SLAA na Kauli Tata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SLAA na Kauli Tata

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Salimia, Mar 18, 2011.

 1. S

  Salimia JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dr. W.Slaa ana sifa nyingi sana za uongozi,, lakini mojawapo ya sifa za kiongozi ni kutoa kauli zenye uhakika hasa unapokuwa kiongozi mkuu. Slaa anatarajiwa kuwa Rais,, sifa hii ya umakini wa kauli anapungukiwa sana hasa ukizingatia kauli kadha ambazo amewahi kuzitoa katika kipindi kifupi cha nyumba.

  Mathalani kuhusu kontena la kura, kifo cha RC shinyanga na nyingine nyingi. Hizi ni kauli nzito ambazo kiongozi makini asingeweza kuzitoa hadharani kabla hajapata uhakika..

  Nashauri ikiwa atakuwa Rais basi ajifunze kuwa na subira, ukisikia jambo usifanye pupa na kuropoka hadharani kuuvuruga muamana.

  Bado naendelea na uchunguzi kujua kama kweli Mbowe na SLAA ni waadilifu. Isije kuwa ni usanii tu.

  Nitarudi

   
 2. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  duh!!!!!

  salimia sasa umeanza kuwachokoza wa chadema shauri yako mi simo maana hawa jamaa wakali sana ili tukuelewe andika mazuri tuu, ukianza hayo utaaribu sasa hivi ngoja tuone majibu yake!

  mimi binafsi Slaa alinivutia pale alipolalamika kuwa wabunge wanalipwa pesa nyingi lakini duuh hili halikupata kuungwa mkono na mbunge yeyote yule wa chama chake, upinzani wala sisiemu sijui kwasasa wakati kuna dalili kadhaa kwamba watz tunaweza kumpa ridhaa atuongoze sijui atathubutu kuliendeleza hili?
   
 3. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Usisahau pia yeye analipwa na Chama chake sh. milioni 13 kila mwezi kwa mkataba waliokubaliana kabla ya uchaguzi hivyo angeanza kwanza na kupunguza mshahara wake ndipo ageukie wa Wabunge!!!
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa alisema kuwa tarifa alizopata ni kwamba mkuu wa mkoa wa Shy amefariki lakini akaongeza kusema kuwa kama hizo taarifa ni za kweli basi alale mahali pema maana jana yake alikuwa amemsema kwenye mkutano wake.. Mbona CCM mnapenda kuzusha upuuzi hoja zilishawaishia mnabakia propaganda,
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Dirty POLITICS!

  Hilo la contena ni la ukweli kwa asilimia 100!

  Ulitegemea polisi wamdhalilishe mkwere na ile mbinu yake chafu hadharani, wakati bado wanamtegemea awalipe madeni ya fedha za uhamisho wanazomdai?

  Hilo la pili, mimi binafsi nina mashaka sana na jinsi inavyosemekana alitangaza!...Binafsi sikuona, ila kuna aina nyingi za usemaji, na watafsiri wako wa aina nyingi!

  Nawasilisha!
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kweli Dr. kiboko bado tu na kampeni zenu kumhusu? Watu hawana naji safi, mfumuko wa bei juu, barabara mbovu, shule ni magofu.

  Embu badilikeni wakumbukeni wananchi maskini waliowapa kura..wanataabika
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu jama vipi? Haya tuambie RC wa Shinyanga yuko hospitali gani na nani kiongozi gani alyeenda kumjulia hali? Yule kafa we sema wanamficha. Swali watamficha hadi lini?

  Kuhusu kura feki, je wewe ulienda kuhakikisha au kwa vile wamezificha, ukweli ni kwamba anayoyasema slaa ni ya kweli na ndio maana wanaogopa kumpeleka mahakamani.

  Tokea Slaa aanze kuongea umeshasikia kuna mtu kamfungulia kesi kwa kusema uwongo? Wote hao wanajulikana na ni ukweli mtupu.

  Jipange, kalete hoja mpya tena
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzushi tu hana lolote na hafai kupewa nchi sababu yeye na wasaidizi wake hawako makini katika kupokea na kutoa habari
   
 9. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Una uhakika na unachokisema, CDM, wanaolipwa ni waajiriwa tu, David Kafulila alikuwa analipwa pamoja na waajiriwa wenzake, lakini viongozi wa juu including Zitto Kabwe wanafanya kazi za kujitolea mkuu.

  Mishahara hiyo CDM haipo labda Utuambie tambwe Hizza analipwa shillingi ngapi tena ana cheo ambacho hata kwenye katiba ya CCM hakipo.

