Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Nimejaribu kukaa kimya lakini nafsi yangu inanisuta. Siwezi kuendelea kukaa kimya. My opinion is unpopular, lakini nitasema.

Nitagusa hoja moja baada ya nyingine kama zilivyotolewa na "jumuiya ya madaktari".

Kuongezwa mshahara: Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia. Ulipotokea mgogoro wa interns wa muhimbili kuhamishwa vituo, basi madaktari wakaibuka na kutaka mshahara wa 3.5 mil na kugoma. Mambo hayafanyiki hivi! Tukiwaambia madaktari waonyeshe barua waliyokwishawahi kuiandikia serikalli kuomba mshahara huo, hakuna atakayetoa barua au ushahidi wowote kwa sababu madaktari wameanza na mgomo moja kwa moja. Siungi mkono mgomo wa namna hii.

Madaktari kupewa nyumba: Mara nyingi adui wa daktari huwa daktari mwenzake. Hili swala la nyumba lilishajadiliwa huko nyuma. Nini

kilitokea? Baada ya madaktari wa muhimbili kuthibitishiwwa kuwa wao watalipwa sh laki 4 kila mwezi basi chama cha madaktari ambacho viongozi wake wengi ni madaktari wa muhimbili wakapoteza interest ya kubargain na serikali ili posho hiyo wapate madaktari wa nchi nzima. Chama hicho kilikataa kabisa mara kadhaa kuitisha vikao vya kujadili posho za nyumba huku wakitoa sababu za kuepusha migomo. Sasa hivi inakuja "jumuiya ya madaktari" na kuilazimisha serikali kutoa posho hizo with immediate effect. Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba? Standing orders za mwaka 1994 zinaeleza kinaga ubaga kuwa daktari anastahili kupewa nyumba, standing orders za mwaka 2009 hazimtaji daktari katika watumishi wanaostahili kupewa nyumba. Maafisa utumishi wote wanatafsiri kuwa standing orders za mwaka 2009 zimemtoa daktari kwenye kundi la watakaopewa nyumba. Ni lini madaktari walienda kujadili hili na wizara ya utumishi? je ni sahihi kuanza na mgomo? Ili madaktari warudishiwe stahili hiyo ni LAZIMA kifungu kwenye standing orders za mwaka 2009 kifanyiwe marekebisho. Je, hilo linaweza kufanyika with immediate effect? Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.

Call allowance: "Jumuiya ya madaktari" inataka call allowance ilipwe kwa half per diem. This is very simple! Kwa nini mnagoma kwenda kazini during working hours? Ni kweli kuwa daktari anastahili kulipwa angalau sh. elfu 40 kwa call lakini solution yake ni rahisi kuliko zote. Madaktari waingie kazini, muda wa kazi ukiisha madaktari warudi nyumbani kama watumishi wengine. Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense. lakini again, jitihada gani zimefanyika awali kuhakikisha call inaongezwa? Can doctors provide evidence of their effeorts? HAKUNA.

Mazingira duni ya kazi: Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari. Hili swala waachieni wananchi wenyewe. Daktari unachotakiwa kujua ni capacity ya hospitali yako, beyond that usipokee mgonjwa. Ukishampokea basi unalea ubovu. MV Bukoba, MV spice zilizama kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake. MV Muhimbili nayo inaingia kwenye hili kundi. Nani alaumiwe? Nahodha lazima awe miongoni mwa watu wa kulaumiwa. Kama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini. hata Ulaya wangekubali kupokea wagonjwa wengi kulikoi uwezo kungekuwa na wagonjwa wanaolala chini. Ila Ulaya swala hilo halipo. Nafasi zikijaa zimejaa, mgonjwa apelekwe wapi, sio swala la daktari. Hata hiyo hospitali unayofanya kazi hujaijenga wewe daktari, ilijengwa kwa sababu mahitaji yalikuwepo. Ukiendelea kupokea wagonjwa wengi kuliko uwezo unaonyesha kuwa mahitaji sio urgent. Wagonjwa wakikosa pa kulazwa ndipo wananchi watashinikiza viongozi wao wawahakikshie facilities za kutosha.

Interns kuhamishiwa hospitali nyingine: Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern. Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.

