Siwezi kuamini nilichoona ziara ya Mbowe mkoani Kagera!

Siwezi kuamini nilichoona ziara ya Mbowe mkoani Kagera!

Ufagio gani? Wa kubambikia watu kesi za ugaidi? Nafikiri hiyo strategy imewashinda kabisa. Kama mlimbeba na mtu mliyemmwagia tindikali, mkazunguka naye kwenye mikutano Arusha ili kuonyesha ushahidi wa ugaidi wa CDM na bado mkapigwa 4 bila, basi nyie ni sikio la kufa tu. Hakuna dawa itakayowatibu kwa sasa.

naona member wa saccos umefura sana kwa hasira, tulieni bwana, inaonesha ni kwa jinsi gani msivyo wavumilivu wa siasa, mtu mmoja tu anaweza kuwachanganya mpaka mnamfanya agenda ya chama?? saccos bado mnayo mengi ya kujifunza, ila saccos yenu itakufa kabla ya kujifunza mengi
 
Chama cha magamba wanafanya kazi ya kuitangaza CHADEMA kwa gharama kubwa, maneno mengi na jasho jingi,... heri kukosa mali ila ujaliwe akili. Mungu zidi kuibariki Tanzania!!
 
ccm kwishinei,huko kwetu busega wananchi walishahama analojia ccm na sasa wapo digital chadema wanavuta oksijen swaaaafi
 
asante kwa taarifa nzuri yenye kuleta matumai ni mungu awalinde...

Safi kamanda wakati mzee wa iramba akijisifu kwamba yeye nikiboko ya cdm makamanda wanachanja mbuga, bila shaka atabaki na iramba yake, hivi uchaguzi wa madiwani waliofukuzwa huko nilini ili ajue kama watu wamechoka.
 
Are you??

Of course I am! Look at my statistics and compare them to yours!

Mine


Join Date : 5th October 2007
Location : Kibaruani
Posts : 13,333
Rep Power : 36810
Likes Received5849
Likes Given2914



Yours

Join Date : 17th February 2012
Posts : 1,876
Rep Power : 754
Likes Received245
Likes Given11
 
Of course I am! Look at my statistics and compare them to yours!

Mine


Join Date : 5th October 2007
Location : Kibaruani
Posts : 13,333
Rep Power : 36810
Likes Received5849
Likes Given2914



Yours

Join Date : 17th February 2012
Posts : 1,876
Rep Power : 754
Likes Received245
Likes Given11

what does those numbers have to do with being serious??
 
what does those numbers have to do with being serious??

Figure out yourself unless you are blind with numbers! For almost two years that you have been here you have thanked(giving likes) 11 times? Is that how appreciative you are to others? ...... even your own cronies from Lumumba Street? Come on!
 
Khaa!! Miye akili hii ya ajabu ya kuchukua idadi ya watu kwenye mikutano ya vyama kuoanisha na kukubalika kwa chama au wingi wa kura huwa inanishangaza sana. Kwenye mikutano ya siasa watu huwa wanakuja kusikiliza tu na si kupiga kura. Wengine wanakuja kuwaona wasanii mlioambata nao. Kuna wengine wapo kazini kama wauza za maji, wezi wa mifukoni, majasusi wa vyama vingine, madada poa na wengine wengi tu. Hebu amkeni kidogo mfanye research itakayo wasaidia kujaribu kukisia idadi ya kura kuliko hii inayowapeleka chaka :bored:
 
Asante kwa taarifa nzuri mkuu ila ninachowaomba CDM mnapaswa katika mikutano hii muwasihi watu wajiandikishe wapata kadi ya mpiga kura na siku ya kura wapige wasiuze. Tatizo unaweza kukuta umati unajaa ila wapiga kura ni wachache. Please, hamasisheni sana hili, pengine muanze theme rasmi kwa ajili ya kutoa elimu ya kujiandikisha tu. Hata mkutano ujae kiasi gani kama hakuna wapiga kura ni kazi bure.
hope nawe utafanya kazi hiyo kwa uwezo wako maana hili zoezi la uhamasishaji likifanyika vizuri mwishoni tutakaofaidika ni Watanzania tulio wengi japo sio wote.
 