  Aacha KUKURUPUKA tu from no where unasema upupu.
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa ni member hapa....anachangia sana na anachukua mawazo pia kwa uangalifu mkubwa na anaiamini JF kama credible source yake ya hoja (from credible members of course sio wakina JeyKeywaUkweli,MS,Kishaga etc)....sasa anapotoa hoja hadharani anaumakini wake...mathalan:
  1. Issue ya CONATINER LA KURA TUNDUMA ilianzia hapa...thread yake ipo ni kubwa tu
  2. Suala la RC Shinyanga lilianzia hapa na thread yake ipo
  3. EPA ilianzia hapa na thread ziko kibao
  4. MEREMETA pia imo humu
  5. RICHMOND, DOWANS zote zilianzia hapa
   
 11. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kama julius mtatiro aliomba gari na nyumba tukamkataa akakimbilia mskitini, bado CDM haijawa na hela ya kulipa kila mtu wengine tunatumia pesa zetu mfukoni
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mpuuzi kweli wewe,we slaa si alisha kujibu upuuzi wako huo kwenye thread ya liberia?
  Bahati yako hamna mods wakatili kama mimi,ungekuwa ukirudia thread moja mara nyingi nakufungia kuanzisha thread
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Umeomba utukanwe? Jamani.... we haya tu.

  Ngoja nimuachie Mkuu hapa chini afanye kazi...... Mie simo, ni mjumbe tu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  sasa mkuu kama wanaolipwa ni waajiriwa tuu ambao kimsingi ni wachache sana sasa haya mamilioni ya SABODO na mabilioni kutoka nje ya nchi wanayopewa CDM yanatumika kwenye nini? maana ofisi za kuhesabu,tungesema wanalipia pango,umeme maji nk! pesa zinaenda wapi? tunaomba tupewe mchanguo la sivyo kuna ufisadi hapo
   
 15. S

  Salimia JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tell me about it!1 Nakwambia hawa wote ni power struggle tu ndiyo inawasumbua. Leo hii na anyoshe mkono mbunge wa CDM au chama kingene chochite aliyekataa Mil 90 za gari? Yu wapi mwenye uchungu wa kweli wa nchi Tanzania? Nani aliyemuunga mkono Slaa juu ya mshahara wa wabunge? Wenzetu wanakula bata sisi huku ndiyo tunatukanana. Ndiyo maana niliacha ushabiki hata wa mpira,, timu ifungwe eti na chakula ususe? Kocha na hata wachezaji hawakujui na wanakula pesa yao kama kawaida!! Acha nikanunulie dagaa wanangu hapa tunadanganyana tu hakuna CHADEMA wala nini,, wote walaji tu.
   
 16. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Mtu hujikuna pale panapowasha. Ni lazima wamseme Dr. kwa saaaana kwa sababu huyo ndiye anayewawasha sana mpaka wanakosa usingizi.
   
 17. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  uko sahihi mkuu,nakumbuka aliropoka kwa kuwataja mafisadi papa pale mwembe yanga,yan list of shame,akiwemo jk,baadae ikathibitika kuwa ni uongo ivo serikali ilimpeleka Dr.slaa mahakamani,nlisikia yuko jela mpaka leo. Pia alisema kuna makampuni ya kitapeli kama Meremeta,iptl na Dowans,kagoda na tangold,kumbe ulikuwa uongo hata kampuni izo hazijawahi kuwepo Tanzania. Cha ajabu akadai kuna ufisadi benki kuu kwenye EPA,serikali ilichunguza ikakuta hamna tatizo na dr.balali hakufichwa mpaka leo anaendelea na kazi wala hakufa wala kuuawa,pia Jk alisema kuwa waliodhaniwa kuiba ela aliwaambia wazirejeshe haraka aliwaomba samahani na kuwaambia wakachukue ela yao kwa sababu alimuelewa vibaya dr.slaa aliyeongopa kuwa kuna ufisadi epa kumbe hakuna. Kweli mleta mada ni mkweli zaidi ya dr.slaa anayedai kuna ufisadi Tanzania wakati Tanzania hamna ufisadi iko shwari wala hamna mtanzania mwenye maisha magumu. Kweli mleta mada we jiniasi kwa kuona uongo wa dr.wa ukweli ukiachana na ukweli wa dr.dr.dr.dr rais ambaye hata izo dr.s ni za kwenye gift pepa.
   
 18. S

  Salimia JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hewala, miye mpuuzi,, lakini hapa chini nanukuu alichonijibu Slaa kwenye thread ya Liberia,, bahati njema ingalipo hai. Soma halafu unijibu swali langu chini yake:
  Sasa wewe Speaker, nionyeshe ni wapi Slaa ameongelea suala la kontena la kura hapo juu?? Au ni wapi amezungumzia kifo cha RC wa Shinyanga kwenye majibu yake hapo juu?
  Hapo sasa wenye hekima watachambua mpuuzi kati yangu na wewe nani?
   
 19. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 462
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Salimia, hatudanganyiki mtasema tutaendelea kumuamini tu.

  Na mtabaki kusalimiana.
   
 20. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi hafif, wewe hukwepo kwenye ile opinion polls ya hapa JF na kwingineko? Mbona Dr Slaa alishinda au kwa vile mechakachua?

  Na mzimu wa uchakachuaji bado unawasumbua mtakoma, na kama hamkuchakachua kwa nini mnahofia nguvu ya uma? wakati ni juzi tu tulifanya uchaguzi?
   
Loading...