huenda akatoa Moja tu kuepuka kazi.
2. Imagine kwenye field outdoor Mwalimu anawezaje kusimamia practical Wanafunzi 500 , matokeo sasa Wanafunzi wengi wamechukulia fursa wanadoji practical outdoor na kuwakamata ni ngumu.
3. Darasani wengi wanadoji, imagine venue Moja Wanafunzi 500+ plus Mwalimu unawezaje kuControl na kujua hata kwa uchache darasa lako lipo vipi na tabia za Wanafunzi ?
Bongo kilakitu hovyo , SUA Ina mambo ya kiwaki hiki chuo kichunguzwe kila siku Wadau wanalalamika wakina The Spirit of Tanzania na wengine kuhusu mifumo yao serikali ipo kimya