Siungi mkono msimamo wa Tanzania, Lakini...

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Baada ya Mataifa makubwa dunia Marekani na Ulaya kuamrisha Afrika iseme msimamo wake na ilaani oparesheni ya Urusi huko Ukraine. Tanzania imetoa kauli ya kwamba sisi HATULAANI, wala HATUUNGI MKONO vita hivyo. Tunachoshauri ni meza ya majadiliano tu. Tanzania ni mwanachama wa kikundi cha nchi masikini zisizofungamana upande wowote kilichoanzishwa enzi za Vita Baridi.

Kauli ya Tanzania inafanana kidogo na msimamo wa China, lndia, na baadhi ya nchi za kiarabu, Hii inamaana kwamba mashirikiano yetu na Urusi hayatasitishwa kwasababu ya vita hivi, Na wala mashirikiano na Marekani na Ulaya hayatasitishwa kwasabu tunashirikina na Urusi pia. Binafsi msimamo huu wa Tanzania huwa siuungi mkono. Nataka nchi iseme kama ni nyeupe iseme na kama ni nyeusi iseme. Lakini yote ni kwasababu ya utegemezi wetu hatuna namna kama nchi, lakini mtu mmoja mmoja anaweza kuwa huru. Huwa naamini unafiki wa Tanzania na Watanzania asili yake ni huu mrengo. Kijasusi kuna dhana inasema, If you are neutral in a situation of injustice, it means that you are supporting the oppressors. Hivyo tumeelewana🤣

Ok leo tuache hayo, Naomba kui-challenge serikali ya Rais Samia, Imejiandaaje kukabili matokeo ya vita hivi? Kila nikiwasiliza watawala wanatoa matamko tu kuwa bei za bidhaa zitapanda, lakini serikali haisemi inachukua juhudi zipi kukabi hayo.

Naishauri serikali kwanza itambue vita vya Urusi na Ukraine ni tofauti na Vita vyovyote vilivyowahi kupiganwa duniani tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili duniani. Utofauti huu unajengwa na sababu kuu tatu zifuatazo;

Mosi, Ni vita inayoihusisha Urusi ambyo ni mdau mkuu wa uchumi wa gesi na mafuta duniani ambao ndio msingi wavuchumi wote duniani.

Pili ni vita inayoihusu Marekani moja kwa moja kuwa upande unaopigana na Urusi na hivyo kushinikiza mataifa mengi duniani yashiriki kuweka vikwazo ambavyo sasa vinaathiri hata nchi ambazo hazihusiki na vita. Tafsiri rahisi nikuwa ni vita kati ya Marekani vs Urusi

Na tatu hii ni vita ambavyo Umoja wa Ulaya kwa ujumla upo kinyume na Urusi inayoendesha vita hivyo, ukilinganisha na vita zingine zote ambapo EU kila vita iliyoendeshwa na Marekani ilikuwa upande wa Marekani au ilikaa kimya na kufanya vita hivyo visiathiri dunia, Sasa leo umoja wa Ulaya nao umeweka vikwazo kwa urusi ambayo ni mzalishaji na msafirisha wa 40% ya mshitaji yote ya gasi na mafuta Ulaya. Tafsiri yake ni vita kati ya Urusi vs USA+EU+Ukraine.

Hapa ndipo unaona sasa kupanda kwa mfuta na gesi duniani kunatokea kwa nguvu kubwa baada tu ya hivi vikwazo, Ulaya na Marekani sasa wanaugulia makali hayo, na jana galoni ilifika dola 6 ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya Marekani. Lakini naamini Wazungu wao wanaweza kupata alternative mapema, lakini sio hapo tu, baada tu ya vikwazo, Urusi imeshikilia ndege zaidi ya 600 za Mataifa ya Marekani na Ulaya ambazo zilikuwa zinafanya biashara katika anga la Urusi nyingi zilikuwa za kukodi na za matajiri kadhaa wa Marekani na Ulaya, hali hiyo imeyumbisha uchumi na na soko la anga ulimwenguni. Kwa namna yoyote vita hii itakavyoisha ukiachiliambali kwamba itaondoa utawala wa Zelensk, nafikiri itabadili mwelekeo wa dunia kisiasa na kiuchumi,

Je Tanzania ambayayo uchumi wao unastawi kwakutegemea mwelekeo wa mafuta na gesi katika soko la dunia, nini Serikali imejipanga kukabili? Nafikiri option ya kwanza kwa makusudi, ili kuzuia mfumko wa bei, gharama ya maisha na uhaba wa bidhaa hasa za majumbani, serikali ichukue jukumu la dharula la kuyalinda makampuni makubwa ya ndani ya uagizaji mafuta, na viwanda vikubwa vya uzalishaji bidhaa muhimu za ndani. Mfano serikali inaweza kutenga 1.5trilioni tu na kuyapa makapuni hayo kama stimulus package ili yaagize na kuhifadhi akiba ya kutosha angalau hata miezi 18 mbele.

