Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

HAYA WALE WA VIDOLE JUU MNAYAJUA HAYA????

Sijaona mahali Jeetu alipokanusha madai ya mama Sofia.Kukanusha kama angekataa kuwa hajampa Tingatinga 200M na wala kuchangia harusi yake.
 

- Hakuna anaye-divert anything hapa na hutishi mtu na hii mi-ID yako mkuu, Sophia ameongea bila usahidi lakini yeye ushahidi upo wazi kwa kuzaa watoto wanne na viongozi wanne ambao ni waume wa marafiki zake, watoto wapo this is a fact, sasa na wewe tuletee facts za wizi wa Malecela na mkewe hapa tuwahukumu, otherwise acha longo longo peleka hasira zako za maisha huko.

- Mimi ndiye niliyesema kwamba Sophia hafai kuwa waziri wa Takukuru, kwa sababu yeye maadili ya binafsi hana sasa itakua sheria na maadili ya taifa, sasa nielimishe ninacho-divert hapo ni nini? Mimi sitishiki na hii mi-ID yako, muhimu ni hoja na facts ambazo huna! nilitaka kupumzika lakini naona hukubali sasa tuendelee kucheza hii ngoma!



FMEs!
 
Field Maeshal aka Hadija Omari Kopa

Huu ni upumbavu wa hali ya juu

Huyu mama Sophia pamoja na uchangudoa wake katupa kakj data ambacho katatusaida watanzania kuwajua na kuwachunguza wapiganaji.

Yaani kwa vile huyu mama katamka haya maneno bila ya kutoa ushahidi wowote basi mnadai mmepata data!!! No wonder mnadanganyika kirahisi sana.

Mtu anapotoa matamshi mazito namna hii basi hana budi aweke ushahidi wa madai yake wazi ama sivyo itakuwa ni kupakana matope tu!!!

By the way je wewe ni mmoja wao?
 
ID unamaanisha nini? Huna uhakika na unachoongea kabisa. Mie siongelei kwa kujificha na kwa taarifa hilo ndio jina langu. Nitafute unione sifanani kabisa na watu wanaotangaza kazi feki.
Na sina sababu ya kuongea kwa kukwepa. Mie binafsi nawaona woote vimeo tu huyo Sofia na Mengi pia. Sihitaji kwenda kuongea nao ndio niwafaham. Sofia alisaidia kwenye kampeni na pesa za ufisadi na Mengi ni ndumi la kuwili anahubiri kuwasaidia Watanzania upande mwingine anawang'aka. Ni huyu Mengi wa NICOL na anayeng'ang'aniza uanachama CCM huku akijua fika chama kimejaa ufisadi. So whaaat unataka tumuamini. Hakuna anayeaminika kati yao. Tunahitaji kujenga Tanzania mpya
 
 

- Hatuwezi kujenga Tanzania mpya na viongozi kama Sophia, haiwezekani mkuu kiongozi yoyote wa taifa anayejaribu kumsafisha Lowassa ni fisadi kama yeye na hatufai, nilichosema ni kwamba sitishiki na Mi-ID mingi kama siafu humu JF, sasa haya yamekugusaje mkuu na wewe huna mi-ID mingi?

FMEs!
 
Sijaona mahali Jeetu alipokanusha madai ya mama Sofia.Kukanusha kama angekataa kuwa hajampa Tingatinga 200M na wala kuchangia harusi yake.

- vipi ni wapi alipokubali mkuu kwani macho unayo wewe tu, ni wapi Jeetu alipokubali kuwa alitowa hizo hela? acha longo longo! Baba zenu wameiba weee sasa mnataka kila mtu aonekane mwizi, ni lazima uwepo ushahidi sio maneno ya kitchen party!

FMEs!
 
