Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Status
Not open for further replies.
Haya ni matokeo ya binary philosophy: either you are a muslim or you are against islam.
 
Reactions: LAT
sichangii kitu chochote.Yaani mada imeletwa na sokomoko nyie mnatarajia nini?
 
Reactions: LAT
Nimeipitia katiba ya chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) ni marufuku mtu yoyote asie kuwa Mkiristo kugombea nafasi yoyote kwenye chama, sasa chama kama hiki unategemea ukiwa na urafiki nacho na wanakupa misaada bila kuwa mwenzao kwenye Ukiristo?

Mbona mnatuaibisha waislamu kwa hoja zenu zisizokuwa na miguu wala vichwa.Tatizo hawa ijana ambao waliishia madrasa uelewa wao ni mdogo.
Mimi sijaona mwislamu mwenye upeo na ilimu yakutosha anaye endekeza upuuzi huu.Ushauri wangu, endapo tutapuuza topic kama hizi zitakufa natural death.
 
Hivi wewe mbona unakuwa Scatty! Kila siku mnajidanganya eti mmesoma, ebu niambie hizo Elimu zenu unazojitapa nazo zimeishaidia nini taifa letu kutoka kwenye umasikini wa kutupwa dunia, au zimewasaidia kufanya ufisadi mkubwa kwenye nchi yetu, halafu nipe kiwango cha Elimu cha YESU, tujadili vizuri
 
Acheni jazba ni vema mkaichambua hii hoja kwa hoja wengi mnatoka nje ya mada sijui ni makusudi ili kupoteza mwelekeo wa mada au na nyie hamna elimu kama mleta mada? Naona ndugu zanguni mnakimbilia hoja nyepesi nyepesi hii mada imekuwa mwiba kwenu. Hii hoja ukijumlisha na symbion unaweza ukapa kitu ila watu mmekuwa vipofu basi hata kusikia hamsikii?
 
Mimi ya Yesu cjui ila najua ya mtume asiyejua kusoma wala kuandika. Mtume wa kwanza kutokanyaga hata ngumbaru. Ala alikuwa na elimu ya juu sana pamoja na kutojua kusoma na kuandika. Alikuwa na elimu ahera. Balaa nakuambia yuko juu mtume wa jangwani.
 
Yusuph Makamba alisoma seminary lakini hakubadili dini na wala hakubadilishwa dini. Ni wazi Sokomoko ni mtu anayependa kuja kuona nchi inaingia kwenye machafuko ya kidini siku moja ndiyo maana hana Post nyingine zaidi ya kuchochea udini. Niweke wazi kuwa Taaluma huongozwa na mitaala na si hisia kwa hisia mbovu kama za sokomoko. Pia ni wazi utambue Dira au Injini,malengo na makubaliano ya Pamoja ya CDM ni katiba yao na si blaa blaa au kuangalia nani anashirikiana na yupi. Katiba ya CDM KATIKA IBARA 3.1.9 inasema' CDM inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya Dola'. Ubinafsi,uvivu wa kufikiri,uchochezi na ufedhuli ndiyo vinavyomuongoza SOKOMOKO. Hii dhambi itakuja kumgharimu. Aachane nayo brazaz.
 
Nimefuatilia kwa muda mrefu hii mada nikaona kinyaa cha kuichangia ila naona sijitendei haki kukaa kimya wakati naweza kuandika japo mistari kadhaa.

