Skendo ya ngono yatikisa kanisa katoliki..

Status
Not open for further replies.
kumbe gazeti la udaku

hivi wewe unafikiria kwa kutumia nini zaidi? nadhani unahitaji kupimwa akili yako

kwa taarifa yako ni kwamba hayo magazeti ya udaku ndiko mambo mengi ya kweli huanzia kama udaku

fikra mgando na hasi
 
Huyu shigongo magati yake yote ni deffermative.ukiangalia juu ya gazeti ameandika "in god we trust" lakini ukisoma between line ya makala zake hayafanani na jina kuu analolitumia kutangazia biashara yake hiyo.sijui nio god gani aliyemuandika.au halina mhariri?hau mharriri wake ni wa kimipashomipasho?ila jamaa kapata mabilioni kwa vihabari hivyo hivyo na wateja wake ni wengi kweli kweli

mimi bado siwaelewi watanzania
kwa hiyo mnataka Shigongo aandike uongo ndio mtafurahia? mbona alichokiandika kipo wazi kabisa? watanzania mala nyingi hampendi kuelezwa ukweli,pindi ukielezwa ukweli basi unataka kurusha ngumi

kwa wenzetu wa walioko nje ya tanzania wanalielewa hili la ukweli,kwani watu weupe huwa hawana kupinda pinda,anakueleza ukweli tu kuwa we bwana ni mchoyo,fisadi,huna akili,kwenu kuna vita ni masikini,wala hawana maneno matamu ya kuzunguka sasa watanzania wengi huwa tunapata tabu sana kwani hatujazoea kuelezwa ukweli ndio tatizo letu

tubadilike na tukubari pale tunapoelezwa ukweli,tusitafute visingizio
 
Kanisa takatifu huzalisha waumini watakatifu waisotenda dhambi maana MUNGU wao wanayemwabudu ni Mtakatifu. Na wanafahamu fika uwa dhambi zao zilibebwa na BWANA YESU pale msalabani. Yaani si waasherati, si wazinzi, si waongo, si walevi, si wala rushwa, si wachawi, si waenda kwa wanganga, si mafisadi, hawafungishi ndoa wadada wenye mimba, n.k. Lipime kanisa katoliki katika haya kisha utapata jibu.

Wewe nawe unachuki binafsi,kuna mwanadamu asiyekosa hapa duniani? Hakuna binadamu ambaye ni mtakatifu,kwa kifupi hakuna mtakatifu anayeishi....Kwani wewe wa dhehebu gani? Nyie ndo walewale wa bwana... Sijui bwana nini,bwana mume wa mtu au? Mnajifanya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu.
 
Naona heading yako ungesema Parokia ya Mburahati yatikiswa na kashfa ya Ngono!
Ukisema kanisa as a whole usichukie ukiambiawa izo habari za Udaku!
Kwa taarifa yako iyo ni moja tuu kati ya over 50 parishes kwa jimbo la DSM.
Alafu on the other hand huyo padre kama binaadamu amekwazwa so yampasa atubu na hana tofauti na wewe unayetembea na nyumba ndogo vyote ivyo ni Uzinzi.Ila kifanya padre naona kwako utaita uzinzi zaidi sijui
 
upuuzi mtupu hii habari imeandikwa kisanii
tangu lini MWASITI jina la kiislamu akafanya kazi nyumba za mapadri?
masista wa mburahati wamejaa tele iweje mwasiti asie mkatoki aje kufanya kazi hiyo
atakebisha abishe hakuna jina la kikristo mwasiti.

mkuu tembea uone

ucje kwenda misri ama algeria ukaanza kushangaa na kutaka wale wote wenye majina ya mwasiti watoke kanisani

ni kwamba,haya majina ni sisi wananchi tulio amuwa kutenganisha majina ya kiislam na kikisto,ni kama vile salamu ya ALSAAM ALEIKUM tunavyo dhani ni salamu ya kiislamu pekeyao si kweli kabisaaaa

ukipata nafasi ya kutembelea nchi za kiislamu utashangaa sana,kwani ukihudhuria kanisani salamu ya kwanza ni ASLAAM ALEIKUM waliokwenda misri,gaza,iraq,kuwait,iran wamejionea wenyewe,lakini pia ukiwa huko majina kama hussen,juma,hamisi,hadija,abdukarim ktk nchi hizo utayakuta kanisani na nakuomba ucje shangaa kwani nao watakushangaa pia
 
