"Intelligence Spinning" na kilichopo chini ya uongozi 'kwa mifano!'

Thinker96

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
347
Reaction score
135
"Intelligence Spinning"
Ni uwasilishaji wa taarifa za kiintelligensia kwa namna iliyopindishwa kwa maslahi ya umma au viongozi.

Yaani kuna taarifa ni kwa ajili ya kuubhagaza umma ili uamini kitu na pia kuna taarifa nyingine zinabhagaza viongozi ili waone wako sawa na salama.

Taarifa inayofanyiwa "spinning" inakuwa ya ukweli kabisa ila uwasilishaji wake ndo unakuwa wa uongo. Mfano "Tumepokea taarifa ya maandamano ya ..... ila kwa taarifa za kiintelligensia kutakuwa na uvunjifu wa amani", na viongozi pia huwanyiwa spinning kwa kupindishiwa taarifa hasa ikiwa parallel state ndo kabisa anaweza akatishwa kwa taarifa za kawaida na kuonekana kubwa ili akae kwa tahadhari na vitu vingine vya kimkakati asifanye kwa ukaribu.

Ila kuna mambo ambayo mara nyingi wengi wetu hudhania ni spinning kumbe sivyo ila malengo yake hutarget umma au uongozi na hitimisho la mlengo ni kama spinning inavyohitimisha mambo hayo ni kama:-

1. Diversionary politics (Siasa za mkwepo)
Kutengeneza issue nyingine ili kuutoa umma au utawala kwenye issue iliyokuwepo awali huenda ilikuwa nzuri au mbaya. Mfano kunakuwa na habari za kuhusu masuala ya uchaguzi watu wamewaka moto kweli kweli wanaweza kuhatarisha usalama inaletwa issue ya udini inapewa promo watu wanahama na wasipo hama wanagawanyika basi issue ya awali inakuwa imepunguziwa nguvu au imeondolewa hatari iliyodhaniwa.

2. Distraction tactics (Mkakati haribifu)
Hii ni ile hali ya kuondoa mtazamo wa umma kwa nguvu bila kuwa na hoja mbadala mfano umma unataka taarifa fulani ambayo itajenga sifa mbaya kwa nchi viongozi wanagoma kutoa hiyo taarifa kwa kutoa sababu isiyo na mashiko kwa umma.

3. Agenda setting/Agenda manipulation(Kuibalaghaza agenda)
Hii ni ile hali ya kuongoza yale ambayo umma unaongea kwa sana kwa kuyapindisha au kuyatengenezea tafsiri ngumu kwa umma kwa mfano " Umma unadai haki moja wapo ni haki ya kuishi ila wataalamu wa kumanipulate wanaishi kwenye hiyo hiyo ajenda wanakuambia unapodai haki hakikisha umetimiza wajibu kumbuka haki inayodaiwa na umma ni haki ya kuishi ila unaambiwa utimize wajibu"

4. Smoke and Mirrors(Moshi na Kioo)
Yaani moshi ukionekana kwenye kioo ni jitu kubwa sana ni kama linashikika hii imekaa hivi kuanzisha mambo madogo ambayo yanachukua nafasi ya mambo makubwa ili kutoa watu kwenye ufuatiliaji wa mambo makubwa. Mfano mambo ya wasanii na michezo yanaweza kupewa nafasi kubwa ilhali kuna mambo ya nchi yanatokota na ni makubwa hayana nafasi, inch fulani deni lipo Trillions za Shilling za kwao 12 ila wao mameshika masuala ya ukabila na upendeleo kwenye vyeo.

5. Red herring (Sill nyekundu)
Hii ni ile hali ya kuiondoa jamii kwenye hoja za kipaumbele kwa kuanzisha hoja mbadala ambazo zitaitoa jamii katika kelele za hoja zao za msingi mfano Goldberg Scandal kwenye nchi hiyo walisema kuna watu wanatengeza taarifa ili kujinufaisha kisiasa na kulichafua kabila fulani, Cashgate scandal kwanini watu mnatengeza hoja za uongo kwa ajili ya minajili ya kisiasa, kuna Scandal ilikuwepo babu wa Loliondo alichukua front page.