Huduma huuzwa na kununuliwa. Bei ya huduma uamuliwa na nguvu za mahitaji na upatikanaji wa huduma. Hakuna daktari aliyelazimishwa kufanya kazi serikali. Kwanini madaktari wanakimbilia kufanya kazi serikalini? Madaktari wawe wakweli na watuambie faida zilizopo serikalini. kwanini madaktari wasitoe notice ya kuacha kazi serikali na kwenda kufanya kazi sehemu bora zaidi. Tanzania kuna soko huria. Kama watu walitumia mamilioni kwenda Loliondo basi hata daktari wanayeamini huduma zake watamfuata popote alipo. Madaktari mnangoja nini kutambua hili?

Mwisho: Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa. Ewe daktari, jiulize ni mara ngapi umeingia kazini kwa muda unaostahili na ukafanya kazi mpaka muda wa kazi kuisha? Je, tabia yako ya kila siku kazini inachangia kuondoa umasikini wa nchi yetu? Kila mtu aweke jibu lake moyoni na kujiuliza tena, je mgomo unaoendelea hivi sasa unapaswa kuungwa mkono? Je, kwa siku hizi mlizogoma mshahara mnauchukua wote bila aibu?

Also: Am just curious, nani analipia gharama za kukodi ukumbi wa mikutano wa Starlight Hotel ambao madaktari wamekuwa
wakikutania kwa siku kadhaa?!

Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

TAFADAHLI FUATILIA HIZO HIGHLIGHTED TEXTS STEP WISE

kWA NINI ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA AILIMIA 500 SIO SAHIHI? HEBU FAFANUA
JE NI SAHIHI KWA NCHI KAMA ZAMBIA KUMLIPA DAKTARI ZAIDI YA MILIONI NNE KWA MWEZI NCHI INAYOTEGEMEA SHABA,LANDLOCKED COUNTRY E.T.C
RWANDA KUMLIPA DAKTARI MSHAHARA ZAIDI YA MARA TATU YA MSHAHARA WA DAKTARI WA TANZANIA? UNAIJUA MWENYEWE RWANDA ILIVYO SIKUFAFANULII

UNA UHAKIKA KUWA MADAKTARI HAWAJAFANYA JITIHADA ZA AWALI KABLA YA KUCHUKUA HIZI HATUA????
kWA TAARIFA KABLA HATA YA SUALA LA INTERNS MADAKTARI WALIISHAFUATILIA HAYA MASUALA HADI KUFIKISHWA KWA OFISI YA WAZI MKUU NA DOCUMENTS WANAZO NAAMINI WEWE ULIKUWA HUFUATILII HILI SAKATA TANGU AWALI (KASORO SUALA LA MSHAHARA)
LAKINI UNAJUA SWALICHOAMBULIA HUKO NI MATUSI TU YA NGUONI HATA KAMA HUAMINI ILA HUO NDIO UKWELI MATUSI MPAKA UJUMBE ULIOKUWA UNATUMWA ULIPOKUWA UNAWASILISHA TAARIFA MACHOZI YALIKUWA YAKIWALENGA WATU WAZIMA...

STANDING ORDER YA MWAKA 2009 WALA HAIJAKANUSHA KAMA DAKTARI HATAKIWI KUPEWA NYUMBA UMECHEMKA LABDA KWA SBB INAANDIKWA KWA KIZUNGU INAWEZEKANA KABISA UMEPATA SHIDA KUTAFSIRI KWA KISWAHILI KWA HILI NAKUSAMEHE...

UNAKEJELI JUHUDI ZETU KAMA KWELI WEWE HUJAWAHI KUZIONA JUHUDI ZETU BASI U MUST BE BLIND AND SOMEHOW DUMB... MAANA YAKE WAGONJWA WOTE TUNAOWATIBIA SISI WANAKUFA(HAWAPONI)

kUMBE WEWE NI KIAZI MWINGINE HUJAFANYA UTAFITI NGOJA NISHIE HAPA WAGONJWA WANALALA CHINI WEWE UNAONA POA TU SASA MIMI DAKTARI NITAWAONAJE HAO WAGONJWA WAKIWA WAMELALA CHINI NA HILI NI MOJA VIFAA VYA KAZI KWA UJUMLA HAKUNA JARIBU KUTEMBELA HOSPITALI SIKU MOJA HALAFU NDIO UJE UANDIKE HUMU TENA ILA MPAKA SASA NAAMINI WEWE SIO MZIMA MUNGU AKUBARIKI KWANI HATA SISI TUNAAMINI KUWA MUNGU ANATUTUMIA TU KUTENDA MIUJIZA YAKE NAOMBA MUNGU AKUPONYE FROM UR INSANITY
 
Mkuu The Marcopollo, toka mgomo huu umeanza, my honest opinion thread yako hii ndio ina make the most sense kwenye issue hii. Wanabodi hata mimi nilisupport mgomo hatua za awali ku blow the whistle kwa serikali kuhusu madai genuine ya madaktari.

