Ndugu Mengi angetusaidia sana kama angekuja na majibu ya maswali aliyoyatoa bwana Mayega badala na yeye kuendeleza mipasho
Majina yao mazito. Wengine mwanzoni sikuwasikia, ningewasikia nisingepanda mbegu zangu pale kwa kuwa wamezoea kujiuzulu. Lakini tumeambiwa kuwa mwana mwema Reginald Mengi, ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya NICOL akiwa na waziri wa zamani aliyejiuzulu, Iddi Mohammed Simba.
Ningependa kujua je, ni kweli ndugu Mengi alihusika katika kuiingiza NICOL kichwa kichwa kwa ununuzi wa Pharmacetical and Beverage Limited (IPBL) iliyokuwa inafilisika kwa kutumia fedha zetu kiasi cha sh bilioni nne?
Sijui kiwanda hiki ni cha nani na sijui kuna uhusiano gani, lakini ni matumaini yetu kuwa bwana Reginald Mengi atatokeza hadharani kutufafanulia jambo hili ili kulinda hadhi yake katika nchi hii. Fundo lililojaa katika mioyo ya wanahisa juu yao kwa ufisadi huu ni hatari kwao kuliko sumu ya nyoka.
Chanzo: Tanzania Daima
Leo Mzee Mengi kakutana na waandishi wa habari (dakika chache zilizopita) na hiki ndicho alichoongea:
TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI
6 NOVEMBA, 2009
_____________________________________________
Ndugu Wanahabari,
Kwa msemo wa kiingereza Dont argue with a fool because people may not know the difference between you and the fool, wenye maana kwamba usibishane na mjinga kwa sababu watu wanaweza kushindwa kufahamu tofauti yako na huyo mjinga!
Hata hivyo wakati mwingine inakulazimu kujibu hoja unapomwona mtu anapotosha mambo kwa makusudi.
Kwanza, kuhusu kuropoka kwamba sitoi misaada kwa CCM, hilo ni jambo linalozushwa na watu binafsi na kwa malengo binafsi. Viongozi wakuu wa CCM ambao ni waadilifu na wanaosimamia ukweli wanajua undani wa jambo hili.
Pili, kuhusu uwanachama wangu wa CCM:
Napenda kuwaambia kwamba mimi ni Mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni Na. B124595, iliyotolewa na Tawi la Kisutu, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Hivyo basi madai yote kwamba mimi si mwanachama au nilijiunga na chama hivi majuzi kama inavyoelezwa na Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora Sophia Simba, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Shaaban Kilumbe Ngenda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM John Guninita ni uongo, uzushi na umbea wenye lengo la kudhoofisha juhudi za viongozi wa juu wa CCM na baadhi ya wanachama za kupiga ufisadi vita.
Ndugu Wanahabari,
Hawa wanaodai kuwa ndani ya CCM hakuna kiongozi msafi ni wazi kwamba wamedandia chama hiki hivi majuzi. Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM.
Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza. Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.
Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.
Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.
Reginald A. Mengi
MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.
Huyu mama anajiamini nini,wasije mkolimba bure???
lakini mimi naona huyu mzee anamis-use media zake!anaentertain public quarrels!
"Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM"
Mkuu Geof hivi Press Conference si waandishi wote wanaruhusiwa kufika ama ni wale wa IPP tu?
hata mimi simuelewi huyu mzee!Yaani kuthbitisha yeye ni mwanachama wa CCM kunahitaji kuitisha press conference? Kweli sasa hizi PC hazina maana tena.
Why all these defensive measures now Mzee Mengi? au kwa kuwa brigade lako lote limteketezwa kule Dodoma na hii ndio namna fulani ya ku surrender?
Unalo hilo unatafuta pa kulitulia zigo lako.
naomba nimpe saluti mzee Mengi kwa kuzungumza mambo machache lakini ya msingi.Sijui Auntie Sophie atasemaje akija kujua kuwa Mzee tangia 77 ana kadi mkononi! Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza
Leo Mzee Mengi kakutana na waandishi wa habari (dakika chache zilizopita) na hiki ndicho alichoongea:
TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI
6 NOVEMBA, 2009
_____________________________________________
Ndugu Waandishi wa habari,
Nimewaita hapa leo kuzungumza nanyi kwa lengo la kuweka rekodi sawa.
Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza. Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.
Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.
Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.
Reginald A. Mengi
MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.
It is the high time that we hear something from JK himself
hata mimi simuelewi huyu mzee!
Yaani nchi hii bwana.
Sasa kama hauchangii CCM unakosa nini?si bora ukae kimya
unachngaia CCM ili iweje?yaani mie nilishachoka kabisa na wafanyabiashara wa kibongo..ufisadi tu na hakuna cha kamanda wala kamandoo..
Vita ya Mengi na Mama simba ni kuhusiana na nini?yule mama wa mipasho lzima tamlipua Mengi tu
hayo ni maoni ya Mayega binafsi akitimiza haki yake ya kujieleza. Mengi mara zote hujitokeza hadharani akiona kuna umuhimu wakufanya hivyo, hii ni hekima kubwa, maana sikuja tu kutoa majibu kwa hoja zisizo nz mashiko.Ndugu Mengi angetusaidia sana kama angekuja na majibu ya maswali aliyoyatoa bwana Mayega badala na yeye kuendeleza mipasho