Tumieni muda mwingi kujiendeleza ili maisha yenu yawe mazuri,mwondokane na ujinga na umaskini.Hakuna muda tena wa kukaa na kuwakosoa wengine.
Nashangaa sana wanafki wanakazana kupost matukio ya aibu yanayosadikiwa kulikumba kanisa takatifu katoliki la mitume,badala ya kukaa na kufanya mambo ya maendeleo.
Kati ya wale waliosulubiwa pamoja na Yesu msalabani,mmoja wao alionekana kumkejeli Yesu kwa yeye kusulubiwa pamoja nao. Lakini mwenzake alionekana kuwa na huruma na kumkemea yule,na Yesu akamuhakikishia kuwa naye.....
Pia,usitoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati kwenye jicho lako kuna boriti,ondoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona vizu kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
Je,nyie mnao anika mapungufu ya wenzenu ni wasafi kiasi gani?
 
View attachment 50310
Skendo ya ngono inaitikisa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mburahati lililopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusababisha mgawanyiko mkubwa kwa waumini.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu zimebaini kuwa skendo hiyo ya ngono inamhusisha Padri Paul Njoka na mhudumu wa nyumba za mapadri ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo aliyejulikana kwa jina moja la Mwasiti.
Taarifa zilizopatikana kanisani hapo zinadai kwamba padri huyo alimjaza mimba mhudumu huyo na hivi sasa amezaa naye mtoto.
Habari hizo zilienea kanisani hapo na kusababisha baadhi ya waumini kutaka suala hilo liwekwe wazi ili kiongozi huyo achukuliwe hatua zaidi, jambo lililomfanya kasisi huyo atafute jinsi ya kujihami.
Chanzo chetu cha habari kinasema kwamba baadhi ya viongozi wa kanisa hilo walifikia hatua ya kutafuta jinsi ya kumficha mtoto huyo baada ya kuzaliwa ili kupoteza ushahidi.
Imeelezwa kwamba Februali 4, mwaka huu Padri Njoka akiwa na muumini aliyejulikana kwa jina la Maria Kaswela walichukua gari na kumsaka Mwasiti, walimpata na kumuingiza katika gari hilo.
Imedaiwa kwamba katika mzunguko wao, Mwasiti hakujua ni kitu gani alichotakiwa kufanyiwa na mtoto wake bali yeye alijua ni matembezi ya kawaida huku akifurahia ni jinsi gani padri anavyompenda mtoto wake na kuamua kuzunguka naye jijini kwa siku hiyo.
Chanzo kilidai kwamba siku hiyo padri huyo na mzazi mwenzake walielekea Sinza,Manzese kisha Magomeni.
MTOTO ATEKWAWalipofika Magomeni habari zinasema walimtuma dukani mama wa mtoto (Mwasiti) na mtoto akawa amebebwa na Maria.
Chanzo kiliendelea kudai kwamba padri aliendesha gari na kuondoka eneo la Magomeni kwa kasi kuelekea kusikojulikana na Mwasiti alipotoka dukani na kwenda sehemu lilipoegeshwa gari hakuwaona na alipowapigia simu hawakupatikana.
TAARIFA YAFIKA POLISIHata hivyo, Mwasiti alipatwa na hofu kwani ilimchukua muda mrefu bila kuwaona, kitendo kichomfanya aende Kituo cha Polisi, Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni kutoa taarifa ya kutekwa kwa mtoto wake wa siku 28 tangu azaliwe.
Mwasiti alifunguliwa jalada lenye kumbukumbu MG/RB/2430/2012 ndipo polisi walipoanza kazi ya kuwatafuta padri na Maria bila mafanikio.
Habari zinasema polisi walifanikiwa kumuona Padri Njoka akiwa kanisani siku ya Jumapili akiendesha ibada ila ilishindikana kumkamata kwa sababu misa ilikuwa ikiendelea.
Kutokanana kitendo cha padri huyo kuendesha misa, askari hao waliacha taarifa kwa mlinzi wa kanisa hilo kwamba baada ya kumaliza ibada afike Kituo cha Polisi Magomeni akiwa na Maria.
