Sitta on DOWANS payment: unanswered questions and painful

Sitta on DOWANS payment: unanswered questions and painful

ushujaa wa sitta kuhoji malipo ya hukumu ya Tan Vs DOWANS ni dhahiri kuwa kuna kitu ambacho hakipo katika hali ya kawaida ..... je tume ya mwakyembe ambayo ndio iliyotoa ushauri kwa serikali kusitisha mkataba na DOWANS walikuwa hawana vithibiti vya uhalali wa haya makampuni.... lets call back Mwayembe report na vithibitisho aya tume tuone..... i stand behind Mr. sitta.... there is something fishy ..... and i smell something wrong here..........!!!!!!!!
 
Watu kama Sitta sio wa kubezwa wala kukatishwa tamaa. Ili wasonge hatua mbele zaidi lazima tuwaunge mkono. Kuna kitu cha ajabu kinaendelea katika nchi hii. Haiwezekani waziri anaelezea malipo tutakayolipa kwa mbwembwe na tabasamu, haonyeshi uchungu wowote, anafurahia nini? Kuna kitu kibaya katika hii hukumu na malipo. Ni kama vile wanawakomoa wale waliopinga Richmond na Dowans. Sitta aungwe mkono ni njia pekee ya kumfanya asonge mbele katika ujasiri anaouonyesha. Tukimbeza atakata tamaa na atakuwa hana njia isipokuwa kuungana nao. Ama awe nasi au awe nao. Njia pekee ya kumfanya awe nasi madamu ameamua ni sisi kumuunga mkono, vinginevyo itabidi awe nao!
 
Sitta anaujasiri wa kufanya haya...?.... inamaana mpaka cabinet iridhie ndiyo malipo yatafanyika..? au sitta anatuweka sawa tu aonekane anapinga malipo hayo.... au anashinikiza ili nae apate mgao

hapana Sita yuko sahihi kwa jambo kubwa kama hili la malipo ya kimataifa na linalo gusa maslahi makubwa ya nchi lazima Cabinet ijadili na kuridhia.
 
Chuma cha pua gani kilichotaka kupambana na Slaa wakati wa kampeni, mdahalo uliokatazwa na Makamba. Hakuna chuma pale, ni plastiki kwa kwenda mbele. Hiki ndicho chuma kilichotoa chozi kisipokwe kadi ya CCM. Mchanganyiko wa chuma na udongo..........
Sidhani kama alitoa chozi ili asipokonywe kadi bali alipata uchungu sana pale alipoona anahukumiwa kwa kunyang'anya uanachama na kuchukiwa kwa kuwa mkweli na kuweka maslahi ya taifa mbele.Tena hasa alipojikuta yuko mwenyewe katika vita ya ufisadi huku wenzie wakiwa pro-ufisadi.kama wewe ukiwa katika hiyo position ndio utaelewa nini maana ya kuhukumiwa kwa ukweli wako.
 
mkuu..... naihisi hiyo hali ni ngumu..... lakini hali hiyo ya uchungu mkubwa na uonevu..... ni watanzania wangapi wanaishi kwa hali hiyo katika muda wote wa maisha yao.... yeye ni siku moja tu anatoa machozi.... na hiyo ndiyo ingekua kujitoa muhanga kwa maslahi ya taifa...... kwani kadi ya uanachama wa CCm inaingia kwenye ATM ........? lazima ushujaa utumike kwa viongozi.....
 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri katika Baraza la Mawaziri ameamua kumkosoa mwenzake hadharani kutokana na uamuzi alioutangaza hivi karibuni kwa Taifa.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ndiye amepata ujasiri huo kwa kumkosoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutokana na kutangaza kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Sh bilioni 94, hatua ambayo anaona hakustahili
kuitangaza yeye

source:HabariLeo | Sitta ampinga Ngeleja malipo fidia Dowans

Sasa waJF hawa mawaziri wa JK hawakai pamoja na kutolea maamuzi ya pamoja kuhusu maswala ya taifa kabla waziri husika hajasema kwa niaba ya serikali maana juzi Cecila Kombani naye katiba serikali haina hela PM tutashauriana na JK
Sasa tumwamini nani au mpaka JK aseme mwenyewe? nisaidieni waJF

Nawakilisha

Unapoona ndani ya nyumba watoto wanafarakana kila kukicha lazima ujiulize wazazi wao wako wapi,kama wapo basi iweje iwe hivyo.Imeshasemwa sana na iko wazi sana kwamba baba mwenye nyumba ndio mwenye mapungufu hapa, hata naye akakurupuka kutangaza marekebisho ya katiba bila kuwashirikisha wenzie.
 
mkuu.... hapa umenena ..... sasa nasema kula tano yangu instantly..... pili baba mwenye nyumba hakustahili kupewa nyumba hii..... nyumba hii ina wenyewe... mungu atato hukumu ya anayestahili nyumba hii... time will tell...cross your fingers
 
jamani naomba nijue huyo ngereja ana qualification gani? because i his capacity of thinking, please help me.
 
Watu kama Sitta sio wa kubezwa wala kukatishwa tamaa. Ili wasonge hatua mbele zaidi lazima tuwaunge mkono. Kuna kitu cha ajabu kinaendelea katika nchi hii. Haiwezekani waziri anaelezea malipo tutakayolipa kwa mbwembwe na tabasamu, haonyeshi uchungu wowote, anafurahia nini? Kuna kitu kibaya katika hii hukumu na malipo. Ni kama vile wanawakomoa wale waliopinga Richmond na Dowans. Sitta aungwe mkono ni njia pekee ya kumfanya asonge mbele katika ujasiri anaouonyesha. Tukimbeza atakata tamaa na atakuwa hana njia isipokuwa kuungana nao. Ama awe nasi au awe nao. Njia pekee ya kumfanya awe nasi madamu ameamua ni sisi kumuunga mkono, vinginevyo itabidi awe nao!

Wakuu nimejikuta nimekumbuka hii article iliyotolewa na habari leo mnamo Aprili, 2009.

Enjoy:

JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd April 2009 @ 07:30

Source: Habari leo

Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited.

Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

"Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans.

Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao.

"Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini.

"Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa. (Well sijui taarifa mlipewa?)

Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili.

Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.

Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa.

"Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa.

Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii.

"Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo.

"Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida. Kuhusu hali ya chakula, Rais alisema bahati mbaya sana mikoa inayopata mvua za masika hivi sasa hazikupata mvua nzuri wakati wa msimu wa mvua za vuli mwaka jana.

Na kwa sababu hiyo, kilimo katika mikoa hiyo kimeathirika, mavuno yamekuwa chini ya wastani na wako baadhi ya wakulima ambao hawakujaaliwa kupata chochote kabisa.

Katika hali hiyo basi, kama katika msimu wa masika hali itakuwa chini ya wastani, ni dhahiri kutajitokeza tatizo kubwa kwa upande wa upatikanaji wa chakula na mapato ya wakulima kwa jumla.

"Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inafuatilia kwa karibu hali hii na tumekuwa tunajiandaa kuchukua hatua zipasazo," alisema. Kuhusu msukosuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unaanza leo London, Uingereza, alisema umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

"Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. (Blaza acha uongo!)

Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini, itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na masikini.

Matajiri watakuwa masikini na masikini watakuwa fukara zaidi," alisema. Alisema kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora.

"Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu masikini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinahitaji sana, bado hazijasaidiwa," aliongeza. Pia alielezea masikitiko yake kwa ajali tatu zilizotokea hivi majuzi, ya magari Mbeya; ya treni mbili zilizogongana Dodoma na ya mgodi kufukia wachimbaji, Geita.

"Kwa ajali zote hizo tatu, moyo wangu uko pamoja na familia za wafiwa na waliojeruhiwa. Majonzi yao ndiyo majonzi yangu. Na machungu yao ndiyo machungu yangu. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wetu hao mahali pema peponi. Amin!" Alisema na kuwaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na juhudi zao za ujenzi wa taifa.

My Take:

Just read between the lines if not words utagundua ni jinsi gani mkulu wetu alivyokuwa mtu wa maigizo na populist. How come alichip in kwenye mchakato wa Bilioni 40 (ununuzi wa mitambo ya Dowans) lakini wakati inaongelewa Bilioni 185 akanyuti, kimyaaaaaaaa!Mpaka tumefika mahali tunatakiwa tulipe hizo Bilioni karibu 100 hajasikika.

Ndiyo maana nilitundika tundiko hilo hapo juu kuonyesha ni namna gani muung`wana anabadilika kama kinyonga and yet kuna wapuuzi wanataka tuamini malipo haya ya Dowans yametokana na resistance ya watu kama Sitta, Mwakyembe etc.
 
mkuu... sijaelewa hapa una compare vitu gani viwili..... clarify
 
mkuu... sijaelewa hapa una compare vitu gani viwili..... clarify

Mkuu kama hujanote kuna kampeni za chini kwa chini kwamba haya malipo kwa Dowans yamesababishwa na akina Sita na wale watu wa kamati ya Mwakyembe. Lakni tukirudi nyuma unakuta yaliyokuwa yakisemwa na akina Sita in the end hata JK alikuja kuunga mkono (As per hiyo hotuba yake). Sasa kinachoshangaza watu wale wale wanaotaka Sitta aonekane ndiye chanzo cha malipo haya hawataki kabisa hata jina la JK litajwe kwenye sakata hili.
 
Back
Top Bottom