zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,039
- 28,689
UTANGULIZI
Tokea tumepata uhuru bara letu la Afrika tumekuwa na changamoto zinazofanana ambazo sio tu zimetuacha maskini bali tumerudi nyuma kimaendeleo kuliko hata kipindi cha ukoloni. Na matatizo haya yameshazoeleka kiasi kila mtu haoni kama yana ufumbuzi na wanabuni msemo "Miafrika ndivyo tulivyo".
Mara nyingi watanzania tukiwa na changamoto mfano za umaskini,ufisadi,ukame,magonjwa ilihali tuna rasilimali zote muhimu, huwa tunakimbilia kulaumu "mfumo" wa jamii kuwa Afrika nzima mambo kama demokrasia au utawala bora hatuuwezi sababu "ndio tulivyo" hivyo haiwezi kubadilika "mpaka kiama".
Hii excuse imetumika sana kutucheleweshea mabadiliko ya kiuchumi,kiutawala na kijamii lakini kwa nchi za wenzetu ambazo zilikuwa na matatizo ya kimfumo kama haya waliweza kuyabadilisha na leo hii jamii zao zimebadilika sana kwa sababu ya mbinu chache tu na ntatumia case ya nestle kutoka Quora kufikisha ujumbe.
NESTLE
Miaka ya 1970 kampuni ya kimarekani Nestle inayotengeneza snacks kama chocolate,kahawa,maziwa n.k ilitaka kupanua biashara zake na kuingia Japan. Kigumu ni kwamba jamii ya japan haikuwa imezoea kahawa bali chai hivyo ilibidi ufanyike utafiti namna gani wataweza teka soko.
Baada ya tafiti kadhaa wakagundua kuna watu wachache wamependa ladha ya kahawa hivyo wakajiridhisha wakianzisha migahawa ya kahawa italipa.
Baada ya miezi kadhaa ikaonekana Japan haikupenda kahawa maana imezoea chai hivyo kiufupi biashara ikawa imeingia hasara kubwa sana kuliko ilivyotarajiwa.
Ili kuokoa jahazi ikabidi nestle ije na mpango mkakati wa kuleta mabadiliko ya soko lake japan na sio tu walimuajiri mwanasaikolojia kama Mkuu wa Idara ya masoko bali waliamua kulenga soko tofauti kabisa kwa kuja na bidhaa tofauti.
Nestle walilenga watoto ili kuwaandaa kama soko lao la kesho. Walifanya hivyo wakiamini kama jamii ya sasa imegoma kubadilika kupenda kahawa basi tunaweza fanya jambo leo ili jamii ya kesho ibadilike.
Waliingiza sokoni pipi za kahawa za aina zote ili kuwazoeza kuhusu ladha ya kahawa, na miaka 10 baadae wakaanza ona matokeo chanya kwa ''jamii'' mpya kuanza kushambulia vikombe vya kahawa na biashara yao ikawa na faida kubwa kwa mauzo kupaa.
FUNZO
Hapa tunajifunza kwamba jamii inaweza kubadilishwa kabisa mtazamo,tabia,haiba na maamuzi maana makuzi ndio kila kitu.
Mfano tatizo la ufisadi kama tokea udogoni katuni zitengenezwe za kuonesha mafisadi ni maadui wa taifa. Hata nyimbo za watoto ziimbwe hivo kama ambavyo tunatumia nguvu kuwakaririsha kuhusu Allah ni mzuri na shetani ni mbaya huko sunday school na madrassa then trust me tungejikwamua hapa tulipo.
Hapa kati nikikatiza uswahilini nikakuta watoto wa miaka chini ya 7 wanaimba nyegezi.... Wengine wanajifanya wanapigana kung fu. Nikajua ni influence ya mambo wanayoyaona kwenye makuzi ndio yanatufikisha taifa letu hapa lilipo.
So tutapiga kelele sana kuwa tabia ni chafu,vibaka wengi,magaidi kuongezeka,ufisadi,madikteta n.k huku Afrika lakini hatujui kiini ni sisi wenyewe tunataka tubane huku juu kwa kuweka sheria kali,kukamata mashoga,kuchoma moto wezi huku tunasahau mizizi ndio iliyooza sio tunda.
MASHIRIKA YA INTELLIGENTSIA
Nchi zetu za Afrika ziache kutumia mashirika ya intelijensia kumaliza wanasiasa au kufanya ''umbea'' tu nchi jirani kuna nini kinaendelea bali watumie muda huo kupandikiza mbegu njema kwenye jamii yetu na hata wanaweza kwenda mbali zaidi na kupandikiza bidhaa zetu kama korosho au mbaazi kupendwa nchi jirani kwa kutumia mbinu za kijasusi ili miaka ijayo tupate soko la uhakika la mazao yetu. Tukifanya haya jamii na uchumi wetu utapaa kuliko kutumia nguvu kudhoofisha wapinzani wako kisiasa.
Kama wanataka sera zao zifanikiwe iwe Tanzania ya viwanda, kupunguza mimba mashuleni,UKIMWI, kuongeza ufaulu masomo ya sayansi n.k kitengo waanze kubuni mikakati ya kuwapatia "pipi za kahawa" watoto wetu ili baadae wakue wakiwa kama ambavyo kitengo wanataka na tutaona mabadiliko kwenye jamii yetu na Afrika nzima.
Naomba kuwasilisha tafadhali