Sasa baada ya kupata mass support vichwa vimewavimba mpaka sasa wanataka ku ublow huu mgomo out of proportion. Nilipendekeza kwenye thread yangu ya jana kuwa serikali itoe tamko la kuyakubali madai yao yote na kwamba itayafanyia kazi na kuwalazimisha lazima waripoti kazini by Jumatatu asubuhi, kinyume cha hapo wawe fired without mercy!. Jumanne zitangazwe nafasi za udaktari masharti yawekwe yale yale wanaotaka waje, wasiotaka na wawe huru kujiendea kokote watajakotaka!.

Madaktari ni watu lakini walimu nao watu, wafanyakazi wa serikalini nao watu, polisi nao watu etc, no preferential treatment kwa madaktari huku ni kutengeza classes!. Maadam tayari tunayo supper class ya wabunge, lets make no more classes!.

Pia nikapandisha thread nyingine kuwa madaktari wasijione they are indispensable!. No body is indispensable hata without them, life goes on the rules of the jungle, wakufa waachwe wajifie wazima waendelee kuishi!.
 
TAFADAHLI FUATILIA HIZO HIGHLIGHTED TEXTS STEP WISE

kWA NINI ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA AILIMIA 500 SIO SAHIHI? HEBU FAFANUA
JE NI SAHIHI KWA NCHI KAMA ZAMBIA KUMLIPA DAKTARI ZAIDI YA MILIONI NNE KWA MWEZI NCHI INAYOTEGEMEA SHABA,LANDLOCKED COUNTRY E.T.C
RWANDA KUMLIPA DAKTARI MSHAHARA ZAIDI YA MARA TATU YA MSHAHARA WA DAKTARI WA TANZANIA? UNAIJUA MWENYEWE RWANDA ILIVYO SIKUFAFANULII

UNA UHAKIKA KUWA MADAKTARI HAWAJAFANYA JITIHADA ZA AWALI KABLA YA KUCHUKUA HIZI HATUA????
kWA TAARIFA KABALA HATA YA SUALA LA INTERNS MADAKTARI WALIISHAFUALTILIA HAYA MASUALA HADI KUFIKISHWA KWA OFISI YA WAZI MKUU NA DOCUMENTS WANAZO NAAMINI WEWE ULIKUWA HUFUATILII HILI SAKATA TANGU AWALI*KASORO SUALA LA MSHAHARA)
LAKINI UNAJUA SWALICHOAMBULIA HUKO NI MATUSI TU YA NGUONI HATA KAMA HUAMINI ILA HUO NDIO UKWELI MATUSI MPAKA UJUMBE ULIOKUWQA UNATUMWA UNAPOKUWA UNAWASILISHA TAARIFA MACHOZI YALIKUWA YAKIWALENGA WATU WAZIMA...

STANDING ORDER YA MWAKA 2009 WALA HAIJAKANUSHA KAMA DAKTARI HATAKIWI KUPEWA NYUMBA UMECHEMKA LABDA KWA SBB INAANDIKWA KWA KIZUNGU INAWEZEKANA KABISA UMEPATA SHIDA KUTAFSIRI KWA KISWAHILI KWA HILI NAKUSAMEHE...

UNAKEJELI JUHUDI ZETU KAMA KWELI WEWE HUJAWAHI KUZIONA JUHUDI ZETU BASI U MUST BE BLIND AND SOMEHOW DUMB... MAANA YAKE WAGONJWA WOTE TUNAOWATIBIA SISI WANAKUFA(HAWAPONI)

kUMBE WEWE NI KIAZI MWINGINE HUJAFANYA UTAFITI NGOJA NISHIE HAPA WAGONJWA WANALALA CHINI WEWE UNAONA POA TU SASA MIMI DAKTARI NITAWAONAJE HAO WAGONJWA WAKIWA WAMELALA CHINI NA HILI NI MOJA VIFAA VYA KAZI KWA UJUMLA HAKUNA JARIBU KUTEMBELA HOSPITALI SIKU MOJA HALAFU NDIO UJE UANDIKE HUMU TENA ILA MPAKA SASA NAAMINI WEWE SIO MZIMA MUNGU AKUBARIKI KWANI HATA SISI TUNAAMINI KUWA MUNGU ANATUTUMIA TU KUTENDA MIUJIZA YAKE NAOMBA MUNGU AKUPONYE FROM UR INSANITY
Mazee acha basi madaktari wetu waende huko kwenye hizo faranga lukuki!. Just let them go!. Mtoto wa Mkulima Mkuu Pinda, kutana nao kesho waambie hali ya nchi, hawataki, fukuzia mbali!.
 