Sababu ya kufanya hivyo huenda ikawa:-

1. Kuhalalisha maamuzi ya serikali.
Mfano: kuhalalisha vita, operesheni ya usalama, au sheria mpya.

2. Kuepusha hofu kwa wananchi.
Wakati mwingine ukweli hufichwa au hupunguzwa ili watu wasipate hofu.

3. Kushawishi maoni ya umma.
Kufanya tishio lionekane kubwa au dogo ili watu waunge mkono hatua fulani.

4. Kulinda vyanzo vya taarifa.
Kuepusha kufichua majina ya watoa taarifa au mbinu za kijasusi.

5. Propaganda / taswira ya kisiasa
Kuifanya taasisi au upande fulani uonekane sahihi zaidi ilhali wamefanya sawa au si sawa lakini hulazimishwa kuonekana ni sawa hata kama ni ufisadi wizi ubadhilifu na mengineyo mabaya kwa maslahi ya umma.

Kama kuna lolote unaliona linaendelea kwa pamoja tunaweza kusaidiana kulichambua na kuliweka katika kundi lake kuwa hilo lipo mlengo gani kama ni kweli au ni mbinu za kuingizana maboya

Nipo tayari kurekebishwa na kueleweshwa zaidi karibuni kwa maoni na kila linalotokea tutaarifiane na kulichambua
 
sahihi, Hili la kutolewa kwenye reli kwa ujinga wowote ni ngumu sana karne hii.
Mkuu ukipigwa "Persuasion principle" vizuri unatoka kwenye reli kabisa na unakuwa mkali
Wakikamata angle ndogo kabisa hizi kwa kuanzia:-
Nini unaamini?
Kwanini unaamini huko?
Kipi unaogopa kupoteza?
 
"SCOPE OF SPINNING DOCTOR(S)"

-Mbinu zinazotumiwa na nchi za dunia ya tatu ni nyepesi sana ukilinganisha na wenzetu wa dunia ya kwanza.

naomba kuuliza "JIRANI YETU ZAKAYO/KASONGO ALIMALIZAJE NDG GEN Z?
 
Kwa maoni yangu binafsi ni kwamba lile suala lilikuwepo la GenZ pale kwake na hasa lilipinga fiscal policy(treasury bill) ambazo zilikuwa zipitishwe na Bunge na zingewaumiza wafanyabiashara wakubwa na raia wa kawaida ila lingeimarisha serikali ndo maana ingawa hawakuwepo viongozi wa kuonekana lakini nyuma yake kulikuwa na akina Bilionea Jimmy Wanjigi, na wengineo na kumaliza aliondoa muswada huo bungeni haukuendelea
 
"Intelligence Spinning"
Ni uwasilishaji wa taarifa za kiintelligensia kwa namna iliyopindishwa kwa maslahi ya umma au viongozi.

Yaani kuna taarifa ni kwa ajili ya kuubhagaza umma ili uamini kitu na pia kuna taarifa nyingine zinabhagaza viongozi ili waone wako sawa na salama.

Taarifa inayofanyiwa "spinning" inakuwa ya ukweli kabisa ila uwasilishaji wake ndo unakuwa wa uongo. Mfano "Tumepokea taarifa ya maandamano ya ..... ila kwa taarifa za kiintelligensia kutakuwa na uvunjifu wa amani", na viongozi pia huwanyiwa spinning kwa kupindishiwa taarifa hasa ikiwa parallel state ndo kabisa anaweza akatishwa kwa taarifa za kawaida na kuonekana kubwa ili akae kwa tahadhari na vitu vingine vya kimkakati asifanye kwa ukaribu.

