Sokoine University of Agriculture (SUA) special Thread

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
18,126
11,936
Introduction
Nimeamua kuanzisha uzi huu mahsusi unaohusu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kama njia ya kukienzi chuo hiki kikongwe na cha kipekee nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Awali ya yote naomba ku declare interest kwamba mimi ni mhitimu kutoka SUA miaka mingi iliyopita wakati huo mfumo wa ufundishaji ukiwa wa Term System. Kwa sasa ufundishaji unafanyika kwa mfumo wa Semester System au ukipenda unaweza kuuita Mfumo wa Mwendokasi.

About the University
Kama jina la chuo linavyosadifu, chuo kilianzishwa kwa jitihada na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama njia ya kuzalisha wasomi kwenye fani ya kilimo (ukulima na ufugaji) mnamo mwaka 1984 na kupewa jina la aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, ndugu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kupata taarifa zaidi kuhusu SUA, tembelea tovuti rasmi ya chuo (Welcome to Sokoine University of Agriculture (SUA) )

1642605239051.png

Nembo ya chuo

Academics
Ili kufanikisha utoaji wa elimu kwa wanafunzi na wadau wengine, chuo kimegawanyika katika colleges 5 na deparments 6 (kwa mujibu wa tovuti ya chuo).

1642605382243.png

Colleges

1642605493815.png

Departments

Mwaznoni chuo cha SUA kilijikita kwenye ufundishaji wa masuala ya kilimo tu na kutoa shahada kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor’s degree) na kuendelea mpaka shahada ya uzamivu (PhD) pamoja na kozi fupi lakini kwa sasa kinatoa hadi kozi za astashahada na cheti katika fani mbalimbali. Sasa hivi kinafundisha masuala mengi yakiwemo ualimu, maendeleo vijijini na mwasiliano (tazama kielelezo hapo chini). Kwa hiyo, hiki si chuo cha kilimo tu kama wengi wanavyodhani bali sasa hivi kinajikita kufundisha kozi mtambuka zinazofundishwa katika vyuo vingine vya kawaida.

1642605585321.png

Kozi zinazofundiswa

Academic facilities
Mojawapo ya hazina ambayo chuo cha SUA kinajivunia ni uwepo wa maktaba kubwa ya kitaifa ya kilimo ijulikanayo kama The Sokoine National Agricultural Library (SNAL) iliyoanzishwa rasmi mwaka 1991. Maktaba hii imesheheni vitabu, journals na machapisho mbalimbali ambayo wanachama wake nchini Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanaweza kuyafikia na kujisomea.

1642605695914.png

The Sokoine National Agricultural Library (SNAL)

Pamoja na uwepo wa maktaba kubwa ya kimataifa, chuo pia kina kumbi mpya na nzuri za mihadhara tofauti na zile nilizoziacha miaka ile. Kwa ujumla miundombinu na huduma za ufundishaji zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

1642605781551.png

Kumbi mpya za mihadhara (MLT9 & 10)

Kwa ushirikiano na wenzangu waliosoma na ambao bado wanasoma kwenye chuo hiki kikongwe na maarufu, tutajitahidi kuwaletea upadates mbalimbali zinzohusu chuo kwa kadri itakavyowezekana. Samahani mods naomba uzi huu uwe pinned ili wadau waweze kuupata kwa urahisi.

Nawasilisha.

Pia soma:

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,378
3,117
Karibu sana mkuu; tupo pamoja. SUASO oyeee! Shule ya SUA si mchezo aisee. Kupenya kwa akina Kazururu, Kasile na Sembuche si mzaha unaambiwa.
Hahahaaa, kama hao jamaa unawajua basi wewe ni mkongwe mwenzangu!
Kazuzuru bado yupo, Sembuche sijui kama bado anafundisha lakini pia Kasile tulipomaliza miaka ya 2000 katikati baadaye nasikia aliondoka akaenda UDOM.

Enzi kazuzuru anatufundisha alikuwa anafuga ndevu sana ila mwaka jana nimemuona ashaachana na ufugaji wa ndevu
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
18,126
11,936
Hahahaaa, kama hao jamaa unawajua basi wewe ni mkongwe mwenzangu!
Kazuzuru bado yupo, Sembuche sijui kama bado anafundisha lakini pia Kasile tulipomaliza miaka ya 2000 katikati baadaye nasikia aliondoka akaenda UDOM.

Enzi kazuzuru anatufundisha alikuwa anafuga ndevu sana ila mwaka jana nimemuona ashaachana na ufugaji wa ndevu
Enzi Kasile anatufundisha alikuwa anafuga sana kucha. Sijui kama baadaye aliachana na ufugaji kucha au la 😂 😂 😂 😂 😂
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
18,126
11,936
Hahahaaa, kama hao jamaa unawajua basi wewe ni mkongwe mwenzangu!
Kazuzuru bado yupo, Sembuche sijui kama bado anafundisha lakini pia Kasile tulipomaliza miaka ya 2000 katikati baadaye nasikia aliondoka akaenda UDOM.

Enzi kazuzuru anatufundisha alikuwa anafuga ndevu sana ila mwaka jana nimemuona ashaachana na ufugaji wa ndevu
Umewahi kufundishwa na Sembuche? Yule mzee anajua sana hesabu. Ni kichwa!
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
18,126
11,936
Na pikipiki yake ile ya yellow, nadhani ilikuwa Suzuki
Yes. Ilikuwa zuzuki fulani hivi. Ila yule mzee nampa credit anajua hesabu si mchezo. Wakati wa ujana sijui alikuwaje. Ile ni mashine sio binadamu aisee!
 
muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,378
3,117
Pole zake jamani, Mungu amfanyi e wepesi mwalimu wangu wa computer na mtaalamu wa crop pathology
Duh, mzee wa kuvalia suruali juu ya kitovu? Anaumwa nini? Pole zake mwalimu wangu wa annual crops, Mwenyezi Mungu na amponye mja wake!!
 
Mr Spider

JF-Expert Member
Feb 28, 2020
230
359
SUA miaka ya hivi karibuni imeanza kupoa sanaa. Halafu baadhi ya wahadhiri hawabadilishi hata notes, tangu enzi hizo wanafundisha mpaka miaka ya hivi karibuni. Inasikitisha sana
 
muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,378
3,117
Yes. Ilikuwa zuzuki fulani hivi. Ila yule mzee nampa credit anajua hesabu si mchezo. Wakati wa ujana sijui alikuwaje. Ile ni mashine sio binadamu aisee!
Balaa sana mwamba huyo, ndiyo maana jina lilikuwa kubwa hapo chuoni. Hata ambao hakutufundisha tunamfahamu!
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
18,126
11,936
SUA miaka ya hivi karibuni imeanza kupoa sanaa. Halafu baadhi ya wahadhiri hawabadilishi hata notes, tangu enzi hizo wanafundisha mpaka miaka ya hivi karibuni. Inasikitisha sana
Umenikumbusha jambo kuna mhadhiri mmoja anaitwa Dr Sarwatt, (marehemu) alikuwa na motes zake kwenye daftari alizoandika miaka ya 70 lakini bado alikuwa anangangania kufundisha notes hizohizo. Yaani hadi daftari limegeuka kuwa rangi ya njano. Ni shida.

Pia kuna baadhi ya wahadhiri wavivu walikuwa wanaenda kwenye internet wanapakua notes na kuja kutubwagia kama zilizvyo na kutumezesha nzimanzima. Tumetoka mbali sana aisee 🤣 🤣 🤣
 
10 Reactions
Reply
Top Bottom