lugamba2001
Member
- Aug 18, 2009
- 12
- 0
Ama kweli mbuzi wa maskini hazai na akizaa ni madume! Napendekeza jamii forums uanze utaratibu wa kuchambua mada zenye kufanana na jina lako! kama umeshanunuliwa kama wale wengine basi tujue, maana sasa tunashindwa, hatuoni cha kusoma, wala cha kuchangia, kila siku mizozo au mashindano yasiyokuwa na mshindi wala manufaa. Niambieni katika mada kama hizi mnaongeza nini kama si kupoteza muda tu? unaacha mambo ili usome kitu ndani ya " The home of great thinkers", unakutana na mada za kupotezeana wakati... Mijadala ya namna hii huwa ni ya kijiweni, watu wakiwa wanasubiria mambo yao, kama madreva tax vile wanasubiria wateja, au wasio na kazi kabisa!! Jamii forums kwa kweli tulikupenda sasa unaanza kutuyeyusha!!