Mi nategemea na waalimu,wauguzi, waandisi, wakulima,....... Woote wagome.
 
Mengi ya madai ya madaktari ni illusion hayawezi kutekelezeka kwa uchumi uliopo...

So kwa madai hayo na kutaka yafanyiwe kazi immediately...inabidi watafute kazi sehemu nyingine..this is free market

Kama unaona muajir wako hawezi kukutimizia maslahi yako kama upendavyo unaweza kwenda kufanya kazi kwa wahindi...au private sector au waanzishe hospitali zao walipane wenyewe kama watakavyoona inafaa..

Mapato ya madaktari ni sawa na ya mwalimu, ni sawa na ya Askari, ni sawa na ya Mkulima????

Natoa hoja.

Nchi maskini lakini inaweza kumlipa waziri 4,000,000/= kwa siku? Hivi unajua kwa kiwango cha posho ya anayodai daktari(40,000/=) hii ni sawa na posho ya miaka miwili kama atakuwa on call siku 2 kwa juma? Nchi ni maskini kwa wengine siyo viongozi/watawala ???? ili nchi hii irudi katika mstari lazima tupate uchungu (tulipe).Uchungu wa mgonjwa anayekufa Muhimbili siyo tofauti na waliopigwa risasi kwa kudai haki Arusha Jan 5, 2011. Yule kijana wa Tunisia hakuwa daktari ila alitosha kuwa kafara.. Siungi mkono nchi hii kuendelea kuwa na tabaka la wateule kwa woga wa kudai haki!!!
 
Kwani serikali lazima iajiri madaktari!?

Very poor argument!

Serikali imetangaza nafasi za kazi madaktari wakaomba wakijua mshahara wa mwajiri wao ni shillingi ngapi?

Kama wanaona hautoshi just QUIT this is free market..waende wakaajiriwe na wahindi au wajenge hospitali zao halafu walipane kama wataweza ..

Waache madai illusions tu..
 
Swala la kumuandikia mgonjwa dawa akakosa pesa ya kununua liko dunia nzima, sio kwenye kituo chako cha kazi tu. Na kama umeelewa mafunzo yako shuleni hupaswi kuwa na sympathy, unapaswa kuwa na empathy. Ukigoma humsaidii huyo mgonjwa aliyekosa dawa, kwa sababu the fact is hakuna serikali duniani yenye uwezo wa kuwanunulia dawa wananchi wake wote. Hata hivyo, swala hilo ni la wananchi na viongozi wao.
Acha kutuaminisha uongo hapa nchini libya huduma za kijamii kama suala la afya lilitolewa bure pasipo kuchangia hata senti kwenye dawa na kuambiwa dawa hazipo kipindi cha utawala wa Gadaffi kwa utawala wa sasa bado cjafanya utafiti.
 
Nchi maskini lakini inaweza kumlipa waziri 4,000,000/= kwa siku? Hivi unajua kwa kiwango cha posho ya anayodai daktari(40,000/=) hii ni sawa na posho ya miaka miwili kama atakuwa on call siku 2 kwa juma? Nchi ni maskini kwa wengine siyo viongozi/watawala ???? ili nchi hii irudi katika mstari lazima tupate uchungu (tulipe).Uchungu wa mgonjwa anayekufa Muhimbili siyo tofauti na waliopigwa risasi kwa kudai haki Arusha Jan 5, 2011. Yule kijana wa Tunisia hakuwa daktari ila alitosha kuwa kafara.. Siungi mkono nchi hii kuendelea kuwa na tabaka la wateule kwa woga wa kudai haki!!!

Mimi naona waanzishe hospitali zao waachane na ajira serikalini..is that too much to ask..

otherwise waache madai ambayo ni illusion, wawe realistic ..uchumi hauwezi kubeba madai yao ..
 
