Siwezi kuamini nilichoona ziara ya Mbowe mkoani Kagera!

Siwezi kuamini nilichoona ziara ya Mbowe mkoani Kagera!

Ikumbukwe ziara hii imefanyika wiki kadhaa baada ya Mwenyekiti wa Ccm taifa (Kikwete) na timu ya mawaziri kumaliza ziara yao hapa!

Wakati wa ziara ya Kiwete watu walisombwa kwa marori na kulazimisha shule kufunguliwa j,mos na j,pili ili kuongeza idadi kwenye mikutano.

Ziara ya Mbowe watu walikodi magari wenyewe kutoka vijijini mbali kufuata mikutano. Mkutano mmoja tu wa Karagwe taarifa niliyopewa na katibu wa jimbo hilo leo, ni kuwa watu waliosaini karatasi za maoni ya chama kuhusu katiba ni 5,811 kwenye mkutano mmoja.

Wanawake sasa wanakuja mstari wa mbele kwenye mabadiliko, nilishuhudia akina mama na wasichana wakianguka wakijaribu kuwagusa tu viongozi wakati wanaingia na kutoka kwenye mikutano. Kwenye mkutano wa Karagwe wasichana ndio waliongoza kwa kuvaa skafu na kofia za Chadema.

Misenyi watu walifunga bara bara ya Mtukula - Bukoba kwa masaa kadhaa kutokana na wingi wa watu. Lakini badala ya wasafiri kukasilika na wao walijiunga kusikiliza hotuba za viongozi!

Katika mkutano wa Kyerwa mama mmoja wa makamo aliangua kilio ndege ilipopaa huku akisema anaogopa wanaweza kupata ajari "Hawa watoto Mungu wangu sijui kama watazunguka nchi nzima na kuimaliza salama na hiyo ndege yao, tuwaombee sana" alisikika akisema mama huyo huku akitokwa na machozi.

Mikutano ilifanyika asubuhi au mchana, lakini watu walijaa huku wakichomwa na jua kwa muda mrefu. Wazee wengi walijitokeza kwenye hali kama hiyo na kusema kero zao wakiamini Chadema pekee ndiyo itawasemea kero zao.

Sijui hayo yote ni kwa nini, ni mpango wa Mungu? wananchi wamechoka utawala uliopo? ni mvuto wa viongozi wa Chadema? Hali hii itaendelea mpaka 2015? Kwa nini juhudi za kuichafua Chadema zinashindwa na watu ndo wanaongeza mapenzi kwake?
Mkuu, naomba nikutaarifu tu kuwa Watz kwenye mikutano hujaa sana hata kwenye mihadhara ya kidini. Mikusanyiko hii si kigezo cha upigaji kura ukiridhika na hadhara hii utasangaa 2015!!!!!!!!!!!!!!!!!! Pwaaaaaaaaaaa.
 
Waambie serikali ya CCM watuandikishe, hata tukiambiwa tujiandikishe tunajiandikisha wapi?
Watu wahamasishwe mapema ili ukifika wakati wa kuandikisha, serikali ya CCM itaandikisha. Ni bora uwe na kadi na mpira kura hata kama watachakachua but itafika mahali watashindwa. Endelea kuhamasisha walio karibu nawe ili muda wa kuandikisha ukifika waende, vinginevyo hakuna ushindi wa kura bila kupiga kura.
 
Khaa!! Miye akili hii ya ajabu ya kuchukua idadi ya watu kwenye mikutano ya vyama kuoanisha na kukubalika kwa chama au wingi wa kura huwa inanishangaza sana. Kwenye mikutano ya siasa watu huwa wanakuja kusikiliza tu na si kupiga kura. Wengine wanakuja kuwaona wasanii mlioambata nao. Kuna wengine wapo kazini kama wauza za maji, wezi wa mifukoni, majasusi wa vyama vingine, madada poa na wengine wengi tu. Hebu amkeni kidogo mfanye research itakayo wasaidia kujaribu kukisia idadi ya kura kuliko hii inayowapeleka chaka :bored:

ni kweli kabisa mkuu kuna wengine wanafuata Original Comedy au kuwaona Wachezaji wa Simba
 
hope nawe utafanya kazi hiyo kwa uwezo wako maana hili zoezi la uhamasishaji likifanyika vizuri mwishoni tutakaofaidika ni Watanzania tulio wengi japo sio wote.

Sure mkuu walio karibu yangu wengine walikuwa wagumu sana kutambua mabadiliko. Ila kwa sasa wanaelewa, hadi kijijini ninakotoka. Ninaamini wale ambao bado ni Thomaso nao watabadilika soon tu. Ninachoamini ni kuwa kama tutatumia busara tunaweza kubadili watu utashi ina fikra kuhusu uongozi wa nchi hii.
 
thread nyingine hata hazifai kuitwa thread,


We mwenyewe umeiita thread, labda ungeiita hilo jina jingine! Wewe,utaifa kwanza, hamida,nk, mkiona thread ya chadema mnapata mshituko kama mmejam...b. ishiwa.
 
Mkuu, naomba nikutaarifu tu kuwa Watz kwenye mikutano hujaa sana hata kwenye mihadhara ya kidini. Mikusanyiko hii si kigezo cha upigaji kura ukiridhika na hadhara hii utasangaa 2015!!!!!!!!!!!!!!!!!! Pwaaaaaaaaaaa.
Munatengeneza mazingira ya wizi wanajaa si kwa sababu wanafurahishwa na kilichowajaza hamtatoka 2015
 
Munatengeneza mazingira ya wizi wanajaa si kwa sababu wanafurahishwa na kilichowajaza hamtatoka 2015

You are right Mkuu...jamaa kwa wizi hawajambo but this time around watapata cha moto. They will never continue to steal for ever; there will be a time of their 40 days, God's willing!

By they way I am back after my self ban..sikupenda walichonifanyia mods though I like them and their wonderful work!
 
Ni wehu tu na wendawazimu kumlinganisha Mbowe na MHeshimiwa Rais Jakaya Kikwete.
Labda unayoyasema yanaweza kuwa kweli. Lakini tusubiri 2015 atakapokuwa M/Kiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni tutajua yeye na Mbowe nani zaidi.
 
Mkuu, naomba nikutaarifu tu kuwa Watz kwenye mikutano hujaa sana hata kwenye mihadhara ya kidini. Mikusanyiko hii si kigezo cha upigaji kura ukiridhika na hadhara hii utasangaa 2015!!!!!!!!!!!!!!!!!! Pwaaaaaaaaaaa.

Tume huru vipi? KAtiba mpya je? Mnaogopa nini?
 
Munatengeneza mazingira ya wizi wanajaa si kwa sababu wanafurahishwa na kilichowajaza hamtatoka 2015

hata Tshvangilai wa Zimbabwe na Odinga wa Kenya walijaa kupita hivyo lakini pwaaaaaa!
 
cdm ni moto wa kuotea mbali! kama ni shabaha, basi wanajua kulenga.
 
ulipatwa na stroke gafla uliposoma huu uzi!!!
 
Last edited by a moderator:
Ni wehu tu na wendawazimu kumlinganisha Mbowe na MHeshimiwa Rais Jakaya Kikwete.

Mwenye macho haambiwi tazama. Bukoba pamoja na kuwa na finali za mpira wa miguu kombe la Kagasheki, bado uwanja wa uhuru (Mayunga) ulitapika watu waliokuja kusilikiza hotuba.
 
Back
Top Bottom