ndetichia
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 27,772
- 6,557
Napita tu wakuu
ukifika wasalimie sawa..
Napita tu wakuu
Tatizo JK kaifanya hii kazi ionekane rahisi sana!!! Sidhani kama enzi zile za Nyerere alishawahi kufikiria haya anayoyasema unless kwenye ndoto!!!
Sasa kama kila mtu anataka uraisi uwaziri mkuu atakuwa nani? Nini kinawasukuma hawa jamaa kuona wao ndo wenye haki ya kutuongoza?
nani ka kwambia kwamba Uwaziri mkuu kwa nyakati ni DEAL!!, wote tunataka Ikulu kupitia tiketi ya Urais bwana uko ndo kila kitu. ata katiba haimugasigasi Rais, hivyo mambo ni mteremko tu.
Hii inanikumbusha nchi ya Haiti, kila mtu unayeongea naye ana ndoto za kuwa rais si utani eti. Hata mhudumu wa nyumba ya wageni niiiyokaa naye alikuwa na ndoto ya kuja kuwa rais, alikuwa ana miaka 50 na hajasoma hata sekondari. Akaniambia hata mama yake alikuwa aged 70+ alikuwa hajakata tamaa kuwa rais.
Heshima sana wanajamvi,
Ndani ya CCM Sitta ni miongoni mwa wanasiasa mwenye uwezo na ujasiri wa kuongoza Ikulu ya magogoni.Rekodi ya utumishi wake wakati akiwa spika wa bunge la JMT kila mwenye macho aliona na mwenye masikio alisikia.Ni Samwel Sitta aliyemwambia Kikwete waziwazi awe mkali kwa mafisadi.Ni Samweli Sitta aliyelifanya bunge letu likawa kama lilivyo leo kamati muhimu kama mashirika ya umma,serekali za mitta na hesabu za serekali alihakikisha zinaongozwa na wapinzani matokeo yake Dr W Slaa,Zitto kabwe nyota zao ziling'aa wananchi tukajua uwezo wao.
Mheshimiwa Samwel Sitta ana mapungufu kama walivyo binadamu wengine wengi lakini alipofanya vizuri lazima tumpongeze bila choyo wala hiyana.
Yote hayo tunayakubali, lakini angalia motive yake ilikuwa nini? Ni ukweli usiopingika kuwa Sitta ana hasira na kikwete kwa kumnyima u-PM. Ndiyo maana anakuwa na kinyongo na kisasi. Binafsi namuona kama mtu ambaye hana uvumilivu pia, hana ujasiri wa kuchukua maamuzi. Ni dhahiri kabisa, kwa mtu wa aina yake angekuwa na uthubutu hadi leo asingeendelea kubaki Chama cha Magamba. Hana huo ubavu. Hii tunaweza kuitafsiri kama woga.
Hatimaye Sitta ameanza kutoboa jibu. Leo akiwa jimboni kwake Urambo amesema kuwa hatua yake ya kutoa misaada makanisani siyo kwamba anatafuata urais. Kwamba kama Urais upo basi utamfuata wenyewe kwa wananchi kumhesimu.
Source: ITV
mkuu ulisikia la urais tu? Au ndo kila mmoja aje na mada yake toka kwenye hiyo hotuba? Kukuongezea tu ni kuwa kasema, kwa mujibu wa sumaye, adui mpya ni ufisadi. Na watapambana hadi kieleweke. Sitta na sumaye wameunda timu
Mimi urais unanifuata hadi chumbani kwangu.
Tatizo JK kaifanya hii kazi ionekane rahisi sana!!! Sidhani kama enzi zile za Nyerere alishawahi kufikiria haya anayoyasema unless kwenye ndoto!!!