MILKYWAY GALAXY
JF-Expert Member
- Dec 12, 2008
- 204
- 87
Mimi napingana kabisa na mtoa mada kwani naona ametumia mtindo kiuandishi tunaita amehodhi hoja.
Awali ya yate ni lazima kujua kuwa upinzani sio uadui, lakini vile vile tunapashwa kujua nia na madhumuni ya kuwepo upinzani ni kuleta hali bora kwa jamii husika. Kwa msingi huo upinzani upo pale kuleta hoja mbadala zenye kuweza kukinzana na zile za Serikali kwa nia ya kuchochea maendeleo ya jamii husika kwa haraka.
Siku zote vyama vinakuwa na ILANI zake ambazo zinaeleza bayana vipaumbele na mtazamo wako katika kuiongoza jamii , lakini ikumbukwe kuwa Ilani hizo sio msahafu au Biblia kuwa haiwezekani kuzibadili kulingana na hali halisi na mwelekeo wa maisha.
Kwa kuwa vyama vyote tawala na upnzani wote wana nia ya kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii basi chama makini ni kile kinachokubali kukosolewa na kubadili mwelekeo wake kwa nia ile ile ya kuleta maendeleo ya jamii . Kwa msingi huo vyama vya upinzani vina wajibu wa kuikosoa Serikali au chama tawala na hata kuwaeleza njia sahihi ya kuleta maendeleo. Ndio maana ILANI zao zinakuwa sio Siri zinawekwa wazi na mtu yeyote anaweza ku borrow na kuzitumia katika kuendeleza jamii.
Kwa msingi huo tunasema Ni jukumu la wapinzani kuikosoa Chama tawala katika kuhakikisha kuwa wanaleta ustawi wa jamii.[/B]
.Chonde chonde Chadema kisiige dhana ya siasa za umamuluki za
kudhoofishana kwa kueneza uongo kuficha udhaifu wake....Kazi ya chama kiadilifu cha
upinzani ni kuwa karibu na wananchi na kujua hasira za wananchi za ukweli ni kuhusu
matendo yepi ya chama kilicho madarakani kwa miaka 50 hadi leo hii...na CCM
kimejidhoofisha na kinazidi kujidhoofisha chenyewe kwa ubaradhuri na jeuri ya
kijinga ya viongozi wake wenye kulemewa na mawazo ya kujilimbikizia mali
yakichanganywa na ulevi wa madaraka yasiyo na ukomo ...... Chama cha siasa makini
daima kikumbuke kuwa wananchi walio wengi si wanachama wa chama chochote cha
siasa...Mara nyingi wananchi , hasa vijana, hawakiamini chama chochote kinachokaa
madarakani kwa muda mrefu huku maisha ya walio wengi yakizidi kuwa ya matatizo
matatizo....Chonde chonde Chadema kisiige dhana za siasa za maji taka zinazotawala
CCM ya mafisadi waliowaengua viongozi wa CCM makini kama Dr. Salim Ahmed Salim
katika mchakato wa uteunzi wa ugombea wa urais mwaka 2005 kwa dhana kuwa urais ni
ulaji na ilikuwa ni zamu ya fulani badala ya fulani kula....Tutafakari kwa kina juu
ya tofauti kati ya nini maana ya upinzani adilifu na upinzani wa umamuluki...
Mwl. Azaveli Lwaitama
Role of opposition parties
Kazi kuu za opposition parties, include, watchdog role (kukosoa serikali iliyoko madarakani), giving alternative viewpoints.The Opposition's main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public.Thus the opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate. Kwa hivyo CHADEMA wanapoonyesha udhaifu wa serikali such as corruption, mismanagement of the national resources, na faulty policies, mimi naona wako sahihi kabisa kwa vile hatutarajii, kwa mfano, serikali iliyoko madarakani ijikosoe yenyewe. Kwa maana nyingine ni kwamba chadema wanapoonyesha madhaifu ya CCM ni dhahiri kwamba wanaidhoofisha serikali in public eyes, (people loose confidence to their government).
Hii ni sehemu ya kudhoofisha chama tawala.Kazi kubwa iliyofanywa na CDM ni pamoja na kuelimisha au kuwafumbua macho milions of Tanzanians ambao walikuwa hawajui jinsi ufisadi ulivyokuwa ukifanywa cladenstinely na madhara yake kwenye jamii yetu.
chadema iCOPY KUTOKA CCM?.
Kwenye article yako umetanabaisha kuwa "CHADEMA kama kweli kinataka kuja kushika madaraka ni lazima kitambue na kianze kufikiri nakutenda kama chama kinachotaka kutawala. Viongozi na wanachama wake, mashabiki na wapenzi wake ni lazima wawe na fikra kama waliyonayo wana CCM na viongozi wao. CCM imejenga imani ndani ya wanachama wake kuwa kinataka kutawala na kitatumia mbinu zozote zile.