Ila kuna mambo ambayo mara nyingi wengi wetu hudhania ni spinning kumbe sivyo ila malengo yake hutarget umma au uongozi na hitimisho la mlengo ni kama spinning inavyohitimisha mambo hayo ni kama:-

1. Diversionary politics (Siasa za mkwepo)
Kutengeneza issue nyingine ili kuutoa umma au utawala kwenye issue iliyokuwepo awali huenda ilikuwa nzuri au mbaya. Mfano kunakuwa na habari za kuhusu masuala ya uchaguzi watu wamewaka moto kweli kweli wanaweza kuhatarisha usalama inaletwa issue ya udini inapewa promo watu wanahama na wasipo hama wanagawanyika basi issue ya awali inakuwa imepunguziwa nguvu au imeondolewa hatari iliyodhaniwa.

2. Distraction tactics (Mkakati haribifu)
Hii ni ile hali ya kuondoa mtazamo wa umma kwa nguvu bila kuwa na hoja mbadala mfano umma unataka taarifa fulani ambayo itajenga sifa mbaya kwa nchi viongozi wanagoma kutoa hiyo taarifa kwa kutoa sababu isiyo na mashiko kwa umma.

3. Agenda setting/Agenda manipulation(Kuibalaghaza agenda)
Hii ni ile hali ya kuongoza yale ambayo umma unaongea kwa sana kwa kuyapindisha au kuyatengenezea tafsiri ngumu kwa umma kwa mfano " Umma unadai haki moja wapo ni haki ya kuishi ila wataalamu wa kumanipulate wanaishi kwenye hiyo hiyo ajenda wanakuambia unapodai haki hakikisha umetimiza wajibu kumbuka haki inayodaiwa na umma ni haki ya kuishi ila unaambiwa utimize wajibu"

4. Smoke and Mirrors(Moshi na Kioo)
Yaani moshi ukionekana kwenye kioo ni jitu kubwa sana ni kama linashikika hii imekaa hivi kuanzisha mambo madogo ambayo yanachukua nafasi ya mambo makubwa ili kutoa watu kwenye ufuatiliaji wa mambo makubwa. Mfano mambo ya wasanii na michezo yanaweza kupewa nafasi kubwa ilhali kuna mambo ya nchi yanatokota na ni makubwa hayana nafasi, inch fulani deni lipo Trillions za Shilling za kwao 12 ila wao mameshika masuala ya ukabila na upendeleo kwenye vyeo.

5. Red herring (Sill nyekundu)
Hii ni ile hali ya kuiondoa jamii kwenye hoja za kipaumbele kwa kuanzisha hoja mbadala ambazo zitaitoa jamii katika kelele za hoja zao za msingi mfano Goldberg Scandal kwenye nchi hiyo walisema kuna watu wanatengeza taarifa ili kujinufaisha kisiasa na kulichafua kabila fulani, Cashgate scandal kwanini watu mnatengeza hoja za uongo kwa ajili ya minajili ya kisiasa, kuna Scandal ilikuwepo babu wa Loliondo alichukua front page.

Sababu ya kufanya hivyo huenda ikawa:-

1. Kuhalalisha maamuzi ya serikali.
Mfano: kuhalalisha vita, operesheni ya usalama, au sheria mpya.

2. Kuepusha hofu kwa wananchi.
Wakati mwingine ukweli hufichwa au hupunguzwa ili watu wasipate hofu.

3. Kushawishi maoni ya umma.
Kufanya tishio lionekane kubwa au dogo ili watu waunge mkono hatua fulani.

4. Kulinda vyanzo vya taarifa.
Kuepusha kufichua majina ya watoa taarifa au mbinu za kijasusi.

5. Propaganda / taswira ya kisiasa
Kuifanya taasisi au upande fulani uonekane sahihi zaidi ilhali wamefanya sawa au si sawa lakini hulazimishwa kuonekana ni sawa hata kama ni ufisadi wizi ubadhilifu na mengineyo mabaya kwa maslahi ya umma.