Inashangaza sana jinsi ambavyo hali ya uchumi inakuwa ngumu kuboresha huduma hii ila haiwi ngumu kuboresha maslahi ya wabunge. Hivi kweli kulikuwa na umuhimu gani wa ku-react immediately na kupanda kwa hali ya maisha ya wabunge Dodoma ila ishindikane kwa huduma za afya?

Hivi ina maana serikali imeshindwa hata kuanza kutoa hivyo vitendea kazi kwanza kabla hawajaendelea na suala la mishahara??
 
Nimejaribu kukaa kimya lakini nafsi yangu inanisuta. Siwezi kuendelea kukaa kimya. My opinion is unpopular, lakini nitasema.

Nitagusa hoja moja baada ya nyingine kama zilivyotolewa na "jumuiya ya madaktari".

Kuongezwa mshahara: Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia. Ulipotokea mgogoro wa interns wa muhimbili kuhamishwa vituo, basi madaktari wakaibuka na kutaka mshahara wa 3.5 mil na kugoma. Mambo hayafanyiki hivi! Tukiwaambia madaktari waonyeshe barua waliyokwishawahi kuiandikia serikalli kuomba mshahara huo, hakuna atakayetoa barua au ushahidi wowote kwa sababu madaktari wameanza na mgomo moja kwa moja. Siungi mkono mgomo wa namna hii.

Madaktari kupewa nyumba: Mara nyingi adui wa daktari huwa daktari mwenzake. Hili swala la nyumba lilishajadiliwa huko nyuma. Nini kilitokea? Baada ya madaktari wa muhimbili kuthibitishiwwa kuwa wao watalipwa sh laki 4 kila mwezi basi chama cha madaktari ambacho viongozi wake wengi ni madaktari wa muhimbili wakapoteza interest ya kubargain na serikali ili posho hiyo wapate madaktari wa nchi nzima. Chama hicho kilikataa kabisa mara kadhaa kuitisha vikao vya kujadili posho za nyumba huku wakitoa sababu za kuepusha migomo. Sasa hivi inakuja "jumuiya ya madaktari" na kuilazimisha serikali kutoa posho hizo with immediate effect. Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba? Standing orders za mwaka 1994 zinaeleza kinaga ubaga kuwa daktari anastahili kupewa nyumba, standing orders za mwaka 2009 hazimtaji daktari katika watumishi wanaostahili kupewa nyumba. Maafisa utumishi wote wanatafsiri kuwa standing orders za mwaka 2009 zimemtoa daktari kwenye kundi la watakaopewa nyumba. Ni lini madaktari walienda kujadili hili na wizara ya utumishi? je ni sahihi kuanza na mgomo? Ili madaktari warudishiwe stahili hiyo ni LAZIMA kifungu kwenye standing orders za mwaka 2009 kifanyiwe marekebisho. Je, hilo linaweza kufanyika with immediate effect? Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.

Call allowance: "Jumuiya ya madaktari" inataka call allowance ilipwe kwa half per diem. This is very simple! Kwa nini mnagoma kwenda kazini during working hours? Ni kweli kuwa daktari anastahili kulipwa angalau sh. elfu 40 kwa call lakini solution yake ni rahisi kuliko zote. Madaktari waingie kazini, muda wa kazi ukiisha madaktari warudi nyumbani kama watumishi wengine. Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense. lakini again, jitihada gani zimefanyika awali kuhakikisha call inaongezwa? Can doctors provide evidence of their effeorts? HAKUNA.

Mazingira duni ya kazi: Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari. Hili swala waachieni wananchi wenyewe. Daktari unachotakiwa kujua ni capacity ya hospitali yako, beyond that usipokee mgonjwa. Ukishampokea basi unalea ubovu. MV Bukoba, MV spice zilizama kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake. MV Muhimbili nayo inaingia kwenye hili kundi. Nani alaumiwe? Nahodha lazima awe miongoni mwa watu wa kulaumiwa. Kama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini. hata Ulaya wangekubali kupokea wagonjwa wengi kulikoi uwezo kungekuwa na wagonjwa wanaolala chini. Ila Ulaya swala hilo halipo. Nafasi zikijaa zimejaa, mgonjwa apelekwe wapi, sio swala la daktari. Hata hiyo hospitali unayofanya kazi hujaijenga wewe daktari, ilijengwa kwa sababu mahitaji yalikuwepo. Ukiendelea kupokea wagonjwa wengi kuliko uwezo unaonyesha kuwa mahitaji sio urgent. Wagonjwa wakikosa pa kulazwa ndipo wananchi watashinikiza viongozi wao wawahakikshie facilities za kutosha.