Bila chembe ya shaka huyu aliyeweka hii mada ni muislamu mwenzangu. Mimi ni muislamu kama yeye japo sijajua kiwango chake cha elimu na uwezo wa kuchakata mambo. Lakini pia sijajua uwezo wake wa kuhimili joto lake kiitikadi. Leo ana ona Cdm ni wadini, juzi aliambiwa Cuf ni wadini na vyama vyote hivi vina wanachama wa dini zote, inawezekana hajui lakini imetamkwa wazi kwenye katiba juu ya uanzishwaji wa vyama vya siasa. Kama Cdm au Cuf kingekuwa cha waislamu au wakristo pekee visingekuwepo. Atambue ccm inatumia ujinga wa wananchi ili kuwagawa na kuleta fikra za udini, na imefanikiwa mara kadhaa kama ilivyofanikiwa kwake. Lakini pia asidhanie wasabato, wakatoliki, walutheri, walokole nk wana kauli ya pamoja kushawishi waumini wao wafuate chama flani, hivyo hivyo shia, sunn, ahmadiyyah nk ndio maana haijawahi na haitatokea viongozi makini wabobezi wa elimu zote wasimame na kuwaambia waumini wao kuwa msifuate chama hiki kwa kuwa ni cha dini hii.

Kulalamika huku wenzetu wakichanja mbuga si dawa. Ulevi wa kiitikadi kuona chama flani nicha udini wakati si kweli ni ukame wa fikra. Tukazanie elimu zote kwa watoto wetu, bakwata ifumuliwe wakae viongozi wenye vision na elimu ya juu ili wasimamie shule zetu vizuri ziwe mfano wa kuigwa kwa kutoa elimu bora ili kuondokana na kizazi cha huyu sokomoko kinacho angalia sarafu upande mmoja.
 

vilaza bana ..... teh tehh tehhh
 
CDU=CHRISTIAN DEMOCRATIC UNION
CDM=CHRISTIAN DEMOCRATIC MOVEMENT-Padree Slaa

we are watching your movement.
 

Nimekuwa nikiwaasa wanajamiiforums hasa vijana wa CHADEMA kuacha kushabikia mambo kibubusa pasi na kutafakari.Evi katika hali tu ya kawaida inawazekanaje taasisiau chama fulani kuunda ushirikiano fulani masherti? Au hujui kuwa Nchi mbalimbali zinapoenda kuomba misaada katika WB na IMF hupewa misaada hiyo kwa masherti?
Sasa 'if that the case' iwaje CDM washirikiane na CDU pasi na masherti? wakati huo ikifahamika kuwa lengo kuu la CDU ni kusambaza
ukristu kama ilivyolengwa na mwaasisi wake? acha ububusa kaka,ukweli ni kwamba,kama CDM wameunda ushirikiano na ,CDU fahamu kabisa chadema kitaendeshwa kwa itikadi ya CDU kwani chama kinapata misaada mingi kutoka CDU
 
Bila ya mafundisho na ustaarabu wa kikristo, basi dunia ingekuwa giza kama akili ya alitoa mada hii
 
Reactions: LAT

mwehu hana alama
 
Kama Katiba ya CDU inatamka wazi kuwa ni Marufuku kwa Mtu yeyote asiye Mkristo kuwa kiongozi basi ni dhahiri Values zake ni tofauti na za CDM, lakini sasa inakuwaje CDM ifanye urafiki na chama chenye "Udini" kama hiki cha CDU?. Hapo kuna mawili either (1) CDM iko sympathetic na ajenda ya "Ukiristo" lakini haitaki kukiri wazi (2) Chadema haijali kwamba kinafanya urafiki na Chama gani kiwe cha kidini au si cha kidini. Lakini hatari ya namba (2) ni hii, ni kwa namna gani CDM itajipambanua kuwa huru dhidi ya kamba za influence kutokana na vyama hivyo vya kidini?.
 

kama mtu hujaenda shule halafu ukajazwa na udini basi unakuwa kipofu kabisa..! hoja yako hapo juu imeshajibiwa mara nyingi kwenye thread hii !
nakuuliza na ujibu kwa hoja! hivi serikali ya CCM inashirikiana na nchi ngapi hapa duniani? CCM yenyewe inashirikiana na vyama vingapi hapa duniani?
Ina maana gani kwa Tanzania kupokea misaada na kushirikiana na nchi ya Kiislamu ya Iran ? Je serikali ya ccm inataka na sisi wote tuwe waislam?
Nyinyi mnaondekeza udini ni watu msio na mbele wa nyuma...nadhani ahueni yenu mtaipata endapo tu machafuko yatatokea!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…