Ipi Historia ya Kweli ya TANU? Sura ya Tatu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
MATATIZO KATIKA USAHIHI WA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

Mwananyamala nje ya nyumba ya Mzee Mwinjuma Mwinyikambi kumewekwa kibao kinachosema kuwa TANU iliasisiwa ndani ya nyumba hiyo tarehe 7 Julai 1954.

Juu ya kibao pameandikwa: ''Kumbukumbu'' na chini yake ndiyo yako maneno hayo kuwa ndani ya nyumba hiyo ndimo ilipoasisiwa TANU.

Bahati mbaya hakuna popote palipoandikwa kibao hicho kimewekwa na mamlaka ipi.

Sina taarifa ni lini kibao hicho kimewekwa lakini toka udogoni kwangu nikimfahamu Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na mkewe bibi yetu Bi. Fatuma bint Agombe mwanamke wa Kingazija.

Bi. Fatuma alikuwa na madrasa hapo nyumbani kwake na akilea watoto yatima.

Mzee Mwinjuma alikuwa mtu maarufu sana pale Mwananyamala na Dar es salaam nzima.

Mzee Mwinjuma alikuwa na ardhi kubwa kuzunguka hii nyumba yake, ardhi iliyojaa miembe na minazi.

Mzee Mwinjuma ni kati ya wazee waliokuwa na sauti kubwa ndani ya Baraza la Wazee wa TANU.

Lakini hili la kuwa TANU iliiasisiwa nyumbani kwake lina tatizo kwa kukosa ushahidi katika historia ya kuasisiwa kwa chama hicho.

Mipango yote ya siasa wakati ule katika miaka ya 1950 wakati wa TAA kuelekea kuundwa kwa TANU ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes aliyekuwa Kaimu Rais wa TAA na Katibu kuazina 1951 - 1953 alipokuwa Kaimu Rais wa TAA, Rais akiwa Julius Nyerere kufuatia uchaguzi wa TAA wa uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 19 April, 1953.

Nyumba hii ya Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu ndiyo nyumba Nyerere alipokutana na Abdul Sykes kwa mara ya kwanza mwaka wa 1952 na ndiyo nyumba alikuja kuishi baada ya kuacha kazi ya ualimu mwaka wa 1955.

Inashangaza kuwa iwe TANU isianzishwe kwenye nyumba hii ije kuanzishwa Mwananyamala nyumbani kwa Mwinjuma Mwinyikambi.

Historia ya TANU imejaa vitendawili vingi sana.

Picha ya kwanza nyumba ya Mzee Mwinjuma Mwinyikambi ikiwa na kibao kinachosema kuwa TANU ndipo ilipoanzishwa hapo.

Picha ya pili nyumba ya Abdul Sykes ambapo harakati za kuundwa kwa TANU zilipokuwa zikifanyika.

Nyumba hii imefanyiwa ukarabati mkubwa lakini sehemu mbili za nyumba hii zilibakizwa.

Sehemu ya mkono wa kulia iliyoko Mtaa wa Sikukuu ndiyo sehemu alipoishi Mwalimu Nyerere kwa miezi mitatu baada ya kuacha kazi na sehemu ya mkono wa kushoto Mtaa wa Stanley ndipo ilipokuwa nyumba kubwa akiishi Abdul Sykes.

Picha ya tatu nyumba ya Abdul Sykes kama ilivyo sasa baada ya kuvunjwa na kujengwa ghorofa.

1706206144434.png

1706206200331.png

1706206239071.png
 
Umewahi kutuambia hizo historia zako zinatusaidia nini? Hasa unapozoleta kwa mlengo wa kidini?
Okw...
Yawezekana hazisaidii chochote.
Kwani hapa hairuhusiwi kuweka post sharti iwe na manufaa?

Nani apimae hiki kina manufaa kiweko hiki hakina manufaa kisiwekwe?

Mrengo wa kidini katika makala ndivyo ilivyokuwa hatuwezi kuibadili historia.

Naona umeghadhibika.
 
Uambiwe nini wakati ni kiherehere chako mwenyewe! Kwani alikuita.
Chifu...
Jambo lolote likitiwa upole litapendeza.

Ndugu yetu kakumbwa na fadhaa.

Ndiyo kawaida ya historia hii inapowadhihirikia.

Hujiuliza kweli haya asemayo Mohamed Said?

Nawaeleza kuwa mtu wa kwanza kufanyiwa dua na TANU alikuwa Rashid Ali Meli, kisha akasomewa Abdulwahid Sykes, kisha Julius Nyerere akasomewa dua Lindi na Sheikh Mohamed Yusuf Badi, kisha ndiyo akasomewa Julius Nyerere nyumbani kwa Mzee Mohamed Jumbe Tambaza Upanga.

Kisha dua ya Mnyanjani, Tanga mwaka wa 1958 kutafuta nusra ya Kura Tatu.

Historia hii inawashtua.

Waislam, Nyerere na dua zao, Waislam, Nyerere na dua zao....

Wanatambua kuwa hivi ndivyo uhuru ulivyopiganiwa.

Huu utambuzi na ukweli wake ndiyo unaowakata maini.

Wanaingia hapa wamekasirika.
 
Mjinga na mpumbafu pekee atakaye endelea kuamini upuuzi na historia za mchongo za mzee huyu islamic propagandist,mwenye mlengo ovu juu ya amani,umoja na mshikamano baina ya watanzania.

Aendelee kupuuzwa.
 
Back
Top Bottom