Interns kuhamishiwa hospitali nyingine: Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern. Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.

Huduma huuzwa na kununuliwa. Bei ya huduma uamuliwa na nguvu za mahitaji na upatikanaji wa huduma. Hakuna daktari aliyelazimishwa kufanya kazi serikali. Kwanini madaktari wanakimbilia kufanya kazi serikalini? Madaktari wawe wakweli na watuambie faida zilizopo serikalini. kwanini madaktari wasitoe notice ya kuacha kazi serikali na kwenda kufanya kazi sehemu bora zaidi. Tanzania kuna soko huria. Kama watu walitumia mamilioni kwenda Loliondo basi hata daktari wanayeamini huduma zake watamfuata popote alipo. Madaktari mnangoja nini kutambua hili?

Mwisho: Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa. Ewe daktari, jiulize ni mara ngapi umeingia kazini kwa muda unaostahili na ukafanya kazi mpaka muda wa kazi kuisha? Je, tabia yako ya kila siku kazini inachangia kuondoa umasikini wa nchi yetu? Kila mtu aweke jibu lake moyoni na kujiuliza tena, je mgomo unaoendelea hivi sasa unapaswa kuungwa mkono? Je, kwa siku hizi mlizogoma mshahara mnauchukua wote bila aibu?

Also: Am just curious, nani analipia gharama za kukodi ukumbi wa mikutano wa Starlight Hotel ambao madaktari wamekuwa wakikutania kwa siku kadhaa?!

Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

mkuu mi napinga hapo unaposema hospitali ikijaa wagonjwa wasichukuliwe..... imagine mama & mtoto wametoka tuseme kigoma wamekuwa refered muhimbili au temeke wafike pale uwaambie vyumba vimejaa rudini mlipotoka .... yanaingia akili hayo maneno yako...?
 
TAFADAHLI FUATILIA HIZO HIGHLIGHTED TEXTS STEP WISE

kWA NINI ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA AILIMIA 500 SIO SAHIHI? HEBU FAFANUA
JE NI SAHIHI KWA NCHI KAMA ZAMBIA KUMLIPA DAKTARI ZAIDI YA MILIONI NNE KWA MWEZI NCHI INAYOTEGEMEA SHABA,LANDLOCKED COUNTRY E.T.C
RWANDA KUMLIPA DAKTARI MSHAHARA ZAIDI YA MARA TATU YA MSHAHARA WA DAKTARI WA TANZANIA? UNAIJUA MWENYEWE RWANDA ILIVYO SIKUFAFANULII

UNA UHAKIKA KUWA MADAKTARI HAWAJAFANYA JITIHADA ZA AWALI KABLA YA KUCHUKUA HIZI HATUA????
kWA TAARIFA KABALA HATA YA SUALA LA INTERNS MADAKTARI WALIISHAFUALTILIA HAYA MASUALA HADI KUFIKISHWA KWA OFISI YA WAZI MKUU NA DOCUMENTS WANAZO NAAMINI WEWE ULIKUWA HUFUATILII HILI SAKATA TANGU AWALI*KASORO SUALA LA MSHAHARA)
LAKINI UNAJUA SWALICHOAMBULIA HUKO NI MATUSI TU YA NGUONI HATA KAMA HUAMINI ILA HUO NDIO UKWELI MATUSI MPAKA UJUMBE ULIOKUWQA UNATUMWA UNAPOKUWA UNAWASILISHA TAARIFA MACHOZI YALIKUWA YAKIWALENGA WATU WAZIMA...

STANDING ORDER YA MWAKA 2009 WALA HAIJAKANUSHA KAMA DAKTARI HATAKIWI KUPEWA NYUMBA UMECHEMKA LABDA KWA SBB INAANDIKWA KWA KIZUNGU INAWEZEKANA KABISA UMEPATA SHIDA KUTAFSIRI KWA KISWAHILI KWA HILI NAKUSAMEHE...

