Kagosi DJ
Member
- May 5, 2020
- 19
- 69
Baada ya kuwasili kwa Makamu wa Rais wa Marekani nchini Tanzania hapo jana, ajenda kadhaa zinatarajiwa kuletwa mezani.
Tanzania imekuwa haifungani na upande wowote ‘non-alignment’ kuhusu Vita inayoendelea Ukraine. Hili limejidhihirisha kwenye mfululizo wa kura zilizopigwa UNGA tangu kuanza kwa Vita hiyo, ambapo Tanzania imekuwa ikipiga kura ya kujizuia kuungana na upande wowote (abstain)
Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani inakuja wakati wa ushindani unaokua wa ushawishi barani Afrika kati yake na mataifa yenye nguvu duniani kama vile China na Urusi.
Moja ya mambo tunayotarajia yataibuliwa ni Tanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Marekani na washirika wake huko Ukraine lakini pia kulaani kile Urusi inachoita Oparesheni ya kijeshi nchini Ukraine.
Swali ni je, Tanzania itatoa msimamo wake?