Ikumbukwe ziara hii imefanyika wiki kadhaa baada ya Mwenyekiti wa Ccm taifa (Kikwete) na timu ya mawaziri kumaliza ziara yao hapa!

Wakati wa ziara ya Kiwete watu walisombwa kwa marori na kulazimisha shule kufunguliwa j,mos na j,pili ili kuongeza idadi kwenye mikutano.

Ziara ya Mbowe watu walikodi magari wenyewe kutoka vijijini mbali kufuata mikutano. Mkutano mmoja tu wa Karagwe taarifa niliyopewa na katibu wa jimbo hilo leo, ni kuwa watu waliosaini karatasi za maoni ya chama kuhusu katiba ni 5,811 kwenye mkutano mmoja.

Wanawake sasa wanakuja mstari wa mbele kwenye mabadiliko, nilishuhudia akina mama na wasichana wakianguka wakijaribu kuwagusa tu viongozi wakati wanaingia na kutoka kwenye mikutano. Kwenye mkutano wa Karagwe wasichana ndio waliongoza kwa kuvaa skafu na kofia za Chadema.

Misenyi watu walifunga bara bara ya Mtukula - Bukoba kwa masaa kadhaa kutokana na wingi wa watu. Lakini badala ya wasafiri kukasilika na wao walijiunga kusikiliza hotuba za viongozi!

Katika mkutano wa Kyerwa mama mmoja wa makamo aliangua kilio ndege ilipopaa huku akisema anaogopa wanaweza kupata ajari "Hawa watoto Mungu wangu sijui kama watazunguka nchi nzima na kuimaliza salama na hiyo ndege yao, tuwaombee sana" alisikika akisema mama huyo huku akitokwa na machozi.

Mikutano ilifanyika asubuhi au mchana, lakini watu walijaa huku wakichomwa na jua kwa muda mrefu. Wazee wengi walijitokeza kwenye hali kama hiyo na kusema kero zao wakiamini Chadema pekee ndiyo itawasemea kero zao.

Sijui hayo yote ni kwa nini, ni mpango wa Mungu? wananchi wamechoka utawala uliopo? ni mvuto wa viongozi wa Chadema? Hali hii itaendelea mpaka 2015? Kwa nini juhudi za kuichafua Chadema zinashindwa na watu ndo wanaongeza mapenzi kwake?

Nawauliza wana JF wenzangu na hii nayo utaita ni THREAD ?
 
Asante kwa taarifa nzuri mkuu ila ninachowaomba CDM mnapaswa katika mikutano hii muwasihi watu wajiandikishe wapata kadi ya mpiga kura na siku ya kura wapige wasiuze. Tatizo unaweza kukuta umati unajaa ila wapiga kura ni wachache. Please, hamasisheni sana hili, pengine muanze theme rasmi kwa ajili ya kutoa elimu ya kujiandikisha tu. Hata mkutano ujae kiasi gani kama hakuna wapiga kura ni kazi bure.

Waambie serikali ya CCM watuandikishe, hata tukiambiwa tujiandikishe tunajiandikisha wapi?
 
Najiuliza hao walikwenda kusikiliza hoja,hotuba ama! Ama walikwenda shangaa mbayu wayu!
Najiuliza tu wajameen,
 
Frankly speaking this is GOOD NEWS for CHADEMA.

Hii inaonyesha kuwa Watanzania wana imani sana na CHADEMA kama chama pekee kitakachoweza kuwaletea Watanzania mabadiliko. Changes they can believe in.

Let the people choose A GOVERNMENT OF THE PEOPLE, BY THE PEOPLE FOR THE PEOPLE SHALL NOT PERISH FROM THE EARTH-Abraham Lincoln-American President (1860-1865).
 
Back
Top Bottom