mludego
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 2,660
- 3,670
Sababu umeomba maelezo basi acha nijaribu kukuelewesha kwa ninavyoelewa:-
Slay queen ni mabinti kuanzia umri wa miaka 16-35 hapo inategemea na umbile la muhusika km litamruhusu kuslay mpk umri huo. Wanakuaga ni warembo wengi wao wenye sura au maumbile ya kuvutia su vyote kwa pamoja!
Pesa zao nyingi hujipatia kutokana na kufanya miili yao mtaji na pesa hizo pia hutumia kwny kujipara kwa hali ya juu ili waonekane wapo standard. Wengi wao wametokea hali ya maisha ya chini ila hujitahidi sana kulikataa hilo kwa kufanya matendo tofauti km udangaji!
Most of them hua hawana elimu japo hata waliosoma wapo pia!
Utawajuaje:-
Wengi wao hupenda kuvaa wigs za gharama kuanzia laki na nusu and above! Kupaka mikorogo ya bei either ya bei ya juu au ya kati...kucha ndefu zilizochongwa mithili ya mdomo wa kuku mikono yote miwili na miguuni.
Wengi hupenda kupaka lipstick zenye rangi zilizokolea mno km ni nyekundu bas ni nyekundu haswaa..hupenda kuvalia mavaz yanayoscha sehemu kubwa za miili yao km maziwa, mapaja na vitovu hupenda kujitoboa mwili mno km kwenye vitovu ulimi kuvaa vikuku na cheni za kiunon hadharani bila kusahau siku hizi wameibua mitindo mipya ya uchoraji wa TATTOO.
Hupenda kupiga picha sehemu nzuri na za maana km mahotelin au akipelekws sehem km marry brown na KFC na kurecord matukio ya bata yyt anayoyafanya.
Kwao kumiliki IPHONE latest ni km kuwini maisha na hupenda kupiga picha kwa mtindo wa kujibinua na kuonyedha makalio huku akibana tumbo(kwa wale wenye vitambi)
Usafiri wao mkubwa ni bodaboda na bajaj akiwa na vijisent kdg anakodi UBER au TAXIFY pia wapo waliopambana kdg wamenunuliwa gari km
PASSO..IST...RAUM..RUNX..RACTIS...SPACIO..ALLEX na mengine yny mfanani km huo ila mengi ni engine ya vvt-I si unajua yanasave mafuta kidogo
Bila kusahau wanapendaga vingereza uchwara maana ht shule yao ni tia maji tia maji...wana mtindo wa kuiganana maisha km ss hv nimeona wamekuja na mtindo wa kuzaa na kujiita "We are single mothers and happy"
Km utakua hujaelews na hapo bas kaka yng itakua ni balaa
Wadada tuache kuact jamani tunajichoreshaga sana!
Nawasilisha♀
Hujampa mifano waldau mwili kama alivyoomba