Dowans yampigilia msumari wa mwisho JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans yampigilia msumari wa mwisho JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Dec 4, 2010.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nimeopoa taarifa hii kutoka maktaba ya HabariLeo. Ni mwaka umepita sasa tangu JK "apigilie msumari wa mwisho Dowans", kwa kuponda maamuzi ya washauri wake. Badala yake, mataizo ya umeme ndio kwanza pamoja na ahadi zote alizotoa. Na kama haitoshi, sasa Dowans ndiyo iliyopigilia msumari wa mwisho JK, TANESCO na uchumi wa Watanzania. Kazi kwetu!

  JK APIGILIA MSUMARI WA MWISHO DOWANS (CHANZO: HabariLeo tarehe 2/4/2009).

  Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

  "Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

  Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao. "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

  "Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini. "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa.

  "Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili. Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.
  Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa. "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

  Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa. Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

  Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii. "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo".

  "Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida".
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Good. This is good. Laiti tungekuwa na reflections za namna hii, wanasiasa wetu wangekuwa na aibu. Lkn bado! Tafakari alichozungumza Mh rais hapo juu last year na kinachotokea sasa hivi, what can you deduce from those statements?
  Aibu!
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tumegeuzwa mandondocha kila siku kudanganywa tuu,rasmali zetu za tumiwa vibaya kutokana na maamuzi mabove eeh Mungu tuangalie viumbe vyako hawa wanyafuzi wa mali ya umma wanatumaliza ,kweli utawala wa CCM ni kichwa cha mwendawazimu
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hehehe.
  na pale ikulu kuna generator linaloweza kutosheleza mahitaji ya umeme kwa dar na morogoro
  jamaa hana wasiwasi na mgao wa umeme. mlie tu
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu nimejikuta nimekumbuka hii article iliyotolewa na habari leo mnamo Aprili, 2009.

  Enjoy:

  JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd April 2009 @ 07:30

  Source: Habari leo
  Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited.

  Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

  "Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans.


  Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

  Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao.


  "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

  Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini.


  "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa. (Well sijui taarifa mlipewa?)

  Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili.


  Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.

  Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa.


  "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

  Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa.


  Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

  Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii.


  "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo.

  "Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida. Kuhusu hali ya chakula, Rais alisema bahati mbaya sana mikoa inayopata mvua za masika hivi sasa hazikupata mvua nzuri wakati wa msimu wa mvua za vuli mwaka jana.


  Na kwa sababu hiyo, kilimo katika mikoa hiyo kimeathirika, mavuno yamekuwa chini ya wastani na wako baadhi ya wakulima ambao hawakujaaliwa kupata chochote kabisa.

  Katika hali hiyo basi, kama katika msimu wa masika hali itakuwa chini ya wastani, ni dhahiri kutajitokeza tatizo kubwa kwa upande wa upatikanaji wa chakula na mapato ya wakulima kwa jumla.


  "Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inafuatilia kwa karibu hali hii na tumekuwa tunajiandaa kuchukua hatua zipasazo," alisema. Kuhusu msukosuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unaanza leo London, Uingereza, alisema umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

  "Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. (Blaza acha uongo!)


  Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini, itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na masikini.

  Matajiri watakuwa masikini na masikini watakuwa fukara zaidi," alisema. Alisema kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora.

  "Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu masikini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinahitaji sana, bado hazijasaidiwa," aliongeza. Pia alielezea masikitiko yake kwa ajali tatu zilizotokea hivi majuzi, ya magari Mbeya; ya treni mbili zilizogongana Dodoma na ya mgodi kufukia wachimbaji, Geita.

  "Kwa ajali zote hizo tatu, moyo wangu uko pamoja na familia za wafiwa na waliojeruhiwa. Majonzi yao ndiyo majonzi yangu. Na machungu yao ndiyo machungu yangu. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wetu hao mahali pema peponi. Amin!" Alisema na kuwaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na juhudi zao za ujenzi wa taifa.


  My Take:

  Just read between the lines if not words utagundua ni jinsi gani mkulu wetu alivyokuwa mtu wa maigizo na populist. How come alichip in kwenye mchakato wa Bilioni 40 (ununuzi wa mitambo ya Dowans) lakini wakati inaongelewa Bilioni 185 akanyuti, kimyaaaaaaaa!Mpaka tumefika mahali tunatakiwa tulipe hizo Bilioni karibu 100 hajasikika.   
 6. g

  gepema Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  We real have a serious leadership problem in this country,how does he keep on changing everyday like chameleon?
   
 7. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa presidaa atakuwa ana brain problems. Hivi inawezekana Rais wa nchi ukawa maamuma kiasi hiki? Jamani inabidi huyu president akabidhi nchi kwa wengine. Mimi nilimuamini sana ila kwa sasa nafuu hata president angekuwa Lowassa. AGHHHHHHHHHHH
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani mkuu we acha tu!
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

  "Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

  Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao. "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

  Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini. "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa.

  Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili. Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.

  Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa. "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

  Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa. Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

  Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii. "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo.

  "Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida. Kuhusu hali ya chakula, Rais alisema bahati mbaya sana mikoa inayopata mvua za masika hivi sasa hazikupata mvua nzuri wakati wa msimu wa mvua za vuli mwaka jana. Na kwa sababu hiyo, kilimo katika mikoa hiyo kimeathirika, mavuno yamekuwa chini ya wastani na wako baadhi ya wakulima ambao hawakujaaliwa kupata chochote kabisa.

  Katika hali hiyo basi, kama katika msimu wa masika hali itakuwa chini ya wastani, ni dhahiri kutajitokeza tatizo kubwa kwa upande wa upatikanaji wa chakula na mapato ya wakulima kwa jumla. "Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inafuatilia kwa karibu hali hii na tumekuwa tunajiandaa kuchukua hatua zipasazo," alisema. Kuhusu msukosuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unaanza leo London, Uingereza, alisema umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

  "Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini, itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na masikini. Matajiri watakuwa masikini na masikini watakuwa fukara zaidi," alisema. Alisema kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora.

  "Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu masikini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinahitaji sana, bado hazijasaidiwa," aliongeza. Pia alielezea masikitiko yake kwa ajali tatu zilizotokea hivi majuzi, ya magari Mbeya; ya treni mbili zilizogongana Dodoma na ya mgodi kufukia wachimbaji, Geita.

  "Kwa ajali zote hizo tatu, moyo wangu uko pamoja na familia za wafiwa na waliojeruhiwa. Majonzi yao ndiyo majonzi yangu. Na machungu yao ndiyo machungu yangu. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wetu hao mahali pema peponi. Amin!" Alisema na kuwaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na juhudi zao za ujenzi wa taifa.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni yapi yametekelezwa? Ni yapi yamekuwa! Tutasubiri hotuba ya mwisho wa mwezi huu!
   
 11. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  Last paragraph always makes me happy
   
 12. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  hii ndio tanzania CCM wanayoitaka BRAVO
   
 13. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Tanzania tanzania.......nakupenda kwa moyo woteeeeeeeeeeeeee....................................nchi yangu tanzania.....................heri yako kwa mataifaaaaaaaaaaaaa..................
   
 14. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  nILALAPO NAKUWAZA WEWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.......................................NIAMKAPO NI HERI MAMA WEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.............................
   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Tanzaniaaaaaaaaaaaa tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa jina lako ni tamu sana..............
   
 16. c

  chama JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mambo ya mgawo tumeshayazoea mheshimiwa Raisi anapaswa kutueleza hatima ya $ 68m za kuwalipa Dowans, pia sijui tumuamini nani katika serikali hii, majuzi tu waziri Ngeleja aliiponda Tanesco kwani ndiyo ilikuwa chanzo cha matatizo ya Dowans kutokana na utendaji wake mbovu leo hii mh. Raisi anaipongeza Tanesco kwa utendaji bora sasa watanzania tumuamini nani?
   
 17. H

  HYDROCHLORIC Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio aachie nchi ikiwezekana kuondoka kabisa nchini kwetu au afungwe maisha.
   
 18. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mungu ibariki TZ kwani kila kitu ni PEACE! watu wanaongea kwa amani, watu wanaiba kwa amani, watu wanabaguana kwa amani, everything is real PEACE!!!!!!!!
   
Loading...