Skendo ya ngono yatikisa kanisa katoliki.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Skendo ya ngono yatikisa kanisa katoliki..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 27, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  FRONTUWAZI2.jpg
  Skendo ya ngono inaitikisa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mburahati lililopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusababisha mgawanyiko mkubwa kwa waumini.
  Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu zimebaini kuwa skendo hiyo ya ngono inamhusisha Padri Paul Njoka na mhudumu wa nyumba za mapadri ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo aliyejulikana kwa jina moja la Mwasiti.
  Taarifa zilizopatikana kanisani hapo zinadai kwamba padri huyo alimjaza mimba mhudumu huyo na hivi sasa amezaa naye mtoto.
  Habari hizo zilienea kanisani hapo na kusababisha baadhi ya waumini kutaka suala hilo liwekwe wazi ili kiongozi huyo achukuliwe hatua zaidi, jambo lililomfanya kasisi huyo atafute jinsi ya kujihami.
  Chanzo chetu cha habari kinasema kwamba baadhi ya viongozi wa kanisa hilo walifikia hatua ya kutafuta jinsi ya kumficha mtoto huyo baada ya kuzaliwa ili kupoteza ushahidi.
  Imeelezwa kwamba Februali 4, mwaka huu Padri Njoka akiwa na muumini aliyejulikana kwa jina la Maria Kaswela walichukua gari na kumsaka Mwasiti, walimpata na kumuingiza katika gari hilo.
  Imedaiwa kwamba katika mzunguko wao, Mwasiti hakujua ni kitu gani alichotakiwa kufanyiwa na mtoto wake bali yeye alijua ni matembezi ya kawaida huku akifurahia ni jinsi gani padri anavyompenda mtoto wake na kuamua kuzunguka naye jijini kwa siku hiyo.
  Chanzo kilidai kwamba siku hiyo padri huyo na mzazi mwenzake walielekea Sinza,Manzese kisha Magomeni.
  MTOTO ATEKWAWalipofika Magomeni habari zinasema walimtuma dukani mama wa mtoto (Mwasiti) na mtoto akawa amebebwa na Maria.
  Chanzo kiliendelea kudai kwamba padri aliendesha gari na kuondoka eneo la Magomeni kwa kasi kuelekea kusikojulikana na Mwasiti alipotoka dukani na kwenda sehemu lilipoegeshwa gari hakuwaona na alipowapigia simu hawakupatikana.
  TAARIFA YAFIKA POLISIHata hivyo, Mwasiti alipatwa na hofu kwani ilimchukua muda mrefu bila kuwaona, kitendo kichomfanya aende Kituo cha Polisi, Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni kutoa taarifa ya kutekwa kwa mtoto wake wa siku 28 tangu azaliwe.
  Mwasiti alifunguliwa jalada lenye kumbukumbu MG/RB/2430/2012 ndipo polisi walipoanza kazi ya kuwatafuta padri na Maria bila mafanikio.
  Habari zinasema polisi walifanikiwa kumuona Padri Njoka akiwa kanisani siku ya Jumapili akiendesha ibada ila ilishindikana kumkamata kwa sababu misa ilikuwa ikiendelea.
  Kutokanana kitendo cha padri huyo kuendesha misa, askari hao waliacha taarifa kwa mlinzi wa kanisa hilo kwamba baada ya kumaliza ibada afike Kituo cha Polisi Magomeni akiwa na Maria.
  Hata hivyo, hawakwenda siku hiyo badala yake walienda kesho yake Jumatatu ya Februali 6, mwaka huu.“Mara walipofika kituoni waliwekwa chini ya ulinzi, walibanwa ili waonyeshe alipo mtoto ambapo walisema kwamba yupo Kigamboni kwa ndugu wa padri huyo,” chanzo hicho kilisema.
  Polisi waliwaamuru watoe namba ya simu ya watu walio na mtoto huyo ili wapigiwe, padri alitoa, ilipopigwa aliye na mtoto akaamriwa amlete kituoni hapo na akafanya hivyo saa 5.00 usiku padri akiwa chini ya ulinzi.
  Hata hivyo, polisi walipomkabidhi Mwasiti mtoto wake alikataa kumpokea na kudai kwamba akapimwe afya yake kwanza kwa vile hakujua alichofanyiwa huko na alikua katika mazingira gani.
  Chanzo kiliendelea kusema kwamba hapo polisi Magomeni alikuwepo pia Paroko Timoth Nyasulu Maganga ambaye ni mkubwa wake wa kazi Padri Njoka.
  Habari zinasema Padri Maganga alimbembeleza Mwasiti amchukue mtoto wake ambaye alikubali kisha alikwenda naye Kinondoni kwa dada wa mzazi huyo. Uchunguzi wetu umebaini kuwa kesi hiyo ipo chini ya mpelelezi mwenye namba WP697 Tiba.
  WARAKA KWA PENGO Kutokana na kitendo hicho, baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliamua kumuandikia barua Februali 8, mwaka huu Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Askofu Polycarp Kadinali Pengo kuhusu udhalilishaji wa Kanisa Katoliki waliodai kufanywa na padri huyo kwa kumteka mtoto.
  Katika barua hiyo (Nakala tunayo) waumini hao wameeleza jinsi wachunga kondoo walivyofikia hatua ya kufanya mapenzi na wafanyakazi, wahudumu wa nyumba ya mapadri na kuwapa mimba.
  Hata hivyo, katika barua hiyo waumini hao wamesikitishwa na kitendo hicho na kudai kuwa gharama kubwa za fedha za kanisa zimetumika kushughulikia suala hilo.''Tunakuomba ufanyie kazi jambo hili kwa haraka inawezekanavyo ili kuepusha uvunjifu wa amani endapo viongozi hao wachafu watabaki hapo parokiani,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
  Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa mapenzi yanayofanyika kanisani hapo kati ya viongozi na waumini yamesababisha utoaji hovyo wa mimba hadi wengine kuzalishwa, kitendo ambacho kinalitia aibu Kanisa Katoliki.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela hakupatikana kuzungumzia tukio hilo lakini afisa mmoja wa cheo cha juu wa jeshi hilo alithibitisha kuwepo kwa madai hayo kuongeza kuwa upelelezi bado unaendelea.
  Aidha, Kadinali Pengo hakuweza kupatikana kuzungumzia malalamiko hayo ya waumini wake.Gazeti hili linaendelea kufuatilia sakata hilo kwa undani zaidi ili kujua ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.skendo ya ngono yatikisa kanisa katoliki... - Global Publishers
   