Hata hivyo, hawakwenda siku hiyo badala yake walienda kesho yake Jumatatu ya Februali 6, mwaka huu.“Mara walipofika kituoni waliwekwa chini ya ulinzi, walibanwa ili waonyeshe alipo mtoto ambapo walisema kwamba yupo Kigamboni kwa ndugu wa padri huyo,” chanzo hicho kilisema.
Polisi waliwaamuru watoe namba ya simu ya watu walio na mtoto huyo ili wapigiwe, padri alitoa, ilipopigwa aliye na mtoto akaamriwa amlete kituoni hapo na akafanya hivyo saa 5.00 usiku padri akiwa chini ya ulinzi.
Hata hivyo, polisi walipomkabidhi Mwasiti mtoto wake alikataa kumpokea na kudai kwamba akapimwe afya yake kwanza kwa vile hakujua alichofanyiwa huko na alikua katika mazingira gani.
Chanzo kiliendelea kusema kwamba hapo polisi Magomeni alikuwepo pia Paroko Timoth Nyasulu Maganga ambaye ni mkubwa wake wa kazi Padri Njoka.
Habari zinasema Padri Maganga alimbembeleza Mwasiti amchukue mtoto wake ambaye alikubali kisha alikwenda naye Kinondoni kwa dada wa mzazi huyo. Uchunguzi wetu umebaini kuwa kesi hiyo ipo chini ya mpelelezi mwenye namba WP697 Tiba.
WARAKA KWA PENGO Kutokana na kitendo hicho, baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliamua kumuandikia barua Februali 8, mwaka huu Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Askofu Polycarp Kadinali Pengo kuhusu udhalilishaji wa Kanisa Katoliki waliodai kufanywa na padri huyo kwa kumteka mtoto.
Katika barua hiyo (Nakala tunayo) waumini hao wameeleza jinsi wachunga kondoo walivyofikia hatua ya kufanya mapenzi na wafanyakazi, wahudumu wa nyumba ya mapadri na kuwapa mimba.
Hata hivyo, katika barua hiyo waumini hao wamesikitishwa na kitendo hicho na kudai kuwa gharama kubwa za fedha za kanisa zimetumika kushughulikia suala hilo.''Tunakuomba ufanyie kazi jambo hili kwa haraka inawezekanavyo ili kuepusha uvunjifu wa amani endapo viongozi hao wachafu watabaki hapo parokiani,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa mapenzi yanayofanyika kanisani hapo kati ya viongozi na waumini yamesababisha utoaji hovyo wa mimba hadi wengine kuzalishwa, kitendo ambacho kinalitia aibu Kanisa Katoliki.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela hakupatikana kuzungumzia tukio hilo lakini afisa mmoja wa cheo cha juu wa jeshi hilo alithibitisha kuwepo kwa madai hayo kuongeza kuwa upelelezi bado unaendelea.
Aidha, Kadinali Pengo hakuweza kupatikana kuzungumzia malalamiko hayo ya waumini wake.Gazeti hili linaendelea kufuatilia sakata hilo kwa undani zaidi ili kujua ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.skendo ya ngono yatikisa kanisa katoliki... - Global Publishers

Pamoja na kwamba kufanya skendo ni vibaya, hatuwezi kusikia upande mmoja wa stori na kuanza kutoa hukumu. Kama ni kosa la kisheria, tusubiri ushahidi utakaotolewa mahakamani. Otherwise, tunachofanya hapa ni majungu/udaku kama stori inakotokea kwenye udaku!
 
Kanisa takatifu huzalisha waumini watakatifu waisotenda dhambi maana MUNGU wao wanayemwabudu ni Mtakatifu. Na wanafahamu fika uwa dhambi zao zilibebwa na BWANA YESU pale msalabani. Yaani si waasherati, si wazinzi, si waongo, si walevi, si wala rushwa, si wachawi, si waenda kwa wanganga, si mafisadi, hawafungishi ndoa wadada wenye mimba, n.k. Lipime kanisa katoliki katika haya kisha utapata jibu.

