Soko la SIDO (Mwanjelwa - MBEYA) linateketea kwa moto sasa hivi

naomba mniwie radhi wakuu kama kumbukumbu yangu itakuwa sio nzuri. Nilishaona sehemu fulani humuhumu JF kuwa matokeo ya kuungua soko Mbeya huwa yanatanguliwa na ajali ya ndege. Na juzi kulikuwa na ajali ya ndege.... Na hii ni mara kama ya tatu hivi ambapo kumeshakuwa na matukio hayo yakiwa yanaambatana, yaani ajali ya ndege kwanza kisha moto..... imekaajae hii wakuu?
 
hivi kwa nini lakini mbeya matatizo ya moto huwa hayaishi? tena kwenye masoko tu?ukiuliza source utaambiwa umeme,inatakiwa ufanyike uchunguzi huru, poleni sana wana mbeya
Sio matatizo ya moto tu, ila pia na ajali ya ndege.
Kuna thread ilituma siku nyingi sana ikielezea kuwa kuna uhusiano wa karibu sana kati ya masoko kuwaka moto na ajali za ndege. Juzi ndege imeanguka, leo soko linaungua.
www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/96661-soko-likiungua-mbeya-ndege-zinaanguka.html
 
Hivi ndivyo mambo yalivyo hapa Mwanjelwa sido mbeya leo. Hapo ilikuwa mida ya saa 5 asubuhi. hali ni tete
16092011272.jpg 16092011273.jpg 16092011275.jpg 16092011267.jpg 16092011266.jpg
 

Attachments

  • 16092011269.jpg
    16092011269.jpg
    68.2 KB · Views: 58
Chanzo cha moto hakijajulikana lakini inasemekana ni hitilafu ya umeme
Mkuu BUJIBUJI wadau wa Mbeya wape pole saana kwa hiyo hasara ya kuunguliwa na moto soko letu la Mwanjelwa!!!!! Nakumbuka nilisha wahi kupeleka nazi kuuza pale toka Tanga Pangani!!!!!! Wape pole wafanya biashara wa sokoni hapo!!!!!!
 
Sina kumbukumbu vizuri lakini hili litakuwa ni tukio la pili bila shaka.
Hili ni tukio la tatu, Kwanza soko la mwanjelwa la kwanza ( mahali panapo jengwa sasa), pili soko la uhindini, tatu hili tukio la leo.

Sina uhakika wanasema matukio yote yanaendana na imani za kishirikina!!!!
 
Soko kubwa la CIDO mbeya linawaka moto toka asubuhi na vifaa vya kuzimia moto hamna mpaka dakika soko lote ninaziditeketea
 
<font color="#0000CD"><font size="3"><b>Mkuu BUJIBUJI wadau wa Mbeya wape pole saana kwa hiyo hasara ya kuunguliwa na moto soko letu la Mwanjelwa!!!!! Nakumbuka nilisha wahi kupeleka nazi kuuza pale toka Tanga Pangani!!!!!! Wape pole wafanya biashara wa sokoni hapo!!!!!!</b></font></font>
Salamu za pole zimefika, na wahanga ntawafikishia
 
Daa!!! Ndugu,marafiki na jamaa poleni sana na tu wote katika kipindi hiki hadi mwisho wa nyakati.

LAKINI...

Hii ni fulsa mpya ya sisi sooote kutafakari mustakabari mzima wa maisha yetu let us use this as an opportunity for new heaven.

Coz no matter what we can rise the dead;mind you ones dead is dead...are properties yes we lost,our capitals yes we lost and many more!!!

But is this end of life???HELL NO!!! LIFE must go on...lets think and work positively coz everything gona be okay and coz mbeya has a great opportunity to do wonders in anything and at anytime..BRAVO FOR THAT.

LETS ATTRACT NOW WHAT WE WANT THEN...THERE IS A GREAT THINGS INFRONT OF US DUE TO THIS...