 2. Fund

  Fund Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe gazeti la udaku
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  shigongo!
   
 4. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  mbona mnakuwa na mawazo finyu ? kwahiyo kama ni udaku sio kweli ?
   
 5. m

  mgadafi Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  N kawaida atakuja papa kulipa fidia au kwa kifupi mahari
   
 6. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  daaah dunia imekwisha, utasikia kahamishwa parokia wala hatafukuzwa.
  Mimi ni mkatoriki na msimamo wangu ni kwamba viongozi wa dini ukosea kwakuwa wao ni binadamu ila wakikosea waadabishwe kama ilivyo kwa mujibu wa utaratibu yani wasimamishwe kazi si kuamishwa na kujaribu kuficha ukweli wa mambo yao maana kwa kufanua hivyo wanachafua hadhi ya kanisa pia wanachochea uovu mwingne.
  Kwa kitendo alicho kifanya ni wazi hafai kuendelea kuwa padri maana kamtia mimba kaficha ukweli, kamteka mtoto. Hii ni too much yani kadhamiria huyu.
  Ni aibu sana na inasikitisha.
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Padre hakupata mshauri mzuri. Angempangishia nyumba huyo mama wa mtoto na kumpa matunzo yote kama wanavyofanya wenzake. Wala hakuna mtu/mwandishi angewahifahamu aliko huyo mzazi mwenzie.
  .
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mapadre ni individuals wenye udhaifu kama mimi na wewe. Matendo yasiyokubaliki ya padre mojawapo hayalitikisi Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume.
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  huyo padri ni kiwembe mno, ila mleta mada ana ajenda kubwa na waktristu na hajaanza leo

  laana'kum!
   
 10. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  mapadri hawajazaliwa kuwa miungu...hivyo huyo ni binadamu kama wewe na anawaka tamaa kama wewe kwa hiyo kunakuteleza kama wewe.
   
 11. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wako wengi sana hao
   
 12. okaoni

  okaoni JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 1,197
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Huyu shigongo magati yake yote ni deffermative.ukiangalia juu ya gazeti ameandika "in god we trust" lakini ukisoma between line ya makala zake hayafanani na jina kuu analolitumia kutangazia biashara yake hiyo.sijui nio god gani aliyemuandika.au halina mhariri?hau mharriri wake ni wa kimipashomipasho?ila jamaa kapata mabilioni kwa vihabari hivyo hivyo na wateja wake ni wengi kweli kweli
   
 13. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Big up Dr Slaa!Yalimshinda haya akajivua gamba mapema!!Jamani upadre ni wito siyo kazi ya kuganga njaa kama nyingine!!
   
 14. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watawa wa kike ( masista) ni chakula halali kwa mapadri. Huyu Mwasiti vipi?
   
 15. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo kama ameandika 'in God we trust' akiona uovu kwnye jamii acseme?we naye??
   
 16. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  upuuzi mtupu hii habari imeandikwa kisanii
  tangu lini MWASITI jina la kiislamu akafanya kazi nyumba za mapadri?
  masista wa mburahati wamejaa tele iweje mwasiti asie mkatoki aje kufanya kazi hiyo
  atakebisha abishe hakuna jina la kikristo mwasiti.
   
 17. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kanisa takatifu huzalisha waumini watakatifu waisotenda dhambi maana MUNGU wao wanayemwabudu ni Mtakatifu. Na wanafahamu fika uwa dhambi zao zilibebwa na BWANA YESU pale msalabani. Yaani si waasherati, si wazinzi, si waongo, si walevi, si wala rushwa, si wachawi, si waenda kwa wanganga, si mafisadi, hawafungishi ndoa wadada wenye mimba, n.k. Lipime kanisa katoliki katika haya kisha utapata jibu.
   
 18. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hao mapidri ni binadamu nao wanahisia km sisi tu na ukizingatia wanakula vizuri maisha safi hakuna fikra zingine lazima ushawishi utakuja tu na mpaka kazaa nae walianza muda mrefu mbona huyo msichana hakusema mpaka mimba.
   
 19. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Unaposema Katoliki au Catholic unamaanisha universal/whole, so skendo ya Mburahati haiwezi kutikisa "universal". Mimi mwenyewe nipo hapa hapa Dar na wala sijatikiswa, itakuwa Catholic? Padre amefanya dhambi ya uzinifu, alitakiwa atubu dhambi zake na Mungu ni mwema, anasamehe. Hakuwa na sababu ya msingi ya kumkimbiza mtoto, kosa si kuzaa, kosa kuzini (kulikopelekea uzazi). Mungu hafichwi kosa hata kama binadamu atafichwa, so alichotaka ni kuepuka aibu tu ya wanadamu wenzake!
   
 20. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umenena vyema...wewe ni mkatoriki siyo mkatoliki...!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...