Tumieni muda mwingi kujiendeleza ili maisha yenu yawe mazuri,mwondokane na ujinga na umaskini.Hakuna muda tena wa kukaa na kuwakosoa wengine.
Nashangaa sana wanafki wanakazana kupost matukio ya aibu yanayosadikiwa kulikumba kanisa takatifu katoliki la mitume,badala ya kukaa na kufanya mambo ya maendeleo.
Kati ya wale waliosulubiwa pamoja na Yesu msalabani,mmoja wao alionekana kumkejeli Yesu kwa yeye kusulubiwa pamoja nao. Lakini mwenzake alionekana kuwa na huruma na kumkemea yule,na Yesu akamuhakikishia kuwa naye.....
Pia,usitoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati kwenye jicho lako kuna boriti,ondoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona vizu kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
Je,nyie mnao anika mapungufu ya wenzenu ni wasafi kiasi gani?
 
Wewe nawe unachuki binafsi,kuna mwanadamu asiyekosa hapa duniani? Hakuna binadamu ambaye ni mtakatifu,kwa kifupi hakuna mtakatifu anayeishi....Kwani wewe wa dhehebu gani? Nyie ndo walewale wa bwana... Sijui bwana nini,bwana mume wa mtu au? Mnajifanya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu.

waebrania 16;3, waebrania 12:14 na 1petro 1:15-16
 
Tumieni muda mwingi kujiendeleza ili maisha yenu yawe mazuri,mwondokane na ujinga na umaskini.Hakuna muda tena wa kukaa na kuwakosoa wengine.
Nashangaa sana wanafki wanakazana kupost matukio ya aibu yanayosadikiwa kulikumba kanisa takatifu katoliki la mitume,badala ya kukaa na kufanya mambo ya maendeleo.
Kati ya wale waliosulubiwa pamoja na Yesu msalabani,mmoja wao alionekana kumkejeli Yesu kwa yeye kusulubiwa pamoja nao. Lakini mwenzake alionekana kuwa na huruma na kumkemea yule,na Yesu akamuhakikishia kuwa naye.....
Pia,usitoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati kwenye jicho lako kuna boriti,ondoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona vizu kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
Je,nyie mnao anika mapungufu ya wenzenu ni wasafi kiasi gani?

.
Ndugu ingekuwa mambo yako kama unavyotaka kutuaminisha na RC ni kanisa takatifu la mitume, basi hata Yuda Iskariote angelikuwa mtume leo na mtu wa kujifunza kwa wale 11 waliobaki jinsi walivyomwombea rehema.
Tatizo lako hujui kutofautisha kati ya bahati mbaya ya mwanadamu na lile la kukusudia kutenda makusudi tena kwa gharama yoyote.
Maana padre kumpa ujauzito mwanamke yeyote ni swala la kughafilikiwa dhidi ya kiapo chake lakini kuteka na kumwiba mtoto mchanga kwa mama huku mama akiachwa barabarani akiwa lonely ni ugaidi wa kupangwa na kutekelezwa.
.
 
quote_icon.png
By MziziMkavu

Imedaiwa kwamba katika mzunguko wao, Mwasiti hakujua ni kitu gani alichotakiwa kufanyiwa na mtoto wake bali yeye alijua ni matembezi ya kawaida huku akifurahia ni jinsi gani padri anavyompenda mtoto wake na kuamua kuzunguka naye jijini kwa siku hiyo.

Hapo ndipo anaponifurahisha Shigongo.. Anajua jinci gani ya kuiremba na kuipa uhai hadithi yake.. Jamaa anajua kuzitega..
 
upuuzi mtupu hii habari imeandikwa kisanii
tangu lini MWASITI jina la kiislamu akafanya kazi nyumba za mapadri?
masista wa mburahati wamejaa tele iweje mwasiti asie mkatoki aje kufanya kazi hiyo
atakebisha abishe hakuna jina la kikristo mwasiti.

Mkuu kama ngumu kutafuna imeze, habari ndio hiyo!!!
 