Wamefanikiwa hivyo kwa sababu wameweza kuidhoofisha serikali na chama kilichoko madarakani.Napenda kuhitimisha kwa kusema kwa kusema kwamba chadema wako on the right path, has few but competent people in all crucial fields.Na ndiyo maana hivi sasa kinaungwa mkono na idadi kubwa watanzania ukilinganisha na miaka ya hapo nyuma.
Ni uchambuzi mzuri sana, ni kweli jukumu la chama cha upinzani si kuishauri serikali wala kuikosoa ili ijirekebishe bali ni kuikosoa(criticize) kwa yale iliyofanya ili kuidhihirishia jamii kuwa serikali haiwezi kutimiza matakwa yao ipasavyo, na kuidhoofisha ili ipoteze ujasiri na ichanganyikiwe. Matokeo yake ni wananchi kupoteza imani kwa chama tawala. .
Good message.ni muhimu tuifanyie kazi.nakupongeza kwa kutumia mda wako mwingi kupigana vita hii ya kutufunza na kutuhabarisha.Na. M. M. Mwanakijiji
SIYO jukumu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukikosoa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ili vijirekebishe na hatimaye viweze kutekeleza majukumu yao vizuri. Siyo kazi ya CHADEMA kuwa mkosoaji mkuu wa serikali ili serikali iweze kujisahihisha na kufanya kazi yake vizuri ya kuwahudumia wananchi. Kwa hakika kabisa siyo jukumu la upinzani nchini kuipatia CCM na serikali iliyoko madarakani mawazo mapya ya mambo ya kufanya ili mambo hayo yafanywe na kila mtu awe na furaha. Ni makosa ya kifikra na kutoelewa siasa kudhania au kukubali kuwa upinzani jukumu lake ni kuikosoa serikali.
Inasikitisha Lwaitama ameweka maneno ambayo mimi sikuyatumia. Kudhoofisha chama tawala haiitaji uongo au majitaka inahitaji mbinu za kisayansi ambazo zinazingatia ukweli. Utaona kwenye makala yangu haihusiani na kuwadanganya umma au kuwafanya wananchi waamini kitu kisicho cha kweli. Huwezi kujenga nchi kwa kusimamia kwenye uongo kwani kutawala kwa kutegemea ulaghai na maneno matamu ndiko kumefanywa na CCM kwa miaka 50.
Hapa Mzee MKJJ hutakiwi kusikitika kwa maana hukueleza mbinu hizo za kisayansi ni zipi. ingependeza kidogo kama ungetoka nje ya Rhetoric na kuivisha nyama kidogo kidogo hoja yako ili tuone unasimamia nini katika hii mada.
Je ni mbinu gani hizo za kisayansi unazoziona!, je Propaganda siyo mojawapo?.
Msingi wa hoja hii ni nini?, kwa sababu binafsi ninaona Chadema toka ianzishwe imefanya na inaendelea kufanya juhudi za kuing'oa CCM madarakani, na uchaguzi wa 2010 ni ushahidi tosha kuonyesha ni jinsi gani Chadema ilikuja CLOSE. na kwa mantiki hiyo basi juhudi za kuidhoofisha CCM zimekuwepo tangia awali na hivi sasa ndiyo zimepamba kasi. Kujaribu kuimply kwamba CHADEMA haiidhoofishi CCM ni kutokuzingatia picha pana ya harakati zake.Kama Chadema wangetaka kweli kuiondoa CCM madarakani kama nilivyosema huko nyuma hakukuwa na wakati mzuri na nafasi nzuri kama katika uchaguzi wa 2010. Chadema (kama chama na kiuongozi) walitaka kupata wabunge wengi ili wawe chama kikuu cha upinzani Bungeni na hivyo siyo viongozi wake wote waliotaka CCM iangushwe mwaka jana. Huwezi kwenda vitani kama walivyofanya US and Allies in the 1990s kujaribu kumuondoa Sadam Husssen Kuwait lakini wakamuacha aendelee kutawala kwa karibu miaka kumi zaidi.
Hatari ni kuwa Chadema inataka kulazimishwa na chama tawala kuwa ni "chama cha upinzani" na hivyo kiwe kinafanya mambo ya "kuikosoa na kuishauri serikali". Katika fikra za baadhi ya wana CCMhiyo ndiyo nafasi ya upinzani. Mada yangu inalenga kuondoa fikra hizo. Huwezi kuwa mpinzani wa kudumu. Upinzani ni nafasi ya muda.
