Sitta: Nilitemwa uspika kwa hila za vigogo

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
56,332
2,000
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta jana alitoa kauli nyingine inayoweza kukitikisa chama chake cha CCM baada ya kueleza kuwa aliondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha spika wa Bunge la Muungano kutokana na hila za viongozi ambao walishindwa kuhimili kasi ya utendaji wake kwenye chombo hicho cha kutunga sheria.

Sitta, ambaye alipata umaarufu baada ya kuliongoza Bunge la Tisa kwa mafanikio, ametoa kauli hiyo wiki chache baada ya kukaririwa na vyombo vya habari akisema bayana kuwa kuilipa kampuni tata ya Dowans fidia iliyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC) ni sawa na kuhujumu uchumi.
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki alijikuta akianguka kwenye kinyang'anyiro cha uspika wa Bunge la Kumi baada ya chama chake cha CCM kuamua kuwapa wanawake nafasi ya kuongoza moja ya mihimili ya nchi na hivyo kupitisha wagombea watatu wanawake katika mchakato uliompa ushindi Anne Makinda.

Jana, Sitta ambaye alikuwa akihojiwa na Mwananchi, alisema utendaji wake wa kasi na viwango uliwatisha viongozi wengi wa serikali na ndio maana wakaamua kutumia kigezo cha jinsia kumwondoa.

"Unajua nataka hili ilieleweke; juzi nilienda jimboni kwangu Urambo Mashariki nikawaeleza wapiga kura wangu kwa nini sasa mimi sio spika tena, maana wanaweza kudanganywa kama kazi imenishinda au nimefukuzwa," alisema Sitta.
"Watanzania lazima wajue mimi sijafukuzwa kazi wala sijashindwa kufanya kazi hiyo, ila kuna viongozi ambao ni wakuu wangu ndani ya chama chetu ambao wameshindwa kuendana na kasi na viwango vyangu ndio maana wakaamua kuweka sharti ambalo kamwe nisingeweza kulitimiza.

"Kigezo hicho cha jinsia walikileta katika hatua za mwisho za mchakato wa kumtafuta spika wakijua kwamba sitaweza kukitimiza na ningejua hilo mapema, nisingepeleka jina langu kuomba kuteuliwa tena."
Sitta alisema ni wazi kamba asingeweza kutimiza sharti kwamba spika aliyetakiwa safari hii ni mwanamke ndio maana hakuweza kuteuliwa tena kuwania nafsi hiyo.

"Mimi ni Sitta na nitabaki kuwa Sitita yule yule kama nilivyozaliwa na kwa vyovyote vile; nisingeweza kufanya chochote ili kuhakikisha sharti hilo nalitimiza," alisema Sitta.
Hata hivyo Sitta alisema kuwa endapo jina lake lingepitishwa, alikuwa na ukakika wa kurudi katika kiti hicho kwa kuwa asilimia kubwa ya wabunge walikuwa wameukubali utendaji wake.

Katika miaka ya mwisho ya uongozi wake wa Bunge la Tisa, Sitta alikuwa akilalamikia kuwepo kwa njama alizodai zinafanywa na mafisadi kutaka kumuangusha kwenye ubunge na wakati fulani alifikia hadi kuomba ulinzi zaidi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisema anatishiwa maisha.

Sitta hajawahi kuwataka hadharani wapinazani wake,


SOURCE:- MWANANCHI
 

MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,154
1,250
Tunashukuru Sitta kwa kupasua ukweli. Yawezekana ukaendelea kuwa mpiganaji pamoja nasi.! sema ukweli tu
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,071
2,000
Sitta is old enough to know that you cannot eat your cake and still have it!! Alitaka aonekane mpambanaji dhidi ya mafisadi at the same time alitaka kuwafurahisha hao hao aliokuwa anawapinga kwa kuuzima mjadala wa RICHMOND bungeni!! Hatma ya undumila kuwili kwake ndio huko KUTOSWA kwenye himaya ya uspika. It is a good lesson to fence-seaters.
 

semango

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
532
195
kama kweli sitta ni msafi na ni mpiganaji kama anavyodai basi ahame chama cha mafisadi ambao anaona dhahiri wanampinga.ila kwa kuendelea kua nao chama kimoja kwangu anaendelea kua mnafiki tu kama wao
 

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,069
1,225
lakini bahati mbaya sasa sitta ameingia kwenye nafasi ya utii hivyo hatakuwa sitta yule wa zamani na mchango wake sasa utakuwa ni malalamiko tu kupitia magazeti. pole mhe sitta. watanzania wanakufahamu ila haki ndiyo iliyokuponza.
 

