String Theorist
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 203
- 179
kuna mama mmoja alikuwa anataka kuokoa pesa kwenye kiduka chake, kwa bahati mbaya akaangusha mtoto na huyo mtoto akafa.
zindiko la mlala hoihayo masoko ya mbeya mbona yaungua sana? kulikoni jamaniiii
mkuu hii ni mara ya 15 masoko yanaungua mbeya katika kipindi cha miaka kama 10 hivi, soko la mwanjelwa hii ni mara ya tatu linaungua, soko kuu uhindini limewahi kuungua zaidi ya mara 4, soko matola limewahi kuungua zaidi ya mara 2, wakati soko la mbalizi limewahi kuungua mara 2 ndani ya mwezi mmoja miaka ya mwanzoni mwa 2000, kuna soko la ipinda pia liliwahi kuungua.
Mbaya zaidi matukio yote haya inasemekana yanasababishwa na hitilafu za umeme. Mimi nina mashaka sana na sababu kama hizi, naomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kina juu ya sababu ya masoko ya mbeya kuungua moto.
Kwa taarifa yenu wana jf, hili soko la sido linaloungua hizi sasa ni soko lililoanzishwa mwaka juzi baada ya soko la mwanjelwa kuungua na hivyo manispaa kuamua kulijenga upya. Kwa hivyo kwa sasa hapa mbeya masoko makubwa mawili yamefungwa na yako kwenye matengenezo makubwa baada ya kuungua kwa moto.
Nawaonea huruma wafanyabiashara ambao kila mwaka wanapata hasara. Uwezi amini kinachotokea hapa sokoni sasa hivi....