[qquote]isipokuwa ninakubaliana na wewe kwamba ni lazima juhudi hizo ziongezeke na ziwe za kisayansi zaidi zenye kuzingatia ukweli. siyo kuidhoofisha CCM for the case ya kuidhoofisha, kwa sababu ukidhoofisha na ilhali huna uwezo wa kudeliver so what?.
Kwa maoni yangu ni dhahiri, Kuimarika kwa Upinzani ndo kudhoofika kwa CCM yenyewe
Hapana kuidhoofisha CCM ni kuitaka ionakene haifai kuongoza na kujitahidi kuhakikisha wananchi wanabadili mawazo dhidi yake na kutumia mbinu zote zinazokubalika kuivuruga na hatimaye kuifanye ione uzito wa kutawala na aidha kusababisha uitishwe uchaguzi kabla ya wakati au kuifanya ifanye vibaya.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba CHADEMA hawaikosoi CCM bali wanaanika UOZO wa baadhi ya watu wa CCM. Mbinu ambayo imewapatia kura si haba mwaka jana. Ukimsoma vizuri Dr Slaa na wenzake wao hawadili na CCM, wanahangaika na watu ndani ya CCM.
Umeongea vema Mwanakijiji, lakini pia TUTAZAME upande mwingine ni wakuu wa vyama hivi-hivi pinzani ambao wengi wao wanaisaidia CCM kujisafisha na kusafika kwa ushauri wao wanaoutoa (pembezoni *indirect speech) na hilo machoni pa watu wa kawaida halionekani lakini kwa watu wanaofikiria WANALIONA na KUFAHAMU.
Huwezi kuwa unagombea mchumba na adui yako kisha UMWAMBIE "wewe utaendaje UKWENI na tongotongo!!?" kisha ionekane wewe na huyo hamna urafiki...
NAREJEA SEMI ZA AWALI:
MAJI HAYASAHAU BARIDI, WALIOTOKA CCM KWENDA UPINZANI WATABAKI KUWA CCM! WATAISHAURI CCM HUKU WAKIUMALIZA UPINZANI KWA SUMU YA POLEPOLE!
Kwa maana hiyo SITOIPENDA CCM wala KUVIAMINI VYAMA HIVI mpaka pale TAKA zote Zitapokuwa haziko.
CDM ni chama ambacho kina kigeugeu when it comes to philosophy. Ni chama ambacho falsafa yake wakati kinaanzishwa ilikuwa ni kupinga siasa ya ujamaa na kuruhusu wawekezaji binafsi zaidi.Globally,that was a movement in the 90s,but now with the emergence of neo marxism especially in South America brought about by the spirit of the Bolivar Socialist revolution,wananchi wengi wa Africa south of sahara,wanageuza mawazo yao na kugundua kuwa privatisation will not take us nowhere instead ina expand gap kati ya masikini na tajiri.
Na. M. M. Mwanakijiji
SIYO jukumu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukikosoa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ili vijirekebishe na hatimaye viweze kutekeleza majukumu yao vizuri. Siyo kazi ya CHADEMA kuwa mkosoaji mkuu wa serikali ili serikali iweze kujisahihisha na kufanya kazi yake vizuri ya kuwahudumia wananchi. Kwa hakika kabisa siyo jukumu la upinzani nchini kuipatia CCM na serikali iliyoko madarakani mawazo mapya ya mambo ya kufanya ili mambo hayo yafanywe na kila mtu awe na furaha. Ni makosa ya kifikra na kutoelewa siasa kudhania au kukubali kuwa upinzani jukumu lake ni "kuikosoa serikali".
WildCard,
Umetusoma vizuri sana. Kudhoofisha CCM ni pamoja na kuanika uozo wao. Mbinu zetu kwa kiwango fulani tayari zimewanufaisha wananchi, km kitendo cha kushasha bei ya sukari baada ya kumpa kikwete siku 9. Kuitaka CCM kutekeleza ajenda za CCM ni mkakati mahususi wa kuidhoofisha.
Watanzania hadi vijijini ambako leo nimekuwa kijiji cha Mambali (wilaya ya Nzega), Bukene na hatimaye Nzega jioni hii imethibitisha Watanzania wanaelewa vizuri tunachofanya, na wakati tumekuwa watetezi wa wanyonge kwa kuanika maovu ya watawala wanaona kabisa kuwa siyo tu tunaidhoofisha CCM, bali tunaifuta kabisa katika uso wa ardhi ya Tanzania. Hata hivyo ushauri wa MMKJ tunaupokea kwa moyo mkunjufu kama tulivyofanya siku zote.
Kikubwa ni dhamira ya kumkomboa Mtanzania na Taifa, mbinu zinaweza kutofautiana kwa kuwa katika mambo haya hakuna formula mmoja kama ilivyo kwa 2+2=4