So, so very painful

So, so very painful

Kwa mara ya kwanza BAK kawa mkali...te te te

Kuna watu wanatia hasira badala ya huruma...

Kwani kipi kisichoeleweka pale unapoambiwa "usije"? Usipende kulazimisha penzi pale ambapo halipo ni kujitafutia majuto yanayoweza kuepukwa kirahisi kabisa. Tia akili kichwani na ushike hamsini zako.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
lol!!!! hahahahahah Kumbe huingii kule jukwaa la siasa eeh!!!! Haya bhanaaa..

Kwa mara ya kwanza BAK kawa mkali...te te te

Kuna watu wanatia hasira badala ya huruma...
 
Siasani kule kuna wahuni ambao hawana hoja, wakiona wanashindwa kwenye hoja basi wanaanza kurusha matusi ya nguoni maana wanajua watu kwa kutopenda kutukanwa au kwa kuogopa kufungiwa basi wakitukanwa watakaa kimya na kuacha kuchangia.

Hawa wahuni wao wana IDs lukuki hivyo wakifungiwa ID moja wanahamia kwenye ID nyingine, lakini akina siye wenye ID moja ukifungiwa ndio mpaka ufunguliwe. Bora ucheze/ubaki huku huku kule kama una roho ndogo kweli unaweza kupandisha pressure kwa jinsi hawa wahuni wanaolipwa buku 7 kwa siku wanavyorusha matusi ya nguoni.


Siasani naingia labda mara moja kwa mwaka...maisha mfupi sitaki kukaribisha pressure...
 
ushaonyeshwa haupendwi......tafuta ustaarabu mwingine......utampata atakayekupenda pia
 
Ukielewa kuwa katika mapenzi ni 60/40 ama 90/10 wala hutopata taabu, there is never 50/50 katika mapenzi. Its either you give much or less and vice versa. Kwa mpenzi wangu najua mm natoa much but sipati shida maana naamini baada ya muda nitapata enough amount of love in return, give it time and keep trying if its worth it.😕
 
Pole Sana.Piga chini huyo mtu usonge mbele japo ni jambo gumu.Kaza moyo muombe MUNGU atakutia nguvu
 
Usjal anasubiri tamko la Ikulu baada ya hapo mambi yatakuwa poa
 
Fanya yako mwaya hamna love hapo.pole inaumiza sana ila jikaze mpotezee
 
Kuendelea kumpenda mtu ambaye unajua kabisa hakupendi ni kujitakia maumivu ya moyo ya bure. Hayuko peke yake duniani. Raha ya mapenzi ni kupendana na sio kupenda.
Yaani kupenda mtu ambaye hakupendi kivile au kiasi hicho hicho inauma sana, maana uwepo wako au kutokuwepo kwako vyote kwake vitakuwa sawa tu, saa nyingine utaonekana kero tu bila sababu.

Fikiria una mtu wako mko mbalimbali, umepata nafasi ya kwenda kumuona, unamuambia anasema sina hela ya nauli, unamwambia basi nitakopa nauli tu nije huko ni muda sijakuona nimekumisi, bado anasema usije, nitakuja mimi baada ya zaidi ya mwezi.

Hivi jamani ni nini hiki?
 
Jamani mbona hapo kila kitu kiko wazi kaa kimya jipange upya. Maisha bila yeye kwani siyanasonga tu. Achana naye.
 
Ndio hivyo kuna watu wamezaliwa kuumiza wenzao!!!ukimpenda tuu anaanza kukupandia bei kama kipande cha dhahabu!!!pole sana IPO cku atakuja jjua thamani yako lkn wakati huo ye ndo atakuwa kachelewa!

Una uhakika!
 
Back
Top Bottom