Pili serikali itazame viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa za ndani ambabazo ni mahitaji ya lazima ya kila siku ya Watanzania (mafuta yakula, sukari, chumvi, cement, nondo, bata nk) navyo vipewe stimulus package kwa utaratibu maalumu ambao return yake inaweza kuwa katika kodi badae au katik muindo wowote ambao serikali itaweza kuthibiti upotezvyo wa stimulus package hiyo.

Kwakufanya hivyo serikali itadhibiti mfumko wa bei na ukali wa maisha utakotokana na kupanda kwa bidhaa duniani. Mfano Urusi baada tu ya vikwazo hasa ilipoondolewa kwenye mfumo wa kibenki duniani wa SWIFT, iliamua kudhibiti uchumi wake kwakutumia mfumo wa kichina kwa dharula, na sasa jana Putin ameamuru biashara zote za kimataifa kutumia sarafu ya Urusi, hatua iliyopandisha thamani ya sarafu hiyo ghafla duniani, mataifa yote duniani ikiwemo Marekani na EU yanayonunua gasi na mafuta Urusi yatalazimika kubadilisha dola na paundi zao kwenda kwenye sarafu ya Urusi ya Ruble ndipo yanunue mafuta na gesi (kununua pesa ya Urusi aina ya Ruble). Hivi ndivyo vita ya wakubwa inavyopigwana, mkubwa mwenzio mpige za puani.... Zingatia Ulaya na Marekani bado wananunua mafuta na gesi Urusi licha ya kelele na vikwazo kila kona.

Pata Kitabu cha Ujasusi kwa bei ya 80,000/= tu. Dar ni free delivery,
Nje ya Dar nauli ni 8,000/=

Nunua sasa kwa;
LIPA NAMBA TIGO 7489022
LIPA NAMBA VODA 5352627

Wasiliana nami kwa 0715865544

Pia Soma vitabu vyote (Soft copy) vya Yericko Nyerere kwa 5,000/= tu kwa wiki kupitia App bora kabisa ya Vitabu Tanzania. Pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote kupitia Play store Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play


IMG_20220324_122633_483.jpg

FB_IMG_1648136193354.jpg
 
Jamaa simwamini kabisa kwa Sasa.Alisema itachukua masaa 72 urusi kuisambaratisha Ukraine.Lakin ni Mwezi Sasa .Hatuoni dalili Urusi kushinda.
Urusi bado inatumia zile mbinu za vita ya pili ya dunia kupigana vita katika karne hii ya 21. Mbinu zao za kizamani ni zile za kupiga mabomu na kubomoa kila kitu, jambo ambalo siyo alama ya ushindi wa vita katika dunia ya leo.

Wana bahati kuwa Ukraine ilivamiwa ikiwa haikujiandaa kwa mzinga ya masafa marefu pia, kwani Putina angekuwa analia smachozi ya damu sasa. Baada ya kuvamiwa mwaka 2014 Ukraine ilianza kujenga upya jeshi lake dogo lakini la kisasa, na kazi yake inaonekana sasa.
 
Urusi bado inatumia zile mbinu za vita ya pili ya dunia kupigana vita katika karne hii ya 21. Mbinu zao za kizamani ni zile za kupiga mabomu na kubomoa kila kitu, jambo ambalo siyo alama ya ushindi wa vita katika dunia ya leo. Wana bahati kuwa Ukraine ilivamiwa ikiwa haikujiandaa kwa mzinga ya masafa marefu pia, kwani Putina angekuwa analia smachozi ya damu sasa. Baada ya kuvamiwa mwaka 2014 Ukraine ilianza kujenga upya jeshi lake dogo lakini la kisasa, na kazi yake inaonekana sasa.
Mkuu Iraq iliachwa jangwa, Libya ikaachwa jangwa.... Syria, Yemen nk kote huko vita imeharibu majengo na miundombinu.... Dunia ya vita vya silaha ndivyo ilivyo
 
Mkuu Iraq iliachwa jangwa, Libya ikaachwa jangwa.... Syria, Yemen nk kote huko vita imeharibu majengo na miundombinu.... Dunia ya vita vya silaha ndivyo ilivyo
Unapoweka Libya na Syria kwenye hiyo list kuwa walipigwa na NATO unakuwa unakosea sana, na nadhani hiyo ya kuelekeza kila baya linalotokea kulipeleka NATO ndiyo maana Putini anaweza kufanya lolote leo akitegemea kuwa lawama zitakwenda NATO, na hata waarabu wenyewe wanapopigana wenyewe kwa wenyewe, watakimbilia kuilaumu NATO. Hiyo tabia ilianza zamani sana hata wakati wa vita biana ya Isarel na Misri mwaka 67, baada ya Misri kupigwa ikailaumu NATO.

Libya na Syria walikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kutaka kuondoa uongozi madarakani. Kwa upande wa Syria, Assad aliuwa watu wake wengi sana akisaidiwa na Urusi na kuiacha Allepo ikiwa magofu tu. Yale Magofu ya Alelpo hayakutokana na bomu lolote la Marekani au la NATO. Mambomu ya Marekani yalikuwa yanalenga vituo vya kijeshi tu.