.
Ndugu ingekuwa mambo yako kama unavyotaka kutuaminisha na RC ni kanisa takatifu la mitume, basi hata Yuda Iskariote angelikuwa mtume leo na mtu wa kujifunza kwa wale 11 waliobaki jinsi walivyomwombea rehema.
Tatizo lako hujui kutofautisha kati ya bahati mbaya ya mwanadamu na lile la kukusudia kutenda makusudi tena kwa gharama yoyote.
Maana padre kumpa ujauzito mwanamke yeyote ni swala la kughafilikiwa dhidi ya kiapo chake lakini kuteka na kumwiba mtoto mchanga kwa mama huku mama akiachwa barabarani akiwa lonely ni ugaidi wa kupangwa na kutekelezwa.
.

Ninachoamini mimi ni kwamba,mungu wetu ni mwenye huruma na mwingi wa rehema.Na husamehe pale unapomwomba msamaha.
Kwani ni mara ngapi wana wa Israeli walimkosea mungu,wakatubu na mungu akawapokea? Kwani unadhani waliyokuwa wakitenda walikuwa hawajui? Ninaamini kwamba,unapomkosea mungu na kutambua makosa yako na kuomba msamaha mungu atakusamehe!
Sio kwamba natetea kilichofanyika kama ni kweli,ila tatizo ni unafki wa wachache humu jf ambao wanajifanya wasafi sana.Mbona skendo nyingine hawakazani kuziport humu? Ila za RC ndo zinaonekana sana.
 
.[/QUOTE]

Mkuu Msafiri, karibu kupata kipande cha mbuzi katoliki wa roma na glasi ya rubisi. Asante kwa juhudi.
 
mnapoteza muda kuchunguza padri kafanya nn
hamwazi kwann mko nyuma kielimu,kwann hamna maendeleo
padri kuzaa sio habari ndio maana magazeti yeney akili hayajaandika
labda ni habari ya msingi kwa nyie wadakuzi
watu ambao hamjui kwann kanisa katoliki halitetereki limesimama hadi leo
kwanini wakristo wameelimika na wako mbele kila kitu.Mtabaki na majungu yenu mtaishia kukaa vibarazani sie twasonga mbele.mtaishia kulaumu serikali lkn serikali hiyo imewabeba mmeshindikana
Nimetembea sana ndugu lkn kanisa halibatizi majina hayo mwasiti.
 
Ninachoamini mimi ni kwamba,mungu wetu ni mwenye huruma na mwingi wa rehema.Na husamehe pale unapomwomba msamaha.
Kwani ni mara ngapi wana wa Israeli walimkosea mungu,wakatubu na mungu akawapokea? Kwani unadhani waliyokuwa wakitenda walikuwa hawajui? Ninaamini kwamba,unapomkosea mungu na kutambua makosa yako na kuomba msamaha mungu atakusamehe!
Sio kwamba natetea kilichofanyika kama ni kweli,ila tatizo ni unafki wa wachache humu jf ambao wanajifanya wasafi sana.Mbona skendo nyingine hawakazani kuziport humu? Ila za RC ndo zinaonekana sana.

Ndugu wale walozaliwa kwa mwili ni wa mwili na waliozaliwa kwa roho ni wa roho. Na wanaoongozwa na Roho wa MUNGU ndo wana wa MUNGU na wanaoongozwa kwa mwili ni wa shetani (Warumi 8:14). Je wewe uko upande gani? Kama alivyosema Kiby kuna mtu kukosea na akatubu sawa, lakini si mtu kuishi maisha ya dhambi kama kanisa katoliki lilivyochagua. Sasa kama unaona kusema ukweli ni chuki binafsi hilo ni tatizo kubwa. Cha kufanya mwamini BWANA YESU kuwa BWANA na mwokozi wako na uachane na propaganda za uongo za kumwamini bikra Maria ambaye alikuwa mwanadamu tu wa kawaida aliyekuwa na hofu ya MUNGU. YESU ni yote katika yote na Yeye ndo mwombezi wetu (Waebrania 7:25 ) na si watakatifu waliokufa ambao hawana sehemu tena katika jambo lolote linalofanyika chini ya jua (Mhubiri 9:5)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom