Sitta: Tuna wakati mgumu

Sitta: Tuna wakati mgumu

Huyu mzee nilikuwa namfagilia hadi kumwona anatakiwa kuwa raisi wetu ajae kumbe ni zinga bogus!
 
mzee 6 amekuwa hovyoooooo, japo tulifurah yeye kuwa mwenyekiti ila kwa sasa ni uozoo mtupuuu
 
Na bado hukumu ya mungu inamsubiri yeye mkewe na ma ccm yote yanayoshiriki kwenye hili la katiba ya kulazimisha.
 
yaani mkewake magreth kamzidi akili mara mia

Magreth ni mkewe kwa nje tu , nyumbani hata vyumba wametengana ni kitambo sana ..... huyo mama alichoka ukatili wa Sita kumpiga mpaka kumvunja mikono na kitendo cha Sitta kuzaa watotot watatu na mwanamke mmoja anaitwa Marium magreth wa watu akaona isiwe tabu wacha tu ajisogeze pembeni.
 
Mnaishi kwa ndoto.
Na ndoto zenu hazina athari kwa 6,ccm wala watanzania. Uzuri ni kwamba, mnatunga uongo kisha mnajidanganya then mnauamini uongo huohuo.
We keep on keeping on. Tunawatungia katiba

We Kalia kutetea uovyo, najua BMK wana Mimba changa wanatematema mate ovyo watazaa mawe tu.
 
Wajanja wamemrushia ndoano bila kutafakari kabugia!Ateme tuone sasa!
Tulisema toka mwanzo, ila kuna usemi unaosema "fumbo mfumbie mjinga, mwerevu alifumbue" hapa mwerevu ni UKAWA, na Kikwete pia kukubali kura zisipigwe ujue kakubaliana na werevu UKAWA, ila mjinga 6 akaendeleza unafki na kujipendekeza kwa ccm wenzake ambao nao wamesha anza kumtosa sasa anaanza kubwabwaja, kwa heri kibabu 6 nenda kafuge wanyama huwezi ongoza watu.
 
Kilakukicha nasikia harufu ya damu nchi masikini duniani but viongozi wake ndo wanaongoza kwa utajir kuliko hata viongoz wanaongoza nchi tajir
 
Tatizo Sitta anaona hili suala la katiba ni suala simple tu analoweza kutumia kujijengea umaarufu...
 
Unafiki wa Sitta Ulianza kipindi cha Nyerere kakachapwa viboko
Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.


Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.


"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
 
Huyo ndiyo mtume akipata anajigawia kwanza kisha anawageuka wanaomtarajia OK boss time to go home you are finnito completo
 
  • Je, yametimia Samweli Sitta ni manafiki kama alivyosema Dr Slaa?


Baada ya uchaguzi Mkuu uliopita katika moja ya majibu ya Dr Slaa dhidi ya Samwel Sitta alipokuwa anaponda kuhusu vyama vya upinzani, Dr Slaa alijibu kifupi kwamba "Samwel Sitta ni mnafiki." Tamko hilo lilionekana kama jepesi na rahisi mno kwa wakati huo wengi tukijua kwamba Samweli Sitta alijijengea jina zuri alipoliongoza bunge akiwa Speaker wa Bunge la Muungano kwa weledi.

Kwa sasa imesomeka vema kwamba Samweli sita kipindi hicho kwa unafiki wake:
Kwa vile alitengeneza mazingira akubalike na Chadema agombee urais kupitia chama hicho alifanya kila awezacho kujikomba kwa vyama vya upinzani ili aonekane anatenda haki kumbe lengo ili akubalike kugombea urais kupitia Chadema, lakini aliwageuka na kuanzisha chama chake kwa siri ambacho alishirikiana na Nape. Kipindi hicho alianza kampeni kama anazofanya Lowasa sasa hivi kupita makanisani na kutunuku vyeti vya wahitimu vyuoni ili kujitangaza.

Sitta alipowaacha Chadema kwenye makutano ya mataa ya Ubungo, huku Dr Slaa akiwa ameshachukua form ya kugombea ubunge jimbo la Karatu, ikabidi Kamati Kuu Chadema warudi Mtaa wa Ufipa kwenye kikao cha dharura na kumbembeleza Dr Slaa asitishe mbio za ubunge na ashike bendera ya Chadema kupeperusha kugombea nafasi ya Uraisi. Hii ilitokana na unafikiwa wa Samwel sitta.

Kwa sasa napata picha kwamba CCM walikuwa sahihi kumwengua katika kiti cha Uspeaker na kumweka mama laini, legelege na anayefuata upepo Bi Kiroborobo kwa vile Sitta alisomeka ni mnafiki, pengine angeendelea kuwa speaker wa bunge angeharibu zaidi ya Makinda.

Mwenyekiti wa awali katika bunge hilo yule mzee wa Visiwani mwenye mvi nyingi kichwani alitumia busara na kuonyesha hekima sana na katika kamati kadhaa alishirikisha wajumbe toka upinzani pia na tulishuhudia hata wajumbe wa CCM walimsifia Lissu kwa weledi alipoongoza moja ya kitengo cha sheria katika utungaji wa sheria za bunge hilo, na wakadiriki kusema angefaa kama angekuwa mwanasheria wa serikali kuliko Werema.

Sitta alipochaguliwa kukalia kiti cha U-speaker alibadilisha upepo na kufanya bunge kuwa ni la CCM kinyume cha matakwa ya wananchi na sheria ya kuunda bunge hilo ambalo ni la kitaifa. Kwa uongozi wa Samweli Sitta katika bunge la Katiba mpya ameligawa taifa badala ya kuliunganisha zaidi kuwa kitaifa. Ameelemewa na uchama badala utaifa alio nao Warioba. Sitta ameendesha Bunge la Katiba Mpya kwa masilahi binafsi badala ya Kitaifa na matokea yake amechafuka na kupoteza kabisa umaarufu aliokuwa nao.

Dhambi ya unafiki ya Samwel Sitta itamfanya maisha yake anayone machungu zaidi akikumbuka alichowaharibia wananchi haki yao, pia kuchafuka kwa Sitta ni nafuu ya akina Lowasa, sasa huyu ndiye anayetaka kuwa Rais wa Tanzania kwa unafiki huu ataipeleka wapi nchi yetu? Katika biblia inasomeka: "Kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho!" Ndicho alichochafuka Sitta.

Mbaya zaidi amemharibia Kikwete heshima aliyojijengea kimataifa kufanikisha kuendesha mchakacho wa Katiba mpya kwa utaratibu na ufanisi bila ushinikishwaji wa vita kama baadhi ya nchi, na sasa Kikwete heshima hiyo imeota mbawa sababu ya unafiki wa Swamwel Sitta.


:juggle: Je, yametimia Samwel Sitta ni mnafiki kama ilivyotamkwa na Dr. Slaa? :juggle:
 
Samuel-Sitta-531x272.jpg


Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.


"Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu," alisema Sitta na kuongeza;

"Mimi napokea matusi kila siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa Chadema wameweka namba zangu katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi niko tayari na mnaniona niko safi tu wala sihangaiki nalo."

"Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura ya mwenyekiti wake," alisema.

Sitta alienda mbali zaidi na kusema, "Kwa hiyo wale wanaoendeleza hayo mapambano tuendelee na tutaendelea kupambana, lakini kazi ya Bunge Maalumu itaendelea na ndugu zangu Watanzania mjue tunaandaa Katiba safi na rafiki kwa wananchi na itapatikana."

Sitta alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kesi ya Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kumekuwa na tafsiri alizosema ni potofu.

Baada ya maelezo hayo alimpa ruksa AG, Jaji Frederick Werema kutoa ufafanuzi.

Jaji Werema alisema Mahakama Kuu, katika kutafsiri kifungu cha 25(1) (2) inakiri kwamba kuna tofauti kati ya kifungu kilichoandikwa Kiswahili na kile kilichoandikwa Kiingereza.

Alisema Mahakama Kuu katika hukumu hiyo imesema mamlaka ya kuandika Katiba Mpya ina maana ni mamlaka ya kuandika na kupitisha katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.

Takukuru yalitesa Bunge

Wakati hayo yakiendelea suala la kuingizwa ama kutoingizwa kwenye katiba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), linaonekana kulitesa Bunge la Katiba baada ya kamati 10 kati ya 12 kulirejesha tena jana.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ililiacha suala hilo kwa maelezo kuwa siyo moja ya mambo ya Muungano na msimamo huo ukaungwa mkono na Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo.
Chanzo: Mwananchi

 
anasema viongozi wa chadema wameweka namba zake kwenye tovuti ili atukanwe...
 
Back
Top Bottom