Kwa Iraq, marekani ilikuwa haingushi mabomu hovyo hovyo kwenye maskani ya watu, na wala hawakuangusha hata bomu moja kwenye auwanja wa ndege Baghdad. Sehemu kubwa iliyoharibu Iraq ni wale suicide bombers wa Al Zarqawi yaliyokuwa yanaripuka kwenye sehemu za watu wengi. Mabomu ya Marekani yalikuwa yanelekezwa kwenye vituo vya kijeshi na majumba ya Saddam tu.
 
Wewe mbona huongelilei na kupaza sauti kabisa kuhusu katiba mpya kama CHADEMA wenzako?! Uko na Urusi tu !
Baada ya Mataifa makubwa dunia Marekani na Ulaya kuamrisha Afrika iseme msimamo wake na ilaani oparesheni ya Urusi huko Ukraine. Tanzania imetoa kauli ya kwamba sisi HATULAANI, wala HATUUNGI MKONO vita hivyo...
 
UONGO,
Sehemu kubwa ya Iraq na Libya ni jangwa kiasili, Wamarekani pamoja na kukaa Iraq miaka 20 na mabomu ya kujitoa mhanga hawajaicha nchi hiyo katika hali ya magofu. Syria aliyeigeuza magofu ni huyu Putin unayemshabikia na alimpa hadi silaha za kikemikali dikteta mwenzake Assad atumie dhidi ya raia waliokuwa wanaandamana aondoke.
Mkuu Iraq iliachwa jangwa, Libya ikaachwa jangwa.... Syria, Yemen nk kote huko vita imeharibu majengo na miundombinu.... Dunia ya vita vya silaha ndivyo ilivyo
 
Unapoweka Libya na Syria kwenye hiyo list kuwa walipigwa na NATO unakuwa unakosea sana, na nadhani hiyo ya kuelekeza kila baya linalotokea kulipeleka NATO ndiyo maana Putini anaweza kufanya lolote leo akitegemea kuwa lawama zitakwenda NATO...
Kabla ya kuchangia tuwe tunajaribu kutafuta facts kidogo.Nikuulize kidogo hivi uharibifu uliofanywa libya iraq na huu unaendelea kufanywa Yemen je umefikia hata robo ya ukraine.

Kifupi kama Russia angeamua kufanya uharibifu basi ukraine ingekuwa magofu tu.lakini wanaangalia na sehemu na makazi ya raia hawapigi hovyo hovyo hizo sehemu wanazopiga wanajeshi wa ukraine wanajificha humo.

Russia inachukua tahadhari sana ugomvi wao ni viongozi sio raia ndio maana hadi sasa hivi ni raia 902 tu wamefariki.Nakuachia swali tafuta vifo Yemen na Iraq.
 
Tunajidanganya tuu (lack of self awareness) kwamba hatufungamani na upande wowote. Tulivyokataa kupiga kura ya kukemea uvamizi wa Putin wa Ukraine kule UN, tumeonekana wazi kwamba tunafungamana na Putin. Israel haifungamani na upande wa Ukraine au Urusi, lakini iliweza kupiga kura ya kukemea uvamizi.

INTERACTIVE_Day_8_UN_Vote_Condem_Russia_02-03-2022.png
 
Kabla ya kuchangia tuwe tunajaribu kutafuta facts kidogo.Nikuulize kidogo hivi uharibifu uliofanywa libya iraq na huu unaendelea kufanywa Yemen je umefikia hata robo ya ukraine.Kifupi kama Russia angeamua kufanya uharibifu basi ukraine ingekuwa magofu tu.lakini wanaangalia na sehemu na makazi ya raia hawapigi hovyo hovyo hizo sehemu wanazopiga wanajeshi wa ukraine wanajificha humo.Russia inachukua tahadhari sana ugomvi wao ni viongozi sio raia ndio maana hadi sasa hivi ni raia 902 tu wamefariki.Nakuachia swali tafuta vifo Yemen na Iraq.
Wewe ndiyo tafuta facts kwani unarudia makosa hayo hayo ya kulaumu nchi za NATO bila kuwa na facts zenyewe halafu badala yake unatetea Urusi kwa kukubali propaganda za Putin.

1. Tafuta facts zao kujua vita ya Libya ilisababishwa na nani na ni nani walioshiriki

2. Tafuta facts kuhus vita ya Yemen ujue kuwa wanopigana ni ni Saudi Arabia na wapiganaji wa huth wanaosaidiwa na Iran, wala Marekani haihusiki kabisa. Ni msimamo wa Marekani kupinga Saudi arabia kutumia silaha inazonunua Marekani kutumia kuuwa watu yemeni unaofanya uhusiano baina ya Marekani na Saudi Arabia uwe mbaya sasa hivi

3. Raia wa Ukraine wamekuwa wanatumia maisha yao kwenye mahandaki na kwenye basement tu, ndiyo maana mabomu yale yanabomoa majumba lakini hayauwi watu. Yaani uwe na factsa halafu uamini kuwa mabomu yote haya yanaangukiwa kwenye maficho ya wanajeshi kweli ? Ingekuwa hivyo warusi sasa wasingekuwa na wakati mgumu kuendelea na vita hiyo kwani wangekuwa wameshafutilia mbali jeshi la Ukraine

 
Back
Top Bottom