Kama kuna lolote unaliona linaendelea kwa pamoja tunaweza kusaidiana kulichambua na kuliweka katika kundi lake kuwa hilo lipo mlengo gani kama ni kweli au ni mbinu za kuingizana maboya

Nipo tayari kurekebishwa na kueleweshwa zaidi karibuni kwa maoni na kila linalotokea tutaarifiane na kulichambua
Kwa watu.smart.hivi vyote havifanyi kazi..kwa lugha ya pamoja vinaitwa mental manipulation
 
Na walikaa meza moja na wanjigi
Kumbuka wanjigi alikuwa ni mmoja wa underground financial supporter wa kasongo wakati wa kampeni zake.

NB: baada ya pascal mayala, nimekupata wewe kuna kitu unacho tena syo kidogo
 
1. Wameona wanaharakati hawana hoja zaidi ya kusubiri makosa ya serikali. Kwa hiyo kwa sasa zinafanyika obvious mistakes na wao kama headless chickens wanayavamia na kuyajadili kwa muda mrefu. Kinachotokea hapo, ule moto wa mwanzo unapozwa kwa sababu kwa serikali, ni kheri kuongelewa kwenye vijora vya wakatholiki kuliko ile massacre..

Ni sawa walivyojadili AI ya ile speech kuliko return ya Gwajima

Na hapa njia bado ni nyingi. Ila kwa mtu mwenye akili atajua tu they, are slowly winning.

Lakini hii itakuwa succesful kama hapo kati hakutotokea issue kubwa ya kukumbusha
 
Kwa watu.smart.hivi vyote havifanyi kazi..kwa lugha ya pamoja vinaitwa mental manipulation
Sawa Mkuu hao watu smart wapo nchi gani tunaweza kutafutiza na mifano yake huenda tukapitia hata mafaili kama ya Panama Papers, Snowden leaks, Mar-a-Lago tuangalie hao na usmart wao walihandle vipi kwa kukwepa Persuasion.
 
Nepal na Madagascar
 
1. Wameona wanaharakati hawana hoja zaidi ya kusubiri makosa ya serikali. Kwa hiyo kwa sasa zinafanyika obvious mistakes na wao kama headless chickens wanayavamia na kuyajadili kwa muda mrefu. Kinachotokea hapo, ule moto wa mwanzo unapozwa kwa sababu kwa serikali, ni kheri kuongelewa kwenye vijora vya wakatholiki kuliko ile massacre..

Ni sawa walivyojadili AI ya ile speech kuliko return ya Gwajima

Na hapa njia bado ni nyingi. Ila kwa mtu mwenye akili atajua tu they, are slowly winning.

Lakini hii itakuwa succesful kama hapo kati hakutotokea issue kubwa ya kukumbusha
Mkuu,
Wanaharakati nao kweli wanashere huwa wanachezeshwa na wakikaa vibaya wanacheza kweli lakini pia hata wasio wanaharakati watu wa kawaida wakiinua hisia kali zenye kuleta uhatari kwenye usalama mwendo ni lazima njia moja itumike hapo ili kuwadhoofu mfano ukikumbuka kipindi cha nyuma kulikuwa na tabia ya migomo ya wafanyakazi ila mbinu moja ilitumika kwamba wanaogoma waorodheshe majina yao na serikali kama mwajiri mkuu ana nafasi ya kuwafuta wote kazi watakaorodhesha majina hiyo kwa raia wa kawaida wanajua ugumu wa maosha wataogopa tu kufanya hivyo na kama wakifanya watagawanyika hawatakubaliana...
 
Nepal na Madagascar
Nepal na Madagascar kote huko walifanya agenda setting yaani hao wanaharakati walileta agenda mbadala zilizowatoa watawala kwenye utawala na kuingiza utawala mpya yaani yale matakwa ya hawa wapya sio kwamba yanawezekana la hasha ila wamemanipulate agenda za serikali iliyokuwepo na kuleta agenda mbadadala kumbuka kuwa hata Andry Rajoelina alimtoa madarakani Mark Ravalomanana(sijui kama nimeandika kwa usahihi) yaani hizi mbinu zinatumika na pande zote ndo maana moja ya lengo lake ni propaganda ndo maana ukiona Andry naye katolewa baada ya wenzake kumanipulate agenda zake na kuona uzushi ila wamesahau kama walimtoa mtu ili yeye aingie kwa imani ya agenda nzuri yaani hata wapinzani au wanaharakati wanaweza kutumia mbinu hizo hizo ili kuaminisha umma kwa mfano kuna kauli unaisikia inasemwa amauwa watu elfu kumi hiyo trick sio nyepesi ni trick nzito sana na imetumika kimakusudi
 
"Intelligence Spinning"
Ni uwasilishaji wa taarifa za kiintelligensia kwa namna iliyopindishwa kwa maslahi ya umma au viongozi.

