Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,925
- 30,273
OFISI YA TANU ILIVYOKUWA MIAKA YA 1960
Kuna mtu kaniletea picha hii ya ofisi ya TANU kama ilivyokuwa katika miaka ya 1960.
Pamoja na picha hiki kaniandikia ujumbe ananambia kuwa picha hii itanikumbusha mengi.
Kweli na hakika picha hii imenirudisha nyuma sana na imenikumbusha mbali katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Hii nyumba ya kushoto ndiyo ilikuwa ofisi ya African Association na ilijengwa na wanachama wenyewe kwa kujitolea kati ya mwaka wa 1929 na 1933.
Ofisi hii ilikuwa kwenye kona ya Mtaa wa Kariakoo na New Street.
Nyuma ya nyumba hii ilikuwa nyumba ya Bi. Mwamtoro bint Chuma ikipakana ua na ofisi ya TANU.
Nyumba hii ya Bi. Mwamtoro ipo hadi hivi sasa.
Wakati wa kupigania uhuru TANU ilipokuwa inataka kufanya mkutano wa ndani Bi. Mwamtoro alikuwa akivunja ua wake wa makuti kuunganisha ua wa nyumba yake na ua wa TANU ili ipatikane nafasi kubwa.
Ofisi hii ikaja kuwa ofisi ya TAA na ndipo ilipoundwa TANU mwaka wa 1954.
Ilivunjwa ofisi ile ya zamani na ikajengwa ofisi hii kwenye picha kabla ya uhuru mwaka wa 1961.
TANU ilipokea uhuru wa Tanganyika ikiwa kwenye ofisi hii.
Mbali na historia hii ya nyumba ya Bi. Mwamtoro picha hii inanikumbusha wanachama wawili shupavu wa TANU waliokuwa wakiishi jirani sana na ofisi ya TANU - Mzee bin Sudi na Iddi Tosiri.
Mzee bin Sudi ni muasisi wa African Association na alipatakuwa President wake.
Mzee bin Sudi alifariki miezi michache baada ya kutoa risala ya kumkaribisha Rais Nimiery wa Sudan alipotembelea ofisi ya TANU akiwa na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1972.
Iddi Tosiri kadi yake ya TANU ni No. 25 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU mwezi August 1954 uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo.
Mkutano huu ulihudhuriwa na wanachama wasiozidi 20.
Iddi Tosiri na Iddi Faiz ni ndugu na ni binamu kwa Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo.
Ndugu hawa ndiyo waliomchukua Nyerere hadi Bagamoyo kumtambulisha kwa Sheikh Ramiyya.
Lakini kumbukumbu yangu kubwa nikitazama nyimba hii kuwa ndani ya nyumba hii mwaka wa 1962 TANU walikaa watu wawili, Abdul Sykes na Dr. Klerruu kuandika historia ya TANU.
TANU iliamua kuandika historia yake kutokana na mazungumzo kati ya Julius Nyerere, Abdul Sykes, Dossa Aziz na Mwalimu Kihere.
Kazi ya kuandika historia ya TANU ilianza lakini haikukamilika kama ilivyokusudiwa kuwa itakuwa ni mswada ulioandikwa na watu wawili mmoja, Abdul akiwa anaijua vyema historia hiyo.
Abdul Sykes alijitoa kabla ya mswada kukamilika mswada ukakamilishwa na Dr. Klerruu peke yake.
Mswada haukuchapwa kitabu.
Mswada huu wa Dr. Klerruu hakuna ajuaye ulipo wala hakuna ajuaye kabla ya kujitoa Abdul Sykes na Dr. Klerruu walifika wapi katika kuiandika historia ya TANU.
Picha:
Mzee bin Sudi.
Iddi Tosiri na Mwalimu Nyerere na viongozi wa Tanganyika African Parents Association (TAPA).
Iddi Faiz Mafongo kwa kwanza kushoto, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadani Abdu Kandoro, Haruna Taratibu, Dodoma Railway Station.
All reactions:
8Alick Barack Khameecy, Beberu La Mbegu and 6 others