Sizonje kashachanganyikiwa,yeye ni kuteua kutengua.kila aliemzunguka hamuamini,anaona yy ni mtakatifu sanaa
Popo mbili zavuka mto!!!Jamani mmeniacha Gizani.sizonje ndo nani
Kwa hiyo Mkwere ana watu wake nda ya timu ya mzee wa hapa kazi tu,ambao ndiyo wanamkwamisha?Sikubaliani na were kuwa kachanganyikiwa; mimi naona kuwa ana mipango yake mikubwa juu ya nchi hii, na anapopangua ni pale anapoona hao waliopo hawana kasi yake ya kuweza kutimiza malengo yake katika muda huu mfupi!! Ili kupata watu wanaoendana na kasi yake hana budi kufanya due diligence ya watu wengi ambao yeye peke yake hawezi kuwafahamu; kuna wasomi wengi wanaoweza kumsaidia lakini system iliyopo ya mkweree haiwapendi!!
Mikataba ya miaka 100 imefanya nini? Ww unafikiri huko pataguswa? punguza ukada wa chama mkuu,hii nchi bado ni ya ahadi, tulia hapo hapo ulipo usubiri.Tatizo lenu mpo kama watoto walioachishwa ziwa kunyonya huwa wanalia usiku kucha wakiona wanaonewa na ni haki yao kunyonya siku zote kumbe hawajui kuna hatua zinazofuatia mbeleni pengine zitakuwa nzuri au mbaya huo ni mfano tatizo sio Magufuli tatizo ni mfumo na maisha tuliozoeya kuishi ya wizi, ulaghai ,rushwa, dhuluma na mengine yafananayo nayo, sasa Rais anajitahidi kurudisha katika misingi na mfumo uliobora wa kuyafikia malengo watu mnaona taabu ,
Hii nchi jama hata angelishuka malaika kwa hali iliyokuwa imefikia hangeweza kuiongoza humu kila mtu msemaji kila mtu mjuaji cheusi kita takatishwa kuwa cheupe inabidi kujitoa ufahamu tu kuiongoza hii nchi watanzania hatubebeki ,
Mmesahau kuna mikataba ya miaka mia moja humu hembu tuwe na utu jama tumsaidie Rais kuendesha hili gurudumu la maendeleo tuache kulia lia Mungu hapendi namalizia kusema asiyefanya kazi na asile na mikono milegevu hujenga paa bovu.
Mimi sio ccm mdau na kamwe haitatokea ila penye ukweli lazima tuseme Rais nae ana moyo na sio wa chuma ni wa nyama haya mambo mdau hayahitaji papara inahitajika hekima busara na maarifa kuweza kuyatatua kwani wahusika bado wapo na wanamaslahi yao binafsi cha muhimu mimi na wewe kumpa moyo na kuikataa rushwa na kuwa wazalendo.Mikataba ya miaka 100 imefanya nini? Ww unafikiri huko pataguswa? punguza ukada wa chama mkuu,hii nchi bado ni ya ahadi, tulia hapo hapo ulipo usubiri.
YohanaJamani mmeniacha Gizani.sizonje ndo nani
Baraza la mawaziri su benchi la ufundi?eti nasikia yeye ndio analishauri baraza LA mawaziri badala ya wao kumshauri,sizonje ni giniaz
Maana ya Catalyst pale ndio umefika!Anakamchapio safi..!! UKIEMBA DUKANI DAI RISITI
Walisema yule akienda pale hamalizi wiki 2 atakuwa amesha kufa. Ajabu wakafa wao! Chezea Mungu wewe?duh........
Anamtoa bodi ti ara ei halafu anamwingiza?...Ndugu msikilizaji nilikosea kumbe ndo kwanza mpira upo katikati ya dimba tunasubiri kocha sizonje afanye mabadiliko mengine.
Mhurumieni kasema alikuwa hana vocha akabip ikajipigaSizonjeee uliona mepesi sasa wajuta Sizonje
Umeelewa nn hapo mpaka useme hivo kaka au imepenyaaaa[emoji3]
Mkuu umezungumzia mikataba, ndicho hicho nilicho uliza,kwamba mikataba imefanya nini? unafikiri huko pataguswa? kumbuka Rais alisema atawalinda wale wazee wasiwe na wasiwasi wakae watulie,ww unafikiri Rais alikuwa anamaanisha nini? tuchangishane tu huku mtaani na si habari ya mikataba ya madini,hayo makaburi yanatisha matambiko iliyofanyiwa hapo si ya pole pole ,mtu anafunga mkataba wa miaka 100 na muwekezaji kuna nini hapo? ni hatari sana mkuu ukisogea tu lile eneo la makaburi unazimia, think big man.Mimi sio ccm mdau na kamwe haitatokea ila penye ukweli lazima tuseme Rais nae ana moyo na sio wa chuma ni wa nyama haya mambo mdau hayahitaji papara inahitajika hekima busara na maarifa kuweza kuyatatua kwani wahusika bado wapo na wanamaslahi yao binafsi cha muhimu mimi na wewe kumpa moyo na kuikataa rushwa na kuwa wazalendo.
Raisi yupi unayemzunguzia mkuu maana wapo wengi. Raisi wa wasafi, rais wa tff, rais wa wagumu family, rais wa Real madrid, rais Syria nk nk. Sasa sijui wewe unamlenga yup maans wewe ndio umeibuka na hilo jinaNi wapuuzi sana hawa, hii nchi imejaa wanafiki sana, angalia majina ya kinafiki anayopewa raisi, nyie ndio mtasababisha hii forum ifungiwe, endeleeni kumchafua chafua, mwenzenu kafungwa kisa ameota, kufungiwa hii ni issue ndogo sana
Hao sijui wanatokea wapi wenzao tunamjadili kocha wetu Sizonje wao wanaleta siasa!!Raisi yupi unayemzunguzia mkuu maana wapo wengi. Raisi wa wasafi, rais wa tff, rais wa wagumu family, rais wa Real madrid, rais Syria nk nk. Sasa sijui wewe unamlenga yup maans wewe ndio umeibuka na hilo jina
Mmmmmh!!Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...
Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....
Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!
Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!
Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!
Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!
Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!
Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!
Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.