Yaani kuna taarifa ni kwa ajili ya kuubhagaza umma ili uamini kitu na pia kuna taarifa nyingine zinabhagaza viongozi ili waone wako sawa na salama.

Taarifa inayofanyiwa "spinning" inakuwa ya ukweli kabisa ila uwasilishaji wake ndo unakuwa wa uongo. Mfano "Tumepokea taarifa ya maandamano ya ..... ila kwa taarifa za kiintelligensia kutakuwa na uvunjifu wa amani", na viongozi pia huwanyiwa spinning kwa kupindishiwa taarifa hasa ikiwa parallel state ndo kabisa anaweza akatishwa kwa taarifa za kawaida na kuonekana kubwa ili akae kwa tahadhari na vitu vingine vya kimkakati asifanye kwa ukaribu.

Ila kuna mambo ambayo mara nyingi wengi wetu hudhania ni spinning kumbe sivyo ila malengo yake hutarget umma au uongozi na hitimisho la mlengo ni kama spinning inavyohitimisha mambo hayo ni kama:-

1. Diversionary politics (Siasa za mkwepo)
Kutengeneza issue nyingine ili kuutoa umma au utawala kwenye issue iliyokuwepo awali huenda ilikuwa nzuri au mbaya. Mfano kunakuwa na habari za kuhusu masuala ya uchaguzi watu wamewaka moto kweli kweli wanaweza kuhatarisha usalama inaletwa issue ya udini inapewa promo watu wanahama na wasipo hama wanagawanyika basi issue ya awali inakuwa imepunguziwa nguvu au imeondolewa hatari iliyodhaniwa.

2. Distraction tactics (Mkakati haribifu)
Hii ni ile hali ya kuondoa mtazamo wa umma kwa nguvu bila kuwa na hoja mbadala mfano umma unataka taarifa fulani ambayo itajenga sifa mbaya kwa nchi viongozi wanagoma kutoa hiyo taarifa kwa kutoa sababu isiyo na mashiko kwa umma.

3. Agenda setting/Agenda manipulation(Kuibalaghaza agenda)
Hii ni ile hali ya kuongoza yale ambayo umma unaongea kwa sana kwa kuyapindisha au kuyatengenezea tafsiri ngumu kwa umma kwa mfano " Umma unadai haki moja wapo ni haki ya kuishi ila wataalamu wa kumanipulate wanaishi kwenye hiyo hiyo ajenda wanakuambia unapodai haki hakikisha umetimiza wajibu kumbuka haki inayodaiwa na umma ni haki ya kuishi ila unaambiwa utimize wajibu"

4. Smoke and Mirrors(Moshi na Kioo)
Yaani moshi ukionekana kwenye kioo ni jitu kubwa sana ni kama linashikika hii imekaa hivi kuanzisha mambo madogo ambayo yanachukua nafasi ya mambo makubwa ili kutoa watu kwenye ufuatiliaji wa mambo makubwa. Mfano mambo ya wasanii na michezo yanaweza kupewa nafasi kubwa ilhali kuna mambo ya nchi yanatokota na ni makubwa hayana nafasi, inch fulani deni lipo Trillions za Shilling za kwao 12 ila wao mameshika masuala ya ukabila na upendeleo kwenye vyeo.