THANKS...nafsi na akili yangu vimesimamisha mwili utafakari vema kabla ya yote.
'YOU HAVE NO CAUSE FOR ANYTHING BUT GRATITUDE AND JOY'.
...the abundance of positive results waitng for us.
NDAGA KYALA...
 
Wadau, nimepata taarifa toka Mbeya kwamba soko jipya la Mwanjelwa linaungua moto hivi sasa....aliye karibu na eneo la tukio atujuze tafadhali...

nipo hapa mwanjelwa hali kimsingi ni mbaya moto umeteketeza vya kutosha mali mbalimbali kwenye maduka. lakini niseme tu pamoja na jitihada za hapa na pale katika kuzima moto huu udhaifu ni wa hali ya juu sana kwa vyombo vyote, yaani halmashauri (kikosi cha fire), jeshi letu la polisi, na mbaya zaidi mpaka wananchi wenyewe imeonekana kuwa kero sana. zoezi limeenda sambamba na uizi/wimbi kubwa la wanyanganyi, maandalizi hafifu (utayari) wa vyombo vyetu, mfano kushindwa kuzuia kundi kubwa la watu na msongamano wa magari kwenye highway, kiasi cha kuzuia hata gari ya zimamoto. pili watanzania kubaki wameduwaa, hata tu namna ya kuchukua hatua ya kuondoa daladala katika stend iliyo jirani na mahala moto ulipo. nadhani imefika wakati vyombo vinavyohusika na usimamizi, uongozi kama wa jiji letu la mbeya kuwajibika mbele ya umma. hasara ni kubwa sana na mara ya tatu sasa na wala hakuna namna viongozi wetu wamechukua hatua kukabiliana na hali hii, kinyume chake wameonekana kuwa watu wenye ziara nyingi za kujifunza miji mingine wangali wakijua kwao hovyo.
 
Hili ni tukio la tatu, Kwanza soko la mwanjelwa la kwanza ( mahali panapo jengwa sasa), pili soko la uhindini, tatu hili tukio la leo.

Sina uhakika wanasema matukio yote yanaendana na imani za kishirikina!!!!

hakuna element ya ushirikina zaidi ya udhaifu mkubwa katika usimamizi wa halmashauri yetu wa kuona soko kama lile haliachwi likijengwa hovyo na pasipo kusipesfy aina ya item za kuuzwa hapo, mfano ni mapipa yaliyokuwa na mabaki ya mafuta kushika moto na hatimaye kulipuka
 
naomba mniwie radhi wakuu kama kumbukumbu yangu itakuwa sio nzuri. Nilishaona sehemu fulani humuhumu JF kuwa matokeo ya kuungua soko Mbeya huwa yanatanguliwa na ajali ya ndege. Na juzi kulikuwa na ajali ya ndege.... Na hii ni mara kama ya tatu hivi ambapo kumeshakuwa na matukio hayo yakiwa yanaambatana, yaani ajali ya ndege kwanza kisha moto..... imekaajae hii wakuu?

upo sahihi mkuu hili limetoke lakini safali hii ilianza ngege kutua porini na ndiyo moto huu mkubwa, ukikumbuka mrehemu akukweti alikuja kuwahani wahanga wa moto by that time siku ya kuondoka ndiyo alipata ajali
 
Kwa mliopo eneo la tukio tungeomba picha zaidi na kama mtaweza pata za vyombo vyetu vya usalama na uokoaji vikifanya kazi tutashukuru zaidi.

Pole kwa wahanga.
 
Kwa mliopo eneo la tukio tungeomba picha zaidi na kama mtaweza pata za vyombo vyetu vya usalama na uokoaji vikifanya kazi tutashukuru zaidi.
Pole kwa wahanga.
Gwa nkaja, faya hawana maji, polisi hawajui wafanye nini, wamebaki kupiga tu mabomu ya machozi. No peace @ all
 
Mbeya huwa hakuna BOMOABOMOA - Wakitaka kujenga soko JIPYA wanachomo moto la zamani!
 
Back
Top Bottom