Ahead
JF-Expert Member
- Jan 11, 2013
- 2,205
- 2,431
Tunaposherekea ushindi wa Yanga jana kuingia robo fainali ya club bingwa,tusiache mbachao kwa msala upitao,Simba alichonga njia kwa machozi na damu kutuonesha ya kwamba inawezekana kushindana na timu zenye misuli mikubwa kibajeti na kimfumo za kaskazini na baadhi za kusini.
Ndipo timu zingine za Tanzania zikaanza kuamka ikiwemo Yanga,Azam fc na Namungo,nimeona mijadala mingi ikiendelea na kuonesha dharau kwa miamba hiyo ya Tanzania inayoongoza mabadiliko chanya ya kisoka kila uchwao na wengine kuigiza au kuboresha,ama hakika kila mwanasoka anapaswa kusema shikamoo simba kwa maana sasa ushindani utaongezeka na hatimae kombe la Afrika litaletwa nchini.
Nb; Masikio hayawezi zidi kichwa.