UNAKEJELI JUHUDI ZETU KAMA KWELI WEWE HUJAWAHI KUZIONA JUHUDI ZETU BASI U MUST BE BLIND AND SOMEHOW DUMB... MAANA YAKE WAGONJWA WOTE TUNAOWATIBIA SISI WANAKUFA(HAWAPONI)

kUMBE WEWE NI KIAZI MWINGINE HUJAFANYA UTAFITI NGOJA NISHIE HAPA WAGONJWA WANALALA CHINI WEWE UNAONA POA TU SASA MIMI DAKTARI NITAWAONAJE HAO WAGONJWA WAKIWA WAMELALA CHINI NA HILI NI MOJA VIFAA VYA KAZI KWA UJUMLA HAKUNA JARIBU KUTEMBELA HOSPITALI SIKU MOJA HALAFU NDIO UJE UANDIKE HUMU TENA ILA MPAKA SASA NAAMINI WEWE SIO MZIMA MUNGU AKUBARIKI KWANI HATA SISI TUNAAMINI KUWA MUNGU ANATUTUMIA TU KUTENDA MIUJIZA YAKE NAOMBA MUNGU AKUPONYE FROM UR INSANITY

Asipoelewa na hii basi katumwa
 
Mkataba ktk kazi ni makubaliano,maridhiano ya pande mbili.sasa inapotokea makubaliano ya pande hizi hayatekelezwi ndipo mizozano huanza kutokea,madaktari ni upande mmoja katika makubaliano na serikali ni upande wa pili ktk mkataba huu,nionacho mimi ni kuwa madaktari wametimiza wajib wao na serikali hawajatimiza makubaliano ndio maana wanakosa ujasiri wa kuleta facts zao.jamani madaktari kwa taaluma yao wanastahili haki zao,nature ya mtu mkimya ni akiamua kureact hakuna wa kumzuia?madaktari huwa kimya muda mwingi na wanapokuja na madai kuwarudisha ktk hali yao ni kuwatimizia matakwa yao.jamani nakiri kusema serikali yetu imepoteza mwelekeo.huwezi kuwasihi watu wawe wazalendo wakati wewe si mzalendo.vema kila mmoja atimize wajibu wake kwa muda muafaka na sio kusingizia kuwa madaktari wamekosa uzalendo.
 
Mkuu zemakopolo kwa sasa siasa hazina nafasi tena linapofika suala linalohusu maisha, yaani hata kama utaandika makala ndefu kiasi gani jamaa hawawezi kukuelewa. Ningekushauli makala yako ungeiandikia serikari kwa kushindwa kuwaheshimu madaktari na si hao tu bali kundi lingine linafuata soon naomba mungu asaidie wasiwe wanajeshi au polisi kwani kwa mshahara wanaopewa siku wakiwashtukia nao watalianzisha. Hapo ndipo mtajua kwa nini mmewaongezea wabunge posho huku walinzi wa wabunge hamjawaongezea. Tuanze kuheshimu professional za watu na sio kupiga siasa na kujenga hoja ambazo mimi naamini kwa sasa hoja hazina maana zaidi ya pesa
 
Mimi naona waanzishe hospitali zao waachane na ajira serikalini..is that too much to ask..

otherwise waache madai ambayo ni illusion, wawe realistic ..uchumi hauwezi kubeba madai yao ..
ndiyo, sumgura huyu ni mdogo ma dr. mlitambue hilo uchumi wetu unaweza tu kuakomodeti mahitaji ya wana siasa tu na kwakuwa maisha yamepanda sana hasa huko dodoma, tuna mpango wa kupandisha posho za wabunge hadi laki 4/seat kutokana na sababu tajwa hapo juu. Nyie madaktari,manesi, waalimu, askari wa majeshi yoote ni marufuku kugoma kwani kazi zenu ni za WITO, jamani narudia tena wito,wito wito, vinginevyo mhamie kwenye kazi za siasa!
 
Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7
Hebu Tujuze wewe mshahara wa daktari ni sh ngapi?

Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.
Wameamua sasa kufuatilia kwa nini usiwaunge mkono?

Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense
Huu nao ni mgomo ambao wewe unasema huungi mkono? ur contradicting urself, halafu huu utakuwa mgomo mbaya zaidi kwa sababu wagonjwa wanokuja usiku wengi huwa ni wa kuhudumiwa kwa dharura ambapo wakikosa matibabu asubuhi hatuko nao.

Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari
Hapa ndugu yangu ndio nimekushangaa sana, kwa nini hili lisiwe la kulalamikiwa na madaktari, ili mgonjwa apone anahitaji mazingira mazuri pia. Daktari hawezi kuwa anamtibu mgonjwa yule yule kila siku haponi kwa sababu ya mazingira wewe unasema daktari asilalamike. Mazingira mabovu huchangia pia wagonjwa kupata maambukizi ya maradhi mengine (Nosocomial infections) ambayo yanaweza kuhatarisha zaidi afya ya mgojwa na kufanya hata tiba kuwa ngumu zaidi, madaktari wana haki ya kulalamikia hili.

Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern
Hata kama wengine wanafanya ambako hakuna vifaa usitake wote wafanye huko, aliyechagua kufanyia Muhimbili, ambako ni kweli kuna vifaa zaidi na specialists wengi zaidi, usimlazimishe akafanyie sehemu nyingine kwa sababu tu amedai haki yake, posho ya kumwezesha kuhudumia wagonjwa vizuri zaidi.

Mgomo ni risasi ya mwisho
Madaktari na watumishi wengine wa afya wameongea sana na hii serikali sikivu iliyoziba masikio mpaka wakaitwa Mbayuwayu bila kusikilizwa, nadhani sasa ni wakati muafaka kutumia hii silaha ya mwisho ambayo ni mgomo.
Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja
But reasonable kwa wabunge kujiongezea maposho overnight.

Naunga mkono mgomo kwa asimilia 100%.
 
Very poor argument!

Serikali imetangaza nafasi za kazi madaktari wakaomba wakijua mshahara wa mwajiri wao ni shillingi ngapi?

Kama wanaona hautoshi just QUIT this is free market..waende wakaajiriwe na wahindi au wajenge hospitali zao halafu walipane kama wataweza ..

Waache madai illusions tu..

sasa kwa nini serikali inapoteza fedha kusomesha madaktari?kwa nini serikali inahangaika kijenga hospittali wakati za wahindi zipo!halafu inaelekea wewe unapapenda india sana.
 
Ni bora kwanza serikali ingetatua matatizo hayo kuliko kuendelea kutunishiana misuli,kuna watu wanasema kuwa madaktari wanajipenda nataka kuwakumbusha kuwa watumishi wengi hawana raha kazini mwao,malipo ni madogo sana kulingana na rapid inflation iliyopo tanzania kwa sasa,wanashindwa tu waanzie wapi nina uhakika asilimia kubwa ya watumishi wa idara nyingine wanaunga mkono madaktari,mimi nilitegemea kuwa waalimu kwa vile ni wengi wangeleta ukombozi kwa matumishi wa nchi hii kumbe ni bure kabisa.

Walimu ni wengi lakini ni wepesi wa kugawanywa kwa vitisho vya serikali,ukweli watumishi wanateseka sana,maelezo kuwa acha kazi ni upunguani mwingine kwa utendaji,kwanini wewe unayeshindwa kutatua shida za watumishi usiache kazi,kwani nchi hii ni yako,tatizo kuna watu wana ubinafsi kiasi kwamba anajiona yeye ndiye anastahili kupata,inashangaza kuwa wakati wabunge wanapojiongezea posho wanatoa kauli kwa kulinganisha na nchi zingine!ni kwanini watumishi wanapodai malipo ya kujikimu kwa kulinganisha na nchi nyingine inakuwa nongwa???,serikali ijue kuwa kamwe haitawaburuza watumishi muda wote ni bora wakae na kuandaa mikakati ya kutatua shida za watumishi.
 
KIFO ndio ufumbuzi pekee kwa matatizo yote yanayo mkabili mwanadamu lakini wajinga hutumia KIFO kama silaha ya kuzuia jitihada za ufumbuzi wa matatizo yao. Ni UOGA, UJINGA, NA NI UPUMBAVU MKUBWA kuwazuia MADAKTARI KUGOMA eti kwasababu wagonjwa watakufa kwani hata LIBYA watu walikufa na ufumbuzi wa walichokiamini ulipatikana. Kama madaktari wameona njia PEKEE ya kutatua matatizo yao kwa sasa ni MGOMO tunawatakia kila la heri WAENDELEE KUGOMA hadi madai yao yote yatakapo tatuliwa ili wasigome tena na wakisitisha MGOMO wao kwa maneno matamu ya wanasiasa WATAKUWA NI WAPUMBAVU NA WAVIVU WA KUFIKIRI hivyobasi hawatakuwa na sababu ya kuwa na vichwa kwani MATUMBO yanawatosha kuhifadhia vyakula wanavyo kula. Tunaimani na madakltari wetu tunawatakia kila lililo jema kuweni majasili wa kuyasimamia yale mnayo yaamini haki yenu MUNGU awabariki
 
Back
Top Bottom