5. Red herring (Sill nyekundu)
Hii ni ile hali ya kuiondoa jamii kwenye hoja za kipaumbele kwa kuanzisha hoja mbadala ambazo zitaitoa jamii katika kelele za hoja zao za msingi mfano Goldberg Scandal kwenye nchi hiyo walisema kuna watu wanatengeza taarifa ili kujinufaisha kisiasa na kulichafua kabila fulani, Cashgate scandal kwanini watu mnatengeza hoja za uongo kwa ajili ya minajili ya kisiasa, kuna Scandal ilikuwepo babu wa Loliondo alichukua front page.

Sababu ya kufanya hivyo huenda ikawa:-

1. Kuhalalisha maamuzi ya serikali.
Mfano: kuhalalisha vita, operesheni ya usalama, au sheria mpya.

2. Kuepusha hofu kwa wananchi.
Wakati mwingine ukweli hufichwa au hupunguzwa ili watu wasipate hofu.

3. Kushawishi maoni ya umma.
Kufanya tishio lionekane kubwa au dogo ili watu waunge mkono hatua fulani.

4. Kulinda vyanzo vya taarifa.
Kuepusha kufichua majina ya watoa taarifa au mbinu za kijasusi.

5. Propaganda / taswira ya kisiasa
Kuifanya taasisi au upande fulani uonekane sahihi zaidi ilhali wamefanya sawa au si sawa lakini hulazimishwa kuonekana ni sawa hata kama ni ufisadi wizi ubadhilifu na mengineyo mabaya kwa maslahi ya umma.

Kama kuna lolote unaliona linaendelea kwa pamoja tunaweza kusaidiana kulichambua na kuliweka katika kundi lake kuwa hilo lipo mlengo gani kama ni kweli au ni mbinu za kuingizana maboya

Nipo tayari kurekebishwa na kueleweshwa zaidi karibuni kwa maoni na kila linalotokea tutaarifiane na kulichambua
Hongera kwa mada nzuri mkuu 🤝
 
Mfano kikwete anasema hadharani"Mungu ndio anafanya watu kuwa viongozi" hivi karibuni!!

Kiintelijensia maana yake "aliejifanya kuwa kiongozi peke yake hawezi kudumu katika nafasi hiyo!!?

Je nini kinaendelea mafichoni huko!!?

Je aliejifanya kiongozi anaendeleaje katika kutimiza majukumu yake!!?
 
Mkuu,
Wanaharakati nao kweli wanashere huwa wanachezeshwa na wakikaa vibaya wanacheza kweli lakini pia hata wasio wanaharakati watu wa kawaida wakiinua hisia kali zenye kuleta uhatari kwenye usalama mwendo ni lazima njia moja itumike hapo ili kuwadhoofu mfano ukikumbuka kipindi cha nyuma kulikuwa na tabia ya migomo ya wafanyakazi ila mbinu moja ilitumika kwamba wanaogoma waorodheshe majina yao na serikali kama mwajiri mkuu ana nafasi ya kuwafuta wote kazi watakaorodhesha majina hiyo kwa raia wa kawaida wanajua ugumu wa maosha wataogopa tu kufanya hivyo na kama wakifanya watagawanyika hawatakubaliana...
Hata wanaharakati sio wa kuwaamini asilimia 100%.wengine wanapambana pia kupata spot kwenye keki ya taifa.

The same watu walivyoamini kila aliyepo CHADEMA ni mwanamageuzi, ila CHADEMA ilipodhoofishwa. Wengi wameamua kula matapishi yao ili wasipotee kisiasa

Kwa umakini kwa activists pia unahitajika
 
Kila kiongozi hasa anayetumia sera kwa kuwashawishi watu mara nyingi lazima atumie njia moja wapo ili kupenya kwa sera zake kwa umma ni nadra sana wakatumia ukweli pekee ili kupenysha sera kwa umma.
 
Hata kuizima JF ni mbinu Yao maana ilikuwa inaleta awareness kubwa sana maana wanaopata Kwa VPNs ni wachache. Na wameweka watu wao kuwa members humu kusifia , kupinga na kuleta hoja za uongo wakiwa kwenye payrols zao na wanapata bundles za maana na wanafanikisha .

CHAMA KIMESHIKA HATAMU NA HAWATAKI UTANI NA KEKI
 
Back
Top Bottom