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
615
195
Ninachofikiria na jinsi ninavyoifahamu SISIEMU, Sitta huko uliko siko. Watakutupotezea si muda mrefu!
 

Kiraka

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
2,790
2,000
Sitta is old enough to know that you cannot eat your cake and still have it!! Alitaka aonekane mpambanaji dhidi ya mafisadi at the same time alitaka kuwafurahisha hao hao aliokuwa anawapinga kwa kuuzima mjadala wa RICHMOND bungeni!! Hatma ya undumila kuwili kwake ndio huko KUTOSWA kwenye himaya ya uspika. It is a good lesson to fence-seaters.

Ndinani
Wewe ni mtu unaemuelewa huyu jamaa, kula tano! tunasema You've nailed it!!
Aende zake ndumila kuwili... eti viwango, mzandiki huyu!.
 

mmakonde

JF-Expert Member
Dec 26, 2009
966
0
Sam Six anatakiwa ku shut up!Kama yuko bitter ,mbona bado yuko kwenye hicho chama cha kifisadi?
Ile ofisi yake ya Bunge huko kwao itafanyiwa nini?
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,374
2,000
Ama kweli tukifanikiwa kuwa na akina sitta 50, akina slaa 10, akina magufuli 70, akina mwakyembe 80, na vyama makini km chadema viwili tu....taifa litakuwa limekombolewa...................lakini kinyume chake, tukiwa na akina rostamu 5, lowasa 10, ,kikwetw 3,na vyama visivyomakini kama cuf na ccm 4 basi hatuna nchi tena tutakuwa km tulivyo milele
naomba tubadilike kwa kuchagua viongozi makini na vyama makini
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,531
2,000
mnafiki sana huyu mzee...kama kulikuwa na hila how come akubali kuwa waziri....
 

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,932
2,000
Mnafiki tu huyo! Uliona msafara wake wa kwenda Urambo jinsi Land Cruiser VX G8 zilivyokua zimejipanga? Ndani ya CCM hakuna mtu MSAFI na mwenye kujali MASLAHI ya RAIA. They are ALL HYPOCRITES.
 

Shapu

JF-Expert Member
Jan 17, 2008
2,090
2,000
Sitta is old enough to know that you cannot eat your cake and still have it!! Alitaka aonekane mpambanaji dhidi ya mafisadi at the same time alitaka kuwafurahisha hao hao aliokuwa anawapinga kwa kuuzima mjadala wa RICHMOND bungeni!! Hatma ya undumila kuwili kwake ndio huko KUTOSWA kwenye himaya ya uspika. It is a good lesson to fence-seaters.

Well said.
 

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
1,250
huyu naye ni zito mwingine ndani ya ccm............ watanzania sijui wanafikiria kwa kutumia magoti??......... nlidhani ni zito wa chadema tu, kumbe hata sita wa ccm naye hajakomaa kwa kiwango hiki??...................... no huyu amekomaa na anajua anachokifanya.............. jina lake zuri ni mnafiki na fisadi kinyonga.....................
 

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,878
1,195
anauma na kupuliza...ondoka ccm kama wamekufanyia hila!! huyu sitta ni ****...anaboa sasa!
 

ngoko

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
573
0
Ama kweli tukifanikiwa kuwa na akina sitta 50, akina slaa 10, akina magufuli 70, akina mwakyembe 80, na vyama makini km chadema viwili tu....taifa litakuwa limekombolewa...................lakini kinyume chake, tukiwa na akina rostamu 5, lowasa 10, ,kikwetw 3,na vyama visivyomakini kama cuf na ccm 4 basi hatuna nchi tena tutakuwa km tulivyo milele
naomba tubadilike kwa kuchagua viongozi makini na vyama makini
Mh!! kumbe tunabahati tunaye JK 1, na RA 1 tu , madhara ni kidogo .. Lol
 

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,158
2,000
Mzee wangu kaa kimya kula hela za mwisho mwisho, angalia wenzako akina samweli wako wapi? - ushukuru hata huo uwaziri maana ulitakiwa ukose kila kitu urudi urambooo...

Pili ningefurahi sana kauli hii ungeitoa kabla ya kuundwa kwa baraza la mawaziri...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom