Siwezi kuamini nilichoona ziara ya Mbowe mkoani Kagera!

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Ikumbukwe ziara hii imefanyika wiki kadhaa baada ya Mwenyekiti wa Ccm taifa (Kikwete) na timu ya mawaziri kumaliza ziara yao hapa!

Wakati wa ziara ya Kiwete watu walisombwa kwa marori na kulazimisha shule kufunguliwa j,mos na j,pili ili kuongeza idadi kwenye mikutano.

Ziara ya Mbowe watu walikodi magari wenyewe kutoka vijijini mbali kufuata mikutano. Mkutano mmoja tu wa Karagwe taarifa niliyopewa na katibu wa jimbo hilo leo, ni kuwa watu waliosaini karatasi za maoni ya chama kuhusu katiba ni 5,811 kwenye mkutano mmoja.

Wanawake sasa wanakuja mstari wa mbele kwenye mabadiliko, nilishuhudia akina mama na wasichana wakianguka wakijaribu kuwagusa tu viongozi wakati wanaingia na kutoka kwenye mikutano. Kwenye mkutano wa Karagwe wasichana ndio waliongoza kwa kuvaa skafu na kofia za Chadema.

Misenyi watu walifunga bara bara ya Mtukula - Bukoba kwa masaa kadhaa kutokana na wingi wa watu. Lakini badala ya wasafiri kukasilika na wao walijiunga kusikiliza hotuba za viongozi!

Katika mkutano wa Kyerwa mama mmoja wa makamo aliangua kilio ndege ilipopaa huku akisema anaogopa wanaweza kupata ajari "Hawa watoto Mungu wangu sijui kama watazunguka nchi nzima na kuimaliza salama na hiyo ndege yao, tuwaombee sana" alisikika akisema mama huyo huku akitokwa na machozi.

Mikutano ilifanyika asubuhi au mchana, lakini watu walijaa huku wakichomwa na jua kwa muda mrefu. Wazee wengi walijitokeza kwenye hali kama hiyo na kusema kero zao wakiamini Chadema pekee ndiyo itawasemea kero zao.

Sijui hayo yote ni kwa nini, ni mpango wa Mungu? wananchi wamechoka utawala uliopo? ni mvuto wa viongozi wa Chadema? Hali hii itaendelea mpaka 2015? Kwa nini juhudi za kuichafua Chadema zinashindwa na watu ndo wanaongeza mapenzi kwake?
 
asante kwa taarifa nzuri yenye kuleta matumai na Mungu awalinde...
 
Asante kwa taarifa mkuu, naamini udhalimu wa maccm upo ukingoni.
 
Mkuu, watu wanaipenda CHADEMA kutoka moyoni, hadi wanaCCM nao siku hizi wanashona uniform zao katika staili ya gwanda za CHADEMA, CHADEMA ni mpango wa Mungu.
 
Sijui hayo yote ni kwa nini, ni mpango wa Mungu? wananchi wamechoka utawala uliopo? ni mvuto wa viongozi wa Chadema? Hali hii itaendelea mpaka 2015? Kwa nini juhudi za kuichafua Chadema zinashindwa na watu ndo wanaongeza mapenzi kwake ?
Hizi unazoita juhudi za kuichafua CHADEMA ndio zinazosaidia kuiinua na kuifanya ijulikane kwa wananchi. Nadhani hapa strategists wa CCM wamekosea njia. Asili ya mwanadamu ni ya ajabu sana kwani huwa inamsukuma kutafuta kujua zaidi kile kitu unachomwambia kuwa ni kibaya sana na hakifai kwa maisha yake. Lakini pia asili ya mwanadamu inamsukuma kuwahurumia watu wanaoonekana kuwa wanaonewa. CCM wangejikita kwenye kueleza jinsi walivyotatua matatizo ya wananchi na mipango mingi waliyonayo ya kuiondoa nchi kwenye umaskini wangepata wafuasi wengi tu.
 
Hapo sipingi kabisa maana Hapa Isingiro ni zaidi ya hicho ulichooona
 
Wananchi wanawashwa mabadiliko mwili mzima.Imagine mtu anaingia gharama ya kuileta Simba ili kutibulia CDM.CDM ni kama mvua huwezi kuzuia mvua
 
Kama Magamba wasipo Temper na Daftari la wapiga Kura 2015, CHADEMA ni Ushindi wa More than 90 Pasenti
 
Nami nimeyashuhudia Kigoma mjini katika viwanja vya Community center hapo jana. Ni hatari kwa magamba na Red Briged wako vizuri kwenye ulinzi. Polisi wawer wanakaa mbali kama ilivyokuwa jana.
 
Ukweli ni kwamba Mtu yeyote anayejitambua na Mwenye akili timamu hawezi kuishabikia CCM.
 
USITARAJIE HATA SIKU MOJA UTAONA UTAONA THREADS INASIFIA CCM, COZ UNAJUA JAMII FORUM KAZI YAKE NINI. iko kiitikad zaid kwa hiyo km wewe ccm usishngae, nenda kwenye field piga kazi achana na porojo kwenye computer
 
Ikumbukwe ziara hii imefanyika wiki kadhaa baada ya Mwenyekiti wa Ccm taifa (Kikwete) na timu ya mawaziri kumaliza ziara yao hapa!

Wakati wa ziara ya Kiwete watu walisombwa kwa marori na kulazimisha shule kufunguliwa j,mos na j,pili ili kuongeza idadi kwenye mikutano.

Ziara ya Mbowe watu walikodi magari wenyewe kutoka vijijini mbali kufuata mikutano. Mkutano mmoja tu wa Karagwe taarifa niliyopewa na katibu wa jimbo hilo leo, ni kuwa watu waliosaini karatasi za maoni ya chama kuhusu katiba ni 5,811 kwenye mkutano mmoja.

Wanawake sasa wanakuja mstari wa mbele kwenye mabadiliko, nilishuhudia akina mama na wasichana wakianguka wakijaribu kuwagusa tu viongozi wakati wanaingia na kutoka kwenye mikutano. Kwenye mkutano wa Karagwe wasichana ndio waliongoza kwa kuvaa skafu na kofia za Chadema.

Misenyi watu walifunga bara bara ya Mtukula - Bukoba kwa masaa kadhaa kutokana na wingi wa watu. Lakini badala ya wasafiri kukasilika na wao walijiunga kusikiliza hotuba za viongozi!

Katika mkutano wa Kyerwa mama mmoja wa makamo aliangua kilio ndege ilipopaa huku akisema anaogopa wanaweza kupata ajari "Hawa watoto Mungu wangu sijui kama watazunguka nchi nzima na kuimaliza salama na hiyo ndege yao, tuwaombee sana" alisikika akisema mama huyo huku akitokwa na machozi.

Mikutano ilifanyika asubuhi au mchana, lakini watu walijaa huku wakichomwa na jua kwa muda mrefu. Wazee wengi walijitokeza kwenye hali kama hiyo na kusema kero zao wakiamini Chadema pekee ndiyo itawasemea kero zao.

Sijui hayo yote ni kwa nini, ni mpango wa Mungu? wananchi wamechoka utawala uliopo? ni mvuto wa viongozi wa Chadema? Hali hii itaendelea mpaka 2015? Kwa nini juhudi za kuichafua Chadema zinashindwa na watu ndo wanaongeza mapenzi kwake?

Ni wehu tu na wendawazimu kumlinganisha Mbowe na MHeshimiwa Rais Jakaya Kikwete.
 
Back
Top Bottom