Tanzania mpya si ya kina Sofia Simba. Na hatuwahitaji viongozi wanaoropoka. Vivyohivyo hatuwahitaji watu wanaoendelea kuchangia ufisadi km kina Mengi au wanatumia janja zao kula pesa za maskini. Na hatuna sababu za kuwatetea bali ni kupambana nao na kuwalekeza hatuwahitaji bila kuwaonea haya. Vinginevyo hatuwatendei haki vizazi vijavyo
 
...sasa na wewe tuletee facts za wizi wa Malecela na mkewe hapa tuwahukumu...

....muhimu ni hoja na facts ambazo huna! nilitaka kupumzika lakini naona hukubali sasa tuendelee kucheza hii ngoma!


FMEs!
Kuishiwa kubaya!
Ma Mdogo...una divert hoja...kama alivyosema Mkuu hapo juu. Kama wewe umejikunjuwa kutetea...kuumeni...lete hizo facts ulizonazo za nani alichangia na nani hakuchangia harusi na kampeni za urais za Malecelas...honestly.
Halafu nakushangaa(as per your name, God really Blest you, FMES) na akuzidishie Neemazake,mpka hapo ujuwe au utakapojuwa kuwa kama Sophia kwake itakavyouwa ngumu kumsafisha Lowassa na Chenge, kadhalika ni vigumu kwa Kilango na Malecela,Mwakyembe na wenzao kuwa wasafi katika chama kichafu...hawawezi kuwa wasafi hata.
Zaidi, hizi habari za uchangudoa za Sophia ndo wewe unaona majibu muafaka ya madai aliyotoa...is there any relevance...nawe unaiyona ipo wakati amekubali kuwa wote si wasafi...kwanini unaendele kuwa mkaidi ma mdogo kuwa Kilango na Malecela wamo katika chama kichafu na wao ni wachafu?
 
 
Hiyo ya mi ID tumia means zozote unaweza kupata ushahidi. Ninasisitiza msimamo wangu mie si wa kujificha.
 
Hakuna ubishi kama kuna conflict of interest...unataka sheria gani tena?
Thanks kwa kukiri kuwa na yeye ni fisadi.
Kama vile ilivyokuwa Sophia hana maadili ya kuwa waziri wa TAKUKURU,kwa matatizo binafsi...ndiyo hivyo hivyo, hakuna mwanachama yoyote wa CCM mwenye haki ya kujipa na kujitapa kuwa yeye ni jamadari na mpiganaji wa ufisadi, provided kuwa tumeshakubalia kuwa nyinyi CCM wote ni mafisadi,sawa...,nashukuru Mkuu angalau umenielewa.
 

Mkuu nirudie mara ngapi ndiyo uelewe mkuu?Mbona umekuwa mzito sana kuelewa>?Hayo ya watoto wake wewe/sisi yanatusaidia nini?Magonjwa ya watoto zake au kufungwa kwa watoto zake yanalisaidia vipi taifa la Tanzania afterall hao watoto washakuwa ni watu wazima wenye maamuzi yao?
Unahitaji kipimo cha DNA kuthibitisha madai yako kwamba Sofia kazaa na wanaume wa watu tofauti tofauti na siyo hii mipasho ya mitaani ya kinamama.

Hunijui,Sikujui.Haya embu taja hizo IDs zangu zote ninazotumia hapa.

Mimi siyo Sofia Mkuu na wala sijawahi kukutana nae au kumjua in person.Nimesimama neutral nikitafuta ukweli na sitadanganyika na bla bla za Malecela kuwa Sofia kichaa bila kuja na hoja ya kupangua madai ya bi mkubwa.

Hayatoshi kumsafisha na 200M za Jeetu zilizofadhili kampeni yake 2005.Kwahiyo mfano wako wa Zitto ni kwamba Malecela kamjua Sofia kichaa kuanzia juzi aliposema Jeetu alimpa 200M?Na ikithibitika mirembe kuwa Sofia ni timamu,mzee Malecela atakuja na hoja gani tena ya kutuzuga?Au ndiyo hii ya kuzaa na wanaume za watu?

