Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,916
- 30,259
Ndugu yangu Kheri katufanyia hisani kubwa sana.
Kaniletea picha hizi za Kariakoo Market na aliyepiga picha hizi kaweka na tarehe mwaka wa 1955.
Huu ndiyo mwaka TANU ilimsafirisha Mwalimu Nyerere kwenda UNO kuidai Tanganyika.
Angalia hizi picha za soko lenyewe kama jengo kisha inamisha macho yako uwaangalie wafanyabiashara ndani ya soko pamoja na wanunuzi.
Kisha geuza macho yako nje ya soko uangalie maduka jirani ya soko.
Ukimaliza haya yote utakuwa umepata picha kamili ya hali za Watanganyika.
Nje ya soko utakuwa umewaona watu wanatembea miguu peku peku, hawana viatu.
Watu hawa uliokutananao ndani na nje ya soko ndiyo waliokuwa wanachama wa mwanzo wa TANU na wengine bila shaka walinunua kadi zao pale sokoni kwenye himaya ya Market Master Abdulwahid Kleist Sykes na wasaidizi wake wawili, Shariff Abdallah Omar Attas na Mshume Kiyate.