1. Badala ya kutafuta riziki yangu kwa kufanya biashara zangu zinazonipatia kipato na kuniwezesha kuishi, eti nifunge biashara zangu kwenda kuandamana na kigezo cha UKUTA, Nipate nini??? Kisa eti UKAWA wapate nafasi ya kuropoka Bungeni?? Sifanyi Mzaha huo kabisa!!
2. Badala ya kutafuta riziki yangu kwa kumwagilia bustani zangu zinazonipatia kipato na kuniwezesha kuishi, eti niache kazi hizo na kwenda kuandamana na kigezo cha UKUTA, Nipate nini??? Kisa eti UKAWA wapate nafasi ya kuzomea Bungeni kwa kigezo cha Demokrasia?? Sifanyi Mzaha huo kabisa!!
3.Badala ya kutafuta Ada za watoto wangu ili wajitegemee baadaye, eti niende kuandamana na kigezo cha UKUTA, Nipate nini??? Kisa eti UKAWA wapate nafasi ya kusema uwongo Bungeni kwa kigezo cha Demokrasia?? Sifanyi Mzaha huo kabisa!!
Kama ni Maandamano watangulie hao Viongozi wetu ili wawe wa kwanza kukung'utwa na kupewa vilema. Mimi motto wa Masikini sitathubutu ng'o!! AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO. ASANTE SANA MZEE JK!! NITAZINGATIA BUSARA ZAKO!