Mkuu unayo ripoti ya daktari wake kuthibitisha huo ukichaa wa Sofia?

Yah siyo kichaa kwa sababu mpaka sasa sijaiona ripoti yoyote ya kitabibu inayoonyesha kuwa Sofia kichaa.Na wewe utatuthibitishia vipi kwamba siyo kichaa na hizi hoja zako mufilisi?

Hakuna filimbi za mitaani mkuu.Hayo madai yako kuwa mama kazaa na wanaume wa watu ndiyo mipasho ya mitaani isiyo na tija kwa taifa.Mama keshamwaga radhi sasa ni wakati wa wadaiwa kukanusha madai kwa hoja au kumburuza mama mahakamani ili akatoe ushahidi wa madai yake.
Hayo mengine ni nonsense sitapoteza muda kuyajibu.
 


Mkuu usichanganye mazingira na utamaduni.Unajua kashfa katika siasa za Marekani inaweza isiwe issue katika siasa za Tanzania.
Hii kuzaa na wanaume za watu ni sawa na kuzaa na wake za watu au kuwa na vimada na zikisimama kama kashfa katika siasa za Tanzania unadhani ni Sofia tu ndiyo atakaangwa?
 
- vipi ni wapi alipokubali mkuu kwani macho unayo wewe tu, ni wapi Jeetu alipokubali kuwa alitowa hizo hela? acha longo longo! Baba zenu wameiba weee sasa mnataka kila mtu aonekane mwizi, ni lazima uwepo ushahidi sio maneno ya kitchen party!

FMEs!

Hoja iliyoletwa ni kwamba Jeetu amekanusha kuipatia kampeni ya Malecela 200M.Wakati ukiisoma hiyo habari,hukuti kitu kama hicho.Sasa mimi sikuja na hoja kuwa Jeetu amekubali.Na la msingi siyo kwa Malecela kumsubiria Jeetu akanushe madai ya mama Sofia.Jeetu alishasema yeye siyo mwanasiasa.Sasa ni high time kwa Malecela kusimama kwa miguu yake na kuuambia umma kwamba kampeni yake haikudhaminiwa na Jeetu na wala haikuwa na pesa za kifisadi.
 
kula tano dada
watu wengine bwana Hujakiona kitufe kimeandikwa Thanks hapo chini?
Aliyekuambia mimi Dada nani? Kwani wewe Nyani? Sio jina wala Avatar ya mtu inakutabulisha jinsia yake kama ambavyo wewe siwezi kuhisi kuwa utakuwa Kima kutokana na jina lako
 
FMES,
Kwakuwa tumefika pahala tumekubaliana kwa hoja...CCM wote si wasafi,nimalizie kwa nukta moja tu, si wananchi wote wa Tanzania wachafu kama ilivyo CCM...ktika Bunge la Tanzania kuna Vyama vingine ambavyo vinawakilisha sehemu ndongo ya Watanzania ambao wamekubali kujitenga na uovu huo wa CCM (mim nikiwa mmoja wao), sasa hili kundi kubwa lililobakia,aidha kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha wa hali halisi ya nchi inavyopelekwa songombingo na genge la wezi(CCM)...wamebaki kuona kuwa bado CCM ni chama kile kile kilicholeta uhuru kumbe hali imebadilika na wao ndo wahanga wa vita vya ulaji ndani ya CCM..kama tunavyoshuhudia...wenye tonge kubwa...wanapambana na wadokozi...waroho wa kutowea...wanawasakama waliokwamwa na miiba kooni..walioshiba wanashindilia kwa maji.
MKUU WANANCHI HAWATAKUWA WAPUMBAVU SIKU ZOTE IPO SIKU WATAJIUNGA NASISI WACHACHE TUNAOONA KUWA CCM IMECHOKA INAHITAJI KUPUMZISHWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…