Mh Rais Dr John Pombe Magufuli ni rais wa watanzania wote. Anatabia yakusifia mazuri nakuponda maovu. Hana macho yahuruma kumkemea muovu.
...
Mkuu wetu hapendi viporo yani boss nitamaliza kesho na kesho usimalize kweli utajuta.
...
Hapendi much know au mambo ya mkato bila fuwata taratibu.
...
Kiufupi ni kiongoz anapenda genius people na kiukweli ukiwa na akili Mh Rais utampenda.
...
Umewahi kujiuliza why nape na bashe wanahaha kumkosoa?
...
Nia yake kuu sana nikumfikishia pesa mwananchi yule fukara kabisa kwakweli naweza kulia anawapenda sana watanzania na anumia sana kuona watanzania ni masikini na mijitu michache ilio vimbiwa inawanyonya zaid ya 40m tanzanian.
Huyu ndie Rais Dr Magufuli sijamaliza.
Katika bandiko lako leo Mkuu
TumainiEl nimependa vipande hivyo, nilivyokunukuu, na mfano wa hao vijana machachari wa CCM.
Kwa kuongezea tu Dr Magufuli ni mwanasayansi mahiri. Anafanya siasa kwa misingi ya kisayansi. Misingi ya sayansi ni matokeo yanayopimika na siyo ya kufikirika.
Kwa sababu hiyo, hakuna mwanasiasa yeyote, kwa sasa, anayeweza kumshinda Dr Magufuli kwa maneno, matendo na muono, kama kiongozi.
Wakati wanasiasa wengi wanajipendekeza kwa wapiga kura kwa maneno ya laghai, Dr Magufuli hajipendekezi kwa wapiga kura bali anatatua kero zao kwa vitendo.
Wakati viongozi wa upinzani na baadhi ya wa CCM, wakikebehi mikakati yake ya kiuchumi, wao hao hawana mikakati mbadala. Sina uhakika kama wanajua vichocheo vya maendeleo kuelekea uchumi endelevu? Nauliza hivyo kwa kuwa mikakati ya Serikali inayoongozwa na Dr Magufuli imejikita katika kuboresha miundo mbinu, kama mkakati mama, ambao unaotafsiriwa na wapinzani kuwa ni wa "kukurupuka" na upotevu wa pesa ambayo ingegharamia kero za jamii. Wenye fikra hizo ni sawa na mtoto anayelilia mkate wakati mzazi wake hata senti ya kununua kitumbua hana.
Serikali inahitaji kuwa na pato la kuweza kumudu kujiendesha na kugharamia huduma za jamii na shughuli za maendeleo. Kipato chake hutokana na kodi. Kodi haiwezi kupatikana kama hakuna uzalishaji mali. Uzalishaji mali hutegemea ubora wa miundo mbinu km barabara, reli, angani, na majini ili bidhaa na malighafi zisafirishwe kwa wakati na usalama. Pia ubora wa miundo mbinu ni muhimu kwa wananchi ili waweze kufika kwenye huduma za jamii (maji, elimu na afya ) kwa wakati na salama.
KUPANGA NI KUCHAGUA - someni ilani ya uchaguzi ya CCM (2015)